Kigezo cha mendeleo ya nchi ni maisha bora ya mwananchi wa kawaida

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1128797153_16566790305501n.png


Pili Mwinyi

Hivi majuzi katika pekuapekua zangu kwenye mitandao ya kijamii nilikutana na msemo mmoja ambao ulinifanya nitulie kwanza na kuutafakari kwa kina. Msemo huu umeshiba busara na hekima kubwa kama utauangalia kwa jicho linaloona, na hata kwa wale ambao msemo huu unawagusa moja kwa moja kwenye maisha yao ya kila siku, naamini watakubaliana nami.

Msemo wenyewe unasema hivi “Ni pale tu ghala litakapojaa ndio watu watajifunza adabu; na ni pale tu watu watakaposhiba na kuvaa vizuri ndipo watakapojua heshima na aibu”. Huu ni msemo wa kale wa Kichina ulionukuliwa na rais Xi Jinping wakati alipokuwa akihutubia kwenye Mazungumzo ya Ngazi ya Juu yanayohusu Maendeleo Duniani yaliyofanyika Ijumaa ya terehe 24 Juni.

Labda kabla ya kuendelea mbele zaidi, kusema kile kilichopo moyoni mwangu, kwanza nikufahamishe tu kwamba msemo huu unatoka Shiji, na hii ni kwa mujibu wa rikodi za ‘Mwanahistoria Mkuu’ yaani kitabu kikubwa cha historia ya China ya kale kilichotungwa miaka 2,000 iliyopita. Tukiangalia kwa kina msemo huu tutagundua unasisitiza kwamba uwepo wa vitu muhimu maishani ndio msingi wa mifumo ya nchi pamoja na maadili ya jamii.

Katika jamii zetu nyingi hasa za nchi masikini, kumekuwa na mwendelezo wa matukio ya kunyonyana kila siku. Laiti serikali za nchi zetu zingeweza angalau kuwapumbaza wananchi wao kwa kuwafanyia mambo au vitu vya msingi, vikiwemo kuhakikisha watu wanamudu kupata chakula bila matatizo tena kwa bei rahisi, au wanapoamua kwenda madukani kufanya manunuzi ya vitu vyao mathalan nguo, vitu vinavyotumika katika maisha ya kila siku, ama huduma rahisi mahospitalini, basi naamini wangeridhika na wasingekuwa na manung’uniko yoyote.

Lakini ukiangalia maisha ya watu wa kawaida, hasa wa nchi za Afrika yanazidi kuwa magumu kila siku, hadi baadhi ya watu wakaamua kuyapa jina la “Vyuma vinakaza” wakimaanisha kwamba maisha hayashikiki, na yamekuwa magumu.

Tunafahamu kuwa China ni nchi kubwa sana na ina watu wengi zaidi duniani. Lakini cha kushangaza ni kwamba ukiangalia maisha ya watu wa kawaida, kweli unaweza kujiuliza mara mbilimbili kwamba je, hivi wenzetu Wachina wamepatia wapi na sisi tumekosea wapi? Mbona maisha yao ni mepesi sana kuliko hata baadhi ya nchi za Afrika ambazo watu wake ni wachache sana?

Baada ya kukaa na kutafakari sana nikagundua kuwa mfumo wa nchi yaani China, ni rafiki zaidi na unajali zaidi mwananchi wa kawaida. Pia mipango inayojiwekea nchi hii. Wacha nitoe mfano, kila baada ya miaka mitano China huwa inajiwekea mipango mbalimbali ya maendeleo ambayo inapaswa kutekelezwa ndani ya muda huo, na cha kupongezwa ni kwamba ndani ya kipindi hicho, mipango yote iliyopangwa inakuwa imetekelezwa kwa asilimia mia moja, na kunakuwa hakuna ubabaishaji.

Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, kulikuwa na kipindi cha kurejesha uchumi hadi mwaka 1952. Kuanzia mwaka 1953, mpango wa kwanza wa miaka mitano (1953-57) uliwekwa na kutekelezwa. Mpango huu ulikuwa wa kujitahidi kufikia kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi na kusisitiza maendeleo katika sekta muhimu kama vile madini, viwanda vya chuma, na teknolojia ikiwemo ya ujenzi wa mashine, huku sekta ya kilimo ikizidi kuendelezwa.

Sambamba na hilo, katika hatua mpya ya kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na wazee, China imeweka mpango wa maendeleo ya mfumo wa huduma za wazee ambao utatekelezwa katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025). Mpango huo unaweka wazi malengo makuu na majukumu ya kipindi hicho cha miaka mitano, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wazee, kuboresha muundo ili kusaidia afya ya wazee, na kuendeleza uvumbuzi na maingiliano ya mifumo ya huduma.

Hii ni mifano michache tu ambayo nimeitaja, na kama utakuwa umekaa China basi utashuhudia yote haya, kwamba mipango hii imewekwa kuanzia kwenye maisha ya wazee, vijana na hata watoto na kupewa kipaumbele kikubwa na serikali kuu.

Waswahili wanasema “Uchungu wa mwana aujuae mzazi” Mzazi tunayemzungumiza hapa ni serikali, na kwa China inaongozwa na rais Xi Jinping, ambaye naye ana uzoefu mkubwa wa maisha ya mtu wa chini, kwani kama itakumbukwa katika miaka ya 60, rais Xi alikuwa mkulima katika Uwanda wa juu wa Loess hivyo ameonja machungu ya kuwa mkulima wa kawaida, na ndio maana sera zake moja kwa moja zinajikita kumuweka mbele mtu wa kawaida.

Viongozi wengi wa nchi zetu huwa hawajapitia machungu anayopitia mwananchi wa kawaida. Ndio maana wanapoingia madarakani wanajisahau na kuangalia matumbo yao binafsi pamoja na familia zao, huku maisha ya watu wa chini yakiendelea kudidimia na kuwa magumu zaidi. Wakati umefika sasa kwa viongozi kumuweka mbele mwananchi wa kawaida, badala ya kujiangalia zaidi wao wenyewe, kwani wakumbuke kuwa waliwaahidi wakati walipokuwa wakijinadi mbele yao ili wawachague. Na pia wasisahau kuwa wananchi haohao ndio waliowaweka madarakani.

Kama anavyoamini rais Xi, kwamba ni kupitia maendeleo endelevu tu ndipo ndoto za watu za kuwa na maisha bora na utulivu wa kijamii, inaweza kutimizwa. Na viongozi wa nchi zetu za Afrika, wanapaswa kuutilia maanani msemo huu“Ni pale tu ghala litakapojaa ndio watu watajifunza adabu; na ni pale tu watu watakaposhiba na kuvaa vizuri ndipo watakapojua heshima na aibu”
 
In Africa people with Ideas have no power, and people with power have no ideas completely. Prof: Lumumba

Kiongozi una mawazo mazuri sana ila huna madaraka. Wenye madaraka ndio vile tena wanabeua tu baada ya kunywa wine
 
Back
Top Bottom