Tusifanye usambazaji wa konekshen za watu kuwa jambo la kawaida, tunaharibu maisha ya watu

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Naona tumefanya unyanyasaji wa mtandaoni uonekane kama kitu cha kawaida bila kujali kwa kufanya hivyo tunaweza kuharibu maisha ya watu wengi sana, kwasababu unyanyasaji au bullying kwa kimombo inaathiri sana afya za akili za watu.

Siku hizi mambo mengi yapo hadharani na yanaelezewa kwa upana na urefu, Matatizo ya Afya ya Akili iwemo. Ni dhahiri kuwa haya mambo yanaweza muumiza mtu katika fikra yake na kusababisha msongo wa mawazo ambapo unaweza kuharibu mfumo wa maisha ya mtu au mbaya zaidi ukaharibu maisha ya mtu kimoja kuanzia kazini, chuoni, shuleni na hata nyumbani.

Mitandaoni ni moja ya sehemu ambayo tunafanyiana unyanyasaji mkubwa sana, tunatukana na comments za kutisha.

Chukulia mfano Mange alivyopost connection ya Gigy, tukumbuke ni jambo la faragha, halituhusu, yeye kupost na sisi kuendelea kusambaza na kushadadia huku tukituna kwa maneno ya kashfa tayari ni kosa na sio uungwana.

Ni kwasababu hatujiweki katika viatu vyao ndio maana tunaona sawa tu kuendeleza jambo hili, lakini fikiria mtu wako wa karibu leo, mama yako, dada yako au wewe mwenyewe unapatwa na jambo hili utaweza kuhimili manyanyaso na masimango yanayokuja kwako? Sasa kwanini tunaendelea kuwa sehemu ya watu wanaendeleza ukatili huu dhidi ya waathirika hawa?

Tubadilike, jamii bora inaanza kujengwa na wewe.
 
Acha kutetea upumbavu. Waambie kwanza hao wanaorekodi video za hovyo waache kufanya hivyo. Pia wakemee wanawake wanaopenda kupiga picha za uchi. Karibu wanawake wote wana picha ambazo wamevaa chupi na bra peke yake kama sio uchi kabisa.
Ni kosa kubwa sana kujirecord ni kweli, ila shida yangu hapa ni kuonesha kuwa kusambaza hizi video zaidi ni kosa kubwa zaidi
 
Maisha ndivyo yalivyo; lazima mmoja aumie mwingine anufaike; ili wewe ushinde lazima awepo mwingine ashindwe, ili wewe upate kazi lazima awepo wa kupoteza kazi, ili hospitali ipate mapato lazima wewe uugue, ili magereza pajae watu lazima wewe upewe kifungo n.k​
 
Naona tumefanya unyanyasaji wa mtandaoni uonekane kama kitu cha kawaida bila kujali kwa kufanya hivyo tunaweza kuharibu maisha ya watu wengi sana, kwasababu unyanyasaji au bullying kwa kimombo inaathiri sana afya za akili za watu...
Bullying imekuwa ikifqnyika miaka yote, mbaya zaidi baadhi ya hizi kampeni za kufanya bullying wakati mwingine huwa zinafadhiliwa kupitia 'kodi zetu'. Kilichoongezeka kwa sasa ni kuongezeka kwa namna au njia zaidi za kufanya bullying.

Je, unafahamu kitu kinachoitwa Black Propaganda? Yellow Propaganda?? Characters Assassination and Smear Campaign Propaganda?

Ni kweli Wapo baadhi ya watu kweli wao wenyewe kwa makusudi wamekuwa chanzo cha kuvuja kwa taarifa zao 'mbaya', lakini wengi wamekuwa wahanga wa 'kutengenezewa' matukio na wabaya (watesi) wao ili kuwachafua makusudi. Mfano mmojawapo ulio hai ni ile video chafu iliyovujishwa ya 'Askofu Gwajima'.
 
Back
Top Bottom