Maisha sio muhimu na bora kama uzima

Philo_Sofia

Member
Oct 4, 2023
60
94
Maisha ni mambo yote tunayofanya. Ni shughuli zote za uchumi na utafutaji wa fedha na mali, na kadhalika. Haya yote ni muhimu, na ni ya lazima kwa ukuaji na maendeleo ya mtu.

Lazima watu wafanye kazi, wazalishe, watengeneze na wauze. Wakabiliane na matatizo na changamoto. Waijenge dunia na waendelee. Lakini katika haya yote, sio kwamba hayo ndio mwisho. Mwisho wako ni uzima. Kumbe mtu ni uzima. Kwa hiyo, uzima ni bora na muhimu kuliko maisha.

Uzima ni uhai. Ni Roho. Ni nishati. Ni akili. Ni nguvu. Ni moyo. Ni pumzi. Ni kile kinachobaki hai. Ni kile kinachoendelea kuwepo baada ya mwili kufa na kuharibika.

Maisha si kwa ajili ya maisha yenyewe. Maisha ni kwa ajili ya uzima, ni kwa ajili ya uhai. Maisha yako hayapaswi kuharibu uzima wako. Kama kwa maisha yako umeharibu uzima wako, umeharibu vilevile maisha ya wengine. Hayo sio maendeleo, sio amani, ni uharibifu.

Maisha sio lengo lako la mwisho wala lengo la binadamu. Lengo lako ni uzima, lengo la binadamu ni uhai. Shughuli zako kama zinaharibu uhai, unaharibu uzima wako. Maisha yako lazima yakuongoze kulinda uzima wako; kwa sababu maisha yako ndio yataamua vile uzima wako utakuwa.

Lazima ukabiliane na maisha, lakini ujue kwamba maisha sio lengo lako la mwisho. Lengo lako la mwisho, ni uzima. Baada ya maisha kuna uzima, ambao uzima huo unategemea wewe uliishije. Maisha yako yalikuwaje.

Wafundishe rafiki zako, kwamba baada ya maisha hapa duniani kuna uzima. Huu ndio unaobaki na ndio unaokuwa hai. Wambie waangalie maisha yasije yakaharibu uzima wao. Kwa maana maisha ni uzima na maisha yanaharibu uzima.
 
Kwa maana maisha ni uzima na maisha yanaharibu uzima.
Maisha hayawezi kuleta uzima, wala maisha hayawezi kuharibu uzima. Yaani mambo ya kila siku kama vile chakula, mavazi, kusali, kazi tunazofanya havina msaada wowote katika kutoa uzima.

Kwa sababu maisha yote yanafanyika katika mwili unaoharibika, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu.
Ukitegemea mwili wako(maisha yako) kukuletea uzima umepotea maana mwisho wa mwili ni mauti
 
Viumbe hai vyote uvionavyo na visivyo onekana ni roho zinazoishi, zilizoishi na zitakazoendelea kuishi.

Roho huishi katika mwili na Kisha mwili huaribika ila roho huendelea kuwepo katika ulimwengu wa roho hadi mzunguko wake wa kuingia mwilini ukifika.
 
wala maisha hayawezi kuharibu uzima.
Shughuli zako za maisha kama zinaingilia uhai maana yake unaharibu uzima wako.

..."Uzima ni bora kuliko chakula." Hii maana yake ni kuwa mahitaji ya mwili ni ya lazima na muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya mwili. Lakini upatikanaji wa mahitaji hayo lazima ufanyike, na uwe halali; na kadiri ya akili.

Maisha yako hayawezi kuharibu uzima wa mtu mwingine isipokuwa uzima wako. Aidha, maisha yako yanaweza kuharibu maisha ya mtu mwingine.

Wewe unafanyaje kupata chakula au mahitaji? Je, hivyo unavyofanya au kutenda, ni haki au si haki? Hivi ndivyo maisha uharibu uzima wako.
 
Uzima na uhai ni vitu viwili tofauti. Uzima sio uhai.

Uhai niwa mwilini yaani kupumua, kuingiza na kutoa hewa.
Uzima niwa rohoni, yaani kuishi milele.

Uzima upo na pia hauna mahusiano na kile unachokitenda katika mihangaiko ya maisha yako duniani.
Uhai pekee(yaani kupumua) ndio kunaweza kuharibiwa na maisha ya kila siku kama magonjwa n.k

Kwahiyo watu wanapaswa kutambua kuwa wao wana uzima, na maisha yao ya kila siku hayana mchango kwenye uzima wao.
 
Kwahiyo watu wanapaswa kutambua kuwa wao wana uzima, na maisha yao ya kila siku hayana mchango kwenye uzima wao.
Yesu ndiye ukweli, na hatima ya kila kitu.

Alisema...."uzima ni bora kuliko chakula..." Alimanisha watu lazima wajishughulishe, na kujishughulisha huko katika maisha yako ya kila siku kwa faa kuwe kwa haki.

Roho ya mtu inaungana au unajitenga na Mungu kwa jinsi unavyotenda katika maisha yako ya kila siku. Unaishi haki?

Kwa kujitenga na Mungu yaani uwepo wa hali ya juu wenye akili, uzima gani roho ya mtu inaweza kuwa nao?
 
Alisema...."uzima ni bora kuliko chakula..." Alimanisha watu lazima wajishughulishe, na kujishughulisha huko katika maisha yako ya kila siku kwa faa kuwe kwa haki.
Ni kweli kuwa uzima ni bora kuliko chakula, lakini Yesu hakumaanisha kuwa watu wajishughulishe kana kwamba kujishughulisha kwao aidha kwa haki ama si kwa haki kunaweza kuwapa uzima bali alimaanisha hivi:

Maisha yetu (mfano, kutafuta chakula cha mwilini) hayana maana bila kujali ni ya haki ama si ya haki bali chenye maana ni uzima unaotolewa na yeye pekee si katika shughuli za maisha yetu bali kwa sababu ya upendo wake kwa wale waaminio.

Roho ya mtu inaungana au unajitenga na Mungu kwa jinsi unavyotenda katika maisha yako ya kila siku.
Si kweli. Mungu anakaa ndano yetu endapo tutakabidhi maisha yetu kwa mwanae Yesu bila kujali kwa wakati huo tunatenda nini.
Kukabidhi maisha kwa Yesu maana yake ni kukiri kuwa kwa nguvu zetu ama kwa matendo yetu ya haki hatuwezi kuwa na uzima kwa sababu hatuwezi kutenda matendo ya haki kikamilifu, hivyo tunamkaribisha Yesu aongoze maisha yetu na yeye hutukamilisha na kutufanya watakatifu yaani kutupa uzima.

Hivyo narudia, huwezi kuwa na uzima wa milele kwa sababu unatenda matendo ya haki e.g kutoa sadaka, kutodhulumu n.k
Utapata uzima kwa kukiri kuwa wewe huwezi bali Yesu ndie pekee aliyekuwezesha bila kujali kwa wakati huo wewe ni jambazi ama mzinzi. Angalia mfano wa farisayo na mtoza ushuru
 
Maisha yetu (mfano, kutafuta chakula cha mwilini) hayana maana bila kujali ni ya haki ama si ya haki bali chenye maana ni uzima unaotolewa na yeye pekee si katika shughuli za maisha yetu bali kwa sababu ya upendo wake kwa wale waaminio.
Waaminio ni watu gani? Nini maana ya "anayeamini", na "asiye amini"?

Huwezi kutenganisha imani na matendo: imani isiyo ya kweli huonekana kwa matendo yake, na iliyo ya kweli hivyohivyo.

Kama roho ndio itoayo uzima, vipi kama mtu huyo amejitenga na Mungu wake? Na je! Nini kinafanya mtu ajitenge na Mungu wake kama sio shughuli zake za kila siku?
 
Yesu ndiye ukweli, na hatima ya kila kitu.

Alisema...."uzima ni bora kuliko chakula..." Alimanisha watu lazima wajishughulishe, na kujishughulisha huko katika maisha yako ya kila siku kwa faa kuwe kwa haki.

Roho ya mtu inaungana au unajitenga na Mungu kwa jinsi unavyotenda katika maisha yako ya kila siku. Unaishi haki?

Kwa kujitenga na Mungu yaani uwepo wa hali ya juu wenye akili, uzima gani roho ya mtu inaweza kuwa nao?
Hii ni kwa mujibu wa imani yako na si ya watu wote.
 
Mungu anakaa ndano yetu endapo tutakabidhi maisha yetu kwa mwanae Yesu bila kujali kwa wakati huo tunatenda nini.
Kukabidhi maisha kwa Yesu maana yake ni kukiri kuwa kwa nguvu zetu ama kwa matendo yetu ya haki hatuwezi kuwa na uzima kwa sababu hatuwezi kutenda matendo ya haki kikamilifu, hivyo tunamkaribisha Yesu aongoze maisha yetu na yeye hutukamilisha na kutufanya watakatifu yaani kutupa uzima.
Mungu anawapenda watu wote:wema na waovu.

Lakini Mungu ni mwema, mkamilifu na msafi wa hali ya juu wa akili; kwa hiyo hachangamani na uchafu.

Yesu alizungumza Heri, katika heri hizo alisema, "...Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu".

Mungu ni kweli anakaa ndani yetu, lakini anakaa ndani ya wale tu wenye usafi; usafi wa moyo na akili.

Mungu akai kwa watu wachafu, hatahivyo, anatupenda watu wote. Ukweli huu ni muhimu kuuelewa, ili tufanye bidii tuwe na usafi wa moyo.
 
Kama roho ndio itoayo uzima, vipi kama mtu huyo amejitenga na Mungu wake? Na je! Nini kinafanya mtu ajitenge na Mungu wake kama sio shughuli zake za kila siku?
Wasema hivi kwa sababu unamchukulia Mungu kama mawazo ya binadamu yalivyo, ndio maana hatuelewani.

Mtu hawezi kujitenga na Mungu wake kamwe, ili mradi Mungu ndie aliyempenda kupitia Kristo. Hivi unafikiri ni nini utatenda ili Mungu asikupende? Unafikiri ukizini au ukiiba Mungu ataacha kukupenda?

Fikria kuhusu upendo wa mama na mwanae tu ambao ni binadamu. Unafikiri mtoto utafanya nini kibaya zaidi ili mama asikupende? Je Mungu si zaidi sana?

Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Rum 8:35‭, ‬38‭-‬39 SUV
 
Hii ni kwa mujibu wa imani yako na si ya watu wote.
Hakuna imani zaidi ya moja. Imani ni moja ni tu; kama ambavyo vitu vyote asili yao ni moja.

Hizo zingine ni kasoro, ambazo zinatokana na ukosefu wa kutoelewa mambo kwa kina na elimu ya vitu.
 
Hakuna imani zaidi ya moja. Imani ni moja ni tu; kama ambavyo vitu vyote asili yao ni moja.

Hizo zingine ni kasoro, ambazo zinatokana na ukosefu wa kutoelewa mambo kwa kina na elimu ya vitu.
Na wengine wa din zaidi ya 10000 wanasema hivyo hivyo kama wewe , imani ni ujinga fulani hivi.
 
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Rum 8:35‭, ‬38‭-‬39 SUV
Wewe umechukua mistari baadhi, na kwa sababu hiyo umepotosha wazo zima la andiko lenyewe: andiko au ujumbe unawahusu akina nani.

Ungeanza kusoma kuanzia Rum 8: 31-39.
 
Na wengine wa din zaidi ya 10000 wanasema hivyo hivyo kama wewe , imani ni ujinga fulani hivi.
Ujinga ni kutojua, na imani ni kujua. Kwa hiyo imani sio ujinga.

Mtu anaweza kuwa mjinga kwa kutojua, na kwa kutojua ndio sababu kuna kasoro mbalimbali.
 
Back
Top Bottom