Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
- Thread starter
- #61
SEHEMU YA 24
Furaha imerejea tena katika maisha ya Genesis, kumrejesha tena Farida halikuwa jambo jepesi. Ni ushindi mkubwa katika maisha yake. Mama yake ameshaamua kwa moyo mmoja kumwacha Genesis arudiane na mpenzi wake akidai kwamba kama mzazi ameamua kuheshimu hisia za mwanaye!
Bianca anaonekana hana furaha kabisa, anajaribu kumpigia mama yake simu na kupanga namna ya kuwasambaratisha tena; Wazo lake linakuwa ni kumuua Farida lakini mama yake anampinga na kumwambia kwamba amwachie mwenyewe atajua cha kufanya.
Upande wa pili tunamwona Farida akiwa na Genesis katika Ufukwe wa Coco, Masaki jijini Dar es Salaam. Farida anaonekana kuwa na jambo zito alilotaka kumwambia mpenzi wake. Baada ya kumzungusha sana, akamwambia kwamba amepata chuo. Genesis anashtuka mno.
Halikuwa jambo rahisi kuaminika kiasi kile. Ghafla Farida akamrukia, wakakumbatiana kwa furaha.
KWA sekunde ishirini walibaki wamekumbatiana kwa furaha huku Farida akishindwa kuzuia machozi yake. Macho yalikuwa chapachapa! Kwake yalikuwa mafanikio makubwa na kama ni kizingiti walikuwa wanaruka cha mwisho!
Aliwafahamu vizuri sana wazazi wa Genesis ambao walipenda elimu kuliko kitu chochote. Kupata nafasi ya chuo, ilikuwa sawa na kumaliza kabisa shahada yake ya kwanza. Aliuamini sana uwezo wake hivyo suala la kusoma lisingekuwa tatizo kwake.
Baadaye waliachiana lakini wakasimama kwa mtindo wa kuangaliana. Genesis akiwa hana la kusema, furaha iliyokuwa ndani ya moyo wake, haikuwa rahisi kuitoa nje kwa maneno.
Hata kama maneno yalikuwepo lakini hakuelewa ni yapi hasa yangeweza kujitosheleza kumwambia mpenzi wake na akaelewa kwamba amempongeza!
Genesis alitulia kama maji yaliyoganda kwenye jokofu akimwangalia Farida ambaye alionekana kuwehuka na furaha aliyokuwa nayo!
“Hongera mama, hongera sana!” Hatimaye Genesis akasema.
“Nashukuru sana baba, ahsante sana mpenzi wangu!”
“Siamini Farida wangu, sasa unakwenda kukata ngebe zote. Hakuna atakayeleta tena kipingamizi. Ni kipi sasa kama tayari umeshapata chuo?”
“Nakwambia nina furaha sana, hebu twende hivi...” Farida akasema akimshika mkono mpenzi wake na kumwongoza kutembea ufukweni.
Nyuso zao zilikuwa zimepambwa na tabasamu pana, walikuwa kama wamezaliwa kwenye ulimwengu mpya wa peke yao.
Ndoto ya muda mrefu ilikuwa imetimia.
“Umepata chuo gani mpenzi wangu?” Genesis akamwuliza.
“Chuo Kikuu Huria cha Arab.”
“Kipo nchi gani?”
“Saudi Arabia.”
“Hongera sana, huko mama lazima muda wote uvae juba na hijabu, najua hutaweza kunisaliti!” Genesis akasema akicheka.
“Hata bila hivyo mpenzi wangu, najua wajibu wangu kwako kwa hiyo hakuna anayenichunga zaidi ya mimi mwenyewe. Niamini mpenzi wangu, mimi sihitaji ulinzi, najilinda mwenyewe!” Farida akasema kwa sauti iliyojaa utulivu.
“Nakutania mpenzi wangu, mimi na wewe tena!”
“Usijali mpenzi wangu, najua hata wewe huwezi kwenda kinyume na mimi!”
“Ni kweli mama, nilisaliti mara moja tu na nilikueleza ukweli lakini hili kamwe haliwezi kutokea tena, nipo makini sana kwa sasa Farida wangu. Siwezi kumruhusu mwanamke mwingine yeyote aujue mwili wangu zaidi yako!”
“Nimefurahi kusikia hivyo.”
“Kozi gani umepata?”
“Sociology!”
“Kozi nzuri sana, utaratibu ukoje lakini? Wamekupa ofa ya nini na nini?”
“Kila kitu mpenzi wangu, ninachotakiwa kufanya ni kuandaa utaratibu wa kupata tiketi tu basi! Nikifika huko kila kitu ni juu yao kuanzia hosteli, malazi, steshenari na mahitaji mengine yote muhimu.”
“Safi sana, hiyo ni bahati ya kipekee.”
“Lakini mpenzi wangu, kuna kitu kinanichanganya kidogo.”
“Nini?”
“Natakiwa kuripoti chuoni baada ya miezi mitatu kutoka sasa!”
“Sasa hapo unapaswa kuchanganyikiwa au kufurahia?”
“Tiketi je?”
“Sasa hilo ndiyo la kukuchanganya? Niachie mimi, nitajua cha kufanya. Kwanza inabidi tusafiri kwenda Zanzibar, tukafanye ‘shopping’ kwanza kabla ya safari yako.”
“Nitafurahi sana mpenzi wangu.”
“Anza kufurahi sasa.”
Siku yao ilikuwa nzuri hakika, Genesis alijiona mwenye bahati sana kuona ndoto zake za kumuoa mwanamke ambaye moyo wake umemthibitisha zikianza kunukia kukamilika. Ilikuwa siku yao ya furaha kupita kiasi.
Jioni Genesis alimrudisha Farida nyumbani kwao Kwa Aziz-Ally. Aliposhuka, aliwasha gari na kugeuza kurudi zake chuoni. Baada ya kuegesha gari lake, akachukua simu na kumpigia baba yake Profesa Mshana.
“Baba huwezi kuamini, ndoto zangu zinakaribia kuwa kweli!” Genesis alianza kusema baada ya baba yake kupokea simu.
“Genesis kwani leo tumesalimia mwanangu?”
“Samahani baba, shikamoo...” akasalimia Genesis.
“Mar-haba mwanangu. Haya sasa niambie hilo ulilotaka kuniambia.”
“Farida amepata chuo baba.”
“Safi sana. Amepata wapi, kozi gani na lini ataanza masomo?” Profesa Mshana akauliza akionekana kufurahishwa sana na taarifa hiyo.
“Amepata Arab Open University, Riyadh, Saudi Arabia, atasoma Sociology!”
“Safi sana, imekuwa vizuri mwanangu maana utaoa mwanamke msomi ambaye hatakuwa mzigo kwako. Unajua Genesis, kama nilivyokuambia mwanzo, ili uwe na familia bora, lazima uwe na mwanamke bora pia. Ninaposema mwanamke bora namaanisha pamoja na elimu.
Kama mwanamke hana elimu ya kutosha, hawezi kuwa bora.
“Ni imani hiyo ndiyo ilinifanya mimi nikamuoa mama yako ambaye ni bora na tukawazaa watoto wetu bora, wenye akili na wasomi. Kwa hiyo nimefurahi sana kusikia habari hizo!”
“Ahsante sana baba, naomba fikisha taarifa hizi hadi kwa mama, simpatii picha jinsi atakavyofurahi!”
“Sawa Genesis, masomo mema.”
“Nawe jioni njema baba.”
“Nashukuru.”
Wakakata simu zao.
***
Ikiwa ni miezi minne tu kabla ya Genesis kumaliza masomo yake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Farida alibakiza miezi miwili kabla ya kuripoti Saudi Arabia katika Chuo Kikuu cha Arab.
Farida na Genesis walikuwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya manunuzi ya mavazi na mahitaji mengine muhimu. Mpaka wakati huo kila kitu kilikuwa tayari, kilichobaki ilikuwa ni kuchukua tiketi ya ndege tu tayari kwa safari ya Saudi Arabia.
Walikaa Zanzibar kwa wiki nzima wakila raha za kila aina. Walifikia katika hoteli nzuri, wakifanya kila kitu isipokuwa ngono! Pamoja na kwamba Genesis alikuwa ameshawahi kufanya mapenzi mara moja na Bianca tangu kuzaliwa kwake, hakutaka kufanya hivyo na Farida.
Alitamani sana kuoa mwanamke ambaye angekuwa mwali kabisa, asiyeguswa na mwanaume yeyote. Kwake ilikuwa fahari kubwa sana kuoa mwanamke aliye bikra. Usiku wa mwisho kabla ya kurejea Dar es Salaam, walijikuta wakitumia muda mwingi sana kunyonyana ndimi, hali iliyoamsha hisia zao za mapenzi.
Mwili wa Genesis ukawaka kama moto wa kifuu. Alijikuta akitamani sana kufanya mapenzi na Farida kwa mara ya kwanza. Msimamo wake aliokuwa nao awali, alijikuta akitaka kuusaliti mwenyewe.
Wakiwa katika zoezi hilo, Farida akitoa mihemo ya ushawishi, Genesis alitaka kuanza kumwingilia Farida.
“Hapana, hapana Genesis, si makubaliano yetu!” Farida alisema akimtoa Genesis pembeni yake.
“Najua mpenzi lakini ukumbuke kwamba hata mimi nina hisia.”
“Sawa lakini si wakati wake Genesis, umesahau makubaliano yetu mara hii?”
“Farida mara moja tu, naomba utibu moyo wangu. Sina hali mpenzi wangu, jaribu kuwa na moyo wa huruma.”
“Sitaweza kuruhusu jambo hili litokee Genesis, nitakuwa nimeidhulumu nafsi yangu lakini pia nitakuwa nimemkosea mama yangu na hata Mungu pia.”
“Kwani hunipendi Farida?”
“Nakupenda mpenzi wangu lakini hatuna ndoa, ni mapema sana kwetu kufanya hivi!”
“Nakuuliza swali na ninaomba unijibu kwa uhakika na usahihi.”
“Uliza.”
“Ni kweli bado unayo bikra yako?”
“Ndiyo mpenzi wangu, ahadi yangu haiwezi kubadilika, hii ni zawadi yako baada ya ndoa. Vumilia mpenzi wangu, najua ni ngumu lakini vumilia!” Farida akasema kwa sauti ya taratibu sana.
“Nakupenda sana Farida, naomba unisamehe kwa hili lililotaka kutokea.”
“Usijali, nimeshakusamehe. Nakupenda pia mpenzi wangu!”
Wakakumbatiana tena, wakavuta shuka na kulala. Penzi lao lilikuwa la dhati.
***
Taratibu zote za safari zikafanyika, kila kitu kilikamilika na hatimaye siku ya safari ikafika. Genesis ndiye aliyempeleka Farida mpaka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na mizigo yake.
Robo saa kabla ya ndege kuruka, Genesis alikuwa anaagana na mpenzi wake Farida, akiwa na majonzi mazito. Alikuwa anakwenda kuanza kipindi kigumu sana cha kuishi mbali na mpenzi wake.
“Farida naumia sana moyoni lakini nenda kasome mama, zingatia kilichokupeleka Saudi Arabia na ujue kwamba Tanzania umemuacha mwanaume anayekupenda sana.”
“Nakuhakikishia hilo mpenzi wangu, hata wewe pia napenda iwe hivyo kwako. Nakupenda sana Genesis, nakwenda kuishi maisha mapya kabisa ya kuwa mbali na wewe. Najua nitaumia sana, lakini nitazoea. Nakupenda sana!” Akasema Farida na kumbusu Genesis katikati ya midomo yake.
Genesis akashuhudia Farida akiondoka na kuingia sehemu maalumu ya abiria wanaosafiri, hakutaka kuondoka mapema uwanjani, alisubiri mpaka ndege iliporuka angani. Bila kujali kama Farida alikuwa anamuona au laa, alipunga hewani akiamini mpenzi wake alikuwa akiona mkono wake.
Ndege ilipoishilia kabisa, akarudi zake kwenye gari na kwenda zake chuoni.
***
Ndege ya Shirika la Ndege ya Emirates iliacha anga na kukanyaga ardhi ya Saudi Arabia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid, jijini Riyadh saa 12:45 za jioni. Abiria walianza kushuka mmoja baada ya mwingine na kupita moja kwa moja hadi kwenye sehemu ya kusubiria mizigo.
Farida alitembea kwa kujiamini, kama vile aliwahi kufika Saudi Arabia lakini ukweli ni kwamba kila kitu kilikuwa kigeni kwake.
Ilikuwa mara ya kwanza kusafiri kwenda nje ya nchi lakini pia ilikuwa mara ya kwanza kupanda ndege! Alikwenda hadi sehemu ya kusubiri mizigo, akaangalia mizigo iliyokuwa ikipita mbele yake, hadi alipoona begi lake na kulichukua! Baada ya hapo akatembea kwa kujiamini akielekea sehemu ya ukaguzi kabla ya kutoka nje.
Aliweka begi lake sehemu ya ukaguzi, akiwa mwenye furaha sana.
Akiwa amesimama, ghafla akashangaa wanaume sita wakiwa wamemzunguka, mikononi mwao wakiwa na bastola. Farida akatoa macho yake kwa mshangao.
“Nini kimetokea?” Farida akauliza kwa mshangao akiangalia begi lake lililokuwa wazi.
“Tulia hivyo hivyo, maelezo mengine utayapata polisi, funga begi lako na ulibebe, kisha tuongozane!” Mmoja wa watu hao alisema.
Farida alipowaangalia vizuri, hakupata tabu kugundua kwamba alikuwa mikononi mwa polisi lakini hakujua sababu ya kukamatwa baada ya mzigo wake kukaguliwa.
Akabaki anatetemeka.
“Chukua begi lako twende!” Mwingine akasema kwa ukali.
FARIDA alikuwa katika taharuki kubwa, ni kweli aliweza kugundua kwamba waliokuwa mbele yake walikuwa ni maaskari, lakini hakujua kosa lake lilikuwa ni nini hadi aamriwe kubeba begi lake na kuongoza kituoni.
“Binti unatuchelewesha, beba begi lako twende!” Askari mmoja akamuamrisha.
“Kwani nina kosa gani?”
“Hujui kosa lako?”
“Ndiyo maana nauliza.”
“Labda tukuulize swali moja jepesi!”
“Ndiyo!”
“Hili begi hapa chini unalitambua?”
“Ndiyo!”
“Ni la nani?”
“Langu.”
“Kweli?”
“Ndiyo ni langu, huoni hata jina limeandikwa Farida Mubaraka, ndiye mimi. Ni langu!”
“Sasa kama ni lako, unatakiwa kulibeba ili tuongozane hadi kituoni, mambo mengine yote utayajua huko huko!”
“Lakini nina haki ya kujua kosa langu!” Farida akasema akitetemeka.
“Paaaa!” Kibao kikali kilitua shavuni mwa Farida.
“Mbona mnanipiga bila sababu?” Farida akauliza, macho yake yakianza kulengwalengwa na machozi.
“Hebu fungua begi lako!” Askari mmoja aliamrisha na Farida akatii kwa kuanza kulifungua.
“Fungua hiyo zipu ya pembeni!” Akasema tena na Farida akatii.
Kitu alichokutana nacho, kilimshtua sana Farida. Alishindwa kuelewa kilifikaje kwenye begi lake, maana hakukijua na wala hakutoka nacho Dar es Salaam.
“Haya beba twende!” Akaamrishwa.
Farida akafungwa pingu na kuongozana na maaskari hao hadi nje, ambapo waliingia kwenye gari lao na safari ya kwenda Makao Makuu ya Polisi, Kitengo cha Upelelezi, jijini Riyadh ikaanza.
***
Ilikuwa ndiyo wiki ya kwanza ya mitihani ya mwisho kabla ya kumaliza chuo, Genesis alikuwa mwenye mawazo sana jioni hiyo. Mpaka muda huo, alikuwa hajapata simu kutoka kwa Farida ambaye walikubaliana atakapofika tu, amjulishe. Moyo wa Genesis haukuwa na amani kabisa. Alichohitaji yeye ni Farida wake kumweleza kama alikuwa amefika salama.
Jambo hilo lilimnyima raha kabisa, akaamua kuingia bwenini mapema sana. Akiwa amejilaza mawazo tele kichwani mwake yakizunguka, rafiki yake Greyson akatokea.
“Mzee vipi mbona unalalalala una hamu ya kudisko nini?”
“Hapana kaka, acha nipumzishe kichwa kidogo!”
“Lakini tupo kwenye mitihani ya mwisho kabisa kaka, kufanya vizuri kwenye test za wiki na assignment hakuwezi kukusaidia, kama utachemka huku mwishoni!”
“Najua Greyson, lakini acha nipumzike, kichwa changu kimejaa sana kaka!”
“Nini tena? Isije kuwa umeshaanza kummisi Farida wakati ni jana tu ameondoka!”
“Pamoja na hilo pia.”
“Lakini hutakiwi kuwaza sana, twende zetu!”
“Wapi?”
“Tukasome!”
“Kaka ng’ombe hawezi kunenepa siku ya mnada, leo sijisikii kusoma kabisa.”
“Sasa?”
“Nini?”
“Umeshakula?”
“Bado.”
“Twende basi tukale, tena leo nina hamu sana na mbuzi choma, twende Udasa Bar, wana nyama ya mbuzi nzuri sana pale!”
“Poa.”
Genesis akajiinua kitandani na kuchukua shati kisha akavaa. Wakatoka na Greyson taratibu wakifuata barabara kuelekea Baa ya Udasa ilipokuwa. Walipofika waliweka oda na kuagiza vinywaji. Sehemu waliyokuwa wamekaa, kulikuwa na runinga mbele yao.
Wakiwa wanaangalia runinga huku wakiendelea na mazungumzo yao, chini ya kioo cha runinga yakapita maneno yaliyosomeka BREAKING NEWS, baadaye maneno mengine yakafuata yaliyoandikwa kwa Lugha ya Kiingereza yakisomeka kwa Kiswahili; ‘Riyadh, Saudi Arabia.
Raia wa Tanzania Farida Mubaraka, amekamatwa na maaskari jijini hapa akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 22, alisema amekuja nchini hapa kwa ajili ya kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Arab. Tutawaletea taarifa zaidi hapo baadaye.’
“Nini?” Genesis alisema kwa sauti akitoa macho.
“Vipi Genesis?” Greyson akamwuliza.
“Ile habari inamuhusu Farida!”
“Farida mpenzi wako?”
“Ndiyo!”
“Si jana tu ameondoka kwenda Saudi Arabia?”
“Ndiyo!”
“Mungu wangu! Unataka kusema kwamba anajihusisha na dawa za kulevya?”
“Kaka kwani hujaona?”
“Yaani sijajua kama huyu mwanamke ana tabia ya kijinga kiasi hiki, halafu anafanya mambo yake kwa siri.”
“Lakini wamesema taarifa kamili itafuata baadaye, kwanini tusisubiri kwanza?”
“Sawa.”
Waliendelea kusubiri, muda wote huku macho yao yakiwa kwenye runinga, kiasi cha dakika ishirini baadaye, Kituo cha ITV walichokuwa wakiangalia, kiliunganisha matangazo yake na Shirika la Utangazaji la CNN, kisha habari na picha zikaonekana!
Genesis alichanganyikiwa, hakuamini kama aliyekuwa akionekana kwenye runinga alikuwa mpenzi wake Farida, lakini ukweli uliendelea kubaki kuwa huo. Aliyeonekana akiwa chini ya ulinzi wa polisi, katika Uwanja wa Ndege wa King Khalid alikuwa ni Farida.
“Si nilikwambia?” Akasema Genesis akiinuka.
“Vipi?”
“Twende hapatufai tena hapa.”
Wote wakainuka na kuanza kutokauelekea bwenini, wakiwa njiani, Genesis akampigia mama yake simu na kumpa taarifa ya tukio zima la Farida.
“Unasemaje?” Mama yake akauliza kwa mshtuko mkubwa.
“Weka ITV mama ujionee mwenyewe.”
“Hebu ngoja niweke!” Akasema mama yake Genesis na kukata simu.
Robo saa baadaye akampigia Genesis. Alikuwa akizungumza kwa sauti ya chini sana, akionesha kusikitishwa na kitendo cha Farida.
“Lakini mwanangu tulikuambia ni vema ukamchunguza kwanza huyo mtu wako kabla ya kuamua chochote, sasa umeona madhara yake. Ungekuja kuoa mwanamke teja!” Akasema mama Genesis.
“Mama sikujua kama Farida ana mambo ya hatari kiasi hicho.”
“Sasa itakuwaje?”
“Itakuwaje vipi tena mama, siwezi kuendelea na teja mimi!”
“Pole sana mwanangu, kwa hiyo unadhani nini cha kufanya?”
“Lazima nizungumze na Bianca tena. Sijui nitaongea nini anielewe maana nilishampa maneno yote mabaya. Lakini mama kuna jambo naomba unisaidie mama yangu!”
“Nini baba, sema kama nitaweza nitafanya hivyo!”
“Naomba unisaidie kumbembeleza Bianca, mimi hawezi kunielewa tena!”
“Unasemaje?”
“Unisaidie kumshawishi Bianca akubali kuwa na mimi, siwezi kuhangaika na teja tena!”
“Huo ndiyo uamuzi wa kiume mwanangu, safi sana. Naahidi kukusaidia!”
“Kweli mama?”
“Nitakusaidia mwanangu!”
Genesis alikata simu akiwa na furaha ya ajabu. Hakuona tena thamani ya Farida, sasa alimtaka Bianca kwa nguvu zote.
Je, nini kitatokea? Ni kweli Farida anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya?