Kifo cha Uaminifu: Madhara ya Kuminya Habari na Mtego wa "Content Creators"

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Mimi ni Mwanahabari na Mtanzania Nasema ...

Kuna huzuni nzito inayotanda ndani ya vyumba vya habari nchini,siyo huzuni ya kukosa vifaa au teknolojia, bali ni huzuni ya kuona taaluma yetu ikigeuzwa kuwa "kipaza sauti" cha upande mmoja, huku misingi ya uhuru wa kutoa maoni na kuchambua ukweli ikimomonyoka.

Ninaiandika makala hii kwa uchungu, lakini pia kama onyo kwa wale wote wanaoamini kuwa kuminya habari ndiyo njia ya "kulinda amani" au "kujenga taswira nzuri ya nchi."

1. Kifo cha Uaminifu ni madhara kwa Serikali na Mashirika​

Jambo ambalo watawala wengi nafikiri hawataki kulielewi ni hili: Ukiharibu kioo ili kisikuonyeshe makovu yako, huujibu ukweli kuwa una makovu,tunapoviminya vyombo vya habari visitoe habari kwa uhuru na weledi, tunaua uaminifu (trust) kati ya chombo cha habari na mwananchi.

Madai ya "kuharibu picha ya nchi" yametumika kuminya uhuru, lakini matokeo yake ni mabaya zaidi. Ikiwa wananchi hawaviamini vyombo vyao vya ndani kwasababu vimekuwa vya upande mmoja, siku ambayo serikali au mashirika ya ndani yatakuwa na jambo la msingi na la dharura la kuwafikishia wananchi, hakuna atakayewaamini. Tutakuwa na taifa linaloishi kwa "tetesi" za mitaani au mitandaoni badala ya habari rasmi.

2. Mtego wa "Content Creators": Njia siyo Uhuru​

Hivi karibuni tumeshuhudia nguvu kubwa ikielekezwa kwa Content Creators na Influencers. Wanapewa mafunzo, watapewa rasilimali, ili kuonekana kama mbadala wa wanahabari wa kitaaluma? Huu ni mtego.

Mkakati huu unalenga kupata njia za kusambaza habari (Distribution Channels) badala ya kuimarisha uhuru wa habari. Content Creator anayetengenezwa na mfumo hawezi kuwa mbadala wa mwanahabari anayehoji na kuchunguza, ikiwa hata hawa wataanza kukatwa ndimi zao kwa sababu lazima mtafanya hivyo pale wanapotoa maoni tofauti, tunawafanya nao wasiaminike. Nafikiri uhuru wa habari siyo kusema "TUNAUHURU" jukwaani, bali ni kuruhusu fikra tofauti zisikike bila hofu ya kunyang'anywa simu, kukamatwa, au kutishwa.

3. Tujifunzeni kwa Wenzetu: Mfano wa Marekani na VOA​

Tazama kile kilichotokea Marekani baada ya kurejea kwa Donald Trump mwezi Januari 2025. Moja ya hatua za kwanza ilikuwa ni kujaribu kuvidhibiti vyombo kama Voice of America (VOA) akidai vina mrengo wa kushoto na havina maslahi kwake. Lakini hivi karibuni, VOA wameshinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kuendelea na kazi yao kwa uhuru.
Hii inatupa somo kubwa: Nguvu ya kiongozi kisheria isiwe rungu la kuua uhuru wa kitaaluma. Kule, hata Content Creators wanaopinga msimamo wa nchi yao kuhusu vita au diplomasia wanaachwa watoe maoni yao kwa maslahi ya taifa lao. Hapa namaanisha kuwa "Uhuru wa kufikiri tofauti ndiyo unajenga taifa imara", na siyo kulazimisha kila mtu aimbe wimbo mmoja.

4. Giza la Miaka 10: Taifa la Hovyo Linatengenezwa Sasa​

Tusidanganyike na utulivu wa sasa,Yale yaliyotokea kwenye Uchaguzi uliopita na namna vyombo vya habari vilivyolazimishwa kuwa "vibaraka" yameua uaminifu wetu kwa jamii.

Tukichambua mataifa yenye uhuru halisi wa habari, utaona uhusiano wa moja kwa moja na ukuaji wa uchumi na maadili. Pasipo na uhuru wa kukosoa, ufisadi unastawi, uzembe unatamalaki, na viongozi wanajisahau kama tulivyo binadamu wote kujusahau kupo, Tukiendelea hivi, baada ya miaka 10, tutakuwa na taifa la watu wasiojua ukweli, wasio na uwezo wa kuhoji, na uchumi uliosinzia kwasababu hakuna "mwangaza" wa habari za uchunguzi.

Hitimisho: Uhuru siyo Msaada, ni Haki​

Uhuru wa habari siyo zawadi kutoka kwa mwanasiasa kwamba Leo huyu ameingia anaminya kesho mwingine anaachilia... Ni hitaji la lazima kwa maendeleo ya taifa.

Content creator hawezi kuwa suluhu ya kuminywa kwa uhuru wa habari. Tunapitia kipindi kigumu, na ni wakati wa kusema: Inatosha. Acheni wanahabari tufanye kazi, acheni wachambuzi watoe maoni yao, na acheni wananchi waone picha halisi ya nchi yao ili washiriki kuirekebisha,msipotoa nafasi hii binadamu tulivyo tutatafuta njia ya kuyasambaza kwenye vyombo vya nje huko!!
Nimalize kwa kusema :-
"Bila uhuru wa habari, tunajenga nyumba kwenye mchanga, Mvua ikija, tutabaki na nchi ya hovyo kuliko tunavyoweza kuwaza sasa".
 

Attachments

  • images (1).jpeg
    66.7 KB · Views: 2
Naunga mkono hoja.

Uhuru wa habari sio hisani ila haki ya msingi kwa raia, japo Waandishi wetu wa habari kwa Sasa wengi wenu ni 'Pro-Establishment'..
 
me najiuliza mara kwa mara, huu ujinga hapa nchini ulipataje kukua kiasi hiki na wakati watu wenye uelewa na waliobobea walikuwepo?
au wazee wetu hapo nyuma na hapa kati walijisahau sana
 
Madhara ya nchi kuongozwa na wajinga
 
Wanahabari wenyewe wanakimbilia teuzi na kugombea nafasi za kisiasa kwa chama tawala.
 
me najiuliza mara kwa mara, huu ujinga hapa nchini ulipataje kukua kiasi hiki na wakati watu wenye uelewa na waliobobea walikuwepo?
au wazee wetu hapo nyuma na hapa kati walijisahau sana
Nachofikiria binafsi si mkongwe lakini kabla ya magufuli angalau kulikuwa na uwezo wa vyombo vya habari na wanahabari kuandika habari ila baada ya magufuli kwanzia miaka ya 2017 🙌🙌mambo yakaanza kuwa magumu kwa vyombo na wanahabari kulitokea kundi la watu wa kusema maagizo kutoka huko juu
 
Wanahabari wenyewe wanakimbilia teuzi na kugombea nafasi za kisiasa kwa chama tawala.
Baadhi na si wanahabari tu kila sekta ipo hivyo na inakuja baada ya kuwa na ulafi kila mmoja anaamini akishaingia kwenye kinachoitwa System baasi ashamaliza badala ya kutumika anaenda kutumikiwa
 
Tanzania hatuna critiko thinker katika media Kuna ushuzi TU hacha ubinywe
Wapo wengi tu tatizo na kuachiwa kufikiria ,,wangapi wameuwawa na wanaendelea kuuwawa baada ya kufikiria na kutoa maoni tofauti na watawala ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…