Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NANE: “dah! kwanini sasa mjomba wako hataki nikuoe?” nilimuuliza Jessenia, tukiwa bado ndani ya gari, lakini nimesha zima, “atajuwa yeye mwenyewe, mimi nachoomba nishike mimba au unibebe tuondoke kwenda dar” alisema Jessenia na kunifanya nitabasamulie moyoni, maana niliona kuwa Jessenia hakuwa anaelewa anacho kisema, wala kukiwaza…….. ENDELEA..
Lakini wakati tunaendelea na maongezi ghafla nikamuona Jessenia anashtuka na kulitazama gari lililokuwa pembeni yetu, “mh! Eric hilo ni gari la mjomba, nadhani atakuwepo hapa” alisema Jessenia kwa sauti iliyojaa uoga na wasi wasi, “lakini bado hajakuona sio?” nilimuuliza Jessenia huku nikijaribu kulitazama gari lile lenye vioo vya giza kama lile tulilokuwa tume panda sisi, hebu nenda kamuone huyo mtu wako tuondoke hapa pahala sio pazuri” alisisitiza Jessenia kwa sauti iliyojaa wasi wasi, nikamtazama Jessenia ambae bado alikuwa anazungusha kichwa kulitazama eneo lile la mbele la kituo kikuu cha mkoa wa kipolisi cha Chake chake, ambalo lilikuwa na watu wengi kiasi wakiwemo waliovalia sale za kipolisi, na watu wengine waliovalia nguo nadhifu za kiraia, ambao kutokana na unyoaji wao usinge hangaika kuwatambua kuwa ni polisi, wapo pia katika kundi lile la uvaaji wa kiraia, walio valia mavazi ya raia wa kawaida, kama ilivyo kawaida ya watu wa kiasiwa hiki, kwa wanawake ni vazi la baibui au gauni refu bila kusahau hijabu, hakika walipendeza kwa kweli, lakini hawakuweza kumfikia Jessenia, ambae ungesema anaenda kufunga ndoa, na kwa upende wa wanaume kama kawaida ya watu wa pemba, wao walivalia mavazi rahisi, ungeona suruali nzuri safi ya kitambaa au ya jinsi na tishert au shati la vishikizo, ambalo ni kama waliambizana kuwa wasichomekee, yani kuvaa mkanda nje kama walivyosemaga vijana wa zamani, ukiachia uvaaji huo wapo wengine waliovalia kanzu nzuri, iwe nyeupe nyeusi au ya kijivu, na kofia ya kibandiko, (baraghashia).
Wapo waliokuwa wapo pale nje wakiongea na wenzao au askari polisi, wapo waliokuwa wanaingia ndani ya jengo lile kubwa la kituo kikuu cha polisi Chake chake, wakipishana na wengine waliokuwa wanatoka na kuondoka zao, nilimtazama Jessenia, ambae ni kama alijuwa nitamtazama, maana na yeye alinitazama na macho yetu yaka kutana, ukweli Jessenia kama angekuwa tunda la mtini, basi asingeuzwa gengeni, lingeuzwa kwenye maduka makubwa ya kisasa yenye hadhi ya super Market, na hakika kama ungebahatika kulinunua usinge hangaika kusubiri ufike nyumbani ndipo ulile, ungelila njiani tena bila kuosha au kulimenya.
Nilimtazama kwa sekunde kadhaa, huku nikijikuta naachia tabasamu laini, na hapo nikamuona Jessenia nae anaachia tabasamu laini, lakini lililojaa aibu, “Jesse sito tenda vyema kama sito kuambia kuwa, wewe ni mwanamke ambae ni mzuri mpaka najionea wivu mimi mwenyewe” nilisema hivyo nikimaanisha utani, lakini Jessenia alipokea kwa namna tofauti na mimi nilivyo maanisha, kwanza nilimuona akikwepesha macho yake huku anaachia tabasamu laini na tamu, ikifuatia na kicheko chepesi cha raha, “hakika Eric, hujui kilichopo moyoni mwangu, lakini kwangu, wewe ni zaidi ya kila kitu nilichowahi kukipenda, natamani kila kitu kiende haraka niweze kusimama na kutangaza kuwa wewe ni mume wangu” alisema Jessenia kwasauti tamu nyororo ya chini, ambayo ili usisimua moyo wangu, nilikoma kuigiza nikaamua nifanye kweli.
Kwanza nikamshika shavu lake la kushoto, kwa mkono wangu wa kulia, nakufanya kama nainua uso wake, na kumfanya anitazame nae akafanya hivyo, na mimi nikaanza kuusogeza uso wangu taratibu kwenye uso wake, nadhani mwanzo hakuelewa nataka nifanye nini, ila nilipomsogezea uso wangu, huku vitu vyote vya usoni vikilengana, yaani macho kwa macho pua kwa pua mdomo kwa mdomo, nikamuona analegeza macho na mdomo, na baadae kufumba macho kabisa, huku midomo yetu ikigusana na bila kumueleza chochote, nikamuona akidaka lips zangu za chini na kuanza kunyonya, huku tukibadilishana niliponyonya za kwake za juu yeye alinyonya za chini, niliponyonya za chini yeye alinyonya za juu, na tukajikuta tukianza kunyonya ndimi zetu, huku Jessenia akionekana kunogewa zaidi, pale alipo zungusha mikono yake mabegani mwangu na kunivutia kwake na kuzidi kuni ng’ang’ania, akionyesha kutokuniacha wala kuacha ule mchezo, mpaka nilipopunguza kasi ya ule mchezo wa makinda ya njiwa na mama njiwa, “ni nzuri Eric, kumbe …… kumbe inakuwaga hivi” alisema Jessenia, ambae alionekana kuvutiwa na ule mchezo, “kwanini kumbe, ina maana hukuwahi kufanya hivi?” nilimuuliza Jessenia kama kumtega hivi, nae akacheka kwa aibu, huku anaitikia kwa kichwa, na nikacheka kidogo huku najiweka sawa tayari kwa kushuka, “unajuwa Jesse, kwa uzuri ulionao na jinsi ulivyoweza kuwa mpaka sasa, ni kama maajabu ya kumi na moja ya dunia” nilisema kwa utani, huku napapasa kwenye kiuno changu, kuona kama AGP yangu, ipo sehemu hiyo, nikaikuta, “nashukuru mwalimu wangu ndie mume wangu” alisema Jessenia tukamaliza kwa kicheko cha pamoja, kisha nikashuka toka kwenye gari na kuanza kutembea kuelekea lilipo lile jengo la polisi.
Nilitembea kwa haraka, huku nikipishana na watu waliokuwepo eneo lile, kichwani kwangu nilikuwa nawaza na kumtafakari Jessenia, ambae nilikuwa nimeshaipata historia yake yote ambayo hata yeye mwenyewe hakuwa anaifahamu, mschana ambae kiukweli alikuwa anaonyesha kunipenda kweli kweli na kuvurugwa na penzi letu jipya, kiasi cha kuto kusikia amri ya mjomba wake kwamba asitoke ndani mwao, nilipo waza hayo nikajikuta nageuka kutazama kule kwenye maegesho, lakini sikuona dalili ya mtu ndani ya gari, nilishangaa kidogo maana sikujuwa Jessenia ameenda wapi, “au amelaza kiti?” nilijiuliza huku nageuka kutazama mbele, ambako nusu nimvae mzee mmoja wa makamo, aliekuwa amevalia kanzu nzuri nyeupe, mwenye na barangashia nyeupe pia, vyote vikiwa vime haririwa kwa nyuzi za rangi ya dhahabu, kosa polisi aliekuwa ameogozana nae kuwahi kunidaka na kunizuia, basi ningekuwa nimeshamvaa mzee huyu, “samahani sana jamani samahani sana” nilisema huku nawatazama kwa awamu, nikianza na yule polisi, ambae alikuwa na nyota mbili mabegani mwake, ambae umri wake ni kati ya miaka 38 mpaka 40, kwa mkadirio, “angalia unakokwenda kijana, unapamia pamia watu kama mlevi, jiangalie wewe, unaweza kulala lupango sasa hivi” alisema yule mzee alieongozana na huyu polisi mwenye nyota mbili, ambae nilipo mtazama usoni, sikuhitaji hata dakika mbili kumtambua, kuwa huyu ni baba yake Ussi, yaani mzee Juma Mohamed, mjomba wake Jessenia.
Mapigo yangu ya moyo yalishtuka kidogo, sio kwa kutishiwa kuwekwa lupango, ila kumuona mzee Juma Mohamed, yaani nilihisi kama amenifumania hivi, “samahani sana mheshimiwa, niwieradhi kijana wako” nilisema hivyo, kwa sauti iliyojaa nidhamu, huku moyoni nikijiuliza kuwa, huyu mzee angefanya nini, endapo angegundua kuwa mimi ndie nilieshinda na Jessenia ile jana, “kijana jaribu kuwa mwangalifu unapotembea, haya potea haraka” alisema yule polisi, mwenye nyota mbili, na hapo nika toa ishara ya kushukuru kwa kukusanya viganja vya mikono yangu usawa wa kifua, huku nainamisha kichwa changu, kisha nikaondoka zangu huku yule mzee akinisindikiza kwa macho yaliyojaa hasira, nadhani ni kwaajili ya ugomvi wake na Jessenia, sasa niliomba asije akamuona ndani ya gari.
Nilitembea huku nikigeuka mara kwa mara kuangalia kama mzee yule aliekuwa anaagana na yule polisi angeenda kwenye gari lake na kugundua kama Jessenia yupo ndani ya gari letu, mpaka nafika kwenye lango la kuingilia ndani, bado mzee Mohamed Juma alikuwa hajalifikia gari lake, japo sasa walishaachana na yule polisi, ambae alikuwa anarudi huku niliko kuwepo mimi, nikasimama pale langoni kusubiri kuona kitakacho tokea, “hallo mbona washangaa hapo unashida gani?” nilishatushwa na sauti ya kiume, iliyosikika kwa ukaribu nyuma yangu, nikageuka huku natabasamu, nikijaribu kujiweka katika hali fulani ya kuto kutiliwa mashaka, nikakutana na polisi mmoja mwenye cheo cha koplo, ambae umri wake nae ulikuwa umeenda kidogo, ukiongeza mustache mrefu juu ya mdomo wake, alizidi kuonekana mtu mzima “yah! ninashida ya kumwona insp Aroub” nilisema kwa sauti ya uchangamfu huku najichekesha kidogo, “hooo! hivyo unamsubiri hapa” alisema yule koplo wa polisi, huku anatazama kule nje nilikotoka, na mimi nikatazama kule kule, nikamuona yule koplo akimtazama yule polisi mwenye nyota mbili, ambae sasa alikuwa amesha karibia pale tulipokuwepo, hapo kengere ya tahadhari ikagonga kichwani mwangu, maana niliona dalili ya jambo fulani, “afande Aroub, una mgeni wako hapa, naona anashangaa shangaa tu!” alisema yule Koplo, huku anamtazama yule polisi mwenye nyota mbili, na hapo ndipo nilipo kumbuka kuwa cheo cha polisi yule ni inspector, na huyu polisi nilie toka kukutana nae pale nje akiwa na mzee Mohamed, alikuwa ndie insp Aroub, hapo nilihisi kupatwa na mgagasiko, maana nilianza kuhisi kuwa insp Aroub, anaweza kuwa anafahamu jambo kuhusu mauwaji yanayoendelea, nilihisi hivyo mara baada ya kumuona akiongea na mzee Juma Mohamed, “hoooo! kumbe zile haraka zote ulikuwa unakuja kwangu, sasa mbona ulinipita kama hunijuwi?” aliuliza insp Aroub, huku ananitazama kama mtu anaejaribu kufanya utambuzi usoni kwangu, nadhani alitaka kuona kama ananifahamu au laa, “unajuwa sikuwahi kukuona mwanzo, lakini tulipo pishana pale nikahisi kuwa utakuwa wewe, ndio maana nikasema kwanza nikusubiri hapa ili nikuulize” nilizuga hivyo huku natupa macho kiujanja kwenye maegesho, ambako niliweza kuona gari la mzee Juma Mohamed linaondoka zake kutoka pale maegesho, “ok! umenipata kijana vipi una ujumbe wangu, una jambo umekuja kulitolea taarifa?” aliuliza insp Aroub, tukiwa tumesimama pele pale mlangoni, ukweli imani yangu kwake ilisha pungua kwa kiasi fulani, hata lile lengo la kushirikiana nae nililiona halifai, japo nilisha panga kushirikiana nae bila yeye kujuwa mimi ni nani, na nina fanya nini, “mzee mimi naitwa Eric Frank, ni mwalimu wa taaluma, lakini nimekuja hapa kwaajili ya kuomba msaada na ushauri na pengine maono juu ya kitabu ambacho ninakiandika kuhusu maisha ya binadamu, na viumbe vinavyoitwa majini” nilimueleza insp Aroub, huku nikijaribu kusoma uso wake, kwamba atalipokea ombi langu au laa….….. ITAENDELEA
 
Weka namba tukuwezeshe abuu
 
Abou Shaymaa ukimuona kaka angu uko Single The Loner naomba uniambie,jana hajarudi nyumbani kwa sababu shemeji yake Daudi1 akisaidiana na jirani Mopak walimsema sana..
Sister mi sio wa kuzira, kwani huyo mumeo siku amekuja kuoa si aliambiwa una ndugu wewe!! na ndugu ndo sisi, hapo kwake sihami na ugali wake nitaubonda sana.
 
Ungetulia na kuwasikiliza wasomaji wako tunge endelea kukuchangia:
Ila ilivyo geuka na kujifanya keki ya sambusa baadhi yetu tumekudharau sana:
Sisi hatuishi kwa hadithi zako za kutunga:
Ila wewe ungeweza kabisa kuishi kwa sisi wasomaji wako kupenda kazi zako:
Hii ndio inayofanya mwafrika mweusi awe masikini:
Ni kwamba akipata followers kiduchu tu wa kumwongezea mtaji, anageuka kuwa Bosi:

Siku nyingine weka episode moja tu kwa siku na uitishe michango:

Na sisi tusio na majukumu ya kutumwa tungekuchangia tu maana tunahitaji simulizi za kututoa upweke hasa hasa usiku

Elewa hivyo Pimbi wewe:
Abou Shaymaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom