KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TISA : hata lile lengo la kushirikiana nae nililiona halifai, japo nilisha panga kushirikiana nae bila yeye kujuwa mimi ni nani, na nina fanya nini, “mzee mimi naitwa Eric Frank, ni mwalimu wa taaluma, lakini nimekuja hapa kwaajili ya kuomba msaada na ushauri pengine maono juu ya kitabu ambacho ninakiandika kuhusu maisha ya binadamu, na viumbe vinavyoitwa majini” nilimueleza insp Aroub, huku nikijaribu kusoma uso wake kwamba atalipokea ombi langu au laa….….ENDELEA….
Ukweli insp haroub alishtuka kidogo, baada ya kusikia hoja yangu na kunitazama kwa mshangao, nilihisi mambo mawili, moja ni kwamba pengine jambo alilotoka kuongea na mzee Mohamed linahusiana na kifo cha jana cha yule mfuasi wa Ussi, au anafahamu jambo kuhusu mchezo unao chezwa na muuwaji anae singizia jini, “kijana unadhani umekuja sehemu sahihi kuomba huo msaada?, mimi kazi yangu ni polisi, sasa nahusiana vipi na majini?” aliuliza insp Aroub, huku ananitazama kwa macho fulani yaliyo jaribu kuchangamka toka kwenye mshangao, huku macho yake yakiwa kama yananikagua hivi, wakati huo yule polisi koplo alikuwa anaondoka zake na kutuacha sisi wawili pale langoni.
Hapo nikaona kuna uwezekano wa kukosa kile nilichokitaka, hivyo nikatakiwa kujiongeza, kwanza nilianza kwa kucheka kidogo, “mzee nyie polisi mnakumbana na mengi, pia alieniambia nije nikuone sidhani kama alikosea, niwazi anautambua uwezo wako mkubwa wakupambana na kesi zinazo husu vitu kama hivi” nilimueleza bwana Aroub, huku nikijichekesha kidogo, hapo insp alitulia kidogo kama vile anawaza jambo, kisha akainua uso wake na kunitazama huku anatabasamu, “bwanaaaa nani vile?” aliuliza insp Arob, kama vile amekubari kunisikiliza, na mimi nikamjibu kwa haraka, “Eric, naitwa Eric Frank” nilimjibu na kutega sikio kusubiri kusikia anachotaka kusema, “ok! Hebu nifuate, na ninakupa dakika tano tu, maana kuna report nahitaji kuikamilisha haraka sana itumwe dar es salaam” alisema insp Aroub, huku anaogoza kuelekea upande wa maegesho ya magari.
Naam!!! baada ya kutembea hatua kadhaa, insp akaanzisha maongezi, “haya bwana Eric, hebu niambie, unatokea kampuni gani na unaulizia majini kwa maana ipi?” aliuliza insp Aroub, huku tukitembea taratibu kuelekea upande ule ule wa maegesho ya magari usawa wa lile Toyota spacio tulilokuja nalo.
Ukweli sikutaka tulisogelee, kwa sababu sikutaka Jessenia asikie ninachoongea na insp huyu mtu mzima, ambae lengo langu ni kushirikiana nae bila yeye kujuwa kuwa na mimi mpelelezi, “labda nianze kujitambulisha tena, naitwa Eric, toka Mbogo Publishers iliyopo dar es salaam” nilisema hivyo huku natoa kitambulisho fake, ambacho tunatumia dar es salaam, maana kampuni yetu ya upelelezi ni ya siri, japo inatambuliwa na serikali akakichukuwa na kukitazama, alitumia muda mfupi sana kukitazama, “mnajihusisha na nini?” aliuliza insp Aroub huku ananirudishia kitambulisho changu, “tuna jihusisha na uuzaji wa vifaa vya maofisini na uchapishaji wa makala na vitabu, pia mimi nina degree ya mipangilio za Tarakishi (computer softwere/program) na sasa nipo hapa Pemba, nime ajiliwa kwa muda kufundisha computer hapo shule ya sekondali ya Fider Castor, mwalimu wa computer” hapo Arobu akanitazama kama vile ananifananisha na maneno ninayosema, “hoooo! kumbe upo vizuri eeh, sasa wewe umesomea computer zipi, yale makubwa au zile ndogo?” aliuliza mzee huyu, ambae niligundua kuwa uelewa wake juu ya computer ni mdogo sana, “mzee unapozungumzia computer, ziwe tarakilishi za mezani na zile mpakato au za mnara, zote zina mifumo ya kufanana tofauti maumbile na matoleo, pia uwezo kupokea mipangilio (program), uhifadhi pia na uzalishaji” nilifafanua na hapo nikamuona tena Aroub ananitazama kwa namna ile ile ya kunikagua, “ok! sasa kwanini msomi kama wewe unaanza kuulizia habari za majini?” insp Aroub aliniuliza swali ambalo nilikuwa nalitamani sana, kwanza tulicheka kwa pamoja, kabla sijamfafanulia, “ni kwamba mzee wakati nikiwa namaliza kidato cha sita, nilikuwa nimeshaanza kuandika kitabu changu kinachoitwa Maisha unapande wa giza, nikijaribu kuandika kuhusu viumbe ambavyo kuna baadhi ya watu wanatoa ushuhuda kuwa wamekutana navyo, na baadhi wanaisi, kuwa ni mambo ya kufukilika, asa kuhusu viumbe vinavyoitwa jinni” nilimueleza insp Arob, ambae sasa alionekana kuanza kuniamini, maana alikubaliana na mimi kwa kichwa, huku ananitazama tena, “ok! sasa kwangu unataka nini maana mimi sio mganga wala mtabiri?” aliuliza insp Aroub, huku tuna ingia kwenye eneo la maegesho na bahati nzuri ni kwamba tulililenga gari moja la polisi ambalo lilionekana halija tembea muda mrefu kidogo, ni kutokana na nyasi chache kwenye matairi yake, “ni kwamba mzee, ujuwe hii project niliisimamisha kwa muda mrefu sana, maana nilikosa dondoo muhimu kuhusu viumbe hivyo, lakini nilipofika hapa pemba nikasikia matukio mawili yanayohusishwa na jini, moja lilitokea week kama mbili zilizopita, na moja nimesikia leo asubuhi, nilipoulizia namna ya kupata hizi habari nikaambiwa nikuone wewe kwa sababu wewe ndie unae chunguza kuhusu vifo hivyo” nilimaliza ufafanuzi na kumuachia Aroub aamue kama kuninyima ushirikiano au kunieleza anacho kijuwa ambacho ndio kitu cha kwanza nilicho kitaka kwa mzee huyu ili niweze kumsoma anachoelewa juu ya matukio haya ya kupangwa na mtu wa kawaida, au kama anafahamu juu ya kinacho endelea.
Insp Aroub, alitulia kidogo kama anawaza jambo fulani, kisha akainua uso wake, “kijana kwanza hongera sana kwa hiyo makala ambayo umeibuni, maana itatoa elimu nzuri sana kwa kizazi cha sasa, ila nikuambie kitu kimoja, ungekuwa umenijulisha ujio wako ungekuwa umefanya jambo zuri sana, maana kwa sasa nitakueleza kwa kifupi, ila ukipata nafasi utakuja tena kupata mengine zaidi, ila kwa sasa wacha nikueleze kwa kfupi” alisema insp Aroub, akionyesha wazi kuniunga mkono katika kuandaa hiyo makala fake.
Mzee Aroub akaendelea kunieleza huku akisimulia mambo mengi niliyosimuliwa, yaani ambayo nilisha yasikia na kuyafanyia uchunguzi, “ukweli kijana haya mambo ni mapana sana, aliekueleza kwamba uje kwangu hakukosea, maana ni mwaka wa tano sasa na chunguza kesi hii ambayo bado sijaipatia ufumbuzi, kuna kiumbe kinachosadikiwa kuwa ni jini, kina fanya mauwaji mara kwa mara tena kwa wanaume tu, mwanzo tulidhania vijana wawili wanafunzi walikufa kwa kuumwa na nyoka, lakini vipimo vilikataa kabisa, hata tulipopeleka sampuli dar es salaam, nao walikosa majibu ya chanzo cha vifo vile, lakini kwa upande wa wazee na wenye elimu ya majini wakasema kuwa vifo kama hivyo hutokea sana kwa watu wanao uliwa na majini ya bahari” alieleza insp Aroub, huku nikijitahidi kumchunguza kama anaficha jambo au anasema anacho kijuwa, “lakini hapa karibu mashuhuda wanasema kuwa marehemu kama wawili hivi waliokutwa na janga hilo la jini, walionekana wakiongozana na mwanamke anae shabihiana, kwa maana maelezo yana mlenga mwanamke mmoja mrefu mwenye umbo la kuvutia, anaevaa baibui na niqab nyie watu wa bara munaita ninja, muda mfupi kabla hawaja uwawa” alisema insp Aroub, na hapo nikamuwahi, “lakini mzee, unadhani huyo mwanamke ndie jini mweyewe?” nilimuuliza insp, ambae alishusha pumzi ndefu, kama vile alichotaka kunieleza hata yeye hajakiafiki, “ndivyo tunavyo amini, maana hatuna viwezeshi kama tungekuwa na vifaa kama ulaya, nadhani tungeweza kulinasa hata tukio la jana usiku, ambapo huyu kijana ameuwawa hadharani kabisa” alisema mzee Aroub, na hapo nilitamani kuamini kuwa haegemei upande wowote, lakini hapo hapo nikakumbuka kuwa muda mfupi uliopita alikuwa na mzee Juma Mohamed, mtu ambae nashuku kuwa anahusika juu ya kila kitu kinachoendelea, “samahani mzee, hivi huyo jamaa alie uwawa naweza kukutana na ndugu zake, pengine anaweza kupatikana mmoja ambae alimuona akiwa na mwanamke au hilo jini” nilimuuliza insp kama mtego, maana nilijuwa fika kuwa lazima mzee Juma alikuja kumuona insp kuhusu kifo cha kijana wa Ussi.
Hapo insp Aroub nikawa kama nime mkumbusha jambo, “huyo kijana ni mgeni hapa Pemba, aliajiriwa na mtoto wa mzee mmoja hivi kama ulimuona niliongozana nae wakati ule ulitaka kumsukuma, ndiyo nilimuita nimueleze hilo jambo, na yeye ndio kwanza anasikia hizo taarifa, hivyo anaenda kufanya utaratibu kama ni kuachia hospital izike au laa, maana amesema kuwapata ndugu zake itakuwa ngumu” alisema insp Aroub, na hapo nikagundua kuwa, insp hakuwa anaelewa chochote juu ya mchezo unao endelea, “hooo! yule mzee niliwahi kumuona mara moja, kwenye msiba wa Vuai hapo msingini” nilimuambia insp Aroub nikijaribu kumleta kwenye ushawishi wa kujiweka wazi kama ni mshirika au la, maana kushiriki sio lazima awe muuwaji, ila akijuwa na kuficha nako ni kuhusika pia, “yah! na yeye anaishi pale msingini, na hao ni vijana wake wa pale mtaani umri wa Vuai ni kama wa kijana wake Ussi” alisema insp Arobu, na hapo nikamchomekea swali tangulizi kabla sijaenda kwenye swali husika, “samahani mzee kwa usumbufu ila naona maswali yanazidi kunijia kichwani, hivi unadhani huyo jini anauwa kwa sababu gani, maana katika dodosa yangu, ni kwamba jini huwa hauwi bila sababu, na kama angekuwa jini korofi basi mimi na wewe pia tunge kuwa hatarini” nilimuuliza mzee Aroub, ikiwa ni njia ya kutambua kama anafahamu ukweli au la, “mh! ukweli ilo ndilo linalotushangaza hata sisi, maana tumewahi kusikia visa vingi vya majini, kama vile popo bawa, jini Chongo, na mengine, huwa yanatokea kwa sababu fulani na kuuwawa watu linalowahitaji kama huyu anavyo fanya, lakini mpaka sasa hatuja pata sababu au kitu ambacho kilitokea na kumnkasirisha” alisema insp Aroub, ambae bado niliona kuwa hakua na muelekeo wa kuwa anatambua ukweli wa jambo hili, hapo nikacheka kidogo, kiasi cha yeye kunitazama kwa macho ya kuuliza, lakini kabla hajauliza lolote nikamuwahi, “samahani mzee unajuwa hili jambo kwa sisi ambao hatuja kumbana na jini huwa tunaona kama hadithi za mbogo edgar, ila mlijaribu kuweka mtego wowote au kuwashuku watu fulani fulania kuhusika na matukio haya?” nilimuuliza mzee Aroub ambae alitabasamu kidogo……… ENDELEA.
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI : alisema insp Aroub, ambae bado niliona kuwa hakua na muelekeo wa kuwa anatambua ukweli wa jambo hili, hapo nikacheka kidogo, kiasi cha yeye kunitazama kwa macho ya kuuliza, lakini kabla hajauliza lolote nikamuwahi, “samahani mzee unajuwa hili jambo kwa sisi ambao hatuja kumbana na jini huwa tunaona kama hadithi za mbogo edgar, ila mlijaribu kuweka mtego wowote au kuwashuku watu fulani fulania kuhusika na matukio haya?” nilimuuliza mzee Aroub ambae alitabasamu kidogo……… ENDELEA……
Ni kama vile aliniona ninazungumza kitu ambacho yeye alisha kifanya, “unajuwa nilikuwa na mawazo kama ya kwako, kwamba kuna mtu anafanya matukio haya halafu anasingizia jini, lakini hatukufanikiwa kupata mshukiwa, na juzi kwenye tukio la kifo cha Vuai, nilipigiwa na watu wa jirani wa Vuai, kuwa ile nyumba ina security, kama tunaweza kuzikagua na kuona jinsi tukio lilivyo kuwa, na kwamba tuangalie kama kweli muuwaji ni jini au binadamu anae uwa kwa mtindo wa kipekee unao fanana na mauwaji ya jini, lakini bahati mbaya tulikuta mfumo wote wa camera ulikuwa mbovu” alijibu insp Aroub, na hapo nilimshangaa kimoyo moyo, “kwanini unasema mfumo ulikuwa mbovu” nilimuuliza insp Aroub kwa sauti tulivu, sikutaka aone mshangao wangu, “yah! tuliona kwa macho Vifaa vilikuwa vimeharibika haikuhitaji kuangalia mara mbili ili kuona” alisema insp, na hapo nilishindwa kuvumilia, “samahani mzee ilikuwa ni mibovu au iliharibiwa” swali langu lilimfanya insp Aroub anitazame kwa macho ya kunikagua, lakini safari hii hakukaa kimya, “kijana wewe ni mwalimu au mpelelezi?” aliuliza insp Aroub, ambae kiukweli, alinishtua na kunifanya nihisi kuwa ninaenda kuumbuka muda mfupu ujao.
Hapo nikajichekesha kibwege, huku nawaza ni mjibu nini ili kumuondoa kwenye hisia zake, lakini wakati nawaza nimjibu nini, insp Aroub akaniwahi “maana una maswali ya kipelelezi, ambayo hata mimi sikuwahi kuyafikiria hapo kabla, ila sishangai sana, waandishi wengi wanakuwa kama wapelelezi” alisema insp Aroub huku anacheka kidogo, “hooo! kumbe nafaa kuwa mpelelezi eeh?” nilimuuliza insp kwa kumzuga ili asigundue kama nilishtuka kwa swali lake, insp Alicheka kidogo, “yah! unamaswali mazuri, naimani kama ningekuwa na wewe toka hapo mwanzo ningefanikiwa kupata jibu sahihi, na pengine ningekuwa nimesha fanikiwa kumuona huyo jini” alisema mzee Aroub, ambae aliendelea kwa kusema kuwa, ukweli mazingira waliyo yakuta yalionyesha kuwa ile computer iliyobeba hard disc ilikuwa imevunjwa na kioo hakikuonyesha kitu, “sasa mzee tufanye marehemu alivunja mwenye security na kutoa hard disc, lakini sasa tujiulize alifanya hivyo kwasababu gani, si angeifungua na kutoa Hard disc, na kama kuna mtu alifanya hivyo ni nani, na kwanini, maana sidhani kama jini ana haja ya kuharibu mfumo wa camera za ulinzi ili kufanya jambo lake” nilimueleza insp Aroub, ambae sasa alikuwa amesha sahau kama anakazi kule ofisini maana tulikuwa tumesimama kwa zaidi ya dakika ishirini.
Insp Aroub alitulia kwa sekunde kadhaa, kama vile anawaza jambo kwa kina, kisha akavuta pumzi ndefu na kuishusha kwa nguvu, “yani hapa najiuliza ni kwanini wakati mwingine tusiwe tuna angalia vipaji kama hiki cha kwako na kuja kufanyia kazi ndani ya jeshi, maana unachokiongea ndicho nilichotakiwa kukichunguza mwanzo, hasa muda ule ambao tulikuwa tumetoka kuchukuwa mwili wa Vuai” alisema Aroub kama mtu anae jilaumu kwa kukosa kuliwaza hilo.
Kama ninge kuwa wewe msomaji, japo ninge mfumbulia fumbo ilo la camera, lakini ukweli lazima ningeingia kwenye matatizo, au kushukiwa katika nafasi ya kwanza, ila sikushindwa kutoa msaada, “ila mimi naona jujachelewa, unaweza kupata jibu ambalo litatusaidia wote, wewe katika upelelezi wako, na mimi katika kukamilisha kitabu changu” nilimueleza insp Aroub, kama vile natania, nikatulia kusubiri aniulize swali, “mh! sidhani kama naweza kupata chochote kwasasa, maana zimeshapita week mbili?” ujuwe kuna raha yake pale unapo kuwa na jibu, halafu unakaa kusubiri swali, “kwani unachotakiwa kujuwa ni kitu gani, mimi nadhani ni kufahamu kama camera zime haribika kabla au baada ya tukio, kama ni baada ya tukio nina uhakika kuwa huyo sio jini ni mtu kabisa ambae anafahamu madhara ya camera hizo endapo zitafika mikononi mwako” nilimueleza insp, ambae aliitikia kwa kichwa kukubaliana na mimi, “sasa nitaanzia wapi unadhani” swali hilo lilonyesha wazi kuwa mzee huyu alianza kuamini kuwa mawazo yangu yana mchango mkubwa sana kwenye kazi yake.
Hapo nikajifanya nawaza kidogo, kama natafuta jibu ambalo tayari nilikuwa nalo, nilitumia kama nusu dakika, kisha nikajifanya nimepata wazo, “hivi hakuna vijana wa karibu ambao walikuwa wanafahamiana na marehemu Vuai huko mtaani kwake?” nilimuuliza insp nae akacheka kidogo, “unaona basi hata hilo wazo sikuwa nalo, yupo kijana ambae muda wa tukio alimpisha Vuai aingie na mwanamke na ndie wa kwanza kugundua kuwa Vuai ameuwawa, nafanya mpango wa haraka sana kumpata kijana huyo” alisema insp Aroub huku anajiandaa kuondoka pale tulipokuwepo, nilitamani kumuongezea wazo jingine la kumpata kijana mwingine wa Ussi, lakini nikasita kwa kuonekana ninafahamu mambo mengi kwa wakati mmoja.
Lakini nilimuona insp Aroub, kama vile amepata hamu ya kufanya kazi muda huo huo, “kijana naona tumeongea mengi, ila nahitaji kumpata yule kijana haraka sana, sitoweza kupeleka report dar es salaam pasipo kupata jibu la camera, hivyo chukuwa namba yangu ya simu, utanipigia kuona kama tunaweza kupata muda zaidi wa kupeana habari zitakazo patikana” alisema mzee Aroub, ambae sasa alionekana kuwa na haraka sana, akanitajia namba za simu, na mimi nikazihifadhi kwenye simu yangu, na mpaka namaliza kusave namba tayari Aroub alikuwa anatembea kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye jengo lao la polisi, nilitabasamu kidogo kwa kuona kuwa mzee huyu hakuwa anafahamu lolote juu ya kilichokuwa kinaendelea.
Nilitembea zangu taratibu kulifuata gari tulilokuja nalo, ambalo ndani yake alikuwepo Jessenia, ambae sasa niliweza kumuona ananitazama huku anatabasamu, tayari nilisha anza kuhisi njaa, maana hata nilipotazama muda kwenye simu yangu ilisha karibia saa tano za asubuhi, “we Eric, yule insp Aroub unafahamiana nae, maana naona mnaongea kirefu haswaa?” aliuliza Jessenia mara baada ya mimi kuingia ndani ya gari, “niliagizwa kwake, ndio akawa ananieleza kuwa, mjomba wako alikuja hapa kuna mtu ameuwawa jana usiku, vipi umeisikia hiyo?” nilimuuliza Jessenia, ili nijuwe kama na yeye alikuwa anajuwa kuhusu mfanya kazi wa kaka yake kuuwawa jana usiku, wakati huo nawasha gari, “hapana sijasikia, wamesema ameuliwa na nani?” aliuliza Jesse kwa mshangao na uoga, “ameuliwa na jini” nilimueleza Jessenia huku naondoa gari taratibu, “weeee! usiniambie, sasa mjomba yeye anahusiana nini?” aliuliza Jeseenia, wakati huo tunaingia barabara kuu nakushika uelekeo wa chake, “insp ameniambia kuwa alie uwawa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa Ussi” nilimueleza Jessenia ambae alishtuka sana, “mamaaaaaa tayari mangeu amesha anza sasa, ndio maana mimi nakuambia tuondoke Eric tukaishi kwenu huko bara” alisema Jessenia kama alie pagawa, na mimi nikajifanya namshangaa, huku namuwekea mkono begani kwake, “kwani sisi inatuhusu nini Jesse, we tulia mimi nimalize kazi zangu nakuja kujitambulisha kwenu kisha tunaondoka zetu” nilimueleza jesse huku nampapasa begani, “yaani mimi nina wasi wasi na wewe na hivi mjomba ndio ameanza kukataa, yani nazidi kuchanganyikiwa kabisaaa” alisema Jessenia, kwa sauti fulani ambayo licha ya kuwa katika unyonge wa kujidekeza lakini ilikuwa tamu sana, hilo usiliwaze Jesse, cha msingi ni wewe kukubali kuolewa na mimi” nilimueleza hivyo huku natoa mkono wangu na kuongeza mwendo kuingia mjini chake chake, “Jesse, hapa chake kuna sehemu ya kupata supu” nilimuuliza Jessenia, “unasikia njaa eeh?” aliuliza Jessenia huku ananitazama “ndiyo sijala toka jana” nilimjibu kwa sauti ya msisitizo huku natazama kwenye eneo la mapaja yake, ambayo licha ya kuwa ndani ya gauni pana lakini niliweza kuona jinsi yalivyojaa na kutuna vyema, “kwani sasa tunaenda wapi si nyumbani kwako, kwanini usiende kula vitongoji?” aliuliza Jessenia na mimi kwa haraka haraka nikaona wazo lake halikuwa zuri, maana lazima nisinge kuta kitu ninacho hitaji kule vitongoji, “mh! sidhani kama itakuwa wazo zuri, maana kule wanamaliza mapema sana” nilimueleza Jessenia ambae tayari alikuwa amesha niondolea uvumilivu wa moyo na akili kwa rangi yake ya mdomo na wanja kwenye nyusi na kope zake za macho, na yeye akanielekeza mgahawa mmoja, uliopo njia ya markiti, kwa kuwa tulisha karibia chake chake, nilipunguza mwendo kidogo huku namtazama mschana huyu, ambae kiukweli siwezi kukuficha, mpaka hapo nilikuwa natamani kama ninge kuwa getoni nafanya kile ambacho nilimfanya jana, na leo nilipania kumfanyia vitu vingi ninavyo vijuwa, hakika sikutaka ajifunze kwa mwingine halafu anitukane wakiwa wanapeana dudu, maana kuna kisa kimoja nilipenda nikudokeze wakati natafuta maegesho hapa chake chake barabara ya marikiti maana ni finyu sana, je unajuwa ilikuwaje.… ITAENDELEA..