KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SABA: aliongea Jessenia kwa sauti ile ile ya chini, “ok! sawa, mimi nime tamani kukuona, nikasema niombe ruksa ili nije nikuone kidogo” nilimueleza Jessenia kwa sauti nzito na tulivu niliyoiweka katika mtindo wa kubembeleza, “nimesha kuwa wako tena mpenzi, we niambie tu unataka tukutane wapi” alisema Jessenia kwa sauti ambayo ilikuwa tamu iliyolegea flani hivi, “tukutane kituo cha mafuta, nitasimama pale kuweka mafuta” nilimuambia Jessenia, ambae alijibu kwa haraka na furaha kubwa, “sawa naingia kuoga, nikitoka nitakuambia” alisema Jessenia na kukata simu… ENDELEA..
Hapo nikajiona nimeingia mkenge, kwasababu lengo langu lilikuwa ni kwenda nae polisi, kisha niende nae airport, halafu nirudi nae mjini tutembee kwa miguu sehemu mbili tatu, nadhani mpaka hapo ningekuwa nimesha pata jibu, hata hivyo nikaona hakija haribika kitu wacha niende kwanza Airport kutuma kile kichupa, hivyo niliondoka zangu kuelekea huko, nikipitia mjini na kununua pair moja ya viatu na kuweka kile kichupa ndani, kisha nikavifungia viatu ndani ya box na kuelekea navyo airport, ambako nilikabidhi box na kufanya malipo ya mzigo ule, nikamjulisha mkurugenzi kuwa mzigo upo njiani, ikiwa ni lengo la kwamba na ofisi ikachunguze na kuhifadhi kama ushahidi hapo baadae, tayari nusu saa ilishakatika.
Naam nikiwa njiani narudi toka airport, nikampigia Jessenia, ambae nilipanga nimpate mapema ili niweze kuzurura nae hapa mjini, nae akapokea lakini kwa sauti ya chini kama mwanzo, “unaweza kuanza kutoka, mimi namsubiri mjomba atoke ndio nitoke” alisema Jessenia kwa sauti ya chini, ukweli nilishangaa kidogo, maana historia ya Jessenia niliyoipata kwa Jesse mwenyewe na babu Mangeu, ilionyesha kuwa Jessenia alikuwa huru kutembea sehemu yoyote muda wowote, iweje leo aseme anamsubiri mjomba atoke au inahusiana na maongezi aliyotoka kuyafanya, “ok! mimi nakaribia macho manne, ukiweza tuonane nina hamu ya kuwa na wewe leo” nilimueleza Jessenia, ambae sikutaka ajuwe kama nataka tujitoa chambo, “ondoa shaka mpenzi, mi mwenyewe nilikuwa natamani sana kujifungia na wewe chumbani, nifidie muda wote ambao natamani tungekuwa wote, yaani toka utotoni mwetu” alisema Jessenia, hapo wote tukacheka kwa pamoja, kicheko cha kivivu, “poa basi utanijulisha” nilisema na kukata simu, japo haikuchukuwa muda mrefu kabla Jessenia hajapiga simu na kuniambia kuwa anatoka nyumbani kwao, ya kwamba tayari mjomba wake amesha toka nyumbani.
Dakika kumi na tano baadae nilikuwa nimesha egesha gari kwenye kituo cha mafuta pale chake chake, nikijaza mafuta kwenye gari nikiwa tayari nimesha pitia duka la juice na kununua bilauli mbili za juice na kuziweka ndani ya gari, nilipomaliza kujaza mafuta nilitoa gari kwenye pump na kuliegesha pembeni, ambapo haikuchukua hata dakika tano, nikamuona Jessenia akitokea pale kituoni, licha yakuwa alikuwa amevaa nicab usoni, lakini pia alionekana amependeza kweli kweli ungesema ni sikukuu ya eid, japo lengo lilikuwa ni kujitoa chambo na kuweka mtego, lakini nilianza kuhisi kiu ya kitumbua, hata Jessenia alipo fungua mlango wa mbele wa gari ilitangulia harufu nzuri ya manukato, ungesema jini, “asalam aleykum” alisalimia Jessenia, na mimi siku mjibu hivi hivi, kwanza nilikamata niqab na kuipandisha juu, nikiacha uso wake wazi, “waalaykum salaam” niliitikia huku namkamata mabega yake na kumvutia kwangu kwa maana ya kumkumbatia, nilifanya hivyo huku nikihisi kuwa Jessenia angekataa kwa kuhofia macho ya watu ambao wangeweza kutuona, lakini haikuwa hivyo, ukweli ni kwamba alijilegeza na kujileta kwangu, na kuniachia kiss ya shavuni, huku akijichekesha kiaibu, “Eric unanifundisha mapenzi kama ya wahindi” alisema Jessenia huku anajitoa kifuani kwangu na mimi nikamuachia, “hata mimi nashangaa” nilisema hivyo huku nawasha gari, na kukanyaga mafuta kuelekea upande wa madungu Centle Polisi, “huku wapi tena au tunaenda mkoani?” aliuliza Jessenia kwa sauti iliyosheheni afya ya furaha, huku anachukuwa bilauli moja ya sharubati ya mabungo na kimrija chake na kuanza kukifyonza, “naenda pale kituo cha polisi, mjomba amenituma nikamuone mtu” nilimueleza Jessenia, kisha nikamkumbusha kuhusu habari aliyoahidi kunisimulia tukikutana, ni kuhusu mjomba wake, “weee acha tu, pemba ndogo hii, yaani sijui hata alipozipata hizi habari” alisema Jessenia huku anacheka kidogo, habari gani hizo Jesse” nilimuuliza Jessenia kwa sauti iliyojaa shauku, ukweli nilitamani kujuwa maongezi yake na mjomba wake, “nashangaa mjomba na shangazi wamesha gundua kuhusu mimi na wewe” alisema Jessenia kwa sauti kama yakuto kujali, kitu ambacho kilinifanya nihisi kuwa, mazungumzo hayo yaliisha vizuri.****
Ilikuwa hivi katika simulizi yake, Jessenia alisema kuwa, ile usiku nilipoachana nae na yeye kurudi nyumbani kwao, aliingia kirahisi tu kama alivyotoka, akaingia chumbani kwake na kujilaza huku akifikiria na kuwaza hatima ya penzi lake la kwanza lenye mafanikio, kwa mwanaume ambae amemfungulisha ukurasa mpya katika maisha yake, ni baada ya kumsimulia juu ya hadithi yake ya ukweli katika maisha yake, kwamba kila mwanaume anae karibia kutembea nae anakutwa ameuwawa, Jessenia alikaa macho mule chumbani mwake, akisubiri simu toka kwangu, mpaka wakati fulani aliposikia gari likiingia pale nyumbani kwao, hakuwa na shaka kuwa ni Ussi anarudi toka kwenye starehe zake, “ni kweli alikuwa Ussi, maana dakika chache baadae, nikaona kitasa cha mlango wa chumba changu unashikwa na kunyogwa, bahati nzuri huwa nafungaga mlango na ufunguo, wakati huo huo nikamsikia Ussi akiniita kwa sauti yake ya kilevi, “we mshenzi hebu fungua mlango haraka, leo ulikuwa wapi?” alisema hivyo huku anagonga mlango wa chumba changu kwa fujo” sikutaka kumsikiliza wala kufanya kile anachoniambia, nilimuacha apige kelele pale mlangoni mpaka achoke nilijuwa ni wivu wake wa siku zote, hivyo sikuhangaika nae, mpaka mjomba alipokuja kumchukuwa nao wakaelekea chini, na sikusikia mjomba alimueleza nini mpaka Ussi akatulia na kwenda kulala” alisimulia Jessenia huku safari yetu inaendelea, nilikuwa naendesha gari taratibu kwasababu kituo cha madungu hakikuwa mbali toka pale tulipoanzia safari.
Jessenia aliendelea kusema kuwa, japo alichukulia kuwa ni wivu tu wa Ussi ndio unao msumbua na kuhitaji kujuwa aliko kuwepo mchana wa siku iliyopita, lakini alikiri kuwa siku ile kama ni wivu ulikuwa mkubwa sana, tofauti na siku nyingine, kiasi kwamba Jessenia alijiuliza kama Ussi amegundua alicho kifanya mchana wa siku ile, na isingekuwa ajabu, maana Ussi alikuwa na marafiki wengi sana ambao wangeweza kumjulisha kilichotokea kule Green House, lakini hata hivyo Jessenia hakuona sababu ya binamu yake huyo kuwa mkali kiasi hicho baada ya kufurahi kwa kuona kuwa lile tatizo la jini limeisha.
Ukweli haikuwa hivyo, asubuhi ya leo ni shangazi, yaani mama Ussi au unaweza kusema ni mke wa bwana Juma Mohamed, ndie aliemuita Jessenia, ambae tayari alikuwa amesha amka na amesha wasiliana na mimi, “Seni unaitwa na mjomba wako kule kwenye chumba cha wageni” alielezwa na shangazi yake ambae kiukweli alionekana kuwa kama amekasirishwa na jambo, “sikujiuliza sana kwanini shangazi alikuwa vile, nilijuwa tayari Ussi alisha waeleza alicho kisikia kuhusu mimi na wewe” alisema Jeseenia, ambae alieleza pia, baada ya kuingia kwenye chumba cha wageni, nilimkuta mjomba nae amekasirika kweli kweli, “Seni, naomba unieleze bila kunificha chochote, jana umefanya chochote na huyo mwanaume kafiri (mtu yoyote asie wa dini ya kiislam)?” hilo ndilo swali la kwanza kabisa ambalo Jessenia alikumbana nalo, mara baada ya kuingia mule chumbani, “sikupenda kauli yake ya kafiri, lakini nilijikaza tu, na kuitikia kwa kichwa” nilidhania kuwa mjomba angefurahi kwa kuwa ni dalili ya tatizo langu kuisha, lakini baada yake mjomba alichukia sana na kukasirika, “umetumahanisha we mtoto, kwanini umefanya ujinga kama huo, ni kwanini ulishindwa kuomba ushauri wa kuanza urafiki na huyo mshenzi tapeli?” aliuliza mjomba wa Jessenia, kwa sauti iliyoonyesha kuwa amekasirika sana, “lakini mjomba huyo mtu sio wakunichezea tutaoana” hivyo ndivyo alivyo jitetea Jessenia, lakini haikusaidia kitu, “sawa Seni, hata kama atakuoa, lakini kwanini ukaruhusu kitu kama hiki kitokee tena kabla hajaja kujitambulisha?” aliuliza mjomba kwa sauti iliyojaa hasira na chuki, “sio kitu mjomba, maana yeye ndie mwenye kunioa, siri yangu ni siri yake, na isitoshe ndugu zake wapo dar, hivo ni rahisi kwa wao kuja hapa haraka, huoni kama ninge mkosa na huyu ndie mwanaume wa pekee alieweza kuwa na mimi bila kudhurika” alijitetea Jessenia, lakini ni kama ilizidi kumchafua mjomba, “nani alikuambia tutakubali akuchumbie huyo kafiri?, kwa taarifa yako hata akikubali kubadili dini, hakuna atakae mkubali huyo mshenzi analolitaka” alisema mjomba wake Jessenia kwa sauti iliyojaa ukali, kitu ambacho kilimshangaza Jessenia mwenywe na kumfanya, aone mambo yana kuwa magumu kwa upande wake, yaani licha ya kuona kuwa tayari amepata ufumbuzi lakini ndio kwanza tatizo jingine linaibuka, hivyo akaona isiwe tabu, “mjomba mimi naomba nionyeshe ndugu wengine basi nimpeleke kwa ndugu wengine, wao ndio watakao pokea barua na mahari” alisema Jessenia kwa sauti ya kulalamika, japo alikuwa anamaanisha anachokisema, kauli ambayo ilimshtua sana mjomba wake, “kwahiyo mimi nilie kulea toka utotoni mwako, unaniona sifai na sasa unataka ndugu wengine?” alisema mjomba kwa hasira na wakati huo huo simu yake ikaita nae akajiweka sawa na kuipokea, “Hallowa kaka, asalam Aleykum” alisalimia mjomba wake Jessenia, huku anatoka mule chumbani, na kumuacha Jessenia peke yake, akitafakari maongezi yake na mjomba wake, japo alikuwa anasikia maongezi ya mjomba wake kwenye simu, lakini hakuweza kusikia upande wa pili wa simu, “yah! nimesikia kaka…. ndiyo ….. ni tatizo kwa kweli, ngoja nije tuonane mara moja” ni maneno ya Mjomba wake Jessenia, ambayo Jessenia aliyasikia kabla mjomba hajaagana na mtu aliempigia na kukata simu, baada ya hapo akarudi chumbani, alikomuacha Jessenia, “jifikirie Jessenia, na kuanzia sasa usitoke humu ndani” alisema mzee Juma Mohamed, na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kwaajili ya kujiandaa kwenda kukutana na huyo mtu wake.
“Mjomba alipotoka tu, na mimi nikatoka, na wakati natoka tu nikamuona Ussi anatoka chumbani kwake haraka na kuniangalia kwa jicho kali, he! shemeji yako ana wivu” alisema Jessenia akimaliza kwa kicheko, wakati huo ndio tulikuwa tunaingia Madungu polisi post na kuegesha gari kwenye magesho ya pale polisi, pembeni ya gari moja zuri la kifahari aina ya range rover, lililokuwepo pale kwenye maegeso kati ya magari kadhaa ya jeshi la polisi, “dah! kwanini sasa mjomba wako hataki nikuoe?” nilimuuliza Jessenia, tukiwa bado ndani ya gari, lakini nimesha zima, “atajuwa yeye mwenyewe, mimi nachoomba nishike mimba au unibebe tuondoke kwenda dar” alisema Jessenia na kunifanya nitabasamulie moyoni, maana niliona kuwa Jessenia hakuwa anaelewa anacho kisema, wala kukiwaza….. ENDELEA..