KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TANO: mimi na mwalimu Aisha tulikuwa tumesimama nyumba ya kikundi cha kidato cha tatu, sijui nini kilinisukuma kutazama wanafunzi waliojipanga mbele yetu, maana ghafla macho yangu yakakutana na macho ya mwanafunzi wakike Maimuna, aliekuwa anageuka kutazama nyuma, akatabasamu na kutazama mbele, sikutaka kumtazama tena, lakini sijui macho yana matatizo gani, usichotaka kukitazama yenyewe ndio yanacho kitazama, ndivyo ilivyotokea kwangu, maana dakika tano baadae nikajikuta nimesha mtazama tena Maimuna mbae kama kawaida alikuwa ananitazama…. ENDELEA….
Nakuachia tabasamu kama lile la mwanzo, tabasamu ambalo mtu yoyote endapo angeliona lazima ange hisi kuwa nilishawai kutembea na mwanafunzi huyu, nikakwepesha macho na kumtazama mwalimu Aisha kama nayeye aliona kilichokuwa kinaendelea, nikamuona yupo busy anamtazama mwalim mkuu aliekuwa anaongea kule mbele ya parade, wakati huo kichwani mwangu nilikuwa nawaza namna ya kuomba ruksa ili niende mjini kufanya nilichopanga kufanya.
Naam nilikaa dakika kama saba hivi nikijizuia kumtazama yule mschana mdogo wa kidato cha tatu, nilifanikiwa kufanya hivyo mpaka parade ilipoisha na sisi kutawanyika tukiacha uongozi wa wanafunzi wanamalizia taratibu za parade na kuwa tawanyisha wanafunzi waelekee madarasani, mimi nikanyoosha moja kwa moja ofisini kwa mwalimu mkuu, ambako niliomba ruksa kwa kutoa sababu za uongo, kwamba nahitaji kutuma fedha nyumbani maana kuna mgonjwa anahitaji fedha za matibabu, nae hakuwa na pingamizi, ukichukulia mimi ndie mwalimu pekee ambae sikuwa na vipindi pale shuleni.
Sasa basi wakati natoka nje ya ofisi nikashtuka kumuona Maimuna anaibuka kutokea pembeni mwa ukuta wa ofisi ile na kupita mbele yangu karibu kabisa, huku akinishika mkono na kuniachia kipande cha karatasi, hakika usingeweza kudhania kama kunajambo limetokea baina yetu, ungesema watu wamepishana tu, hakika nilishangaa kwa uwezo wa haraka wa mwanafunzi huyu, lakini sikutaka kujiuliza sana, niliweka lile karatasi mfukoni na kueleka staff office, ambako niliaga na kuelekea zangu nyumbani kwaajili ya kuchukuwa ile chupa ndogo niliyoipata jana kwa wale jamaa wawili wafanyakazi wa Ussi.
Nilipofika nyumbani nikakumbuka kutazama lile karatasi nililopewa na Maimuna, lilikuwa na ujumbe tena ujumbe wa kusisimua, ambao niliusoma mara mbili huku nafananisha sura na umri wa Maimuna kile alicho kiandika ndani ya karatasi, “mpenzi sitojari hata kama upo na mwalimu Aisha na dada Seni, ninachohitaji mimi ni kulipata penzi lako, na siwezi kusubiri zaidi kupata kinacho wachanga wanawake hao wawili, nahitaji nikutane na wewe ili unipatie kile ulichojaaliwa, naomba unipigie kwa namba 0677164798.” ndivyo ulivyosema ule ujumbe ambao mwisho wake ulimalizia kwa namba za simu, nilijikuta nacheka kidogo, maana nilikumbuka kuwa mschana huyu mdogo aliniambia kuwa hajawahi kuruhusu dudu ipite kwenye kitumbua chake, sasa inakuwaje kana tamani dudu kiasi hiki, nilikikunja kile kikaratasi na kukitumbukiza chooni na kuflash kwa maji, halafu nikachukuwa kile chupa na kutoka nacho nje, moja kwa moja kwenye gari na kuondoka zangu kuelekea mjini, lakini kabla sijalimaliza eneo la Ali Kahamis camp, nikasikia simu yangu inaita, nikaichukuwa toka mfukoni na kutazama mpigaji, “mkurugenzi Win” ndivyo ilivyosomeka kwenye kioo cha simu
Hapo nikashusha pumzi ndefu, kwa maana nilikumbuka kuwa toka juzi sikuwa nimempigia mkurugenzi kumpa taarifa yoyote, nikasimamisha gari pembeni ya barabara na kuzima gari kabisa, kisha nikapokea simu nikiwa nimepandisha vioo mpaka juu kabisa, “shikamoo boss” nilisalimia kwa sauti tulivu ya mikwaruzo, ungesema nina toka kuamka, “hivi we dogo, unajuwa nakushangaa sana, hivi Pemba ni sehemu ya kulala hivyo kweli, yaani matukio yanaendelea na wewe unalala tu, hakuna taarifa hakuna uchunguzi, ndio tuamiani kwamba jini ameuwa tena jana usiku?” aliongea mkurugenzi kwa sauti ya kunikalipia, ni kitu ambacho nilikitegemea, maana licha ya kupenda masihara lakini boss hakutaka uzembe katika kazi.
Kwa uongeaji wa boss Winfrid, ilionyesha wazi kuwa kuna taarifa aliipata, nayo sio nyingine ni ile ile ya jana usiku, “hooo! boss kwani kuna taarifa gani umeipata” niliongea kwa sauti ile ile ya kama ninatoka usingizini, “umesikia juu ya taarifa ya huyo mtu mwingine alieokotwa huko gombani akiwa ameuwawa na hicho kitu kinacho sadikiwa kuwa ni jini?” aliuliza mkurugenzi, sikushtuka sana kwa swali lile, ila nilihisi kuwa pengine kuna mpelelezi mwingine ametumwa huku pemba, “hapana sijasikia, mtu huyo wa jinsia gani?” nilimuuliza Boss, nikitaka kuichezea akili yake, na yeye akajibu kwa hasira, “nani kakuambia lile jini linauwa mademu?” aliuliza mkurugenzi kwa sauti ya kunishagaa, hapo sikuwa na jibu, sio kwamba sikulijuwa, ila nilikuwa natafakari kuhusu hisia zangu na kifo kilichotokea, na mkurugenzi akaendelea kuongea, “lile jini linauwa wanaume tu, na unaambiwa ni wanaume wenye uchu wa wanawake, sasa na wewe endelea kujifanya ni mvuvi wa wanawake” alisema mkurugenzi, huku mimi natabasamulia chini, maana alijiona kuwa amenitangulia hatua moja mbele, “wewe umepata wapi hiyo taarifa?” nilimuuliza huku nikijifanya kushangaa, “acha uzembe Eric, umesahau kuwa mtu alietupatia kazi ya kuchunguza mauwaji haya yupo huko Pemba?” aliuliza mkurugenzi Winfred kwa sauti kama ya kuchukia kidogo.
Ukweli jambo hilo nililisahau kabisa, sasa niliona kuna umuhimu wa kumfahamu mtu alietoa kazi ya upelelezi “ndiyo nafahamu, lakini nilipaswa nikutane nae ili niweze kupata mawili matatu toka kweke, si unajuwa kuwa hatua ya kwanza inaanzia nyumbani kwako” niliongea kwa namna ya utani sikutaka boss aendelee kuchukia, “ina maana unahisi alietoa kazi ndie muuwaji?” aliuliza mkurugenzi kwa namna ya kunishangaa, “sina maana hiyo ila naamini tutapata chochote kupitia yeye” nilimjibu hivyo na hapo bila kusita, boss akafunguka, “silifahamu jina lake ila nafahamu email yake aliyotumia kuwasiliana na sisi,
j_jos@gmail.com ukweli hata sisi hatuja muona kwa sura, maana alitoa kazi kwa njia ya mtandao, na malipo ya mwanzo alifanya kwenye account ya bank, sidhani kama vitakusaidia katika kazi yako” alijibu mkurugezi, “ana husikaje katika hili, yaani yanamuhusu vipi kiasi cha kutaka uchunguzi?” niliuliza ili kupata mwanga kidogo, maana jina lake halikuwa wazi, “hilo ndio tatizo, katika maelezo yake amekataa kusema anahusikaje juu ya hilo, na pia hajasema kwa nini anaamua kugharamia uchunguzi” alisema mkurugenzi na kuniacha njia panda, “sawa boss naomba masaa mawili nitakupigia” huo ndio ulikuwa mwisho wa maongezi yetu, na mimi nikakata simu na kuwasha gari na kuelekea mjini, nikipita pale ngerengere nilipofanya tukio la kupigana na wale vijana wawili, lakini sikuona alama wala dalili ya chochote kinachohusiana na tukio la jana usiku.
Dakika kumi na tano baadae, nilikuwa naegesha gari kwenye maegesho ya hospital ya chake chake, ambapo palikuwa na magari kadhaa na pikipi aina ya vesper ndizo zilizo ongoza kwa uwingi pale maegesho, siku hangaika nazo, nilitembea kufuata baraza ndefu (korido), kuelekea upande wa maabara, huku natazama mazingira ya pale hospital ambayo yalikuwa yametawaliwa na watu wengi waliokaa kwa makundi, iwe wafanyakazi wa mazingira na usafi, wauguzi na waganga, wagonjwa na wasindikizaji, walionekana wakijadili jambo fulani, na jambo hilo lilikuwa ni kuhusu kifo kilichotokea jana huko Gombani, hata nilipofika maabara, nako niliwakuta wafanyakazi wa pale wakiwa wanajadili, “kiukweli hata sielewi mwisho wa hili jini litauwa mpaka lini?” aliuliza mmoja kati ya wale madoctor wa maabara, “unajuwa mpaka nina hisi kuna mkono wa mtu, yaani ni miaka na miaka hili jini linauwa” alisema mwingine, wakati huo mimi najitahidi kutazama kati yao, pengine ningemuona Doctor Hafidhi, lakini sikumuona hivyo nikaamua kuulizia.
Hivyo niliwasogelea wale waliokuwa wanajadiliana, kisha nikawasalimia na kuulizia kuhusu doctor hafidhi, “yupo ofisini, unaweza kwenda kumuona” alisema mmoja wao, huku ananionyesha mlango mmoja kati ya minne iliyokuwepo ndani ya maabara, niliufuata ule mlango na kuugonga, “ingia” ilisikika sauti toka ndani ya ofisi ile, nikafungua mlango na kuingia ndani ambako nilimkuta doctor hafidhi, alienitazama kwa macho ya mshangao, “kweli kijana kuna jambo nyuma yako, yaani hapa nilipokaa nasoma report ya uchunguzi wa kimaabara wa mtu aliekutwa ameuwawa huko gombani, nikakukumbuka haswaaa, nikasema ungekuwepo ungeweza kujionea mwenyewe, na bahati nzuri na wewe mwenywe huyu hapa” alisema mzee hafidhi, ambae alionyesha kuni kumbuka, “imekuwa bahati, maana nilikuja kwa inshu nyingine kabisa” nilimuambia mzee hafidhi katika hali ya uchangamfu kama vile ni watu tunao fahamiana muda mrefu, japo ilikuwa ni mara ya pili sisi kukutana, “ok! nadhani ungeeleza jambo lako, kisha twende ukajionee jinsi mwili wa mtu alieuliwa na jini anavyokuwa” alisema mzee hafidhi, ambae nilimueleza kuhusu kile kichupa, ambacho nilitamani kufahamu kililichokuwepo ndani, japo sikumueleza nilipokitoa, “sawa usijari, nitawakabidhi wachunguze halafu sisi twende mutual kuona mwili wa kijana yule ambae mpaka sasa bado ndugu hawajajitokeza kuja kuutambua” alisema mzee hafidhi, na ikawa kama alivyosema aliwakabidhi kile kichupa ambacho nilisisitiza kuwa nitakihitaji mara baada ya uchunguzi, na sisi tuka elekea kwenye jengo la kuhifadhia miili ya marehemu, huku tukiacha uchunguzi ukiendelea.
Naam dakika kumi baadae tulikuwa ndani ya jengo la mutually, na moja kwa moja tukaenda kuutazaa mwili wa marehemu huyo ambae naweza kusema ilinishtua kidogo, maana niliutambua mwili ule kuwa ni wa mmoja wa wale vijana wawili walio nivamia kule ngerengere, kwa maana llrahisi ni kwamba, huyu ni mmoja wa vijana wa Ussi, ni yule ambae nilimuwahi kabla haja puliza kile kifimbo kifupi, alicho weka kitu alicho kichovya ndani ya kile kijichupa, “doctor una sema huyu mtu alikutwa sehemu gani?” nilimuuliza doctor hafidhi, ambae alisisitiza kuwa alikutwa ameuwawa huko Gombani, “aliletwa na jeshi la polisi baada ya watu kutoa taarifa kuwa amekutwa eneo hilo la gombani” alisema mzee hafidhi, ukweli ni kwamba japo sikutaka kumueleza ukweli wa sehemu halisi aliyofia huyu jamaa, lakini niliamua kujiridhisha mimi mwenyewe juu ya kifo cha huyu jamaa kama kina husiana na kile kichupa, “sahamani doctor report inasemaje juu ya kifo cha huyu jamaa?” nilimuuliza doctor hafidhi, huku namtazama yule jamaa ambae siku ya onyesho la music wa taarab ni kama alitumwa na Ussi kuja kufuatilia maongezi yetu na Jessenia, “taarifa ni kama ile ile ya siku zote, amekauka damu yote mwilini mwake” alisema mzee hafidhi, na hapo nilianza kupata picha fulani juu ya kilicho mtokea yule jamaa, ambae licha ya kuwa mweusi kwa asili, lakini alizidikuwa mweusi mara dufu, “doctor nikuambie kitu, unaweza kugundua kitu ndani ya mwili huu” nilimueleza doctor hafidhi, ambae alinitazama kwa mshangao kidogo, “una mana gani kijana, yani kwa kutumia maabara au kwa macho?” aliniuliza kwa sauti ambayo ilikuwa katika mashaka ya wazi kabisa, “kwa macho ya kawaida doctor, unaweza kugundua kilichomsibu huyu jamaa, lakini ni lazima ufanye upasuaji mdogo kwenye koo la huyu jamaa” nilimueleza doctor hafidhi ambae aliutazama mwili wa yule jamaa kisha akanitazama kwa macho ya kutilia mashaka, “una uhakika kijana, maana kuuchunguza mwili siyo kesi wala kosa, ila kumbuka huu ni mwili wa binadamu na tunapaswa kuuheshimu” alisema doctor hafidhi kwa sauti ya kutahadharisha, “nafahamu doctor ila sidhani kama tutakuwa tumeudharau mwili endapo tunahitaji kufahamu ukweli halisi ambao utawasaidia wengi” nilimueleza doctor hafidhi, ambae alinielewa na kuitisha vifaa vya kufanyia upasuaji….. ENDELEA..
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SITA: “una uhakika kijana, maana kuuchunguza mwili siyo kesi wala kosa, ila kumbuka huu ni mwili wa binadamu na tunapaswa kuuheshimu” alisema doctor hafidhi kwa sauti ya kutahadharisha, “nafahamu doctor ila sidhani kama tutakuwa tumeudharau mwili endapo tunahitaji kufahamu ukweli halisi ambao utawasaidia wengi” nilimueleza doctor hafidhi, ambae alinielewa na kuitisha vifaa vya kufanyia upasuaji…..ENDELEA…
Ulikuwa ni upasuaji mdogo, japo haukupendeza sana machoni, licha ya kutoboa koo la mtu huyu, hakuna hata chembe ya damu iliyotoka pale shingoni, ambapo baada ya kupasua pale shingoni, doctor hafidhi hakutumia muda mrefu kupata kisindano kidogo sana mfano ofisi pin, (nusu pini) inayong’ang'ania shingoni, nikamuona doctor hafidhi akinitazama kwa macho ya mshangao na kutokuamini, “kijana wewe ni mwalimu, mwandishi, au mpelelezi?” aliniuliza doctor hafidhi kwa sauti ya kunitilia mashaka, lilikuwa ni moja kati ya maswali ambayo nilitegemea kabisa kuulizwa na doctor huyu, japo sikuwa nimeandaa jibu lake, “doctor wewe nielewe kama unavyo nielewa kwamba mimi ni mwalimu ambae ninaandaa makala yanayohusu majini” nilimjibu kirahisi huku natabasamu, “kwahiyo unataka kuniambia nini mwalimu, kwamba mauwaji haya yanafanywa na jini?” aliuliza doctor hafidhi na mimi sikuweza kumpa jibu la kweli, “sidhani kama naweza kukupa jibu sahihi, ila naamini kuwa wewe ndie utakuwa wa kwanza kupata jibu” nilimueleza doctor hafidhi, ambae sasa alikuwa anashona kwenye shingo la yule jamaa, “ok! basi nieleze umejuwaje kama kuna kitu kama hiki shingoni mwa huyu jamaa?” aliniuliza doctor hAfidhi, likiwa ni swali la pili kati ya maswali niliyo yategemea, nalo pia sikuandaa jibu, “nadhani hilo sio swala muhimu kwa sasa, ila wakati ukifika nitakueleza, chamsingi ni kwamba lazima utambue kuwa, hiki tunachokifanya kitazua maswali mengi sana, na pengine mmoja wetu kupelekwa jela kwa kujibu tuhuma za mauwaji na mmoja mwenyewe ni wewe ambae miaka mingi umekuwa ukisema kuwa vifo hivi vinatokana na jini” nilimtahadharisha doctor hafidhi, ikiwa ni kama kumnyamazisha doctor hafidhi, ambae ni kama maneno yangu yalimuingia na kuyaelewa, lakini vipomo vilikataa kusoma aina ya vifo vya watu hawa” alisema Doctor hafidhi, wakati tunarudi kule maabara, akiwa amebeba kile kisindano kwenye kibebeo maalumu, “dakika chache baadae tutapata jibu ambalo naomba usiliweke katika report ya kifo cha mtu huyu ili kujuwa chanzo cha mauwaji” nilimuelimisha doctor hafidhi ambae sasa alikuwa ananitazama kwa macho ya kipekee.
Naam ile tunaingia maabara tu, doctor akauliza kuhusu majibu ya kile kichupa ambacho sasa kilikuwa kimechunguzwa kwa lisaa na nusu, “majibu yapo ofisini kwako, ila tunaomba siku nyingine doctor kitu kama hiki kihifadhiwe kwenye tube (kibebeo) maana ni hatari sana kwa maisha ya binadamu” alifafanua yule mtu aliepewa jukumu la kuchunguza ile chupa, akionyesha kushtushwa na kile alicho kigundua kwenye ile chupa, “ok! Hebu nikagulie na hii sindano, uwe makini isikuchome sehemu yoyote, alisema doctor hafidhi, huku anamkabidhi yule doctor mwenzie kile kibebeo chenye sindano, nae akakipokea na sisi tukaingia ofisini.
Ndani ya ofisi doctor hafidhi alionekana kuwa na hamu ya kusoma ile taarifa, alianza kuisoma haraka tena kimya kimya, huku mimi nikimtazama usoni mwake na kusoma jinsi anavyo yapokea, nilimuona akikunja uso na kubadilika mara kwa mara kila alipokuwa anasoma ile taarifa, na alipomaliza akanitazama kwa macho ya mshangao, “hii chupa umeitoa wapi kijana?” aliuliza doctor hafidhi, huku ananitazama kwa mshangao na mashaka, “vipi kwani jibu limeanza kupatikana?” nilimuuliza swali juu ya swali lake na yeye akatikisa kichwa kwa masikitiko makubwa, “hii sumu ni mbaya sana, inapatikana kwenye kiumbe hatari cha baharini kinacho fahamika kwa jina la Stone fish kisanyansi kinaitwa synanceia, kwa kishwahili unaweza kumuita samaki jiwe, nilishawahi kusikia habari zake, kwamba ana gamba gumu sana mithiiri ya kioo au chupa ngumu, ambalo lina miba ndefu na endapo una mkanyaga yeye hutoa sumu mfano wake ni ngisi au pweza anavyo fanya, sumu yake ikigusana na maji maji ya mwili wa binadamu, humkausha damu ndani ya dakika moja, leo ndio nimegundua kuwa kiumbe hicho ndicho watu hukiita chunusi, wakidhania kuwa ni jini kumbe ni aina ya samaki” alisema doctor hafidhi, na sasa nilipata jibu kuwa muuwaji wa wanaume wa Jessenia hakuwa jini, ila ni Ussi na vijana wake.******
Naam baada yakumalizana na doctor hafidhi ambae alinipatia ile sumu ikiwa imeifadhiwa vyema kwenye chombo maalumu cha kimaabara kwaajili ya kuhifadhia vimiminika hatari kama hiki, nikatoka zangu na kuelekea kwenye gari, nikimuacha doctor hafidhi anapitia tena ile taarifa ya uchunguzi wa kikemia, huku mimi nikiwa nimesha maliza kazi yangu iliyonileta Pemba, nadhani unakumbuka niliagizwa kuja kuchunguza kama vile vifo ni vya jini kweli au ni binadamu kama bwana
j_jos@gmail.com alivyohitaji kujuwa, lakini kiukweli nilisha ingia kwenye mkataba mwingine mpya kabisa, ambao naweza kusema ulikuwa ni wakujitakia, ni kuhakikisha na mlinda Jessenia mwanamke mrembo alietokea kuweka imani yake kwangu.
Nilitembea huku nikiwaza mambo na maswali kadhaa kichwani mwangu, moja ni namna ya kujilinda mwenyewe na kumlinda Jessenia na Mangeu, maana ni wazi kwa kifo cha huyu kijana mmoja wa Ussi, usalama wa wawili hawa utakuwa mashakini, pale muuwaji atakapo ona siri inakaribia kufichuka na kuamua kuwauwa wahusika wakuu, ambao hawa kuwa na ndugu wa karibu ndani ya pemba hii, swali jingine, ni wazi Ussi anahusika juu ya hili, hata nilipokumbuka siku aliyo uwawa Vuai, Ussi alionyesha dalili za wazi kuwafuatilia Vuai na Jessenia, tena huyu marehemu wa jana usiku na mwenzie walimletea kile kijifuko kama ambacho wao walikuwa nacho jana usiku, ambacho ndani yake kulikuwa na kichupa na kile kitu kama filimbi, sasa swali likabakia Ussi anayafanya haya yote kwaajili gani, pengine ni kwasababu aliambiwa kuwa mwanaume atakae muowa Jessenia ndie atakae kuwa na haki ya kumiliki nyumba na magari anayo tamba nayo, sasa je, mambo haya anayafaya peke yake au anasaidiwa na nani kuyafanya haya anayo yafanya, inawezekana baba yake anahusika, na kama ndio kwanini mzee Juma Mohamed ameamua kuyafanya haya, ni ni vipi nitamtia nguvuni nikiwa na ushahidi, “nitaupataje ushahidi?” nilijiuliza huku naendelea kutembea kuelekea kwenye maegesho,
Niliwaza hayo mpaka nilipoingia kwenye gari, ambapo nilikuwa nimesha pata majibu mawili, moja ni kwamba, nikiwa najuwa kwamba mimi ndie windo kuu la watu ninao wafuatilia, hivyo nitajitumia mimi mwenyewe kama chambo kuwabaini watu wote wanao husika na mauwaji hayo, na njia ya kufanikisha jambo hili ni kujiweka hadharani mimi na Jessenia, pili nilipanga kushirikiana na insp Aroub kwa msaada wa haraka, endapo nitauhitaji, lakini sikutakiwa kujitambulisha mimi ni nani na nimekuja Pemba kwaajili gani.
Nikiwa ndani ya gari pale maegesho ya hospital, nikaanza mara moja mpango wangu wa kwanza, nilichukuwa simu yangu na kupiga namba ya Jessenia, ambae nilishangaa kidogo licha ya kukaa masaa manne bila kumtafuta lakini hakuwa amepiga simu yoyote kwangu, simu iliita muda mrefu bila kupokelewa mpaka ilipokatika, nikarudia tena kupiga ikawa vile vile, yaani iliita bila kupokelewa mpaka ilipokatika, nikaamua niachane nayo kisha nikapiga kwa mkurugenzi Winfred, ambae ni kama alikuwa anasubiria simu yangu kwa hamu kubwa sana, maana aliipokea mara moja, “masaa matatu na dakika arobaini na nane, lisaa limoja na dakika arobaini na nane zaidi, nipe report” alisema mkurugenzi, kwanza nilivuta pumzi ya kujiamini, “tulia boss ukiona hivyo ujuwe kazi haikuwa ndogo, kazi yangu imekamilika” nilimuambia mkurugenzi kwa sauti ya kujiamini nikamsikia anacheka kicheko cha raha, “nakuaminia mkono wa jini, nipe report” alisema mkurugenzi kwa sauti iliyochangamka.
Na hapo kwa kujiachia na kujiamini nikamueleza mkurugenzi, “kwa kifupi mkuu mauwaji haya haya husiani na jini, watu hawa wameuwawa kwa sumu hatari sana ya stone fishi, ijulikanayo kikemia kama (synanceia) wengi wanamfahamu kama samaki jiwe au huaminika kama jini chunusi, sumu ambayo ikigusana na maji maji ya ndani ya mwili wa binadamu, hugandisha damu kwa haraka na kumfanya mtu apoteze maisha kwa haraka” nilimueleza mkurugenzi, pia nilimueleza kuwa nina sample ya ile dawa ambayo nitaenda kumtumia kwa njia ya huduma ya vifurushi vinavyosafirishwa kwa ndege, nilipanga kufanya hivyo mara baada ya kutoka kuonana na insp Aroub, “muuwaji ni nani, na kwanini anafanya hivyo?” mkurugenzi aliuliza swali ambalo, sikutaka aniulize kwasababu sikutaka kumpa jibu, niliamini kuwa jibu la kweli lingemfanya aniambie niondoke pemba, kwamba nimemaliza kazi, na ukweli ni kwamba inanilazimu kubakia pemba kwa siku kadhaa, ili nimuache Jessenia na Mangeu wakiwa salama kabisa, “muuwaji bado sijamfahamu, ila amesha gundua kuwa nina mfuatilia, maana jana usiku niliandamwa na vijana wawili ambao niliwathibiti, na mmoja ni huyo ambae alimeza sindano ambayo ilikuwa ije kwangu na ndio aliepoteza maisha jana usiku” nilimueleza boss, pia nikamsisitiza kuwa asimueleze kwanza mtu alietoa kazi hii, ambae ameficha utambulisho wake, mpaka tutakapo juwa nia na dhumuni la muuwaji kufanya mauwaji haya, na boss alikubaliana na mimi.
Yap, nilipomaliza kuongea na boss Winfred, nilikata simu na kuwasha gari tayari kwa kuondoka, lakini kabla sijaondoa gari nikakumbuka kutazama simu, niliona messed call mbili za Jessenia, nikasitisha kuondoa gari na kubofya ile namba ili niipige, lakini kabla sijaipiga, simu ikaanza kuita, na mpigaji alikuwa ni Jessenia, nikaipokea mara moja, “ulikuwa unaongea na nani?” aliuliza Jessenia, kwa sauti yenye uchangamfu kiasi, japo ilikuwa ya chini, kwa maana ya kuongea taratibu, “nilikuwa naongea na mjomba wangu yupo dar, vipi mbona wewe hukupokea simu yangu?” nilimuuliza Jessenia, ambae aliachia kicheko laini kidogo, “punguza wivu mpenzi, kuna jambo nilikuwa naongea na mjomba na shangazi, nitakueleza tukikutana” aliuongea Jessenia kwa sauti ile ile ya chini, “ok! sawa, mimi nime tamani kukuona, nikasema niombe ruksa ili nije nikuone kidogo” nilimueleza Jessenia, kwa sauti nzito na tulivu, niliyoiweka katika mtindo wa kubembeleza, “nimesha kuwa wako tena mpenzi we niambie tu! unataka tukutane wapi” alisema Jessenia kwa sauti ambayo, ilikuwa tamu iliyolegea fulani hivi, “tukutane kituo cha mafuta, nitasimama pale kuweka mafuta” nilimuambia Jessenia, ambae alijibu kwa haraka na furaha kubwa, “sawa naingia kuoga, nikitoka nitakuambia” alisema Jessenia na kukata simu… ENDELEA