KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA: Nikamtazama vyema mwanamke huyu, ambae aliinama kuokota ule mpira na kunirushia, hakika nilitoa macho sio tu kwa mshangao, ila ni mshangao wa uoga maana mwanamke huyu alikuwa ni yule yule ambae amekuwa akininyima amani toka nimeingia hapa Pemba, ni yule mwanamke mwenye asili ya uchotara wa kiarabu na kibantu, uso wa kiarabu umbo la kibantu, mrefu wa kupendeza alievalia gauni refu rangi ya dhahabu lenye fito nyeupe na blue, zilizo haririwa kwa usanifu mkubwa, kichwani mwake alikuwa amejitanda kitambaa cheupe (hijab), na kufunika macho yake kwa miwani nyeusi, tabasamu laini alikukauka mdomoni mwake…..…….ENDELEA….
Nilidaka mpira huku najitahidi kuficha mshtuko wangu, na haraka sana niligeka na kuingia uwanja kuendelea kucheza mpira, huku nikijaribu kufanya uchunguzi wa siri kama wenzangu walikuwa wanamuona yule mwanamke, ambae mpaka mida hii nilikuwa naamini kuwa ni jinni, kama ninavyomuona mimi, ni kweli walikuwa wanamuona kama vile ninayo muona mimi, na kumbuka kuna wakati baadhi ya watu walikuwa wanamshemesha na yeye akajibu kama kawaida, “Seni, ijumaa kuna taarabu staring messi, vipi utaenda?” aliuliza mmoja kati ya vijana waliokuwepo nje, “he! We umemsikia nani kuna taarab staring mess?” aliuliza yule mwanamke ambae siku zote nilidhania ndie jini linalowamaliza watu, ambao toka nimeanza kufuatilia ni wanaume tu” inamaana jioni hii hujasikiliza redio au TV, wametangaza kutakuwa na taarab ijumaa JKU wanakuja” alisema yule jamaa ambae alikuwa anaongea nae kwa sauti ya juu, kutokana na kuwa mbali kidogo, “kama ni kweli itakuwepo basi nitaenda” alisema yule mwanamke, ambae mpaka hapo nilianza kuamini kuwa siyo jini, lakini je anaweza kuwa ndie yule ambae alipakizwa kwenye piki piki na Vuai, na kama ni yeye kwanini alimuuwa Vuai na alimuuwaje kiasi cha mtu kuonekana kuwa hakuwa na hata tone la damu kiasi cha madoctor wasomi kuamini kuwa kifo kilisababishwa na jini au hisia zangu hazipo sahihi kwamba kuna mwanamke mwingine, na sio huyu ambae anaitwa Seni, jina ambalo niliwahi kuwasikia wakina Malambo wakilizungumzia.
Nikaachana na mawazo hayo na kuendelea kucheza mpira, japo sasa nilipunguza ustadi wa kucheza, ila niliona Seni akivutiwa na uchezaji wangu, kwasababu nilimuona akipiga makofi mara kadhaa kwa kunipongeza, nilijikuta nikicheza huku nikiwaza kuhusu huyu mwana mke kwamba kweli ni mschana ambae alikuwa na dalili zote kuwa ni mwanamke wa kawaida na sio jinni kama nilivyokuwa namfikiria siku zote, kuna wakati nilijaribu kumtazama ili kujiridhisha kama bado yupo na muonekano wake ni wa kibinadamu kweli, kitu cha ajabu nilikuta na yeye akinitazama, na macho yetu yalipokutana,
aliachia tabasamu pana, ambalo kwa haraka haraka usingeweza kulitambua kuwa ni tabasamu, japo lilifanya azidi kuwa mzuri, lakini kwangu liliniogopesha, “au pengine ni jini, limechukuwa sura ya mwanamke anae fahamika, sasa linaamua kunitega” niliwaza hivyo, huku nikijitahidi kuto kumtazama mwanamke huyu, ambae alionekana kuwa ni mwenyeji sana pale uwanjani, maana alikuwa akiongeleshana na vijana wale.
Tuliendelea kucheza, huku nikiwa nimemsahau kabisa Maimuna, na kumbuka dakika kumi kabla adhana haija sikika yule mwanamke ambae alitajwa kwa jina la Seni aliondoka zake na mimi sikuacha kumsindikiza kwa macho nikiangalia jinsi alivyo jaaliwa sehemu za mgongo, yaani makalio alikuwa tofauti na waschana wa kisiwa hiki, jinsi walivyo wengi huwa na maumbo mazuri kama ya waarab, yaani wembamba ule wembamba wakuvutia, na kama ni mnene anakuwa mnene wa kuchukiza, lakini huyu mschana alikuwa na urefu wa kisukuma, tako la kinyakyusa weupe wa kichotara wakiarabu, sijui nywele maana alikuwa amezificha kwa hijab.
Ukweli nilikiona nilichohitaji kukiona, japo alikuwa amevaa gauni pana na refu, lakini bado niliweza kuona jinsi makalio yake yalivyokuwa yana tikisika kila alipopiga hatua kueleka upande wa mjini, yaani kule markiti, nilisahau kabisa kuhusu Maimuna ambae nilimkumbuka mwishoni mazoezi ni mara baada ya adhana kusikika na watu kumaliza mazoezi, huku nikialikwa kwenye mechi ya kesho mida ya jioni, na mimi sikutaka kuchelewa pale uwanjani nikichelea kujawa na hofu kama mara ya mwisho ilivyokuwa baada ya kujikuta nipo peke yangu, hivyo haraka sana nikavaa track na tisht, kisha nika kagua begi langu kama bastora yangu ipo, nilipoiona nikabeba begi langu na kuanza kuondoka, lakini kabla sijafika mbali, nikasikia “kwaheri ticha tutaonana kesho” ilikuwa ni sauti ya Maimuna, hapo nikageuka nakumuona akiwa peke yake, amesimama karibu na geti la kuingilia pale kwao, “hooooo! Mai, poa kesho bwana” niliitikia huku nikiamini kuwa kesho yenyewe ni jioni kwenye mechi, japo sikuwa sahihi,
Niliondoka zangu nikimuacha Maimuna akiingia ndani huku akionekana mwenye uso wa furaha, sikuelewa maana ya Maimuna kuwa katika hali kama ile, zaidi ya kumuona akiniingiza majaribuni, hata hivyo nilichukulia kama ni mzoea ya kawaida tu, ambayo kwa kule Tanzania bara nilisha kutana nayo mara nyingi sana, niliondoka pale kwa kukimbia kuelekea upande wa markiti, huku nikiwaona watu wakielekea msikitini, ule msikiti wa karibu na soko, nilitegemea kumuona yule mwanamke lakini sikumuona kabisa, hata nilipopita msikiti na baada ya hapo hapakuwa na watu tena nilibakia peke yangu, hivyo nikakumbuka kutoa simu mfukoni na kumpigia Mwasenga huku naendelea kukimbia kuifuata barabara kuu itokayo mkoani kwenda wete.
Simu iliita mpaka ikakatika bila kupokelewa, nikaipiga tena na wakati huo nilikuwa natokea barabarani, na wakati simu inaendelea kuita nikaweza kuliona gari la jeshi likiwa limesimama mita chache toka kwenye ile njia ninayotokea sambamba na mtu ambae alikuwa ubavuni kwa gari lile usawa wa mlango wa dereva, akiwa amekaa kwenye pikipiki aina ya Vesper, nikajuwa kwa nini hakupokea simu ni kwa sababu alikuwa amesha karibia kunifikia.
Nilipo lisogelea gari ndipo nilipomtambua yule aliekuwa ana Vesper kuwa ni bwana Ussi, kijana tajiri mwenye kula bata la nguvu, “oya kaka vipi?” aliuliza Ussi kwa maana ya kunisalimia, “fresh bro, pole sana na msiba” nilimpa pole kwa maana ya msiba wa marehemu Vuai, hapo ni kama Ussi alionyongea kidogo, “dah! ndiyo hivyo kaka kazi ya mola haina makosa” alisema Ussi kwa sauti iliyo nyongea na kujawa na huzuni, na mimi nikaona nitumie wakati huu kuuliza swali, “hivi bro unadhani ni kweli aliuliwa na yule mwanamke aliembeba kwenye pikipiki ile jana?” niliuliza kwa sauti ya kama ninahuzuni kama yeye, hapo nikamuona kama anashtuka kidogo, “hivi tulikuwa wote wakati anapita yule mwanamke?” aliniuliza Ussi, “ndiyo si ile jana mchana” nilimjibu Ussi ambae alionyesha kuhuzunika sana, “dah! yani kaka inahuzunisha sana” alijibu Ussi akiniaminisha kuwa yule mwanamke ndie muuwaji, “samahani bro, kwahiyo yule ni demu wake wa siku zote?” nilimuuliza tena Ussi, “mh! kaka unadhani jini anaweza kuwa demu wa mtu wa kudumu, yaani lile linakuteka tu akili ukilitongoza lina kukubari, sasa ole wako uende ukaligonge, una uwawa hapo hapo, yani linakukausha damu kama wa juzi” alielezea Ussi, na yeye nikagundua kuwa anaimani kuwa Vuai ameuwawa na jini, hivyo nikaona kama nikiendelea kuhoji ni kupoteza muda, hapo tukaagana na sisi tukaondoka zetu kuelekea upande wa macho mane, huku Ussi akielekea kule Msingini kule ulikotokea msiba, huku akisema kuwa baadae angeenda messi ambako kwa siku za ijumaa jumamosi na juma pili kuna kuwa na disco.
Mimi nilikuwa mmoja kati ya watu waliokuwepo messi usiku wa siku ile, ambao pia ulikuwa na watu wachache sana, ni baada ya kufika Ali Khamis camp na kuoga nikavalia jinsi na tishet, kisha nikaondoka zangu, huku nikikumbuka fedha kidogo kwaajili ya burudani, na sikuacha A. G. P -5.2mm yangu na risasi kumi, maana huwezi kujuwa ya mbele,na simu zangu mbili, saa mbili na nusu tayari nilikuwa nimesha kula pamoja na wakina Malambo, kisha nikaungana na Mwasenga kwenye ukumbi wa vinywaji, ambako kulikuwa kunapigwa music mkubwa,
kwa maana ya disco, tulichagua meza yetu na kukaa, ilikuwa kama siku iliyopita mimi ndie nilienunua vinywaji kwa Mwasenga, ambae alisema kuwa bado kwake hali haikuwa mzuri kiuchumi, “ila bro nadhani siku mbili hizi mambo yangu yatakuwa poa sana, si unajuwa tarehe zinakaribia” alijinasib Mwasenga wakati tunaendelea kupata vinywaji, huku akisisitiza kuwa nijitaidi kuhudhuria onyesho la music wa mwambao wa kisasa, yaani modern taarab.
Wakati huo tayari Ussi alikuwa amesha fika na wanamke mwingine kabisa hakuwa mmoja kati ya wale wanawake wake, “cha msingi mwanangu, tuna kamata meza yetu kabisaaa, maana tukichelewa kidogo tutakunywa bia huku tumesimama mpaka mwisho wa onyesho” alisisitiza Mwasenga, ambae nilikuwa na mtafutia nafasi nimuulize kuhusu mwanamke anaeitwa Seni, “lakini si unao watu ni wachache sana, wanaogopa jini, watakuja kweli ijumaa?” nilimuuliza Mwasenga, ambae alinihakikishia kuwa wakazi wa kisiwa hiki wanapenda sana music huo, “yani kaka hata kama ingekuwa leo lazima wangejaa, wasinge jari kuhusu jini wala nini” alisema Mwasenga, na hapo nikaona nichomeke swali langu la msingi, “enheeeee! Nimekumbuka, kuna demu mmoja anaitwa Seni unamfahamu” nilimuuliza Mwasenga nae akashtuka kidogo na kunionyesha ishara ya kukaa kimya, kisha akamtazama Ussi ambae alikuwa busy na mwanamke wake wakiwa wametandaza vinywaji mezani pao, “yani kufika tu umesha mjuwa Seni, ni mkari kinyama, yani ni demu mzuri kinoma, ni binamu yake Ussi” alisema Mwasenga ambae licha ya kuwa na sauti kubwa ya music lakini aliongea kama vile ananong’ona, nilishangaa kusikia vile, maana sikutegemea kama Seni ndie dada yake Ussi ambae amekuwa akizungumziwa, “hooo kumbe, sasa kwanini yeye anazuia dada yake kuwa na mwanaume” niliuliza kwa sauti ya chini kama yeye alivyoongea, “hapana ile si unajuwa wapemba mwanangu hawataki utani kwa dada zao, isitoshe demu mwenyewe haingiliki kizembe, hata mazowea ya hovyo hovyo hatakagi, labda kwa wapemba wenzake” alisema Mwasenga, ambae tuliendelea kupata pombe mpaka saa sita za usiku niliponunua chupa kadhaa za maji, kwaajili ya kesho jumapili, siku ambayo nilipanga kushinda ndani nikitazama movie mpaka mida ya jioni ambapo ningeenda kutazama mechi ya mpira wa kikapu kama wale jamaa walivyo niambia.******
Jumapili ilianza vizuri, kwanza kabisa niliamka saa tatu ya asubuhi, nikiwa nahisi kichwa kizito kwa pombe ya jana usiku, niliamka na kuingia bafuni kuoga nikidhania kuwa itaondoa hangover kichwani mwangu, lakini nilipomaliza kuoga nikaona bado hali ile ipo kichwani mwangu, japo ilipungua kidogo sana hivyo nikaona itakuwa vyema kama nitaenda kupata soda moja aina ya Cola, tena ya baridiiii ili inikate mning’inio, nikavaa track na tishet na chini kivaa sendo, open shoes, na kutoka pale Green house taratibu huku napekuwa simu kutazama kama kuna ujumbe au miseed call zilizoingia wakati nimelala, nashukuru sikuona sms wala messd call toka makao makuu, yaani MSC, japo kuna ujumbe mmoja ambao uliambatana na messed call ulinishangaza kidogo.
Ulikuwa ni kutoka kwa mwalimu Aisha, “naomba nikukute hapo kwako nakuja nipo njiani” nilishangaa kidogo kwa siku kama ile ya jumapili, mwalimu Aisha ambae aliwahi kunieleza kuwa ana mwanaume wake, kuja kunitembelea pale Green house, siku mjibu kwasababu sms ile haikuhitaji jibu, zaidi ya hapo niliweka simu mfukoni maana wakati huo tayari nilikuwa nimesha fika dukani, ambapo nilinunua soda ya baridi ambayo nilipoinywa ilikata hangover, na kusababisha njaa, ambayo niwazi kuwa nisingeweza kuimaliza kwa chai na mkate wa boflo, hivyo niliuliza na kuelekezwa sehemu ambayo panapatikana supu ya kuku wa kienyeji.
Dakika kumi na tano baadae tayari nilikuwa nimesha pata supu nzuri ya kuku wakienyeji yenye pili pili nyingi sana, ambayo niliamini kuwa itanizidishia hamu ya kula, ambayo ilisindikiza chapati mbili zilizotengenezwa kwa ufundi mkubwa, kisha nijkarudi Green house, ambako Aisha angeingia muda wowote, huku njiani nikiwaza kitu ambacho kilikuwa kinamleta Aisha pale kwenye makazi yangu, tena makazi ya chumba kimoja, yaani kitanda humo humo isitoshe sikuwa na uhakika wa sheria za kambi hili la kijeshi juu ya nyumba ile ya kijani, kama naruhusiwa kuleta mgeni wa kike.
Lakini wakati nakaribia pale Green House, nikamuona yule askari Koplo alienipokea kwa mara ya kwanza nilipofika hapa, akinionyesha chumba hiki, “ulikuwa wapi Ticha, bahati nzuri mlango ulikuwa wazi maana nilimkuta mgeni wako akishangaa shangaa hapa nje nikaja kukugongea, nilippona haupo nikamwingiza ndani” alisema yule askari koplo, na hapo nikakumbuka kuwa sikuwa nimeufunga mlango kwa funguo, “hoooo! asante sana kaka, lakini si hakuna noma yoyote yeye kuja hapa?” niliuliza huku najaribu kujipapasa mfukoni kuona kama ninafunguo, “hakuna noma yoyote kaka, we kale maisha” alijibu yule askari ambae leo alikuwa amevalia mavazi ya kiraia na sio sale ya kijeshi, huku anaondoka zake kuelekea upande wa maofisini na mimi nikaeleka ndani, ambako ile nakaribia mlango wa kuingilia ndani sio ule wa chumbani ni kaanza kusikia harufu ya udi, harufu ambayo hapo mwanzo hakuiacha, nikajuwa ni mwalimu Aisha ndie alieingia na hayo manukato, lakini kabla sijaingia ndani nikaona gari linasimama barabarani usawa wa pale ninapoishi, macho yangu ya umbea yakashawishika kutazama aliekuwa anashuka.
Nilichokiona moyo wangu ukalipuka kwa mshangao, ni mara baada ya kumuona mwalimu Aisha anashuka toka kwenye gari na kulipa nauli kwa kondakta, kisha akaanza kufuata uelekeo wa kuja upande wa Green messi, hapo nikahisi mapigo ya moyo yana nienda mbio, “nani atakuwa ameingia chumbani kwangu, au sio mwanamke?” ndio swali nililo jiuliza huku napiga hatua za tahadhari kuingia ndani, ambapo mlangoni nikakutana na viatu vya kike huku harufu ya udi ikizidi kunukia kwa nguvu, nikajipapasa kwa lengo la kutoa bastora yangu ndogo aina ya A. G. P -5.2mm, lakini sikuwa nayo, hapo nilitaka niachie tusi zito, lakini nilijizuia kwa kuchelea kumshtua aliekuwa ndani, lakini kwa kuwa nilikuwa na uwezo mkubwa wakupambana kwa mikono yangu nika aamua kuingia ndani, “nikafungua mlango haraka na kuingia ndani, ambako nilijikuta nimetoa macho kwa mshangao kwakile nilichokiona….. je ni nini hicho amekiona teacher Eric?