Kifo cha ghafla cha Mfugale sawa na Prof. Chachage: Kuna viashiria vyote vya kupewa sumu. Serikali ichunguze

Huelewi kilichoandikwa basi.

Hao madaktari wamesema kwene ripoti yao kwamba hakuna dalili nyingine zozote, na kwamba walichoandika ndicho kichukuliwe kama hitimisho juu ya ugonjwa huo?

COVID-19, bado ina'evolve', hakuna anayejua dalili zote na madhara yote inayosababisha kwa watu wote wanaopata ugonjwa huo.

Kwa hiyo, wewe hapo unakazania maoni ambayo hujui yanazungumzia kitu gani, na unayakomalia kweli kweli kama unavyoonyesha hapa.
Lakini hiyo si ajabu, kwa sababu unajulikana kukomalia mambo ambayo hata hayana msingi wowote, kama ule uwanja wa ndege wa Chato.
Inawezekana hukusoma hiyo paper, na kama umesioma basi inawezekena umesoma ukiwa na mindset ambayo inakufanya ushindwe kutafsiri data walizoweka pale. Ugonjwa kuendelea kuevolve ni kitu kimoja kwani kumekuwa na variants mbalimbali za virus hiyo zikijitokeza; hata hivyo variants hizo hazijabadilisha tabia ya jinsi gani mwili wa binadamau unavyorespond.
 
Mimi sitaki kutilia shaka sababu nimeshuhudia watu kufariki ghafla tu tena sana mtu mzima mara anajisikia vibaya anapoteza maisha. Shida yangu moja tu kwa yule sijui katibu mkuu aliyekuwa anasimulia tukio. Kwa mujibu wa maelezo yake kajisikia vibaya akamwambia nenda ofisini kapumzike kikao kiendelee baadae akasema ngoja nikamwangali kaenda kamkuta kwenye kitu ila wazi hali yake sio nzuri akauliza wasaidizi kimetokea nini wakasema aliomba tu AC iongezwe iwe baridi basi akakaa mpaka alivyokuja na kumkuta.

Tuseme yote ni kweli ila hivi mtu kasema najisikia vibaya utamwambia nenda ofisini na wasaidizi walichofanya kuongeza AC sio mara moja kuandaa usafiri kumpeleka Hosp au kuita huduma ya kwanza bila kusubiri mpaka katibu mkuu aje ndio aratibu magari hivi kweli goverment city hakuna hata first aid clinic?

Kwa hapo kuna uzembe mkubwa sana katika ku deal na emergency case sisemi watu hawafariki lakini kuwe na hatua za haraka za kujitosheleza unaweza kuokoa maisha ya mtu yoyote. Kwenye hili haliko sawa na sio kwa marehemu tu kwa wafanyakazi wote linaweza kutokea.
Hili hayo yote yafanyike juu ya afya ya mgonjwa ni lazima uwe na watu wa karibu wanaojua historia ya afya yako, wapo watu anasema anajisikia vibaya waliomzunguka wanampa maji kumbe ana tatizo la sukari kushuka, mwingine anapewa soda kumbe sukari yake inapanda nk.
 
Kumbe naye alikoswakoswa Kama Lisu na Mwakyembe na Kubenea.
Mkapa alivyonitoa serikalini nilimlaumu sana, lakini nikiangalia nyuma na kumkumbuka Dr. Fupi naona aliniokoa. Maana Mimi Nina kiherehere halafu siwezi kuwa YES man na kumtukuza mtu hasa nikijua namzidi elimu ama umri.
Kwa huu mstari wa mwisho unaonesha huna elimu na ni mtoto mdogo. Mtu mwenye elimu na umri wa kutosha asingeandika hivyo
 
Inawezekana hukusoma hiyo paper, na kama umesioma basi inawezekena umesoma ukiwa na mindset ambayo inakufanya ushindwe kutafsiri data walizoweka pale. Ugonjwa kuendelea kuevolve ni kitu kimoja kwani kumekuwa na variants mbalimbali za virus hiyo zikijitokeza; hata hivyo variants hizo hazijabadilisha tabia ya jinsi gani mwili wa binadamau unavyorespond.
Kwanza hata inakuwaje huu uwe mjadala hapa.

Mada inayojadiliwa ni tofauti kabisa na haya yako unayoyaleta hapa, pamoja na kwamba huna uelewa juu yake.
 
Habari wana JF.

Leo nimefuatilia live wakati Eng. Mfugale anaagwa Dar. Kwa maelezo machache ya familia, idara na wizara ni wazi kabisa Eng. Mfugale alipewa sumu.

Wito wangu kwa Serikali ifanye uchunguzi wa kina kwa kutumia vyombo na njia zote. Kwa sababu bado hajazikwa nafasi ya uchunguzi wa kina bado ipo.

Kifo cha Eng. Mfugale kimefanana kabisa na kifo cha Prof. Chachage pale Kibaha kwenye kikao.

Nina sababu nyingi za kwanini nasema hivyo, nachelea ziandika hapa kwa sababu inaweza ishia toa hints zangu (taaluma na kazi yangu). Nimefunzwa vyema maeneo hayayalehayale (sitaki toa codes).

Pia nilifuatilia vyema issues za Prof. Chachage, Dr. Mwakyembe, Dr. Omary A. Juma kwa kutaja wachache.

NB: Pia nipo JF kitambo sana; wauaji au serikali wanaweza kuja na hoja mufilisi ya ugeni wa akaunti yangu. Hii ipo kimkakati na hii ndiyo chapisho langu la kwanza.

Best Regards;
Uviko 19 in 2021.
Hawa walikula meza moja na JPM nafikiri watakwisha wote.
 
Jamaa angekuwa 40 yrs ningeungana na hoja hii ila 70 plus alikuwa anamalizia spare time tu!
 
Back
Top Bottom