Kifo cha ghafla cha Mfugale sawa na Prof. Chachage: Kuna viashiria vyote vya kupewa sumu. Serikali ichunguze

uviko19

Member
May 25, 2021
5
28
Habari wana JF.

Leo nimefuatilia live wakati Eng. Mfugale anaagwa Dar. Kwa maelezo machache ya familia, idara na wizara ni wazi kabisa Eng. Mfugale alipewa sumu.

Wito wangu kwa Serikali ifanye uchunguzi wa kina kwa kutumia vyombo na njia zote. Kwa sababu bado hajazikwa nafasi ya uchunguzi wa kina bado ipo.

Kifo cha Eng. Mfugale kimefanana kabisa na kifo cha Prof. Chachage pale Kibaha kwenye kikao.

Nina sababu nyingi za kwanini nasema hivyo, nachelea ziandika hapa kwa sababu inaweza ishia toa hints zangu (taaluma na kazi yangu). Nimefunzwa vyema maeneo hayayalehayale (sitaki toa codes).

Pia nilifuatilia vyema issues za Prof. Chachage, Dr. Mwakyembe, Dr. Omary A. Juma kwa kutaja wachache.

NB: Pia nipo JF kitambo sana; wauaji au serikali wanaweza kuja na hoja mufilisi ya ugeni wa akaunti yangu. Hii ipo kimkakati na hii ndiyo chapisho langu la kwanza.

Best Regards;
Uviko 19 in 2021.
 
Pia nilifuatilia vyema issues za Prof. Chachage, Dr. Mwakyembe, Dr. Omary A. Juma kwa kutaja wachache.
Mkuu, kwenye matukio ya hao watu, ilithibitika wazi kwamba walipewa sumu?

Ushahidi upo, au niyale yale ya semwayo mitaani?

Sina sababu za kutilia mashaka utaalam wako kama ulivyojieleza hapo juu, lakini swali langu liko wazi kabisa. Naomba ulijibu bila ya wasi wowote.

Kuna kitu hata mimi bado kinanishangaza mimi.

Inakuwaje ndugu wa marehemu wawe wanalalamika tu, huku wakikubali kwenda kumzika ndugu yao kabla ya kujiridhisha kwamba hakufanyiwa mchezo mchafu?

Ninashindwa kabisa kulielewa hili. Sasa wakishazika, wataendelea tena kulalamika?

Kwa kawaida ningetegemea, hata bila ya ndugu kuhimiza:

1. Hospitali wawe wameufanyia postmortem mwili ili kujua chanzo cha mauti yake, matatizo ya moyo, upumuaji ,n.k.; lakini sijui kama haya yalifanyika (itakuwa ni ajabu kama haikufanyika postmortem); na kwa kifo cha ghafla kama hiki, na uwezekano wa uwepo wa mchezo mchafu, ndugu nao wangekaribishwa, au wangeombwa/wangeomba awepo mwakilishi wao katika uchunguzi huo.

2. Sasa hivi, uwepo wa COVID-19, itashangaza sana, kama hapakuwepo vipimo vya COVID-19, ili kujiridhisha kwamba haikuwa sehemu ya matatizo yaliyomsababishia kifo.

3.Sampuli za damu, masalia ya chakula tumboni mwa marehemu, ndugu wangehakikisha sampuli hizo zinachukuliwa na kufanyiwa uchunguzi, chini ya uangalizi wao

Sasa sijui kama yote haya yamefanyika. Kama yamefanyika, basi kama ni sumu kapewa, kuna uwezekano ikajulikana ni sumu gani, halafu huo utakuwa ni mwanzo wa kumtafuta aliyefanya kazi hiyo.

Maelezo yaliyotolewa na wizara kufuatia kifo cha Mfugale yanaacha maswali mengi juu ya kifo chake.
 
Umesikiliza maelezo ya waziri wake? Najua ugonjwa wake uliokuwa unamsumbua muda.
Ila kilichotokea muda mfupi kabla ya yeye kufariki kitaalam hakina uhusiano wowote na kupanda au kushuka kwa lile tatizo lake.
Sijui hilo tatizo lake unalojua ni tatizo gani; lakini kwa hali ya sasa, na hili la COVID-19, ukiwa mtaalam huwezi kamwe kuhitimisha kama unavyofanya hapa.

COVID-19 ina mambo mengi sana ambayo bado hayafahamiki/hayaeleweki; huwezi ukawa mtaalam wa kuondoa hilo tatizo alilokuwa nalo, eti haliwezi kuwa sababu, huku ukijua kwamba COVID-19 inayo mambo mengi sana yasiyofahamika hadi sasa.
 
Mangula ana bahati sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe naye alikoswakoswa Kama Lisu na Mwakyembe na Kubenea.
Mkapa alivyonitoa serikalini nilimlaumu sana, lakini nikiangalia nyuma na kumkumbuka Dr. Fupi naona aliniokoa. Maana Mimi Nina kiherehere halafu siwezi kuwa YES man na kumtukuza mtu hasa nikijua namzidi elimu ama umri.
 
Wangekumaliza mapema mno!
 
Mkuu, kwenye matukio ya hao watu, ilithibitika wazi kwamba walipewa sumu?

Ushahidi upo, au niyale yale ya semwayo mitaani?

Sina sababu za kutilia mashaka utaalam wako kama ulivyojieleza hapo juu, lakini swali langu liko wazi kabisa. Naomba ulijibu bila ya wasi wowote.

Kuna kitu hata mimi bado kinanishangaza mimi.

Inakuwaje ndugu wa marehemu wawe wanalalamika tu, huku wakikubali kwenda kumzika ndugu yao kabla ya kujiridhisha kwamba hakufanyiwa mchezo mchafu?

Ninashindwa kabisa kulielewa hili. Sasa wakishazika, wataendelea tena kulalamika?

Kwa kawaida ningetegemea, hata bila ya ndugu kuhimiza:

1. Hospitali wawe wameufanyia postmortem mwili ili kujua chanzo cha mauti yake, matatizo ya moyo, upumuaji ,n.k.; lakini sijui kama haya yalifanyika (itakuwa ni ajabu kama haikufanyika postmortem); na kwa kifo cha ghafla kama hiki, na uwezekano wa uwepo wa mchezo mchafu, ndugu nao wangekaribishwa, au wangeombwa/wangeomba awepo mwakilishi wao katika uchunguzi huo.

2. Sasa hivi, uwepo wa COVID-19, itashangaza sana, kama hapakuwepo vipimo vya COVID-19, ili kujiridhisha kwamba haikuwa sehemu ya matatizo yaliyomsababishia kifo.

3.Sampuli za damu, masalia ya chakula tumboni mwa marehemu, ndugu wangehakikisha sampuli hizo zinachukuliwa na kufanyiwa uchunguzi, chini ya uangalizi wao

Sasa sijui kama yote haya yamefanyika. Kama yamefanyika, basi kama ni sumu kapewa, kuna uwezekano ikajulikana ni sumu gani, halafu huo utakuwa ni mwanzo wa kumtafuta aliyefanya kazi hiyo.

Maelezo yaliyotolewa na wizara kufuatia kifo cha Mfugale yanaacha maswali mengi juu ya kifo chake.
Hujui kuwa mfano Dr.Mwakyembe aliwekewa sumu?Unaishi wapi?
 
Back
Top Bottom