Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

Habari wapendwa wangu? Nipo ziarani huku kijijini kwetu, kwa kweli hali niliyokutana nayo huku inasikitisha sana! Familia nyingi mlo ni taabu kweli kweli, watu wana hangaika sana, maisha magumu mno kwao, kwa kifupi wamekata tamaa kabisa ya haya maisha.

Kilichonisikitisha zaidi nimekutana na baadhi ya wastaafu, maisha yamewapiga vibaya mno. Wananiambia huu ni mwezi wa sita tangu wamestaafu, lakini mafao yao hayaeleweki yatatoka lini! Jamani CCM mmefikia hatua ya kudhurumu Wazee? Mnafikiri hawa watu wanaishije? Kwanini wasipate pesa zao kwa wakati?

Mwigulu badala ya kuhangaikia kwenda Ikulu, ungepigania hili kwanza. Fanya juu chini hawa wastaafu wapate pesa zao kwa wakati, unafikiri wanaishije na hawana mishahara tena? Wewe unaweza kuishi zaidi ya mwezi bila kipato chochote?

Wamenihakikishia walifuata taratibu zote, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nyaraka zao zote kwenye ofisi za PSPF, lakini hadi leo mambo hayaeleweki tu!

Mkitaka ahueni ya maisha ya kipindi cha miaka 10 ijayo, msiichague kabisa CCM ndugu zanguni, ni waharibifu sana!!
Ukilinganisha limbukeni wa CCM wanavyoshindwa sera Za kugawa mapato ya nchi na kubaki kujigawia ukwasi kwa njia mbalimbali unaweza ukapata uchizi ghafla hasa ukilinganisha na mtanzania wa chini kabisa kijijini
 
Haa haa lini serikali hìi ya ccm inaenzi wazee? Ulizia wazee wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki, wameishia wapi? Kuna walimu wastaafu walikuwa wakifundisha kwa mkataba, pesa yao ya kumaliza mikataba yao imetafunwa na wajanja, na hao wezi wako toka hazina mpaka mawilayani. Wakihangaika kufuatilia wanaambiwa cheki zilishatoka siku nyingi, wajanja wamelamba! Ndani ya serikali hii ya ccm kila mfanyakazi wa umma anatafuta nafasi ya kudhulumu! Ccm ni janga kwa taifa!
 
CCM imeanguka ni ndoto ambayo leo naiota mara 5,nimeota Imeanguka Ktk Uchaguzi Mkuu Huu Wa Oct 2015,imesimamisha Mgombea Asiye na Political Charisma Hadi ikashindwa,ccm iliyoshindwa kulinda maisha ya albinos wanauawa as if wanaishi ktk kisiwa cha peke yao kisicho na serikali,ccm imeifanya Tanzania Kuwa Taifa La Ajabu Kuliko Yote Duniani,taifa Wa Washirikina,ushirikina Kila Kona,ushirikina Hadi Bungeni,vijana Hawana Dira Yoyote Ya Maisha,imeua Makampuni,viwanda,thamani Ya Tsh Imeporomoka Kwa Zaidi Ya %200 Ktk Miaka Kumi Iliyopita,serikali Ombaomba,ni Miaka 53 Ya Uhuru Taifa Lipo Kwenye Sifuri Kila Kitu Hadi Msaada,taifa Linasaidiwa Hadi Vyandarua,hii Ni Zaidi Ya Aibu,kwa Heri CCM Oct ndo mwisho wako.
 
Kwa kwa kwaaaaa!!! Mkajiandikishe na mkapige kura sasa. Sio mnasema tu na hampigi kura. Tunawazika rasmi mwaka huu hawa wezi
 
Nchi ambayo rais anategemea ulinzi wa sheikh yahaya haya ndo matokeo yake. Hata sheikh yahaya inategemea nguvu za albino. Nasikia lowasa kawekeza kuua albino kwa ajili ya kuusaka urais
 
ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa tanu, hatimaye ccm bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya mwalimu jk nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.

Ni ukweli usiofichika cccm na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na mgomo wa madaktari, ajali za zanzibar, suala la muungano,kilimo n.k vyote vinatabiri kifo cha ccm, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.

Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa ccm!

Na hicho ndicho kifo cha ccm 2015!

-------------------------------

r. I. P. Ccm..
 
Back
Top Bottom