Mimi kama mwananchi mwenye kuipenda nchi yangu, nasikitika kwa ninayoyaona kwa miaka hii. Na kwa haya napenda kuitahadharisha serikali kuwa Michezo yao ndio mauti yetu. Tumefikia mahali, kila kitu kinakwenda hovyo hovyo. Si elimu, si afya, si nishati, si madini, si usalama wa nchi. What the hell is going on? A bunch of overgrown teenagers are running the country into chaos, viongozi wapo wanachekelea tu. Nchi inapiga siasa, asubuhi mpaka jioni. Hata vyombo visivyo vya kisiasa na vyenyewe vimejikita kwenye siasa.
Tanzania imekuwa kama Somalia, Afghanistan! where is the government and its institutions? Nimeangalia tukio la hivi karibuni la kuhusu Lwakatare na kwa kiasi kikubwa nimeshangazwa kuwa wapo watu au kikundi cha watu walioko juu ya sheria na sheria za nchi haziwahusu wao hata kidogo.
Hivi kama polisi wangekuwa wanatenda haki, yule kiongozi wa kisiasa aliyesema ana mkanda wa video kuonyesha viongozi kadhaa wakipanga mauaji, je waliwahi kumkamata na kumuhoji? Na iweje aseme yeye halafu baada ya muda ndio video hiyo ionekane, je si yeye aliyeiweka kwenye you tube? Yeye ndiye suspect wa kwanza kwenye hili.
Naiasa serikali kuwa Michezo Yenu Ndio Mauti Yetu. Amani ya nchi ikipotea kuirudisha ni ngumu, mifano ipo mingi. Na wenzangu tunaoshabikia vitu havina mbele wala nyuma vya kutoka sijui twitter, you tube na face book, tunaofurahia na kuendeleza ubaguzi wa kisiasa, kidini, kikanda n.k hatutakuwa salama mambo yakiharibika. Hata wenye dhamana ya vyombo vya ulinzi na usalama, hamtakuwa salama hali ya amani ya nchi ikitoweka.
Oneeni huruma watoto wenu hata kama ninyi mmechoka kuishi.Tuungane kulaani kwa nguvu zote matukio ya kihuni tunayoyashuhudia kwenye nchi yetu, mauaji na mateso ya raia wasio na hatia. Upendeleo wa waziwazi wa polisi na kukosa uwajibikaji wa dhati kwa wananchi walioapa kuwalinda pamoja na mali zao. Siku moja haki itapatikana na watanzania tutarudi kuishi kwa amani tukijua sote tu sawa mbele za sheria.
Mungu Ibariki Tanzania.