Kadri siku zinavykwenda naona dalili zote za CCM kuanguka. Hakuna atakayeweza kuiokoa chama hiki kongwe. Naona anguko hilo litatokea ndani ya miaka kumi na tano (15). Watakaokingusha CCM ni wana CCM wenyewe, si vyama vya upinzani.
Zifuatazo ni dalili ya kuanguka kwa CCM
1. Upendo kati ya wanachama umekwisha, ni ugomvi usiokwisha ( Sitta camp Vs Rostam camp)
2. Fedha ni kipaumbele siyo Sera au hoja.
3. Wasemaji wa chama ni wapayukaji ( makamba, Hiza Tambwe, Sofia simba)
4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)
5. Familia ya viongozi wamekiteka chama ( Makamba's, JK's, )
6. Kampeni zimebadilika kuwa concert ( wanamuziki kibao)
7. Kununua wapinzani
8. Kukataa midahalo ( mchakato majimboni- TBC)
9. Ahadi nyingi wakati huu wakati za mwaka 2005 hazijatekelezwa ( Mikopo ya wanafunzi maisha bora kwa kila mtz n.k)
10. Chama kujadili issue binafsi zaidi badala ya maslahi ya wananchi.
CCM kwa sasa ina uwoga sana kuliko cha chama chochote hapa nchini. Wanaelewa wanakoelekea.