Katika hali ya kusikitisha na ya kuhuzunisha,ccm wapo kama hawapo kuanzia mwenyekiti,makamu mwenyekiti,katibu mkuu na viongozi wengine wandamizi pamoja na wanachama wote.Mfano,niliwahi kushuhudia KIONGOZI FULANI KATIKA CHUO KIKUU FULANI,ALIWAHI KUSEMA HIVI,WALE WANACCM NAOMBA TUONANE HAPO NJE,NILISHANGA KUSIKIA WATU WANACHEKA,nikauliza kulikoni? Watu wakasema,haaa kumbe kuna wanaccm,nikauliza kwani nini tatizo, watu(wanafunzi) wakajibu ni aibu..kwanza wanaona aibu kusema kuwa ni wanaccm,hii ni dhahiri kuwa watu kuzungumzia ccm basi yuko chumbani na mke wake na sio mbele ya kadamnasi imekuwa ni aibu na kuonekana kuwa wewe ni mshamba.
Kwanza kabisa nawapa pole kwa dhahama inayokuja ahead of you.Nikitafakari jinsi viongozi na wanachama wa ccm,wanajipa matumaini ya kushinda chaguzi zilizoko mbele yao.Hii ni hatari sana,wamekaa wamebweteka hawajishughulishi na mambo yoyote ya chama,wabunge wake wakitoka kwenye vikao Vya Bunge Dodoma ni kwenda Dar kubweteka huku wakiwasahau wapiga kura wao wakitegemea ushindi kwa kuwapa kanga,t.shirt,kofia na pombe.Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati.
Chukulieni mfano,CHADEMA wamekuwa wakizunguka nchi nzima kuongea na wananchi lakini CCM mmejiridhikia tu..mkiamini kuwa mtakuja kushinda,mnajidanganya! Inapotokea mmeshindwa ndio hapo mnaanza kurusha mabomu pamoja na kuiba kura ili muonekane kuwa ni washindi.Huu uvivu wenu wa kufikiri usituletee machafuko.Na hatuko tayari kuvumilia,yaani nyinyi mkae tu..halafu mwisho wa siku mtake kuwa washindi.Hapatatosha kwa kweli.Mabomu unipige,kesi unifungulie mwenyewe niliyepigwa,wananchi niwaelimishe mwenyewe halafu mwisho wa siku utake ushindi...nasema siku hiyo hapatatosha.
Nawashauri,japo hata kushauriwa hamtaki kwa kuwa mmevaa miwani ya mbao na kuweka pamba masikioni,zungumzeni na wananchi mjue wanataka nini,lini,wapi na kwa wakati gani..ili mtimize matakwa ya wananchi,bila kufanya hivyo mtawamaliza watu kwa mabomu yenu,watu wamepoteza matumaini kabisa.Huwezi kuwa na marketing strategies kama hujui wateja wako wanataka nini.Hapa lazima business fall down.Pili,acheni matumizi makubwa ya vyombo vya dola..kwa kuwa mnajenga chuki kati ya serikali na wananchi.Tatu,acheni siasa za matusi,kejeli na dharau kwani zinawaangusha mno.Nne,Nchemba na Nape sio brand nzuri ya chama pigeni chini.
Ni maoni yangu