Ni jambo la kusikitisha sana kuona leo CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimebadilisha sana namna ya kuendesha siasa, badala ya kutangaza sera,Kiburi cha kutawala muda mrefu na matusi majukwaani ndio zimekubalika kuwa sera halali za chama Tawala. Sasa sio jambo mbaya wala geni mahali walipo CCM wakiendesha mikutano yao ya kampeni kuwasikia watu kama Mwigulu Nchemba(MAKAMU KATIBU MKUU CCM),Livingstone Lusinde(MBUNGE-Mtera) na Nape M.Nnauye(KATIBU ITIKADI NA UENEZI-CCM) wakiporomosha matusi kwa CHADEMA na vitisho kwa wananchi. Siasa safi na Uongozi bora kwa CCM na Serikali yake vimekuwa ni bidhaa Adhimu saaana. Ndio maana wanawakumbatia watu wabovu kama Mwigulu Nchemba mtu standi wa kubuni clips feki na kuwabambikiza Akina Rwakatare, HUYU kijana sio mtu mzuri hata kidogo. JK usiposhtuka utajikuta Nchi imedumbukizwa kwenye machafuko na vurugu za kutisha, Huenda Mwigulu akikutana na JK anajaribu kumtumainisha kila wanalolipanga ni zuri na litazaa matunda ya kukisaidia CCM kubakia madarakani,NATAMKA MAPEMA KABLA HAYAJATUKIO MAMBAYA ZAIDI ya tuliyoshuhudia;Mwigulu Nchemba ni kijana ambaye asipoonywa, kudhibitiwa,kuzuiliwa,kurekebishwa na kupata maongozi mazuri na sahihi TUTAKUJA KUJUTA. Baadhi ya Viongozi wa ngazi za juu wa Serikali ya CCM wakiwemo maafisa wa Idara ya Usalama,kama hamtakuwa na njia mbadala ya makusudi ya kuwazuia Wale wanaom-remote Mwigulu ama Mwigulu kuendelea kuwa-remote ili kuweza kuikabili au kuiua CHADEMA AMANI ya Nchi yetu itabakia kuwa Hadithi . TANZANIA HAITAKUWA KISIWA CHA AMANI TENA,TUTAJIKUTA KWENYE GIZA NENE LA MAUAJI YA HALAIKI.Na kwa kauli aliyoitoa M.Nchemba kata ya Kimandolu Arusha kwamba kama WANANCHI hawataichagua CCM Watakufa. HUKO NI KUDHIHIRISHA NI JINSI GANI MWIGULU NCHEMBA NDIYE MVURUGAJI NA MTOWESHAJI WA AMANI YA TAIFA LETU.CHUNGENI SANA HII NAMBA NI HATARI KULIKO TUNAVYOAANDIKA NA KUSIMULIANA. TANZANIA NI ZAIDI YA MWIGULU NCHEMBA.