Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

bila shaka wewe umechanganyikiwa? kitendo cha ccm kutoa maoni juu ya rasimu ya katiba ni cha kawaida. subiri dr slaa arudi kwa maliberali wenzake alikoenda kupata maoni utasikia mengi

Sijachanganyikiwa na najua ccm kama chama na taasis nyingine wanayo hiyo fursa, mimi ninachosema ni ile kuchanganyikiwa ! kwani wewe ukumsikia Sitta akisema watahamasisha watu wakatae serikali 3 hata kwa kuandamana je huko si kuchanganyikiwa ?
 
Ndugu yangu umenikuna haswa! Mimi pia bado ni m-CCM ninayejiuliza maswali mengi bila majibu. Hivi ni kweli viongozi wetu ndani ya chama na serikalini bado wanaelewa nini hasa waTZ wanataka sasa? Je mawazo yao bado ni represantation ya wale wanaowaongoza? Hivi inahitaji tafiti gani kufahamu waTANGANYIKA wameshachoshwa na wadogo zao toka ZENJI kuhusu Muungano? Hivi nii kweli bado tunawaamini wenzetu wenye nchi yao, katiba yao, raisi wao, baraza lao la uwakilishi, bendera yao na wimbo wao wa taifa huku watanganyika tukikejeliwa kama wakoloni weusi ng'ambo ya bahari ya Hindi? Nafikiri anayemshangaa mzee WARIOBA tumtafakari vilivyo, pengine upstairs palishafilisika siku nying. HONGERA SANA SINDE NA TIMU YAKO
 
I real like this battle between the two rivals. To my side yangu macho
 
Hizi ni ndoto za alinacha,halafu nadhani utakuwa umetoka chooni,hivi unaweza ukazungumza kirahisi hivi na kutoa sababu mchekea hivi?!,walahi hizi siasa za Tanzania,hivi unasahau kujua kwamba CCM ndo chama tawala,hivi unasahau kwamba ndicho chama kinachoongoza nchi hii?!na ndiyo maana unaona CHADEMA wanajitahidi sana kufurukuta ili kwenda ikulu lakini hali ni tete?!,watatumia kila mbinu kuhakikisha tu wanabaki madarakani,kinachotakiwa kwa chama chochote katika nchi hii kama kinataka kuingia ikulu kuhakikisha kwamba kinakua kisafi kama theluji na si kuwa na kashafa,kama za mauaji,ugaidi,wizi wa fedha na kadhalika.
 
hizi ndoto za chagaboyz hizi! hivi ulimsikia kwa masikio yako NAPE NAUYE akitoa msimamo wa chama! au unashikiliwa akili yako na magazeti(ambayo yote yamegeuka udaku??)
nyie malengo yenu kama chama hayavuki2015
 
hizi ndoto za chagaboyz hizi! hivi ulimsikia kwa masikio yako NAPE NAUYE akitoa msimamo wa chama! au unashikiliwa akili yako na magazeti(ambayo yote yamegeuka udaku??)
nyie malengo yenu kama chama hayavuki2015

Punguza jazba ndugu yangu, kusema magazeti yote yamegeuka kuwa udaku sio sahihi, sasa tusipo amini vyombo vya habari tumuamini nani ?
 
hizi ndoto za chagaboyz hizi! hivi ulimsikia kwa masikio yako NAPE NAUYE akitoa msimamo wa chama! au unashikiliwa akili yako na magazeti(ambayo yote yamegeuka udaku??)
nyie malengo yenu kama chama hayavuki 2015 wakati CCM wana malengo ya MILLENIUM, kwenu ninyi 2015 ni kufa na kupona wakati CCM 2015 ni mwala wa uchaguzi kama chaguzi nyingine zilizopita na wataingia ktk uchaguzi wakiwa na mtaji mnono wa sera,historia na wapiga kura huku wakiutumia vizuri udhaifu wa upinzani juu ya mashaka ya UZALENDO WAO. na kwa sababu ni halika isiyo na shaka kuwa 2015 ushindi uko wazi kwa CCM! hivyo basi hilo litaenda sambamba kabisa na anguko la CDM, kwa sababu kile kinachoifanya CDM kuwa chama kitakuwa kimekosekana, binafsi sina hofu yoyote ya ushindi wa CCM bali hofu yangu ni kwamba "NI NANI MIONGONI MWA WANA CCM ATAKAYESIMISHWA"
Ili tusije tukapata raisi mwana demokrasia kama JK na kuzidi kuwapa hawa MAGAIDI nafasi ya kuiharibu hii nchi iliyobarikiwa. CCM inahitaji ichague mgombea asiyeamini katika democrasi ili kukichimbia kaburi na kukizika kabisa hiki CHAGA DEVELOPMENT MOVEMENT AGENCY
 
hizi ndoto za chagaboyz hizi! hivi ulimsikia kwa masikio yako NAPE NAUYE akitoa msimamo wa chama! au unashikiliwa akili yako na magazeti(ambayo yote yamegeuka udaku??)
nyie malengo yenu kama chama hayavuki2015

unataka kutuambia tusiamini vyombo vya habri? hata mm sijamsikia kwa maskio yangu ila nmesoma magaztini na humu kwenye mitandao.
 
ccm suala la udini mlilianza nyinyi wenyewe limewagharimu, sasa mnazungumzia ukabila oneni aibu hata kidogo, hivi hao wachaga mnaosema chama chao ni kweli ? si kweli kabisa, Ubungo wamemchagua- Mnyika, Mbeya -Sugu, Mbozi -Silinde, Maswa- Shibuda, Kigoma -Zitto, katika wabunge wote wa kuchaguliwa wanaotoka moshi ni wawili 3, na 1, Lema -Arusha

Wachaga walipata elimu mapema, wana uelewa ndio maana mabadiliko wameyapokea mapema, hutaki kuamini unaacha , ukipenda kuendelea kutoamini ni mgumu wa kuelewa
 
CCM wananishangaza sana kwenye hili la rasimu ya katiba...nimesikia wanaipeleka kwa wanachama wao waone kama wataikubali au laa....sasa najiuliza kwani wanachama wa ccm na wananchi wengine kuna tofauti...maana rasimu ni ya wananchi sasa wao wanapeleka kivipi...yaani panachnganya hapo...lakini huko CCM kuna mtu amebaki mwenye mawazo mbadala kweli kuna mtu anafikiri sawasaw au wamepanick....uwezo wao unatia shaka
 
Mkuu natamani iwe kama bandiko lako linavyosomeka,lkn sio kirahisi namna hiyo,CCM kina dola,CCM kina uzoefu na kina mbinu safi na chafu za kuweza kusaidia kujibakiza madarakani, naamini wananchi walio wengi wamechoka na hiki chama na walio wengi pia hawajui washike wapi,CCM kimeishiwa sera,wamejaribu kupandikiza udini,ukanda na ugaidi kwa CDM lkn wenye upeo na uelewa mnasema wameshindwa,je ni wangapi wanaamini kuwa wameshindwa,hakika sio wote.....wazo langu kwa CDM wakae wakijua hawana muda,kila dk kwao inatakiwa iwe ni mkakati kuelekea 2015,wapange washambuliaji wao uzuri kabisa na wahakishe hakuna namluki nadani ya chama,maana kuna watu kama shonza na wakitoka kwenye chama na kuanza uchafu huwa inakuwa ngumu sana kuukanusha......vinginevyo kazi njema sana
inafanywa na CDM na mpenda maendeleo yeyote angetamani CCM ikae pembeni 2015 kuangalia wengine wanavyoonga nchi.
 
Back
Top Bottom