Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

ni ukweli mchungu kwa ccm.leo nimeshuhudia kijana akimpa ukweli mzee wa ccm.kijana huyu aliongea kama vile anasoma comments za wanaJf.
 
Mbona CCM imeoza Kitambo!au mmemsahau yule mzee aliyesema CCM imeoza?
 
Nimechoswa sana na serikali ya CCM, wakati sasa kwa watawala na wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi kujipima wenyewe, Umma umeshachoshwa na jeshi la Polisi, pamoja na wanasiasa wachache kama Mwigullu Nchemba na wezake. Kauli ya waziri mkuu Pinda ni ya kiongozi punguani na mwenye nia mbaya na tanzania. Tusichoke wana mapindunzi ndio dalili za vyama vya ukombozi vilivyoshindwa kuwatumikia watu wake kuondoka madarakani.
 
Vyama

vingi vya siasa vilikubali utashi wa wa tz kwenye chaguzi kuu kadhaa
zilizopita.ccm inaonyesha haiko tayari,kwao ni bora taifa liishie
kwao.Sasa wanaua,kutesa,kufunga,kusingizia,nina wasi wasi wataondoka na
utaifa wetu.Wapinzani wamekuwa wakikubali yaishe,mf.wanashinda na
kuibiwa kisha wanaamriwa waende mahakamani ambako tayari hukumu inakuwa
imewatangulia,juzi ccm wametuua,wametumida risasi za moto saa 4 asubuhi
mbele ya polisi sengerema primary na hawajafanywa kitu,yangu
macho.KAMANDA MAWAZO.
 
Jibu hoja dada acha kuongea kama mlevi.

Hoja gani we kiwete wa fikra,aaah ok,kwa hiyo kwa kutambua kuwa Arusha na Moshi ndo ngome ya ya CDM ndo maana mnataka kuiua kwa kuripua mabomu...unapigaje kivuli badala ya mwenye kivuri?ueni watu wote kwanza.
 
hivi chama tawala CCM badala ya kusahihisha makosa kinapingana na wapinzani kwa maneno na hata kwa vitendo kama na wao ni wapinzani ina maana hakuna washauri ndani ya CCM au imekaaje hii.....sasa watanzania tuwaeleweje watu hawa??? mimi kama mtanzania nashauri nao wapewe upinzani 2015 ili waonyeshe umaarufu wao kiupinzani wanaoonyesha mapemaaa kabla hawajapewa sifa hiyo yakua wapinzani
 
Ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa TANU, hatimaye CCM bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya Mwalimu JK Nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.

Ni ukweli usiofichika CCCM na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na MGOMO WA MADAKTARI, AJALI ZA ZANZIBAR, SUALA LA MUUNGANO,KILIMO n.k vyote vinatabiri kifo cha CCM, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.

Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa CCM!

NA HICHO NDICHO KIFO CHA CCM 2015!

Matanga ni lini?
 
Ccm ni kama mgonjwa aliye ICU, tafakari kwa makini angalia kinachotokea sasa ndani ya ccm, chama kimeparaganyika hawako wamoja tena! Wanaogopana wanafanyiana fitina na hila, hawaaminiani! Anayeongea tofauti na wao anaoneka katumwa na upinzani hawajiamini! Wala hawaaminiki tena, CDM ndio kivuli wanachokiogopa kuliko kitu kingine chochote!!! Ishu ya mgombea urais kwa tiketi ya ccm imewafitinisha wao kwa wao, mafisadi na ufisadi ni mwiba mwingine mbaya kabisa kwao ...nk nk kwa ufupi ni suala la muda tu kabla ccm haijashuhudia anguko lake!! Natamani iwe hata kesho
 
Ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa TANU, hatimaye CCM bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya Mwalimu JK Nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.

Ni ukweli usiofichika CCCM na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na MGOMO WA MADAKTARI, AJALI ZA ZANZIBAR, SUALA LA MUUNGANO,KILIMO n.k vyote vinatabiri kifo cha CCM, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.

Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa CCM!

NA HICHO NDICHO KIFO CHA CCM 2015!

Umedata wewe, huwezi ota ndoto Kama hizi mchana kutwa. Unajidanganya sana CCM haing'oki kamwe kwa mtutu wala kwa maandamano. CCM itaendelea kuongoza kwa miaka 100 ijayo!!!!!! Tafakari chukia CDM
 
CCM haiwezi kufa labda CDM ndicho kitakuwa cha kwanza kufa tena akina hata miaka 2 Mbele yangu macho. Tusubiri kiama cha CDM coming soon!!!!!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa ccm iko mahututi na muda sio mrefu tutashuhudia anguko la ccm, sababu za anguko la ccm ni hizi
1.Uhuru waliopewa vijana hawa,Nape,Mwigulu,Shonza na Mtela hasa uhuru wa kusema chochote ndicho chanzo cha anguko lake,hawapimi kauli zao na hawajui siasa.Hii ni kutokana na kauli zao za kuropoka ambazo hata ukimwambia kichaa kuzungumza hawezi.Kauli kama hizi zina impact kubwa sana katika jamii,kwani wananchi wana reason na kujua ukweli uko wapi.

2.Kauli tata za viongozi wa chama na serikali.Hawa ni kutokana na kauli zao za kukejeli(wassira-kibanda ni nani),kuchochea mauaji(pinda-wapigeni tu maana tumechoka),na kauli hizi zinafocus kwa wananchi moja kwa moja.CCM mkumbuke kuwa mtaji wenu ni kwa wananchi kuwaletea maendeleo ya huduma za jamii,sasa mnapodharau,kutukana,kukejeli,kuua wananchi sijui mnategemea nini.

3.Matumizi makubwa ya nguvu ya dola.hapa tunaona waziri mkuu anabariki kuua raia kinyume na katiba ya nchi ibara ya 13 ibara ndogo ya 6(a),(b),(c) na (e),pia kinyume na utawala wa kisheria.Pinda akumbuke kuwa hakuna mtu anayependa kudharauliwa,kunyanyaswa,kudhalilishwa na kunyimwa haki yake.Hapa watu uvumilivu umefika mwisho.

4.Umaskini uliokithiri.Kila awamu imekuja na kila aina ya kaulimbiu ili kunadi sera,mfano MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,leo hii iko wapi? Wananchi wanahoji maisha bora yapi,mbona hatujayaona? Huku mkitamba na kujisifu majukwaani kuwa mmeleta maendeleo,kujisifu sio kazi yenu bali ni kazi ya wananchi kuwasifia.Mfano nani anatakiwa kumsifia mwenzake kati ya muuzaji(serikali) na mteja(wananchi),bila shaka ni mteja.Halafu kujisifia wakati ni wajibu wenu ni upuuzi,dharau na kejeli.

5.Udhaifu wa jk na serikali yake.Hapa tunashuhudia madudu ya kila aina kama kwa watumishi wa serikali, rushwa,ufisadi,wizi,matumizi mabaya ya madaraka,huku rais akiwachekeachekea kwa kuwa ni maswahiba wake na pengine ndio walimfanya kuwa rais.Wananchi wanahoji rais hayaoni haya?

Rais akizumgumzia basi sio kukemea,kuonya au kukaripia bali ni kulalamika.Na kulalamika ni dalili za kushindwa.

Ushauri,ccm mkitaka kuzinduka Nape,Mwigulu,Mtela na shonza wapigeni chini na/ au wafute kauli zao zinaleta picha mbaya,kwani zinachochea vitendo viovu kwa jamii na kwenye chama.Pia viongozi kama wassira,pinda,Lukuvi wawajibike kwa kujiuzulu na/ au kufuta kauli zao na kuomba radhi kwa wananchi,bila haya kufanyika ccm haitopona kamwe.
 
Na hizi kauli kama TUPO KWENYE MCHAKATO, TUNAJIPANGA, TUNATEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM, TUNAFATA UTAWALA WA SHERIA, NCHI YETU INASIFIKA KWA AMANI nk. wakati wananchi tunaona zinakwenda kinyume kabisa na matendo yao.
 
Back
Top Bottom