Katika awamu ya nne ya urais,tumeshuhudia mengi matendo ambayo kiuhalisia ni kinyume na haki za binadamu,pia ni kinyume na utawala bora.Lakini ni nani anajali?
1.Mauaji ya raia wasio na hatia
kifo cha mwangosi mkoani Iringa nidhahiri kuwa hakuna anayejali,matokeo yake ni kupandishana vyeo n.k.Mauaji ya padri Mushi huko Zanzibar ni dhahiri kuwa hakuna anayejali na kuona utu wa binadamu si lolote si chochote katka utawala.
2.Utesaji na uonevu
Hapa tunaona,jins Dr.Ulimboka na kibanda wanafanyiwa kitendo cha kinyama km kung'olewa meno na kucha,kutobolewa macho na matendo mengine ya kinyama.
Lakini hakuna anayejali,na matokeo ya waziri anasimama na kusema kibanda yeye ni nani? Hii ni dharau tosha dhidi ya utu wa binadamu na kinyume na haki za binadamu.
Kwa hiyo kuteswa kwa kibanda,hakumpi shida mzee wassira.Pia tulisikia kauli za kwamba tukio la Ulimboka ni siri ya taifa.Sasa najiuliza taifa ni nini?.Pia kauli ya Mzee Pinda ya liwalo na liwe na likawa kweli inatia mashaka.Pamoja na haya yote hakuna anayejali,wakati serikali ndiyo jukumu la kulinda raia wake.Na mengine mengi huko mtwara,morogoro,songea,Arusha nk.Yote haya ni yametokana na matumizi ya dola iliyochini ya serikali ya CCM.
3.Rushwa na ufisadi.
Matumizi mabaya ya mali ya umma,rushwa n.k pamoja na kuwa na majina ya wahusika wa rushwa na ufisadi lakin hakuna hatua zozote zilizochukuliwa juu yao.mfano The list of shame,sakata la David Jairo na ufisadi mwingi tu katika mashirika ya umma na migodi ya madini.
n.k:Lakuna anayejali.
4.Biashara ya madawa ya kulevya.Pamoja na kuwa na madai mengi juu watu wanauza madawa ya kulevya,hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hii ni kutufanya kuwa na mashaka na wahusika,inawezekana kuna usiri mkubwa unaondelea juu ya suala hili.Matokeo yake ni kuharibu kizazi cha taifa la kesho,mali waibe wao,ufisad wafanye wao,hata kizazi wakiharibu wao kwa madawa ya kulevya hii haiwezekani hata kidogo.
6.Maisha magumu.Hii inajulikana kwa kila mtanzania mwenye kujua maana ya maisha na mwenye akili timamu.Kama una akili zisizo timamu utasema tuna maisha bora,kumbe ni bora maisha n.k