Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

Sikweli kwamba CCM wanapenda Amani na Utulivu wa nchi hii kuliko vyama vingine, CCM watapenda Amani na Utulivu wa nchi hii kama utawasaidia kubaki madarakani, isipokuwa hivyo watatumia dhana ya kutoweka kwa Amani na Utulivu kama silaha ya wao kubaki madarakani! Na hiki ndo wanachofanya kwasasa kujifanya wanapenda Amani na Utulivu kuliko vyama vingine, wakitumia kila fursa wanayopata mbele ya watanzania kuwaaminisha hivyo, huku wakisahau kuwa wao ndo waanzilishi wa siasa za udini hapa nchini! Mtu huwezi kudanganywa mara mbili....
 
ccm ndo wenye dhamana ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu. vyama vingine kazi yake ni kuhakikisha amani na utulivu inatoweka ili nchi isitawalike. rejea tamko la dr slaa na mbowe juu ya kauli kuwa nchi haitatawalika. tafsiri yake ni nini?
 
Naunga hoja mkono na ukweli kuwa ccm wanatumia kigezo hicho cha amani ili waendelee kututawala na kuiba raslimali zetu.
 
Nimefurahishwa na majibu ya Msigwa ya kumruhusu Jangili-Wanted aende mahakamani kabla ya siku 21 moja alizotoa kuisha. Iwapo Jangili huyu ataenda mahakamani, na ushahidi lukuki walionao na watakaoupata Chadema kuthibitisha ujangili wa Kinana, je hicho ndicho kifo cha CCM? Nawaombeni Mwigulu na Nape mshaurini Babu yenu huyu wa kufikia, asithubutu au kujaribu kutia mguu mahakamani maana ataumbuka mchana kweupee..!
 
Ni haki yake kwenda mahakamani...let (her) go..
 
Tatizo ni kwamba nchi haina utawala wa sheria. Mahakama badala ya kuwa mahali pa kuwawajibisha watu kwa mujibu wa sheria hapa katika utawala wetu mahakama ni mahali pa kuwasafishia mafisadi na kuhalalisha ufisadi wao! Pitiable nation indeed!
 
kuna shughuli pevu 2015 ccm hawataki kutoka na wananchi hawawataki.
 
wakati fulani niliwahi kusema ccm imechokwa ila chadema haijajipanga... ni kweli kila mwenye akili timamu atakua amechoshwa na yanoyofanywa na ccm ispokuwa tu kwa wale wote wenye kufaidika na yote wanayofanya ccm,,,, CHADEMA you have to wake up wananchi tunawaamini ni kaz kwenu sasa kuunganisha uuma wa tanzania, kuweka tofauti zenu pembeni ili kuzidi kujenga imani kwa watanzania ambao wamelemewa na mzigo huu muda mrefu (CCM); Kwa kufanya hivyo ni lazma 2015 ccm watupishe.
 
Mambo inaenda haraka sana.Evolution ya mambo ni haraka sana ukilinganisha na uwezo kifikra na urasimu wa chama hiki analogia.Chama digital hakikupata shida kutumia digital.

Sasa hivi kila mazungumso ni kampeni tosha za kuondoa analogia ktk maisha ya matanzania: Sasa hivi maneno km :Magaidi, watoa kucha, poachers, magamba, viwango duni,watoboa macho, tembo dentist, tusker, wachakachuzi, wauza tembo, majangili, watupa vitu vizito.. tusker, ndovu, serikali sikivu.etc.

Chama analogia msishangae wakati manjipitisha mitaani kusikia mkishangiliwa au kuozmewa huku maneno hayo yakitoka kwa sauti kubwa huku watu wakicheka sana.Kwa ujumla mpo detached sana a watanzania, mpa na laana kubwa sana, kwa ujumla mkiongea ni kama mulugo,lusinde, mkijitetea ni kama aliyesema ni upepo tuu utapita, mkiahidi hamuaminiki pengine mlazimishe na mjikute ktk taabu ingine.

Maskini wee mtapita wapi?Mengi mfanyayo sasa hivi mnajidanganya wenyewe kuliko mdanganya mtu.Ndio maana mnachekwa tuu.
 
Nikweli kabisa sisi wananchi tumekichoka hichi cha dhalimu, wauwaji wakubwa huku wakijidai wanatutea bungeni pia ni mafsadi. Magamba wakubwa na tutawang'oa 2015
 
Nilibaki hoi nilipotonywa katika ujio wa mkubwa,uongozi wa mkoa na wilaya ulihaha kuhakikisha watu wanapiga nguo za kijani,wanachama mfu wakatuna wakidai hawawezi kuvaa kwani zinawaletea mgongano na jamii inayowazunguka.,Wakapigwa chapaa kulingana na uwezo wao,wako waliokomaa na kuvuta hadi kilo wengine nusu kilo,elfu ishirini,kumi,tano,ili mradi mbuzi ale urefu wa kamba yake ndo akavae gamba.,Kaazi,kwelikweli!!!
 
Nilibaki hoi nilipotonywa katika ujio wa mkubwa,uongozi wa mkoa na wilaya ulihaha kuhakikisha watu wanapiga nguo za kijani,wanachama mfu wakatuna wakidai hawawezi kuvaa kwani zinawaletea mgongano na jamii inayowazunguka.,Wakapigwa chapaa kulingana na uwezo wao,wako waliokomaa na kuvuta hadi kilo wengine nusu kilo,elfu ishirini,kumi,tano,ili mradi mbuzi ale urefu wa kamba yake ndo akavae gamba.,Kaazi,kwelikweli!!!

Huwa nayachukia yale marangi kweli, wakikusanyika utadhani shamba la alizeti.Nadhani ndio maana Singida watu hupata shida watambua.
 
Back
Top Bottom