Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

na waliosema nchi haitawaliki wako wapi ktk kundi hili .cdm. kamateni kwanza slaa na jopo lake ugaidi utakwisha
Mkuu unajua kama unataka kufanya maovu unachofanya kwanza ni kujifanya kuwa wewe haujui maovu yako, na ndicho wanachokifanya hawa CDM. Watanzania walifikiri kauli ya Slaa Kuwa nchi haitatawalika ni jambo dogo. Hatukujua kuwa kwa kauli hiyo maadui wa watanzania watakuwa wamefurahi sana kwa sababu wanaweza kufanya lolote na ikaonekana kuwa ni CDM, watu wa kwanza kabisa kulaumiwa endapo amani ya nchi itatoeka ni CHADEMA, hawa wanaweza kuwa wamehusika moja kwa moja ama kupitia kauli zao.
 
Ndugu wanaJF habari za wakati! Bila shaka watu wengi wanamitazamo tofauti na hali ilivyo sasa nchini kwetu lakini yote hayo yametokana na uongozi na ukilaza wa serikali ya ccm. Kilichotokea Arusha ni mseto wa vitu viwili uchochezi wa kiGAIDI na UDINI ambavyo vyote vimeasisiwa na ccm. Walibeep kuhusu udini watu wakafanya kweli wakapika haitotosha ccm wakongeza tena uchochezi wa ugaidi watu wakahamasika wakafanya kweli na ndio hayo yaliotokea Arusha. Tusubirie lile alosema mwigulu ambalo litakuwa kubwa kuliko hayo tuangalie litakuaje nafikiri hilo atakalolitoa mwigulu litatupeleka kama rwanda ya mwaka 94. Binafsi naiombe Mungu nchi hii iondokane na viongozi hawa wabinafsi pia nawapa pole wale wote walioguswa na kuthirika na uchochezi huu wa ccm.
nimeanza kuwa na wasiwasi na hqivi vyama rafiki wa vyama vya upinzani vinavyokuja kimya kimya nchini na hata kupewa fursa ya kuhutubia kwenye majukwaa ya kisiasa ni hatari sana kwa taifa letu.
 
na waliosema nchi haitawaliki wako wapi ktk kundi hili .cdm. kamateni kwanza slaa na jopo lake ugaidi utakwisha

Kauli zao zilitokana na kuwa na serikali goigoi isiyojali raia wake, pana ubaya kuambiwa hujasoma wakati ndivyo ulivyo!Uhai wa shamba ni virutubisho.
 
Mkuu unajua kama unataka kufanya maovu unachofanya kwanza ni kujifanya kuwa wewe haujui maovu yako, na ndicho wanachokifanya hawa CDM. Watanzania walifikiri kauli ya Slaa Kuwa nchi haitatawalika ni jambo dogo. Hatukujua kuwa kwa kauli hiyo maadui wa watanzania watakuwa wamefurahi sana kwa sababu wanaweza kufanya lolote na ikaonekana kuwa ni CDM, watu wa kwanza kabisa kulaumiwa endapo amani ya nchi itatoeka ni CHADEMA, hawa wanaweza kuwa wamehusika moja kwa moja ama kupitia kauli zao.

Habib na thatha sikilizeni CD ya Ilunga mjue GAIDI ni nani? Kwa nini makanisa yachomwe moto? Kwa nini wakristo wauawe?.. Msikae jamvini kutetea dini yenu tu!...
 
Source ya udini inafahamika, ni chadema na cuf, hao ndo wahusika wakubwa!
 
na waliosema nchi haitawaliki wako wapi ktk kundi hili .cdm. kamateni kwanza slaa na jopo lake ugaidi utakwisha

Ulipogombea Ubunge Kibaha haya hukuyasema, Uliponunuliwa umeanza kuuthibitisha Udini wako!.. Ugaidi huu unafanywa na nani?... Kwa nini wanauawa wakristo tu?.. Kwa nini ni makanisa tu yanayochomwa moto?.. Kwa nini viongozi wanamtaja mtu mmoja tu mkristo kwenye tukio la Arusha? Hivi ILUNGA kwenye CD yake kasema gaidi ni nani?
 
Mimi kama mwananchi mwenye kuipenda nchi yangu, nasikitika kwa ninayoyaona kwa miaka hii. Na kwa haya napenda kuitahadharisha serikali kuwa Michezo yao ndio mauti yetu. Tumefikia mahali, kila kitu kinakwenda hovyo hovyo. Si elimu, si afya, si nishati, si madini, si usalama wa nchi. What the hell is going on? A bunch of overgrown teenagers are running the country into chaos, viongozi wapo wanachekelea tu. Nchi inapiga siasa, asubuhi mpaka jioni. Hata vyombo visivyo vya kisiasa na vyenyewe vimejikita kwenye siasa.

Tanzania imekuwa kama Somalia, Afghanistan! where is the government and its institutions? Nimeangalia tukio la hivi karibuni la kuhusu Lwakatare na kwa kiasi kikubwa nimeshangazwa kuwa wapo watu au kikundi cha watu walioko juu ya sheria na sheria za nchi haziwahusu wao hata kidogo.

Hivi kama polisi wangekuwa wanatenda haki, yule kiongozi wa kisiasa aliyesema ana mkanda wa video kuonyesha viongozi kadhaa wakipanga mauaji, je waliwahi kumkamata na kumuhoji? Na iweje aseme yeye halafu baada ya muda ndio video hiyo ionekane, je si yeye aliyeiweka kwenye you tube? Yeye ndiye suspect wa kwanza kwenye hili.

Naiasa serikali kuwa Michezo Yenu Ndio Mauti Yetu. Amani ya nchi ikipotea kuirudisha ni ngumu, mifano ipo mingi. Na wenzangu tunaoshabikia vitu havina mbele wala nyuma vya kutoka sijui twitter, you tube na face book, tunaofurahia na kuendeleza ubaguzi wa kisiasa, kidini, kikanda n.k hatutakuwa salama mambo yakiharibika. Hata wenye dhamana ya vyombo vya ulinzi na usalama, hamtakuwa salama hali ya amani ya nchi ikitoweka.

Oneeni huruma watoto wenu hata kama ninyi mmechoka kuishi.Tuungane kulaani kwa nguvu zote matukio ya kihuni tunayoyashuhudia kwenye nchi yetu, mauaji na mateso ya raia wasio na hatia. Upendeleo wa waziwazi wa polisi na kukosa uwajibikaji wa dhati kwa wananchi walioapa kuwalinda pamoja na mali zao. Siku moja haki itapatikana na watanzania tutarudi kuishi kwa amani tukijua sote tu sawa mbele za sheria.

Mungu Ibariki Tanzania.

Hi Pax,

Talking like you're in my mind. Big up.
Ulichoongea hapa ni ukweli,ukweli mtupu. Ile Imani ya TANU enzi za Mwalimu inayosema kwamba NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO umeitimiza hapa.

Kwangu mimi labda kwa kuongezea tu ni wamba kwa sasa kiukweli hatuna serikali. CCM wameshapoteza mwelekeo kwasababu ya hofu ya kuondoka madarakani. Kwa hofu hiyo basi wameamua kushambulia upinzani kwa kutumia SIASA ZA MAJI TAKA kama ilivo desturi ya CCM. Issue ya Lwakatare kuhusishwa na Video fake iliyoandaliwa na Mwigulu Nchembe ni sehemu ya Mikakati hiyo michafu ya CCM kujaribu kuwachafu Wapinzani hasa CDM!

Hata juzi kukamatwa kwa Mbunge Lema baada ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha ni mbinu zilezile! Kwamba mauaji yametokea chuoni na yamefanywa na watu walioonekana wamepanda pikipiki badala ya Jeshi la Polisi kuwasaka wauaji likakimbilea kumkamata Mbunge Lema kana kwamba yeye ndo muuaji!!!Hivi ni vichekesho ambavyo vinazidi kuimaliza CCM!

Kuna matukio mengi tu ambayo tunashuhudia yakifanywa na CCM kwa mwavuli wa kisiasa ili kusambaratisha Upinzani. Tunaona Bunge linavoendeshwa KIBABE na bila shaka kwa maelekezo ya Vigogo wa CCM. Kuzima hoja za upinzani hata kama ni za msingi na zenye manufaa kwa Watanzania. Kuwasimamisha au kuwafukuza Wabunge wa Upinzani toka Bungeni kwa madai ya utovu wa nidhamu ilhali wanadai na kujadili mambo ya msingi kulingana na KANUNI!

Wabunge wa CCM wakiropoka na kutukana wapinzani hawatimuliwi Bungeni wala hawazuiliwi kuongea. Huu ni uhuni amabo hauwezi kuruhusiwa kuendelea.Watanzania wote ni mashahidi na wanaona huu ushenzi unaoendeshwa Bungeni na CCM kwa vile wao ni wengi na wana dola.

Hakika kwa upuuzi huu lazima CCM walipie.
 
Kuitabiria kifo CCM ni kama binadamu kumtabiria kifo Shetani halafu ukadhani tu kitatokea!Vilio vya waliokandamizwa,na machozi ya mnyonge,pale vitakapomfikia Mwenyezi Mungu,CCM itaanguka!na itatokea kutokana na magenge yaliyomo humo yenye uchu wa utajiri kutokana na rasilimali zetu,kutofautiana na kusalitiana!Magenge hayo,kwa sasa yanasubiri dakika za mwisho mwisho kabla ya uchaguzi.Hakika Mungu ndiye atawapigania wanyonge!Zetu dua na sala.Mungu yupo upande wa wanyonge,na wanaodhulumu na kutukandamiza,ujira wao u karibu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tumefanya uvumilivu wa hali ya juu lakini kwa kero hizi na mipango michafu ya CCM katika mchakato wa katiba mpya ya wananchi, sasa ni wakati wa wananchi wenyewe kusema kama wanataka KATIBA MPYA YA CCM au wanataka KATIBA MPYA YA WANANCHI.

Yan wan shindwa elewa nchi na wanachi wanaumuhimu gan kwako .........dei c us as stupids w agree entng dei wsh
 
Ukifuatilia mwenendo wa mambo hapa nchini kwa sasa utaona kwamba hali ya mambo si nzuri kwa chama tawala. Manung'uniko ya watumishi juu ya uduni wa maslahi yatolewayo kwao, shida za maji na umeme, wizi na ubadhirifu wa fedha za serikali bila ya hatua stahiki kuchukuliwa kwa wakosaji, kuporomoka kwa kasi kwa elimu na matokeo ya kutisha ya wanafunzi katika mitihani ya taifa, kuporomoka kwa moyo wa uwajibikaji mongoni mwa watumishi na kushindwa kuwajibishana na la mwisho migongano na migogoro mikubwa baina ya viongozi na makada maarufu wa ccm unaopelekea kugawanyika kwa chama tawala. Tuelezane kati ya sababu au matatizo niliyoyataja hapo juu unadhani ni yapi makubwa matatu yatakayohalalisha safari ya ccm kuelekea kaburini 2015?
 
kubwa ni moja tu, ufisadi na kuwakumbatia mafisadi, hilo lazima liwatoe kwenye nafasi ya kwanza na kuwa nafasi ya NNE mwaka 2015, kama unabisha utaona mfano kwenye uchaguzi wa madiwani Arusha lazima washike namba nne nyuma ya chadema CUF na TLP
 
Kulingana na yale yanayoendelea kuibuka kambi ya CCM siku za hivi karibuni, watu inabidi tukajiulize ya kwamba ni kwa nini chama tawala cha leo kifike mahala kiwe kinahangaika kushoto kulia kiasi hiki; mara

(1) kusambaza wana-CCM kote wilayani ndio wawe wajumbe wa bunge la katiba,

(2) mara uchaguzi wa watu hao msimamo wa aina mpya ya demokrasia mle ni kutokurudiwa uchaguzi,

(3) na leo hii tunasikia mambo ya muswada kubana haki za binadamu - yote haya ya nini jamani????
 
Kinachofanya CCM izidi kuporomoka ni kukimbia matatizo, chama hiki kinakwepa makusudi ukweli kuhusu matumizi mabaya ya ofisi, ubadhirifu wa mali za umma, kauli mbovu za viongozi wa chama na kudharau maoni ya wapinzani hata kwenye masuala ya msingi na yenye tija kwa taifa.
 
Hakika chama cha mapinduzi kimepoteza mvuto kwa wananchi masikini, jembe na nyundo vilivyopo kwenye bendera vimegeuzwa silaha za kuua upinzani badala ya kujenga taifa.R.I.P Chukua Chako Mapema (CCM)
 
Ukifuatilia mwenendo wa mambo hapa nchini kwa sasa utaona kwamba hali ya mambo si nzuri kwa chama tawala. Manung'uniko ya watumishi juu ya uduni wa maslahi yatolewayo kwao, shida za maji na umeme, wizi na ubadhirifu wa fedha za serikali bila ya hatua stahiki kuchukuliwa kwa wakosaji, kuporomoka kwa kasi kwa elimu na matokeo ya kutisha ya wanafunzi katika mitihani ya taifa, kuporomoka kwa moyo wa uwajibikaji mongoni mwa watumishi na kushindwa kuwajibishana na la mwisho migongano na migogoro mikubwa baina ya viongozi na makada maarufu wa ccm unaopelekea kugawanyika kwa chama tawala. Tuelezane kati ya sababu au matatizo niliyoyataja hapo juu unadhani ni yapi makubwa matatu yatakayohalalisha safari ya ccm kuelekea kaburini 2015?

Hii BIASHARA ndio inaimaliza CCM kuelekea 2015 maana ukiona hadi viumbe wa mwenyezi Mungu wanakichukia chama ujue kinaelekea shimoni.

View attachment 92860
Kinana Strikes Again
 
Mkuu unajua kama unataka kufanya maovu unachofanya kwanza ni kujifanya kuwa wewe haujui maovu yako, na ndicho wanachokifanya hawa CDM. Watanzania walifikiri kauli ya Slaa Kuwa nchi haitatawalika ni jambo dogo. Hatukujua kuwa kwa kauli hiyo maadui wa watanzania watakuwa wamefurahi sana kwa sababu wanaweza kufanya lolote na ikaonekana kuwa ni CDM, watu wa kwanza kabisa kulaumiwa endapo amani ya nchi itatoeka ni CHADEMA, hawa wanaweza kuwa wamehusika moja kwa moja ama kupitia kauli zao.
Jibu swali enyi majambazi na majangili wa CCM mtakubali kuachia ngazi? au mpaka mkombe raslimali zote na mabwana zenu mnaowaita wawekezaji? Tabia hii ndiyo itawafanya maskini wa tanzania wawafurushe kwa nguvu!! mtake msitake!!! RIP MAGAMBA RIP MAJANGILI NA MAJAMBAZI!!!!!!!!
 
Hakika chama cha mapinduzi kimepoteza mvuto kwa wananchi masikini, jembe na nyundo vilivyopo kwenye bendera vimegeuzwa silaha za kuua upinzani badala ya kujenga taifa.R.I.P Chukua Chako Mapema (CCM)
Ni kweli kabisa kabisa unachokisema, CCM wanajua kabisa kuwa hivi sasa hawana tena uwezo wa kupambana na CDM majukwaani, na ndiyo maana hivi sasa Mwigulu, Nape na Kinana,hawaishi kupanga mikakati miovu ya kutaka kuiangamiza CDM!

Kwa bahati mbaya sana kwao,na bahati nzuri sana kwa CDM,ni kuwa Mungu si Athunani, na ndiyo miti yote imeanza kuwateleza!

Walianza na CDM chama cha wachaga, WAKAFELI!

Wakaja na CDM,kuwa chama cha wakristo,mpango huo nao UKAFELI!

Hivi sasa wamekuja na CDM ni chama cha kigaidi,hoja hiyo nayo kama tilivyouslkia mahakama ya rufaa leo, WAMEIPANGUA!!

Kwa maana hiyo kwa sasa wananchi wengi watakuwa weshajua,kumbe magaidi halisi wa nchi hii ni akina Mwigulu Nchemba!!!!
 
Tumefanya uvumilivu wa hali ya juu lakini kwa kero hizi na mipango michafu ya CCM katika mchakato wa katiba mpya ya wananchi, sasa ni wakati wa wananchi wenyewe kusema kama wanataka KATIBA MPYA YA CCM au wanataka KATIBA MPYA YA WANANCHI.

Mkuu, umenena. Nchi hii inalilia mabadiliko makubwa.
 
CCM kwisha!! uovu wao unawacost mpaka wamepoteza mwelekeo. Uovu wa CCM unaitia sana aibu Tanzania. CCM imebaki kutetea tu uovu na kuiletea laana Tanzania yetu nzuri. Naomba Mungu asimame kuitetea Tanzania dhidi ya waovu wote na uovu wote uliokithiri...........
 
Back
Top Bottom