Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

CCM ni chama cha Siasa chenye heshima kubwa sana hapa barani Africa.

Ukombozi wa nchi nyingi za kusini mwa Africa umechagizwa na CCM.

Ni ujinga kufikiri kwamba CCM itakuja kutoka madarakani.

Sent from my hp EliteBook 8460p using JamiiForums
niwelevu pia kutambua kwamba kila lenye mwanzo halikosi mwisho.
 
ujikumbushe ahadi kumi za mwana tanu.
1.binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja.
(ufafanuzi;yaani walivyoishiwa walifikiri binadamu walikaa afrika peke yake)
kama kuna mwenye kituko cha tanu na ccm akiweke hapa.
 
ni ujinga mara mia kufikiria ccm itabaki madarakani milele. hakuna kisichokua na mwisho. Kanu kipo wapi?
 
CCM ilikuwa iNatetea usawa ambaokwa sasa haupo. Ilikuwa inapinga unyonyaji ambao sasa umekomaa. Ilikuwa ikikataa matabaka ambayo sasa yamejizatiti. ilikuwA inasisitiza maadiliya uongozi ambayo sasa hayapo. njia kuu za uzalishaji haziko tena mikononi mwa umma. elimu ya kujitegmea no! ujamaa kwishne! kwa hivo CCM imekufa kiitikadi na kimalengo. ikiwa Watanzania waliiuga mkono kwa mambo hayo sasa watawaiungaje mkono kam ahayo hayapo? huko ndiko kua KWA ccm
 
Udini, ukabila, ukanda, na sasa ugaidi ni propaganda ambazo zimetawala kwenye vichwa vya wanaccm dhidi ya chadema na zimekuwa zikitukera sana wanachama, wafuasi na wapenzi wa chadema huku ikiwa ni shangwe na furaha kwa ccm wakiamini kuwa chama hichi kitakufa hivi karibu kutokana na propaganda hizo

Nianze kwa kusema tu kwamba mchimba kaburi huingia mwenyewe kabla ya marehemu kuzikwa.Hivyo basi mchimba kaburi hulijua vizuri joto, mazingira na dhahama japo kidogo ya kaburi.Nianze kuzifafanua hizi propaganda za udini, ukabila, ukanda na ugaidi na ni jinsi gani zitaipeleka ccm kuzimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015

udini
Moja. Kama chadema ni chama cha udini yaani chama cha wakristo basi tunaomba wakristo wote warudi kwenye chama chao na wakipigie kura chama chao kwa misingi ya dini zao. Na kwa maana hiyo mwaka 2015 wakristo wote wakipigie kura chadema.watu hao kama wakina Pinda, Job ndugai, Mkapa, Malecela,Membe,anna makinda na wakristo wengineo

Pili. Kwasababu ndani ya chadema kuna waislamu safi kama Zitto kabwe, Prof. Safari, Mh Arfi, Mh Halima na wengine basi tunaomba waislamu wote wanaowasupport hawa makamanda wawapigie kura na kuuaminisha umma kuwa chadema siyo chama cha udini ndiyo maana kuna waislamu safi ndani ya chama. Hivyo basi mwaka 2015 kuna kundi kubwa la waislamu wanaokisupport chadema na hawaamini hii propaganda za udini watakipigia kura chadema

ukabila
Moja. Kama chadema ni chama cha kikabila basi tunaomba wachaga wote warudi kwenye chama chao na kukipigia kura chadema mwaka 2015 kwa misingi ya kabila lao. Watu hao kama Sumaye,Mama anna mkapa, Mrema na wachaga wengineo

Pili. Kwasababu kuna makabila kama wasukuma ambao wana wabunge wengi kuliko hata hao wachaga. Basi wasukuma, waha, wahehe, wafipa, wanyiramba na makabila mengine yenye wabunge wa chadema yaikomoe ccm kwa kuichagua chadema mwaka 2015 na kuionesha ccm kuwa chadema siyo chama cha kikabila ndiyo maana makabila mengine yana wabunge wengi kuliko hao wachaga

ukanda
Moja. Kama chadema ni chama cha kikanda basi tunaomba kanda ya kaskazini yote yaani Arusha, kilimanjaro mi mikoa mingine ya kanda ya kaskazini warudi kwenye chama chao na kukipigia kura chadema mwaka 2015 kwa kufuata misingi ya kanda zao

Pili. Kwasababu kuna kanda ambazo ni ngome ya chadema na haziamini kuwa chadema ni chama cha kikanda hivyo basi kanda ya ziwa yaani mwanza na shinyanga zenye wabunge wengi wa chadema, kanda ya kusini na kanda nyingine ziikomoe ccm kwa kuionesha kuwa kanda zao ndiyo zenye wabunge wengi kuliko hata hiyo kanda ya kaskazini hivyo basi chadema siyo chama cha kikanda

ugaidi
Moja. Kama chadema ni chama cha magaidi basi tunawaomba magaidi wote wakiwemo wale wa usal.... na watekaji wote warudi kwenye chama chao na kukipigia kura chadema mwaka 2015 kwa misingi ya kuwa ni chama cha ugaidi

Pili. Kwasababu kuna watanzania wengi wasioamini kuwa chadema ni chama cha kigaidi. Hivyo basi watanzania wote tusioamini kuwa chadema ni chama cha magaidi wapige kura kuichagua chadema mwaka 2015 na kutuma salamu kuwa wanaokiita chadema ni chama cha magaidi wao ndiyo magaidi ndiyo maana wanawateka wapenzi wa haki na wanaharakati wanaopinga uonevu na dhuluma ndani ya taifa hili

hitimisho
Kwa idadi hii ya wapiga kura wa chadema. Chadema itashinda kwa zaidi ya asilimia 70. Lakini hoja ya msingi hapa ni kwa propaganda hizi za udini, ukabila, ukanda na ugaidi je zinaingia akilini. Je kama tuliyempa madaraka anakuwa muongo wa kuzushia watu mambo ya mabaya je yeye atakuwa salama. Je ni kwanini anazusha mambo hayo ukizingatia kuwa yeye amekaa madarakani miaka mingi?
Basi hizo ndiyo sababu zitakazoiua ccm kutokana na propaganda za udini,ukabila,ukanda na ugaidi inayozushiwa wa chadema

Mohamed ally aliwahi kusema ukiona watu wanakusemasema sana ujue wanakuogopa na ni changamoto zinazoashilia upo karibu kufanikiwa
baada ya miaka kupita Mohamed ally alifanikiwa na kuwa the greatest boxer in the world

NAOMBA NIWASILISHE WADAU
 
labda ni kuchokwa kwa siasa na wanasiasa jijini mwetu Mbeya, mapokezi ya Mh leo hayakuwa kama enzi hizo, watu wanalazimishwa kushangilia kwa uchache wao, mabango mawili moja la bodaboda lingine la ccm vyuo vikuu, msafara wenyewe umeishia kutoa kafara tu, imetokea bonge la ajali maeneo ya nzovwe baada ya msafara wa mh kupita, sijajua bado watu wangapi wamepoteza maisha,dah
 
Chadema sio chama cha kidini, kikabila wala cha kikanda ingawa kama zilivyo taasisi nyingine kunaweza kuwa na watu wenye tabia hizo binafsi ndani ya chadema.

Hoja ya msingi ni kwamba chadema HAINA UWEZO wa kusimamia serikali.
 
Kilipewa lini serikali kikashindwa kuisimamia? Tumedhamiria kukipa serikali 2015 na hoja yako tutaipima 2020.
 
Nimekuwa nikitafakali sana juu ya mwenendo mzima wa Chama changu kilichonilea namaana CCM,kwa kutambua kiliponitoa mpaka hapa nilipo siwezi kukwepa fadhila juu ya hili
Wasiwasi wangu ni huko tuendako je kuna dalili za kupata hata nafasi ya kuonekana kwenye ya sura nzuri kwa wapiga kura wetu?
Kila kukicha tunazidi kupoteza mvuto kwa wananchi na ndiyo maana kwa mala ya kwanza nasikia chama changu kinashindwa kupata ushindi uchaguzi wa selikali ya mtaa?kibaya zaidi vijijini
Je tumeshindwa kujua ni wapi tumekosea na nini cha kufanya ili kurudisha imani kwa wananchi wetu?

Napata shida sana hata kuamini kuwa tunaowapa majukumu ya kutuongoza wana fikra gani za kutufikisha huko tuendako?

Kila kukicha ni kashfa tu na kinachonikatisha tamaa ni jinsi ya kujibu hoja za wapinzani tunatoa majibu mepesi sana ambayo ni vigumu kuaminika kwa wapiga kura wetu,

Tufikilie ni nini cha kufanya kukinisuru cham chetu bila hivyo tujiandae kufanyiwa send off na wapinzani

Hayo Ni mawazo yangu tu
 
Well said mkuu.
Mpaka kitakapojifahamu na kukubali mapungufu hapo ndipo kitakapoanza kujirekebisha. Unajua si vizuri kuamini kua kila mara wanaposema baya juu yako basi wanakusingizia kwa sababu hawakupendi. Wakati mwingine ni vema kusimamam na kujiuliza kua je ni kwanini wananisema mimi tu kila siku je ni kweli sina kosa . Hapo lazima utajiona wapi umekosea na kuanza safari upya, ndio zipo changamoto kama kuchekwa na kuzomewa lkn ukiianza upya wengi watakusifia na kuiona hekima yako badala ya kubishana tu kila siku.
Jitahidini kukodoa macho na kuziona kero za wananchi, tuna vilio vingi tu amabavyo vimesababishwa na ninyi kama mngekuwa mnatusikiliza tusingefika hapa tulipo. Tunalia na Elimu , huduma za afya na mengine mengi tu. Hivi ni kweli mmeshindwa kabisa kutatua matatizo haya na mengine .Mbona mnaweza chukueni hatua ili muweze kung'aa mbele ya wapiga kura wenu. Wanasema asiyekubali kushindwa si mshindani. Pindi mnaposhindwa kwenye chaguzi mbalimbali basi shirikianeni na alieshinda ninyi ndio wenye dola sasa msiwaadhibu wananchi kwa ushindi wa mpinzani wenu wote ninyi lengo lenu ni moja kutuvusha tufike ng'ambo salama sasa msigombanie uongozi.
 
Chadema sio chama cha kidini, kikabila wala cha kikanda ingawa kama zilivyo taasisi nyingine kunaweza kuwa na watu wenye tabia hizo binafsi ndani ya chadema.

Hoja ya msingi ni kwamba chadema HAINA UWEZO wa kusimamia serikali.

hakika wewe ni sehemu ya watu walioamua kujitoa ufahamu na kukubali kudharaulika kwa maslai ya chama ili tu tumbo lako lipate chochote
 
Chadema sio chama cha kidini, kikabila wala cha kikanda ingawa kama zilivyo taasisi nyingine kunaweza kuwa na watu wenye tabia hizo binafsi ndani ya chadema.

Hoja ya msingi ni kwamba chadema HAINA UWEZO wa kusimamia serikali.

Hivi wewe ze makopo Ni dr wa nini�� sababu sikuelewi unamaanisha nini unaposema chadema haina uwezo wa kuisimamia serekali, Si kazi ya Chama cha siasa kuisimamia serekali, hiyo Ni kazi ya bunge. Chama cha siasa kina lengo la kuchukuwa dola Na kuunda serekali Na wabunge ndo husimamia serekali itekeleze wajibu wake kwa wananchi. Sasa wewe umetangaza kuwa unania ya kuwa mbunge Na kumbe hujui majukumu ya bunge kweli unafaa wewe? Jihoji mwenyewe Mimi nakuona hutoshi Na Ni aina ya wabunge Kama akina Lusinde samahani huwa wanaanza kuita mheshimiwa.
Waachie watu makini wawe wabunge nao watatoka Chama makini Kama akina Mnyika, Zito, Mdee nq hazina zingine ndani ya chadema Chama makini umeshaikosa kura yangu.
 
Akili za bavicha hizi.
 
CHADEMA msitafute public sympathy kwa madai yenu kuwa mnasingiziwa udini, ukabila wala ukanda, kuhusu ugaidi napenda kutoongelea hilo.

Kama hayo mambo yanasemwa basi ni hisia za wananchi wenyewe na wala sio msimamo wa chama, chama cha mapinduzi hakina sababu ya kuleta propaganda za kidini wala kikabila wakati ilani yetu ya chama inasimamiwa ipasavyo na serikali.

Tunaporudi majukwaani wala hatuna haja ya kufanya siasa za majitaka kwani tuna jiamini na wananchi walio wengi wanatuamini, sasa ya nini kutumia propaganda za kukashfu wengine??
 
Tehe tehe tehe he he heee heeeee ...!!!!!!!!!!!!

Vipi Mhe 'Yote Yote' A-Z, umemaliza kilio chako?? Swali la pili liko jirani kidogo ili upate kujibiwa humu jazba mkuu????

CHADEMA msitafute public sympathy kwa madai yenu kuwa mnasingiziwa udini, ukabila wala ukanda, kuhusu ugaidi napenda kutoongelea hilo.

Kama hayo mambo yanasemwa basi ni hisia za wananchi wenyewe na wala sio msimamo wa chama, chama cha mapinduzi hakina sababu ya kuleta propaganda za kidini wala kikabila wakati ilani yetu ya chama inasimamiwa ipasavyo na serikali.

Tunaporudi majukwaani wala hatuna haja ya kufanya siasa za majitaka kwani tuna jiamini na wananchi walio wengi wanatuamini, sasa ya nini kutumia propaganda za kukashfu wengine??
 
Ni baada ya kufanya vioja na vitimbwi vingi kuhakikisha ccm inakosa mvuto kwa waTz.

Kwanza alianza kwa kuhakikisha rafiki yake kipenzi Mh.Lowassa anachafuliwa kisiasa na kutoweza kusafishika milele na kumpa uwaziri mkuu mzee wa kulialia ili serikali ya ccm ionekane dhaifu.
HATIMAE ALIFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM.

Pia alihakikisha Mh.Sitta Mzee wa ubora wa viwango na spidi ktk kuliendesha bunge hapati tena uspika,bali anapatiwa Bi.MAKINDA mama wa kuharibu na kutibua,aliyesababisha wabunge wa ccm waonekane wasiojali maslahi ya taifa na wenye matusi hadi ya ndani ya nguo.mf.Selukamba na Nkamia.
KIKWETE KAFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM

Kikwete amesababisha sherehe ya Mei mosi ndiyo iwe siku ya wafanyakazi kudai maslahi yao badala ya kuwa siku ya kupongezana na kutafakari namna bora ya kuboresha utendaji wao.
KIKWETE KAFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM

KIKWETE ndiye rais wa kwanza kusababisha serikali ya ccm kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kushitakiwa na LHRC Ktk mahakama ya ICC Kutokana na mauaji yenye utata.
KIKWETE KAIDHOOFISHA CCM

Kikwete amefanikiwa kumpa ukatibu mkuu MSOMALI KINANA JANGILI LA KIMATAIFA ili azidi kuichafua ccm mbele ya waTanzania na duniani kote. KIKWETE
AMEFANIKIWA KUICHAFUA CCM.

Kikwe....
Endelea...
 
Ni baada ya kufanya vihoja na vitimbwi vingi kuhakikisha ccm inakosa mvuto kwa waTz.

Kwanza alianza kwa kuhakikisha rafiki yake kipenzi Mh.Lowassa anachafuliwa kisiasa ingawa alijua fika kwamba Lowassa alikuwa akijiandaa kugombea urais 2015 na kutoweza kusafishika milele na kumpa uwaziri mkuu mzee wa kulialia ili serikali ya ccm ionekane dhaifu.
HATIMAE ALIFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM.

Pia alihakikisha Mh.Sitta Mzee wa ubora wa viwango na spidi ktk kuliendesha bunge hapati tena uspika,bali anapatiwa Bi.MAKINDA mama wa kuharibu na kutibua,aliyesababisha wabunge wa ccm waonekane wasiojali maslahi ya taifa na wenye matusi hadi ya ndani ya nguo.mf.Selukamba na Nkamia.
KIKWETE KAFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM

Kikwete amesababisha sherehe ya Mei mosi ndiyo iwe siku ya wafanyakazi kudai maslahi yao badala ya kuwa siku ya kupongezana na kutafakari namna bora ya kuboresha utendaji wao.
KIKWETE KAFANIKIWA KUIDHOOFISHA CCM

KIKWETE ndiye rais wa kwanza kusababisha serikali ya ccm kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kushitakiwa na LHRC Ktk mahakama ya ICC Kutokana na mauaji yenye utata.
KIKWETE KAIDHOOFISHA CCM

Kikwete amefanikiwa kumpa ukatibu mkuu MSOMALI KINANA JANGILI LA KIMATAIFA ili azidi kuichafua ccm mbele ya waTanzania na duniani kote. KIKWETE
AMEFANIKIWA KUICHAFUA CCM.

Kikwe....
Endelea...

Kwa hayo machache mh.Kikwete ameamua kuanza maandalizi ya kukabidhi ikulu kwa wapinzani.
 
Back
Top Bottom