Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

Yaani leo ndio nimeamini kwanini Charles Kenyera ameacha Majukumu yake ya msingi ameanza kusaka machangudoa.
Mleta uzi Bange zitakufanya uharishe mpaka mbele za wakubwa.
Kwani wewe ni nanii??
 
Tumefanya uvumilivu wa hali ya juu lakini kwa kero hizi na mipango michafu ya CCM katika mchakato wa katiba mpya ya wananchi, sasa ni wakati wa wananchi wenyewe kusema kama wanataka KATIBA MPYA YA CCM au wanataka KATIBA MPYA YA WANANCHI.
 
Najaribu kuangalia mwenendo wa Bunge letu linavyoendeshwa na jinsi hoja za wananchi kupitia wawakilishi wetu ambao ni wabunge zinavyojibiwa ni dhahiri wazi zinaashiria chama hiki kufikia mwisho na mfumo wake kushindwa kabisa kuongoza nchi kwa mfumo sheria na haki ya binadamu. Spika Anna Makinda anaendelea kukitengenezea chama cha mapinduzi njia ya anguko lake na yeye mwenyewe kuondoa kabisa uwezekano wa Anna Makinda kurudishwa bungeni.

Japokuwa dalili hii inaweza kuwa haimstui Spika Anna Makinda, ipo haja ya watanzania kukaa kwa pamoja ili na ikiwezekana tuiweke katika katiba yetu kuwa iwapo mbunge ataonekana kwa namna moja au nyingine anafanya kazi yake kwa kulinda au kutetea maslahi ya kikundi cha wavunja sheria au katiba kuwe na namna ambayo itakuwa wazi na mamlaka yake yawe mikononi mwa wananchi umuwajibisha mbunge huyo kama akina Anna Makinda, Jobu, na mnadhimu wa serikali nk. Hatuwezi kuona wezi na baadhi ya viongozi wakiendelea kutamba, kudhihaki na kuwabeza watanzania kwa kufanya kile ambacho wao wanaona kinawafaaa kwa mmstakabali wa maisha ya familia yao huku Taifa likiendelea kuibiwa, kuuzwa ,kuteseka na kukandamizwa na watu wachache.

Na wazi kila mtanania sasa anaelewa, anaona na anafahamu kuwa hatuwezi kwenda mbele kimaendeleo kama tutaendelea kuongozwa na chama cha mapunduzi. Hivyo basi makundi yote isipokuwa wachache ambao wanaojinufaisha kwa wizi wa mali ya umma pamoja na watoto wao. Yaani wasomi, wakulima na wafanyabiashara wote wamesubiri siku ya kuwwwajibisha ccm na vibaraka wake kwa kuwaondoa madarakani kwa aibu.

Hivyo basi ni wazi kuwa chama ch mapinduzi CCM kinazidi kujichimbia kaburi lake chenyewe kwa mgando wa mawazo na ufinyu wa fikra kikizani watanzania bado wamelala. Niwakumbushe kuwa watanzania sasa wameshaamka sio wale wanaodanganywa kuwa kudai haki ni uchichezi wala kuondoa serikali dhalimu ni uasi bali hata waliowafanya mazuzu nao pia hawakubaliana na mfumo uliop kwa sasa na wapotayari kulipigania taifa lao.
 
CCM kama chama cha siasa kimekuwa kikiendelea kuongoza taifa, sio kwa kuwa wametekeleza vizuri ilani yao,sio kwa kuwa wanasera nzuri zakiuchumi,kiafya,kielimu,kimichezo na kiutamaduni bali kwa sababu wahujumu uchumi,majangili,mafisadi na mamluki waliopandikizwa kwenye vyama vya siasa.Tokea mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini CCM imekuwa ikitumia mbinu mbali mbali kuhakikisha wanaendelea kubaki kutawala ambazo kwa sasa ni dhahiri ziko wazi na CHADEMA ni dhahiri wameweza kushinda kimkakati baadhi ya mbinu hizo.Inamaanisha uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi wa 2015 CHADEMA wameshang'amua mbinu zakukabiliana njama zote zakuondoa mfumo huu wa utawala ulioshindwa.
 
Ikiwa ccm inaelekea kufa inaonekana haitaki kufa peke yake inataka ife na roho za watanzania historia inaonyesha kwa bara la africa haya mavyama yaliyoshiliki kutafuta uhuru huwa hayatoki madarakani salama kwa haya yanayoendelea hapa nchini ni mwendelezo wa haya mavyama yaliyozeeka ki sera kwa hiyo sera yake kubwa inakuwa kuwatisha wananchi ili wawe na hofu yenyewe yaendelee kukaa madarakani sasa ni jukumu letu wananchi kuwa makini na hili lichama lililozeeka mungu ibariki tanganyika yangu asante sana
 
Naomba niwe muwazi kama serikali ya ccm ingekemea maneno ya viongozi wao kama nchemba kuhusu udini tusingefikia hapa.mlipuko arusha ndani ya kanisa mbele ya balozi wa papa ni aibu kubwa,wapi uamsho wapi sheikh ilunga sasa hili bomu la arusha lazima serikali ya kikwete ifanye mawili.1 chama kikubali makosa yote ya udini wameyaanzisha wao kuanzia wakati wa cuf.2 ccm ivunjike ili taifa lipone hapa nina maana wajitolee muhanga wamueleze kikwete waziwazi kama anataka nchi kumwachi muislamu basi ccm ife mungu ibariki tanzania na walaani wote walio nyuma ya mikakati mibaya ya taifa letu kwa maslahi binafsi.
 
Wanasiasa kutoka CCM kwa muongo sasa wameweza kwa kiasi kikubwa kupandikiza mbegu hii KWA KUTENGENEZA PROPAGANDA NA KUVISHUTUMU VYAMA PINZANI KUWA NI VYA KIDINI. CCM wanajua fika kuwa kazi ya kuchunguza udini ni ya TENDWA na anatakiwa kukifuta chama cha aina hiyo,CHA AJABU TOKA CCM waanze kuvinyoshea kidole CUF na CHADEMA hakuna chama kilichofutwa na hii inadhirisha kuwa si vyama vya kidini ila ccm ndio wanashabikia udini na kuona taifa linatumbukia kwenye mgogoro na vita ya udini.

CHADEMA NA CUF sasa wanawaeleza watanzania kuwa hizi ni propaganda za CCM, HII PIA INAWAAMUSHA CCM KUJITETEA KUWA WALICHOKISEMA NI KWELI na matokeo yake wapo wanaamini na wasioamini na matokeo yake kila mtu anafanya kwa kadri alivyoamini&uelewa wake,NA HAPA TAYARI CCM WAMELIGAWA TAIFA.

RAI YANGU
1.TENDWA AFUTE VYAMA VYA UDINI KAMA VIPO na afanye kazi yake
2.CCM wala chama kingine chochote wasinyoshe kidole kuwa chama fulani ni cha kidini mana kazi hiyo ni ya Tendwa
3.Iwe marufuku kwa chama kukituhumu chama kwa udini,ukabila na ukanda.
 
Africa ....Africa tuuu....Simba hawez kukaa na katika kundi la tembo...
 
Ndugu watanzania wenzangu,poleni na tukio la kusikitisha lililo tokea kule arusha,ni ukweli usiopingika,kwa mtanzania yoyote mwenye kumbukumbu nzuri tangu 1995 kulipo kuja chama cha nccr mageuzi,kuna kakitengo kalia nzishwa,na ccm kua kikisha kana vunja nguvu ya mh mrema,na chama chake cha nccr mageuzi,kitengo hiki kilikuja na demo ya chama cha wachaga,nakumbuka ziliwekwa video za kuonyesha machafuko na vita ya wenyewe kwa wenyewe kule rwanda na burundi,watanzania tukaambiwa majukwaani tusichague upinzani kwa kua chama chaupinzani yaani nccr kitaleta vita,kwa kweli watanzania wakakubali kulishwa dhambi hiyo,baada ya uchaguzi,na ccm kupata ushindi wakubwa wakakutana na kupongezana kwa kazi nzuri walioifanya na kukipatia chama ushindi,tukaja 2000 cuf kikapata nguvu,ccm kikawa alikalika,tena wapiga zumari wake apawakaja na demo mpya,cuf ni chama cha kidini wakiwalenga waislam,hapa napo chama kikafanikiwa kwa mara nyingine kuwalisha sumu watanzania,wakubwa wakakutana tena na kupongezana,kwa kazi nzuri na kukipatia chama ushindi,tukaja 2005 kasheshe lili anzia kwenye chama kumpata mgombea urais wa ccm,hapa lika zaliwa,genge linaloitwa wana mtandao,hapa ilikua kila anayeonekana ni hatari kwa bwana mkubwa nilazima achafuliwe,nazani wengi mnafahamu,mipasuko ndipo ilipoanza ndani ya ccm,sumu ikaanza kuwa tafuna wenyewe,hapa wanamtandao baada ya kumpata mtu wao,waka kaa chini watoke vipi kwa watanzania bara,wakaja na slogan ya [maisha bora kwa kila mtanzania] huku bara slogan iliwa levya kweli kweli,ngoma ikawa zanzibari,wanamtandao waka hamia znz na kuendelea kukishugulikia cuf,hapa cuf kikaongezewa jina chama cha kiislam na kigaidi,hapa napo wakafanikiwa kuwalisha sumu watanzania,kivumbi ikawa 2010,wanamtandao walifanya kazi ya ziada kumnasua bwana mkubwa,maana slongan yao ya [maisha bora]iligonga mwamba,sasa hapa chadema ilisha anza kukubalika,naweza kusema dozi ya sumu ilizidishwa watanzania wakanywa kama kikombe cha babu wa loliondo,chadema ni chama cha kidini kikabila na kikatoliki,hapa napo wakapenya kwa taabu sana,kama kawaida wakapongezana,bila kujua madhara ya sumu hii,sasa matunda yake ndio haya,sasa hivi kameundwa kakitengo cha itikadi na uenezi,hapa hutamkuta kpt,nape wakisaidaina na kibajaji nchemba,na new poison,kwa chadema ni chama cha ukanda ukabila na ugaidi,na vyombo vya ulinzi na usalama vinawa chekeatu,wakizidi kuligawa taifa,kwa maslai ya ccm,leo nchimbi anasema serikali aitawavumilia wanao wagawa watanzania,kwanza kabisa vyombo vya usalama vianze na nape mwigulu na kibajaji,na wanamtandao,kisha chama kitubu kwa dhambi hii,vinginevyo hatuta wahelewa,mnaibomoa tanzania kwa mikono yenu wenyewe na kusingizia vyama vya upinzani,ccm mtubu mtubu,msipo tubu dhambi hii itawatafuna,
 
Mkuu prince crown, umeongea points , lakini maccm ni sikio lililokufa ni viziwi ..hawawezi kuelewa.cha kufurahisha watanzania wa leo sio wa miaka kumi iliyopita...watu wamechoka.tunahitaji system nzima iliyowekwa na ccm itoke..tuwe na system mpya.kwa hiyo basi kwa hapa tulipofikia ccm hata waje na propaganda gani hatuwezi kuwasikiliza...it's time for them to get out..no way ni lazima tuwatoe tujaribu na chadema....so hizi sumu zao safari zitagonga mwamba.kikwete ataondoka na liccm lake no way...tumechoka!
 
Ndugu wanaJF habari za wakati! Bila shaka watu wengi wanamitazamo tofauti na hali ilivyo sasa nchini kwetu lakini yote hayo yametokana na uongozi na ukilaza wa serikali ya ccm. Kilichotokea Arusha ni mseto wa vitu viwili uchochezi wa kiGAIDI na UDINI ambavyo vyote vimeasisiwa na ccm. Walibeep kuhusu udini watu wakafanya kweli wakapika haitotosha ccm wakongeza tena uchochezi wa ugaidi watu wakahamasika wakafanya kweli na ndio hayo yaliotokea Arusha. Tusubirie lile alosema mwigulu ambalo litakuwa kubwa kuliko hayo tuangalie litakuaje nafikiri hilo atakalolitoa mwigulu litatupeleka kama rwanda ya mwaka 94. Binafsi naiombe Mungu nchi hii iondokane na viongozi hawa wabinafsi pia nawapa pole wale wote walioguswa na kuthirika na uchochezi huu wa ccm.
 
na waliosema nchi haitawaliki wako wapi ktk kundi hili .cdm. kamateni kwanza slaa na jopo lake ugaidi utakwisha
 
Ndugu wanaJF habari za wakati! Bila shaka watu wengi wanamitazamo tofauti na hali ilivyo sasa nchini kwetu lakini yote hayo yametokana na uongozi na ukilaza wa serikali ya ccm. Kilichotokea Arusha ni mseto wa vitu viwili uchochezi wa kiGAIDI na UDINI ambavyo vyote vimeasisiwa na ccm. Walibeep kuhusu udini watu wakafanya kweli wakapika haitotosha ccm wakongeza tena uchochezi wa ugaidi watu wakahamasika wakafanya kweli na ndio hayo yaliotokea Arusha. Tusubirie lile alosema mwigulu ambalo litakuwa kubwa kuliko hayo tuangalie litakuaje nafikiri hilo atakalolitoa mwigulu litatupeleka kama rwanda ya mwaka 94. Binafsi naiombe Mungu nchi hii iondokane na viongozi hawa wabinafsi pia nawapa pole wale wote walioguswa na kuthirika na uchochezi huu wa ccm.
Wa kulaumiwa hapa ni LWAKATARE, inawezekana kabisa tukio la arusha kuwa na wafuasi wake, au la basi walitekeleza matukio hayo wametumia nafasi ya kuwepo gaidi LWAKATARE. Lakini pia najiuliza kwa nini Arusha? Jimbo la LEMA, mbunge ambaye kwa takribani miezi mitano iliyopita amekuwa akiimba udini, udini, huku akikashfu imani za wengine, je na mbona baada ha tukio lile la arusha LEMA amekuwa kimya sana? Au ndo tuamini kuwa anahusika ili kuuaminisha umma kuwa aliyokuwa akiyahubiri sasa yametokea? CCM isilaumiwe katika hili hata kidogo, Midomo michafu ya wanasiasa kwa malengo ya kujitafutia umaarufu ndiyo matokeo yake haya.
 
Back
Top Bottom