Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

CCM wameamua kuachana na siasa za Analogia kwasababu zimekuwa zikiwachelewesha katika kufikia malengo yao ya kukimaliza na kukifutilia mbali chama cha HADEMA.Sasa wameamua kuja na siasa za kidigitali zaidi hii ni kuwabambikizia wapinzani wao kesi zisizokuwa na Kichwa wala miguu.
Uhalifu wowote unaotokea sasa iwe ujambazi,uvamizi wa aina yeyote iwe utekaji nyara na utesaji,Mafuriko watu wa mabondeni ,machafuko kama yaliyotokea kule Lindi na Mtwara n.k CCM hawaumizi kichwa tena zaidi ya kusema ni CHADEMA ndiyo wahsika wa kuu.

Kwahiyo napenda kuwashauri CCM kuwa wayaongezee yafuatayo katika hayo ili wakifutilie mbali chama hiki kibaki historia tu:

1. Kesi ya EPA -wahusika CHADEMA
2.Utoroshwaji wa wanyama hai- CHADEMA
3.Kiwango cha Elimu kushuka, wanafunzi kufeli -CHADEMA
4.Rushwa na Mafisadi-CHADEMA
5.Tuhuma za Kagoda,Meremeta, ufisadi UDA-CHADEMA
6Ufisadi TRL -CHADEMA NK

Mkuu umenichekesha, Hawa jamaa umewa-note vizuri. Hawana aibu hata kidogo. Kama wanasema kifo cha Mwangosi ni CDM watashindwaje kusema hayo uliyoyataja? Kilichobakia hata mafuriko ya dar mwaka juzi watasema cdm. Utaniambia tu, kuna vijana wao kutoka Lumumba kwa kazi hiyo.

Kinacho shangaza ni kuwa wao wanafikiri tzn ni ile ya '47. Zaidi wanafikiri kuficha huso wakati kiwiliwili kingine kinaoneka.
 
Nadhani upinzani wajifunze kuishi na mama wakambo,,,,,,Unapokuwa unaangalia sehemu zenye upungufu tu nakusahau kuwa kunasehemu za mema o mazuri hayo ni mawazo ya kimasikin ,,,,, Kwa sababu utasahau kuendeleza mema na kukazania mabaya..Wabunge si wa CCM tu jamani hata CHADEMA situna waona wanatetea chama chao bunge baadala ya kuwa silisha malalamiko ya majimbo yao..Tufikie wakati tuwe tuna utanzania ,Kwa taafsiri nzuri heshima, hekima ,busara na mengi yenye manufaa.TUKIANZA KUTAJA WALIO FANYA SEREKALI SIYO MADOGO KAMA TUNAVYO YA KUZA.unapo nyosha kidole kwa mwenzako jua vitatu vinakurudia..

Sasa malalamiko yatatokana na mazuri au mapungufu?
 
Duu...hayo mabilioni huwa yanazaa riba?..na je yako mfumo gani dolaz..poundz au madafuz.?
 
Naona umekosa usingizi ukaona ujifariji na post ili na wewe uonekane tu umeanzisha thread

Just imagine ata mafuriko unasema CHADEMA,shame on u,huko mnaenda mtasema jengo lile la gorofa 16 limeangushwa na CHADEMA,pamoja na magorofa yote yenye nyufa zimesabishwa na CDM,kweli mnajizika taratibu.
 
Hali ya matukio ya kisiasa kwa sasa ni kiashiria kuwa uhalisia wa misemo ya wazee wetu wa zamani kama vile ngoma ikivuma sana mwisho wake inapasuka, mfa maji haishi kutapatapa, mkataa pema pabaya panamwita inatimia kwa kupitia viongozi wa serikali ya ccm.Tukio liliotokea Arusha la kifo cha mwanachuo na jinsi uongozi wa mkoa ulivyolihandle linasikitisha sana kwa kuwa viongozi wanakuwa na kiburi kwa sababu ya kuwa na kinga ya dola ambayo hufanya kazi kwa amri za wakubwa wao ambao huzitoa hizo amri kwa hasira na fitina bila kujari taratibu za kazi. Hakuna jambo lolote chini ya jua lililokuwa na mwanzo halafu likakosa mwisho ccm kwa sasa wamepoteza mvuto na imani kwa umma na kwa sasa ni mfano wa mfa maji ambaye huwa anatapatapa kwa mbinu nyingi kama vile kutoonyesha bunge luningani kisa ni matusi ya wabunge wakati bunge huendeshwa kwa kanuni, wanaohoji na kutimiza wajibu wao kwa umma wanatolewa nje eti kwa kosa la kuongea sana. CCM tueni maji nywele mjiandae kunyolewa 2015 maana fikra za watanzania wa sasa si za enzi zile za zidumu fikra za mwenyekiti, sasa ni mfumo wa liberal politics
 
CCM walitufikirisha na kutuaminisha ule usemi usemao penye miti hapana wajenzi. mfano,serikali ilisign mikataba mbovu kisa hatuna wataalam wanasheria! watoto mashuleni wanakaa chini wakati tunamisitu ya kutosha. pamoja na maliasili zote bado TZ ni maskini! trip hii imekula kwao mura,watapiga mbizi kwenye lami
 
Matukio mbali mbali ya matumizi ya mabavu badala ya busara ya vyombo vya usalama katika serikali iliyo chini ya CCM vina kila dalili kwamba uoga wa kuondolewa madarakani na vyama vya upinzani nchini umeanza kukifanya chama tawala nchini CCM kuelekea kwenye mfumo wa ki-Nazi, kama ilivyokuwa kwa chama cha Nazi chini ya utawala wa Hitler miaka ya 1930.

Ni wazi CCM itadai kwamba haiwezi kulaumiwa kutokana na matendo ya viongozi wa serikali na dola mmoja mmoja, kutia ndani na uongozi wa Bunge, Usalama wa Taifa, Polisi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Mawaziri, nk, lakini jambo la kukumbuka ni kwamba hawa viongozi wa serikali na dola wanafanya haya kwa lengo la kuifurahisha CCM, na CCM kwa upande wao wanafurahia matendo ya ki-Nazi yanayofanywa kwa niaba yao, hata kama CCM kama chama hakijatoa maelezo ya moja kwa moja au kuwatuma wakayafanye. Na mbaya zaidi ni kwamba kumekuwa na tetesi nyingi kwamba viongozi hao wa dola na serikali wanafanya wanayofanya kwa maagizo ya CCM.

Chama cha Nazi pale Ujerumani kilianzishwa kama chama cha kawaida cha kisiasa kama ilivyo tu kwa CCM, lakini taratibu killingiwa na kirusi kibaya na kikaanza kukandamiza vyama vingine vya siasa na wananchi wa kijerumani, na hatimaye kuja kuwa janga la kimataita. Hatutegemei CCM kuja kufikia kiwango cha kimataifa kama chama cha Nazi cha Ujerumani miaka hiyo ya 1930, lakini kwa hali ilivyo sasa hapa nchini ni rahisi mtu yeyote kukata kauli kwamba CCM imeanza kuonyesha kila dalili za ugonjwa wa u-Nazi.
 
Kuna taifa moja hapa duniani linakabiliwa na utawala wa kishetani!Katika taifa hilo watu wanaopigania haki na usawa wanakamatwa, kuteswa, kunyanyaswa, kubambikiziwa kesi na kufanyiwa kila aina ya dhuluma, uonevu na udhalilishaji!

Hata hivyo, katika taifa hilo wezi wa mali ya Umma, mafisadi na wahujumu uchumi wanalindwa na kutetewa kwa gharama yoyote ile na hata kuombwa warudishe fedha walizoiba! Eti tunaambiwa watu hao kushitsakiwa ni hatari kwa mustakabali wa taifa! Ila cha ajabu katika nchi hiyo, fanya jambo lolote la kizalendo lisilowapendeza watawala uone nguvu itakayotumika kukukamata!

Watawala hawa wanapaswa kujua kuwa kuna wengi walipita kabla yao na sasa wamebaki raia wa kwaida tu na waombe utawala wa nchi hiyo ubaki wa chama chao jambo ambalo dalili zote zinaonyesha kuwa ni vigumu kama ilivyo kwa "Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano"

Nyanyaseni watu ila mwisho wenu unakuja na haijalishi itachukuwa muda gani kwani kumbukumbu zipo na haziwezi futika wala kufutwa.
 
Anzia kwenye list of shame, EPA, Twiga, Meno ya tembo, mikataba...uwiiiiiiiii, Mungu shuka uone dhuluma, bustani yako innajisiwa.....
 
Nimeipenda,
Ni heri vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu.
 
"In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU." - Julius Kambarage Nyerere, 1968.

Baada ya TANU kushindwa kutekeleza mambo iliyo waahidi Wa-Tanganyika kwa kipindi kile,ili declare failure na kuruhusu vmfumo wa vyama vingi.

ANGALIZO
zaidi ya asilimia 95 ya members wote waliokua TANU walihamia CCM nakuendelea kufuata njia zile zile TANU ilizopita

kwa maneno marahisi kabisa - CCM ni chama kilichokua kimekufa kabla hata ya kuzaliwa
- CCM ilishashindwa kutekeleza majukumu yake kwa WATANZANIA toka zamani.
 
hawa mashet..ani waliokamatwa na video wakipanga ushe...tani lazima tuwalaani kwa pamoja
 
wabaya sana hawa, wanatembea na sumu mchana kweupe ili wawalishe wenzao
 
Acha mafumbo, sema Tanzania kuna utawala wa ki***ni, unaficha nini wewe? Anzia kwenye list of shame, EPA, Twiga, Meno ya tembo, mikataba...uwiiiiiiiii, Mungu shuka uone dhuluma, bustani yako innajisiwa.....

Nimependa alivyoanza. Uandishi wa aina hii unafaa sana kutumika katika uandishi wa vitabu katika nchi kama Tanzania. Ujumbe umefika. It's only through fiction that one can tell a hard truth.
 
Hizi nchi za namna hii zipo nyingi hapa duniani hasa huku barani Afrika.

Ila hapo naona umekusudia Tanzania yetu mkuu, na hii ni kweli wala hujakosea japo ulivyoandika wengine wanaona kama unatumia lugha ya kificho vile, lakini ujumbe unafika tu maana pamoja na ushetani wao wanauelewa wa kujua watu wanachosema kama ulivyosema wewe hapo juu kwenye andiko lako.

Tanzania na utawala wa shetani.
 
Mm sina chama, lakini kila ninayekutana naye hataki
sikia kuhusu CCM, kila mtu CHADEMA CHADEMA CHADEMA; mpaka sasa hivi
nikikutana na mtu hata kama simjui na assume ana sura ya
ki-CHADEMA, kudadeeeeeeeeeeki mamangi ni noma
 
Back
Top Bottom