Kifo cha Andrew Sanga, What is next?

Kifo cha Andrew Sanga, What is next?

Heshima nyingi sana kwa wanajamvi wote wa JamiiForums.
Salaamu,

View attachment 346018
Tumemzika andrew aliyeuawa kikatili marekani je nini kinafuata? au itakuwa kama ilivyo kawaida yenu kuficha taarifa za mauaji kama mlivyofanya kwa watanzania wengine (waliochomwa visu, waliochomwa moto, n.k n.k)?

Wakuu Nimekuja kwenu kwa heshima na taadhima kuwaomba watanzania wote wanaoishi houston kutoa taarifa zozote muhimu wanazozijua juu ya mauaji ya mtanzania mwenzetu, kijana mwenzetu, mzazi mwenzetu na zaidi ya yote mhanga wa maisha ya ughaibuni.

Hata kama unaogopa kufanya hivyo fanya kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya nchi yako Tanzania, na yule mwanaye ambaye amempoteza mtu muhimu katika maisha yake.

Kwanini nimeileta JamiiForums?

1. Aliyepigwa risasi ni mtanzania hivyo basi ni jambo jema kuwa mzalendo na kutoa taarifa zitakazopelekea kupatikana kwa haki.

2. Watanzania wengi wameuawa vifo vya kikatili kama hivi huko Marekani ila watanzania hata wale ambao wana taarifa za wahusika waliamua kukaa kimya kuwalinda wauaji. Kumbuka leo ni Andrew kesho inaweza kuwa wewe. Tena bora ya Andrew amepata wa kumsafirisha akazikwa kwao, wewe unaweza usipate hata wa kulipia jeneza lako lije Tanzania uombolezwe na nduguzo. Hivyo basi kupatikana kwa wauaji ni njia moja wapo ya kutuma salamu kwa wengine wenye nia ya kujeruhi au kuua kwamba hakuna atakayewafichia siri.

3. Kulingana na taarifa ya Alex wa Swahili tv ni kwamba Andrew alipigwa risasi eneo ambalo palikuwa na watu meaning kwamba hakuwa peke yake. Anaendelea kusema kwamba watanzania waliokuwepo eneo la tukio walimuona muuaji na wanamjua iweje leo waamue kukaa kimya? Na yule jamaa aliyemuokota na kumpatia pumzi kama first aid baada ya kushutiwa na kuanguka chini na yeye ameamua kukaa kimya? Kama mnampenda Andrew kama mlivyojiliza na kama alivyokuwa anawanunulia bia na kuklia bili zenu basi ninawaomba mumtetee leo kwa kutoa taarifa zitakazopeleka kupatikana kwa muuaji kwa kuwa hawezi kujitetea yeye binafsi.

4. Taifa limepoteza nguvukazi ya taifa (hata kama alikuwa hafanyi kazi Tanzania bado alikuwa anatuma remittances ambazo zilichangia kukua kwa uchumi wetu) hivyo basi ninawaomba moderator muuache huu uzi hapa ili kwamba mwenye taarifa yoyote kuhusu hili tukio aiweke hapa na mwisho wasamaria wema waweze kuzipeleka kwa vyombo vya dola vya marekani.

5. Ubalozi wa Tanzania Marekani uweze kuona na kuchukua hatua haraka. Balozi zetu zimekuwa zikikaa kimya mauaji kama haya yanapotokea tumechokaaaaaa na ukimya wenu. Mmnatumia kodi za nchi kwa kazi mnazoitiwa huko ubalozini sasa kwanini mnashindwa kuwatetea watanzania ughaibuni? Kwanini mnashindwa kusimama kama wakala wa Tanzania Marekani mhakikishe raia wenu wanapata haki zao?

Tutazika ndugu zetu kwa vifo vya kinyama kama hivi hadi lini bila haki na sheria kuchukua mkondo wake? Ubalozi kazi zake sio tu kuandaa maonesho ya utalii bali kusimama bega kwa bega kwenye masuala kama haya.

Mwisho kabisa ninawaomba kutoka moyoni mwangu jitoeni mpeleke taarifa ili haki itendeke kwa ajili ya mtanzania mwenzetu. Juzi ile alikuwa mazula, juzi kati jamaa aliyechomwa kisu na mtanzania mwenzake, leo ni andrew kesho nani ajuaye yaweza kuwa wewe au ndugu yako.

Usipochukua hatua usifikiri kwamba hata wewe utakuwa salama.
#justiceforandrew

Bongo bhana kila mtu anakuwa maarufu huyu naye (Marehemu, ,,Apumzike kwa Amani") ati ni maarufu ukiuliza kafanya nini kupata umaarufu eti alikuwa anawanunulia watu bia na kulamba mademu wakali, na watoao sifa hizi wanaishi first World country, Duh!
 
Kwani sifa za kua "mtu maarufu" ni zipi mkuu?
 
Kwani sifa za kua "mtu maarufu" ni zipi mkuu?

Inategemeana na jamii husika, kuna nyingine mtu maarufu ni Mwanasayansi mgunduzi, Mhandisi au labda Daktari aliyeokoa maisha ya binadamu kuna wengine kama sisi mtu maarufu ni mwenye mademu wengi na ambaye hutununulia ulabu!
 
Nchi nyingine watanzania wanaishi kama wakiwa. Balozi zina kazi ya kutuma maombi ya passport uhamiaji dar na kutengeneza madili wakati mambo ya msingi wameyakalia kimya.
Ni kweli mkuu yaani mpaka aibu, kuna maafisa wa ubalozi bila aibu kabisa wanapiga vijisenti vya ndugu zao huko majuu ili wawape pasi za kusafiria tu...
 
sidhani ..alikufa 2pac mpaka leo muuaji wake hajulikani....Waafrica wanaonekana mbwa tu Marekani
 
Duu inauma kweli.. Ndio mzee wa mabebizzzz lemutuz aliamua kujirudia tu home japo napo kageuka baba swaleheeee
 
kibebi Kutotoa taarifa polisi sio tatizo la wabongo tu, ni tatizo la karibu jamii ya watu wote weusi wanao ishi Marekani. Wanaita " ANTI- SNITCHING CAMPAIGN". 50 Cents baada ya kupigwa risasi tisa, aliulizwa na polisi " Unawajua walio kushoot?' akasema " NAWAJUA!". Unaweza kuwataja ? Akasema HAPANA! Suge Knight aliulizwa " Kama ungewajua walio muua Tupac, je ungewataja ? Jibu lake likawa HAPANA!. Kibaya zaidi kama aliye muua marehemu ni mnugu ( Niga) au Okata kama wanavyoitwa na wawest, tena wa kutoka maghetoni ( Thug )kwa sababu hawa jamaa ni washenzi sana na hakuna kitu wanakipenda kama kusikia mtu mweusi anashirikiana na polisi kwenye kesi ambayo mshukiwa ama mtuhumiwa ni mtu mweusi. Wanakushoot fasta. Hata 50 Cents sababu hasa ya kupigwa risasi tisa hiyo mwaka 2000, alifanya kitu wanaita " DRY SNITCHING" kupitia wimbo wake ukiitwa " GHETTO QURAN" . Humo alitaja majina ya drug dealers maarufu wa mitaa ya Jamaica Queens . So ni vigumu sana kwa wabongo kuonyesha ushirikiano katika hilo.
 
Easy....hapo prosecuting attorneys watapinga hiyo line of questioning na most likely kama key witnesses ni illegals basi wanaweza kupewa immnunity flani ili kuwezesha kesi ya upande wa mashtaka.

Objection your honor!
...,,,sustained........overruled
 
kibebi Kutotoa taarifa polisi sio tatizo la wabongo tu, ni tatizo la karibu jamii ya watu wote weusi wanao ishi Marekani. Wanaita " STOP SNITCHING CAMPAIGN". 50 Cents baada ya kupigwa risasi tisa, aliulizwa na polisi " Unawajua walio kushoot?' akasema " NAWAJUA!". Unaweza kuwataja ? Akasema HAPANA! Suge Knight aliulizwa " Kama ungewajua walio muua Tupac, je ungewataja ? Jibu lake likawa HAPANA!. Kibaya zaidi kama aliye muua marehemu ni mnugu ( Niga) au Okata kama wanavyoitwa na wawest, tena wa kutoka maghetoni ( Thug )kwa sababu hawa jamaa ni washenzi sana na hakuna kitu wanakipenda kama kusikia mtu mweusi anashirikiana na polisi kwenye kesi ambayo mshukiwa ama mtuhumiwa ni mtu mweusi. Wanakushoot fasta. Hata 50 Cents sababu hasa ya kupigwa risasi tisa hiyo mwaka 2000, alifanya kitu wanaita " DRY SNITCHING" kupitia wimbo wake ukiitwa " GHETTO QURAN" . Humo alitaja majina ya drug dealers maarufu wa mitaa ya Jamaica Queens . So ni vigumu sana kwa wabongo kuonyesha ushirikiano katika hilo.
Sababu zako hazina mashiko kwa sababu kutoa info ya uhalifu sio lazima uji-expose. Kama una inside information unaweza kutumia njia za panya na polisi wakajua undani wa issue na wakaanzia hapo kufanya uchunguzi.
 
Criminals are very smart my brother. Watafatilia na watajua tu nani kawachoma!
 
Criminals are very smart my brother. Watafatilia na watajua tu nani kawachoma!
Mkuu siku hizi kuna njia nyingi sana na si lazima uende physically kituoni. Kwa mfano internet ni njia nzuri kabisa na unaweza kutumia public computer ukaandika kila kitu kwa kurefu na kuwaachia polisi kumalizia. Mimi hii thread imenifanya niamini kuwa watanzania tuna matatizo makubwa kama kweli kuna wanaojua muuaji na wakaogopa kumtaja. Ingekuwa Tanzania ningeelewa lakini sio Marekani. Bado siamini kama ni kweli kuna mtu anayejua muuaji wa huyo jamaa na akaogopa kumtaja.
 
kibebi Kutotoa taarifa polisi sio tatizo la wabongo tu, ni tatizo la karibu jamii ya watu wote weusi wanao ishi Marekani. Wanaita " STOP SNITCHING CAMPAIGN". 50 Cents baada ya kupigwa risasi tisa, aliulizwa na polisi " Unawajua walio kushoot?' akasema " NAWAJUA!". Unaweza kuwataja ? Akasema HAPANA! Suge Knight aliulizwa " Kama ungewajua walio muua Tupac, je ungewataja ? Jibu lake likawa HAPANA!. Kibaya zaidi kama aliye muua marehemu ni mnugu ( Niga) au Okata kama wanavyoitwa na wawest, tena wa kutoka maghetoni ( Thug )kwa sababu hawa jamaa ni washenzi sana na hakuna kitu wanakipenda kama kusikia mtu mweusi anashirikiana na polisi kwenye kesi ambayo mshukiwa ama mtuhumiwa ni mtu mweusi. Wanakushoot fasta. Hata 50 Cents sababu hasa ya kupigwa risasi tisa hiyo mwaka 2000, alifanya kitu wanaita " DRY SNITCHING" kupitia wimbo wake ukiitwa " GHETTO QURAN" . Humo alitaja majina ya drug dealers maarufu wa mitaa ya Jamaica Queens . So ni vigumu sana kwa wabongo kuonyesha ushirikiano katika hilo.
Asante kwa "ilm" mnugu Likud.
 
Kwahiyo kwa maaelezo yako ina maana wabongo au niseme marehemu alikuwa anaishi gheto Amerika???!
 
Kwahiyo kwa maaelezo yako ina maana wabongo au niseme marehemu alikuwa anaishi gheto Amerika???!

Sijui kama alikuwa anaishi Ghetto au Lah, ila walio mshoot, kwa vyovyote vile watakuwa na vinasaba vya maisha ya ghetto.
 
Heshima nyingi sana kwa wanajamvi wote wa JamiiForums.
Salaamu, Usipochukua hatua usifikiri kwamba hata wewe utakuwa salama.
#justiceforandrew

Poleni kwa msiba, kwa kweli inauma mno, tunatumaini mtapata nguvu muwekeze mrudi, ikishindikana rudini tu hivyo hivyo, huku nyumbani, kwenu ni kwenu hata kama hakuna ma burgers, blonds au la..
Tumeshuhudia wenzetu wa kibongo wakinyanyaswa hata kule India, achana na the West..rudini tuijenge nchi yetu, twawasubiri kwa hamu, kwenu ni kwenu hata iweje wandugu zetu...
 
Kwa nini nyie mlio huko kwenye community zenu msijipange mkatafuta private detective akafuatilia suala lenu. Kwa sababu nchini kwenu zaidi ya watu 10,000 wanauwa kwa kupigwa risasi kila mwaka sasa Idadi hiyo ni kubwa Na sio rahisi vyombo vya usalama kufuatilia step by step hadi mwisho bila nyie ku push.
 
Mkuu siku hizi kuna njia nyingi sana na si lazima uende physically kituoni. Kwa mfano internet ni njia nzuri kabisa na unaweza kutumia public computer ukaandika kila kitu kwa kurefu na kuwaachia polisi kumalizia. Mimi hii thread imenifanya niamini kuwa watanzania tuna matatizo makubwa kama kweli kuna wanaojua muuaji na wakaogopa kumtaja. Ingekuwa Tanzania ningeelewa lakini sio Marekani. Bado siamini kama ni kweli kuna mtu anayejua muuaji wa huyo jamaa na akaogopa kumtaja.

Kama witness hana makaratasi lazima aogope kusombwa na ICE
 
Back
Top Bottom