Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,665
- 25,689
umaarufu wake ulitokana na nini sana huko USA ..?
Mkuu, kwani wewe siku ukijikuta unaambiwa unaitwa Almaarufu fulani hivi utapokeaje wasifu huo?
umaarufu wake ulitokana na nini sana huko USA ..?
Huu ni upumba.vu wa hali ya juu. Wewe ni nani? Credentials zako ni zipi? Hata kutumia jina lako halisi JF huwezi ndiyo unataka upewe ushahidi. Halafu Kazi ya police, investigative agencies na ubalozi wa Tz USA ni zipi. Acheni kutafuta sifa za kijinga kupitia misiba.kwa walio na taarifa zitakazosaidia upelelezi ila hawana makaratasi ninaomba mnitumie inbox au mzilete hapa kwa uzi kwa kutumia utambulisho bandia. ikiwezekana ni vyema utumie public internet (mfano kwenye grocery stores, au penginepo ambapo sio rahisi mtu kupata data binafsi akimuamua).
Balozi zetu ni majanga sana. Kama wewe umewahi kuwa nje ya nchi utaniambia, yaani unaweza kuwa upo hata UK ila balozi wa UK hajui hata kama upo. Niliwahi kuishi na jamaa wa U.S, yaani wao walikuwa wanawasiliana na balozi na ubalozi uliweza kumpatia taarifa mablimbali. Ila balozi zetu hawana ushirikiano ni wazembe, wavivu, wabinafsi na wanajiona wao ni wao na pia ni waongo waongo, na wanakuwa wanawaona watanzania wanao wakontact kama vile ni masikini sana watahitaji msaada, yaani kwa ufupi wanakukwepa wakati huo huo ni kodi zetu ndizo zinawafanya wanye
"Mbwa ukimjua jina wala hakupi shida".
Umejaribu.Njoo nyumbani uwaite mbwa wangu majina yao (Hitler, Sadam Hussein, Changudoa) wakusalimie. By the way, walisha mchana pumbu mlinzi wa Ultimate Security. Karibu sana.
Taratibu-taratibu mkuu!
Kweli kabisa mkuu wakati hao wageni wakija Tanzania wanaishi kama kwao vileNchi nyingine watanzania wanaishi kama wakiwa. Balozi zina kazi ya kutuma maombi ya passport uhamiaji dar na kutengeneza madili wakati mambo ya msingi wameyakalia kimya.
Kweli kabisa mkuu wakati hao wageni wakija Tanzania wanaishi kama kwao vileNchi nyingine watanzania wanaishi kama wakiwa. Balozi zina kazi ya kutuma maombi ya passport uhamiaji dar na kutengeneza madili wakati mambo ya msingi wameyakalia kimya.
Mkuu,japo vijipost vyako si vya aya nyingi,lakini vinabeba ilm nzuri sana.Kama witness hana makaratasi lazima aogope kusombwa na ICE
Mjomba hao wajomba wa ICE wasikie hivyo hivyo tu esp. kama mtu uko US na karatasi huna.Mkuu,japo vijipost vyako si vya aya nyingi,lakini vinabeba ilm nzuri sana.
maswala ya makaratsi si tu huko ughaibuni,hata huku mavumbini yapo.
ukizinguana na mhindi,mchina au mtu ambaye si raia wa tanzania,atakuwa radhi mmalizane kishkaji lakini msifikishane polisi.
Maana anajua akifika tu polisi osterbay au chang'ombe,polisi wetu walivo na njaa lazima watachomekea maswali kuhusu uhalali wa ukaazi wake.
Public internet service utaipata kwenye public libraries only, na isitoshe kwenye hizo libraries kuna CCTV inamulika 24/7. Wajomba wakiipata ip address iliyotumika kutuma huo ushahidi wako wataenda kwenye hiyo library na watakuona tu kwenye records zao. Hujasepa hapo.kwa walio na taarifa zitakazosaidia upelelezi ila hawana makaratasi ninaomba mnitumie inbox au mzilete hapa kwa uzi kwa kutumia utambulisho bandia. ikiwezekana ni vyema utumie public internet (mfano kwenye grocery stores, au penginepo ambapo sio rahisi mtu kupata data binafsi akimuamua).
alikuwa anampatanisha nani na nani?
Unauzoefu na huku nje.Ugumu unakuja pale witness akiwa hana makaratasi. I'm just saying
Sio ilmu ni elimu, hahaa wanugu ndiyo wakina nani haoAsante kwa "ilm" mnugu Likud.
Yap, nimekaa Queens for more than 20 yrskibebi Kutotoa taarifa polisi sio tatizo la wabongo tu, ni tatizo la karibu jamii ya watu wote weusi wanao ishi Marekani. Wanaita " ANTI- SNITCHING CAMPAIGN". 50 Cents baada ya kupigwa risasi tisa, aliulizwa na polisi " Unawajua walio kushoot?' akasema " NAWAJUA!". Unaweza kuwataja ? Akasema HAPANA! Suge Knight aliulizwa " Kama ungewajua walio muua Tupac, je ungewataja ? Jibu lake likawa HAPANA!. Kibaya zaidi kama aliye muua marehemu ni mnugu ( Niga) au Okata kama wanavyoitwa na wawest, tena wa kutoka maghetoni ( Thug )kwa sababu hawa jamaa ni washenzi sana na hakuna kitu wanakipenda kama kusikia mtu mweusi anashirikiana na polisi kwenye kesi ambayo mshukiwa ama mtuhumiwa ni mtu mweusi. Wanakushoot fasta. Hata 50 Cents sababu hasa ya kupigwa risasi tisa hiyo mwaka 2000, alifanya kitu wanaita " DRY SNITCHING" kupitia wimbo wake ukiitwa " GHETTO QURAN" . Humo alitaja majina ya drug dealers maarufu wa mitaa ya Jamaica Queens . So ni vigumu sana kwa wabongo kuonyesha ushirikiano katika hilo.
Unatumia 5th amendment kwamba u dont have to answer it or answer something that incriminates youUkiwa cross examined na defense attorney na akikutupia hilo swali kuwa "are you a citizen or legal permanent resident of US?" Utajibu vipi?
Mauaji kila kesehemu ni lazima yakemewe...pamoja na demokrasia yao ya kufa mtu (wasemavyo kwa Trump) nashangaa Watanzania wako kimya kwenye hili...hata Mange?!Heshima nyingi sana kwa wanajamvi wote wa JamiiForums.
Salaamu,
View attachment 346018
Tumemzika andrew aliyeuawa kikatili marekani je nini kinafuata? au itakuwa kama ilivyo kawaida yenu kuficha taarifa za mauaji kama mlivyofanya kwa watanzania wengine (waliochomwa visu, waliochomwa moto, n.k n.k)?
Wakuu Nimekuja kwenu kwa heshima na taadhima kuwaomba watanzania wote wanaoishi houston kutoa taarifa zozote muhimu wanazozijua juu ya mauaji ya mtanzania mwenzetu, kijana mwenzetu, mzazi mwenzetu na zaidi ya yote mhanga wa maisha ya ughaibuni.
Hata kama unaogopa kufanya hivyo fanya kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya nchi yako Tanzania, na yule mwanaye ambaye amempoteza mtu muhimu katika maisha yake.
Kwanini nimeileta JamiiForums?
1. Aliyepigwa risasi ni mtanzania hivyo basi ni jambo jema kuwa mzalendo na kutoa taarifa zitakazopelekea kupatikana kwa haki.
2. Watanzania wengi wameuawa vifo vya kikatili kama hivi huko Marekani ila watanzania hata wale ambao wana taarifa za wahusika waliamua kukaa kimya kuwalinda wauaji. Kumbuka leo ni Andrew kesho inaweza kuwa wewe. Tena bora ya Andrew amepata wa kumsafirisha akazikwa kwao, wewe unaweza usipate hata wa kulipia jeneza lako lije Tanzania uombolezwe na nduguzo. Hivyo basi kupatikana kwa wauaji ni njia moja wapo ya kutuma salamu kwa wengine wenye nia ya kujeruhi au kuua kwamba hakuna atakayewafichia siri.
3. Kulingana na taarifa ya Alex wa Swahili tv ni kwamba Andrew alipigwa risasi eneo ambalo palikuwa na watu meaning kwamba hakuwa peke yake. Anaendelea kusema kwamba watanzania waliokuwepo eneo la tukio walimuona muuaji na wanamjua iweje leo waamue kukaa kimya? Na yule jamaa aliyemuokota na kumpatia pumzi kama first aid baada ya kushutiwa na kuanguka chini na yeye ameamua kukaa kimya? Kama mnampenda Andrew kama mlivyojiliza na kama alivyokuwa anawanunulia bia na kuklia bili zenu basi ninawaomba mumtetee leo kwa kutoa taarifa zitakazopeleka kupatikana kwa muuaji kwa kuwa hawezi kujitetea yeye binafsi.
4. Taifa limepoteza nguvukazi ya taifa (hata kama alikuwa hafanyi kazi Tanzania bado alikuwa anatuma remittances ambazo zilichangia kukua kwa uchumi wetu) hivyo basi ninawaomba moderator muuache huu uzi hapa ili kwamba mwenye taarifa yoyote kuhusu hili tukio aiweke hapa na mwisho wasamaria wema waweze kuzipeleka kwa vyombo vya dola vya marekani.
5. Ubalozi wa Tanzania Marekani uweze kuona na kuchukua hatua haraka. Balozi zetu zimekuwa zikikaa kimya mauaji kama haya yanapotokea tumechokaaaaaa na ukimya wenu. Mmnatumia kodi za nchi kwa kazi mnazoitiwa huko ubalozini sasa kwanini mnashindwa kuwatetea watanzania ughaibuni? Kwanini mnashindwa kusimama kama wakala wa Tanzania Marekani mhakikishe raia wenu wanapata haki zao?
Tutazika ndugu zetu kwa vifo vya kinyama kama hivi hadi lini bila haki na sheria kuchukua mkondo wake? Ubalozi kazi zake sio tu kuandaa maonesho ya utalii bali kusimama bega kwa bega kwenye masuala kama haya.
Mwisho kabisa ninawaomba kutoka moyoni mwangu jitoeni mpeleke taarifa ili haki itendeke kwa ajili ya mtanzania mwenzetu. Juzi ile alikuwa mazula, juzi kati jamaa aliyechomwa kisu na mtanzania mwenzake, leo ni andrew kesho nani ajuaye yaweza kuwa wewe au ndugu yako.
Usipochukua hatua usifikiri kwamba hata wewe utakuwa salama.
[HASHTAG]#justiceforandrew[/HASHTAG]
Nasubiria jibu mwaka wa pili sasa silioni.Diaspora huko majuu si muanzishe mfuko/umoja angalau kwa mwezi mnachangia 50 USD ili ikitokea shida mnatoa kwenye mfuko huo kuliko kuitana harambee kila mtu akifariki? Siku wakafa 5 kwa mpigo si ndo itakuwa aibu jamanii? Kwani huko ughaibuni mnafanya kazi gani ndugu zetu?