Kifo cha Andrew Sanga, What is next?

Kifo cha Andrew Sanga, What is next?

Balozi zetu ni majanga sana. Kama wewe umewahi kuwa nje ya nchi utaniambia, yaani unaweza kuwa upo hata UK ila balozi wa UK hajui hata kama upo. Niliwahi kuishi na jamaa wa U.S, yaani wao walikuwa wanawasiliana na balozi na ubalozi uliweza kumpatia taarifa mablimbali. Ila balozi zetu hawana ushirikiano ni wazembe, wavivu, wabinafsi na wanajiona wao ni wao na pia ni waongo waongo, na wanakuwa wanawaona watanzania wanao wakontact kama vile ni masikini sana watahitaji msaada, yaani kwa ufupi wanakukwepa wakati huo huo ni kodi zetu ndizo zinawafanya wanye
Kodi zako unalipia wapi huko ughaibuni?
 
mods Active Fang Moderator tafadhali wekeni hii update kwenye uzi.

UPDATE KESI YA RAFIKI YETU MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA

Tunapenda kuwashukuru ndugu , jamaa , marafiki na Wanajumuiya wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote hiki cha kufuatilia kesi ya mauaji ya kinyama ya mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ( Baba Zoe ).

Tunapenda kuwafahamisha kuwa kesi imeisha rasmi leo ( 02/18/2019) saa 4 asubuhi kwa mtuhumiwa Villere Henderson Johnson kukiri makosa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela bila parole.

Tunamshukuru Mungu kwa sala zenu.

Ahsanteni sana,

Emmy Matafu na Zoe Sanga
huyo jamaa alikuwa mnugu au mbongo mwenzake??
 
Issue ni kwamba wabongo wengi waishio ughaibuni hawana issue na ndiyo maana unaona hata birthday tu, watu wanajazana na kuvaa nguo za mitoko ya Oscars huku sura ngumu. Mademu wengi wao wana vitambi, obese, wanajichubua, vicheche wa kujiuza kwa Nigerians cheaply.
hao nigerians ni kwamba wana hela au wanapenda sana kununua??
 
Naongelea from experience!
Mimi ni deportee kwa taarifa yako na nilibebwa na wazee wa ICE at 4am from my crib sababu Ya issues kama hio Ya ku testify na nikarudishwa bongo a few months after testifying in front of the grand jury. Karatasi nilikuwa sina. Hakuna Cha immunity wala my fart. I'm a living testimony. Nilikaa Alabama pale Etowah immigration detention facility then Louisiana detention for 3 months then wakanileta bongo.
Acha kubisha kwa vitu usivyovijua
Pole sana brother
 
Hapana nimeona za msiba tu! nilikuwa simfahamu kabla ... labda mtujuze! je alikuwa kiongozi wa wa tz huko ng`ambo ama?
Alikuwa ni mtu wa watu. Ukiwa mtu wa watu unazikwa vizuri sana
 
Watanzania kule naona walisahau mabango ya kudai haki yake!
Labda hawakujipanga. Ila ughaibuni ni shida sana sana. Sawa kuna umoja. Ila siyo kivile hasa ukichukulia wengine kuishi kwa makaratasi mangumashi. Twajuwa maisha popote ila yanapotokea majanga ya vifo au matatizo kama haya basi yawa songombingo sana. Dawa ni kurudi tu. Nyumbani utaishi hata kama hela za nchi zinapondwa na wachache kwa fujo wizi na ulafi
 
Nchi nyingine watanzania wanaishi kama wakiwa. Balozi zina kazi ya kutuma maombi ya passport uhamiaji dar na kutengeneza madili wakati mambo ya msingi wameyakalia kimya.
Wafanyakazi wa Balozi za Tanzania huko nje kazi yao kuwapeleka shopping viongozi wanapotembelea nchi walipo na wao wenyewe kutangaza njaa kwa kufanya biashara za kununua vitu na kupeleka bongo!! Huduma kwa raia kutoka nchini kwao is not their priority!
 
Watanzania kule naona walisahau mabango ya kudai haki yake!
Labda hawakujipanga. Ila ughaibuni ni shida sana sana. Sawa kuna umoja. Ila siyo kivile hasa ukichukulia wengine kuishi kwa makaratasi mangumashi. Twajuwa maisha popote ila yanapotokea majanga ya vifo au matatizo kama haya basi yawa songombingo sana. Dawa ni kurudi tu. Nyumbani utaishi hata kama hela za nchi zinapondwa na wachache kwa fujo wizi na ulafi
Maisha popote hata nyumbani mbona watu wanauawa. Si bora yeye muaji alikamatwa na akafungwa. Ebu jiulize ushawahi kupata jibu la wale vijana watano waliopotea?
 
Heshima nyingi sana kwa wanajamvi wote wa JamiiForums.
Salaamu,

View attachment 346018
Tumemzika andrew aliyeuawa kikatili marekani je nini kinafuata? au itakuwa kama ilivyo kawaida yenu kuficha taarifa za mauaji kama mlivyofanya kwa watanzania wengine (waliochomwa visu, waliochomwa moto, n.k n.k)?

Wakuu Nimekuja kwenu kwa heshima na taadhima kuwaomba watanzania wote wanaoishi houston kutoa taarifa zozote muhimu wanazozijua juu ya mauaji ya mtanzania mwenzetu, kijana mwenzetu, mzazi mwenzetu na zaidi ya yote mhanga wa maisha ya ughaibuni.

Hata kama unaogopa kufanya hivyo fanya kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya nchi yako Tanzania, na yule mwanaye ambaye amempoteza mtu muhimu katika maisha yake.

Kwanini nimeileta JamiiForums?

1. Aliyepigwa risasi ni mtanzania hivyo basi ni jambo jema kuwa mzalendo na kutoa taarifa zitakazopelekea kupatikana kwa haki.

2. Watanzania wengi wameuawa vifo vya kikatili kama hivi huko Marekani ila watanzania hata wale ambao wana taarifa za wahusika waliamua kukaa kimya kuwalinda wauaji. Kumbuka leo ni Andrew kesho inaweza kuwa wewe. Tena bora ya Andrew amepata wa kumsafirisha akazikwa kwao, wewe unaweza usipate hata wa kulipia jeneza lako lije Tanzania uombolezwe na nduguzo. Hivyo basi kupatikana kwa wauaji ni njia moja wapo ya kutuma salamu kwa wengine wenye nia ya kujeruhi au kuua kwamba hakuna atakayewafichia siri.

3. Kulingana na taarifa ya Alex wa Swahili tv ni kwamba Andrew alipigwa risasi eneo ambalo palikuwa na watu meaning kwamba hakuwa peke yake. Anaendelea kusema kwamba watanzania waliokuwepo eneo la tukio walimuona muuaji na wanamjua iweje leo waamue kukaa kimya? Na yule jamaa aliyemuokota na kumpatia pumzi kama first aid baada ya kushutiwa na kuanguka chini na yeye ameamua kukaa kimya? Kama mnampenda Andrew kama mlivyojiliza na kama alivyokuwa anawanunulia bia na kuklia bili zenu basi ninawaomba mumtetee leo kwa kutoa taarifa zitakazopeleka kupatikana kwa muuaji kwa kuwa hawezi kujitetea yeye binafsi.

4. Taifa limepoteza nguvukazi ya taifa (hata kama alikuwa hafanyi kazi Tanzania bado alikuwa anatuma remittances ambazo zilichangia kukua kwa uchumi wetu) hivyo basi ninawaomba moderator muuache huu uzi hapa ili kwamba mwenye taarifa yoyote kuhusu hili tukio aiweke hapa na mwisho wasamaria wema waweze kuzipeleka kwa vyombo vya dola vya marekani.

5. Ubalozi wa Tanzania Marekani uweze kuona na kuchukua hatua haraka. Balozi zetu zimekuwa zikikaa kimya mauaji kama haya yanapotokea tumechokaaaaaa na ukimya wenu. Mmnatumia kodi za nchi kwa kazi mnazoitiwa huko ubalozini sasa kwanini mnashindwa kuwatetea watanzania ughaibuni? Kwanini mnashindwa kusimama kama wakala wa Tanzania Marekani mhakikishe raia wenu wanapata haki zao?

Tutazika ndugu zetu kwa vifo vya kinyama kama hivi hadi lini bila haki na sheria kuchukua mkondo wake? Ubalozi kazi zake sio tu kuandaa maonesho ya utalii bali kusimama bega kwa bega kwenye masuala kama haya.

Mwisho kabisa ninawaomba kutoka moyoni mwangu jitoeni mpeleke taarifa ili haki itendeke kwa ajili ya mtanzania mwenzetu. Juzi ile alikuwa mazula, juzi kati jamaa aliyechomwa kisu na mtanzania mwenzake, leo ni andrew kesho nani ajuaye yaweza kuwa wewe au ndugu yako.

Usipochukua hatua usifikiri kwamba hata wewe utakuwa salama.
#justiceforandrew

====================

UPDATE KESI YA RAFIKI YETU MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA

Tunapenda kuwashukuru ndugu , jamaa , marafiki na Wanajumuiya wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote hiki cha kufuatilia kesi ya mauaji ya kinyama ya mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ( Baba Zoe ).

Tunapenda kuwafahamisha kuwa kesi imeisha rasmi leo ( 02/18/2019) saa 4 asubuhi kwa mtuhumiwa Villere Henderson Johnson kukiri makosa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela bila parole.

Tunamshukuru Mungu kwa sala zenu.

Ahsanteni sana,

Emmy Matafu na Zoe Sanga
Diaspora mnatumika sana na CCM msitusumbue.
 
Watanzania kule naona walisahau mabango ya kudai haki yake!
Labda hawakujipanga. Ila ughaibuni ni shida sana sana. Sawa kuna umoja. Ila siyo kivile hasa ukichukulia wengine kuishi kwa makaratasi mangumashi. Twajuwa maisha popote ila yanapotokea majanga ya vifo au matatizo kama haya basi yawa songombingo sana. Dawa ni kurudi tu. Nyumbani utaishi hata kama hela za nchi zinapondwa na wachache kwa fujo wizi na ulafi
Akiliza ndezi hizi. Dunia imekuwa kijiji siku hizi na watu wanahamasishwa kutembea na kuishi maeneo tofauti tofauti ili kujifunza. Wewe kwa ujinga na inferioty complex yako unaona kusafiri na kuishi nje ya nchi ni kuhangaika.
 
Back
Top Bottom