Birthday waachie watoto na wanawake hawa wanaume Wa namna hii kama yako mnatutia aibu....Si pesa zake kwani alikuomba mchango wa hiyo Birthday kama umekuwa ni wewe wengine bado wanaakili za kitoto
Ndugu yangu acha kabisa,nina rafiki mcanada siku ya birthday yake sikumuwish,kidogo urafiki ufe *****.Aiseee! Nimeshangazwa na rafiki yangu ni mtu mwenye familia yake kunialika kwenye birthday part yake khaaa! Hivi vidume tumekuwaje sikuhizi? Kidume mzima unaanzaje kuimbiwa happy birthday tu yuuu na wewe umekaa tu unakenua meno? Yani na wewe uvae taji eti kisa birthday!
Haya mambo ebu tuwaachie wavulana wa vyuoni high school na wanawake yani sikuhuzi ungangali wa wanaume wenzangu unapungua ebu tuache utoto wa kusherekea birthday kijinga hivyo. Pia kumekuwa na kamchezo ka mtu kumwagiwa maji hivi izo akili za hivo mnatoa wapi?
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]Wanaume wa dar mnavyopenda kulalamika ili mbembelezwe kama mademu...
Ngoja kwanzaaa... Ivi ulithubutu kumchana mwenyewe ana kwa ana, au ndio umekosa ujasiri na kukimbilia kubonyeza button?
nimemchana sana aisee sasa nimeshtuka kuwa hata umu kuna weza kuwa na watu wa namna hii ya rafiki yangu ndio nimekuja kuwachana
Endeleza mkuu maisha ni haya tu yafurahie.Jana nimemuona Obama CNN akiomba udhuru situation room Pentagon, kwamba asiulizwe maswali mengi ili awahi birthday (yake) dinner na familia.
Hii mnaizungumziaje vidume wa nguvu wa JF?
Mimi kwa maoni yangu nafikiri ni life style tu. Nikiwa peke yangu huwa sifanyi ila tukiwa hom nakumbuka baba alikuwa anatoa hela ya champaign na mama alikuwa anakupikia ur favorite food tunakula familia nzima dinner
Nakaribia kuoa natarajia kuendeleza hii tradition
Sio ushamba mkuu sema ujinga wa kutaka kupangia watu maisha.Naomba muweke ushamba wenu pembeni na tumtakie happy birthday Rais wa dunia leo ni siku yake ya kuzaliwa.
Happy birthday, President Obama!
View attachment 376391
Kuhisisha kila usichopenda na ushoga ni ishara kuwa una hisia za kishoga kwa hiyo unakuwa na wenge flani tafuta dawa ya saikolojia ukae sawa usipofanya hivyo utalaumu watu siku moja.Obama anasapoti ushoga kwavile kafanya obama na ww unaona iko poa?
Endeleza mkuu maisha ni haya tu yafurahie.
Na kama alishindwa,basi na yeye kaongeza behewa la wanaume wanaopunguza uanaume.
Mkuu hakuna maradhi mabaya huku duniani kama poverty and lack of exposure, ndio ugonjwa unaowasumbuwa baadhi ya hashki majinun wa humu JF.
Anayeamini yeye ni kidume humu JF zaidi ya Tata Madiba Nelson Mandela na asogeze wowowo lake hapa mbele atueleze aliwahi kufanya lipi la maana hapa duniani?
View attachment 376495View attachment 376497View attachment 376498View attachment 376499View attachment 376500
Kitu ambacho nimegundua watu wengi waliochangia hapa wako desperate na maisha na wanatafuta namna ya kuwa sawa kifupi tukio mnalo pigia kelele na kulihusisha na gender na utoto ni la kawaida sana na huwa linafanyika kawaida sana kwa mda wa kawaida sana na kuwaalika watu wachache sana ambao huwa unaamini wanamchango kwako kifupi watu wanaogusa maisha yako moja kwa moja tukio hufanyika baada ya kazi na haliathiri siku ijayo ya kazi
Wazungu ambao wamekuwa wakifanya hili tukio Mara kwa Mara wako mbali kimaendeleo kwa maana hiyo halijawahi kuleta umaskini au kuzuia uanaume popote pale
Binafsi huwa napania sana kufanya ila nasahau na inatokana na kuwa sikukulia kwenye utamaduni huo sana ila kwa wanaofanya sioni kosa kwao mpaka kuwarushia maneno kana kwamba we ndio mwalimu wa maisha sasa kila mtu aishi unavyoishi.