Kidhibiti mkononi, unapewa wiki 1 kujitetea... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kidhibiti mkononi, unapewa wiki 1 kujitetea...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisoda2, Jun 18, 2010.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Wadau habari hii nimeisikia jana toka radio sauti ya Amerika.Imenifanya nijiulize maswali mengi kuhusu kauli ya mtu alie pewa dhamana na taifa kusimamia taasisi hii(EWURA)

  Katika sakata na mafuta ya petrol na aina nyinginezo za nishati hiyo kukumbwa na mtindo kuchanganywa na aidha maji ama aina nyingine ya nishati ili kujipatia faida kubwa kunakofanywa na wafanyabiashara hapa nchini kulisababisha mtafaruku katika msafara wa rais(muungwana)huko Moshi.
  Mtendaji mmoja toka taasisi hiyo(EWURA) alisema wahusika katika sakata hilo wamepewa wiki moja wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua kwa kitendo hicho.
  Hivi kweli kwa kauli kama hii tutafika?
   
 2. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida - EWURA inafahamu fika kwamba "mafuta yanafanyiwa cocktail" na inajua nani anafanya hivyo - tatizo ni nani anaweza kumfunga paka kengele! - Kwani Mh Rais mwenyewe mara ngapi anasema "wauza madawa ya kulevya tunawajua" - "wala rushwa tunawajua" e.t.c - Ni hatua gani zinachukuliwa?
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo utakapowa-admire wachina. Wangeshaekwa kwenye electric car zamaaani.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Naskia eti sheria ya kuwachukulia hatua haipo(bado haijatungwa).
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ipo sheria inayowapa mamlaka ya kuadhibu, sema sheria yenyewe ndo hii ambayo ina urasimu usio wa lazima
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Suala la UCHAKACHUAJI ni gumu kulizima kwa sababu kuu moja nayo ni "Biashara ya mafuta" Imeshikwa na wanasiasa pamoja na maswahiba wao, sasa kuwachukulia hatua hawa ni sawa na kuwachukulia hatua watawala. Nchi hii inatakiwa kurudi kwenye enzi za Mwl. JKN kuwa kiongozi wa umma ama familia yake hairuhusiwi kuwa na hisa kwenye kampuni binafasi, kwa maana hiyo ukiisha ingia kwenye uongozi wewe na familia yako mnatakiwa kuachana na biashara zenu, au vinginevyo mfuate moja kati ya biashara na siasa. EWURA hawawezi kufanya chochote kwani nao wao wapo pale kwa ajili ya their "livelihood" ukimkamata mtu baada ya muda unapata kimemo au call kuwa umwachie ni mtu wa fulani, sasa utaendelea kumg'ang'ania uletewe majungu ama upewe transfer "Tandahimba"?. Hii system yote imeoza inahitaji mtu dictator asiye na urafiki wala ujamaa kwenye masuala ya kitaifa kwa muda wa miaka mitano kabla ya kuirudisha kwenye msitari.

  Leo hii kila mfanyabiashara ni kada wa CCM unatarajia Serikali hiyohiyo ya CCM iwachukulie hatua makada wake?, halafu ikishindwa uchaguzi wamlaumu nani?
   
 7. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mrisho Mpoto alisema katika wimbo wake wa Mjomba - Mtu ameshikwa na mchuzi wa kuku na bado unaambiwa ushahidi bado (not exact words, but generally thats what he meant).
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na kwanza ni kwa sababu ni magari ya muungwana ndo yalipata shida ya mafuta hayo, la sivyo hamngekuwa mnayaongelea hayo. Kwa taarifa nilizonazo kituo hiki kiliwahi kupigwa faini ya shilingi milioni tatu kwa kosa kama hilo. Kituo hiki kiliwahi kumfidia mzungu mmoja kwa kosa kama hilo pia. Juzi muungwana kaipata. Kuna akina siye huku matatizo ni hayo hayo tunayapata. Kuna kampuni moja ya utalii inaweka mafuta pale, wana magari mapya landcruizer wanaziita macho ya panzi mpya kabisa wameshafungua injector pumps kwa ajili ya mafuta machafu pia. Hasara tunayopata Sreikali haioni na bado inaendelea kuwalea watu hawa. Ukifika pale kwenye kituo kile kinachotuhumiwa utakuta ana workshop ya kutengeneza pump. Anajua kuwa mtakuja tu. Ufike wakati sasa watu waliopewa dhamana na nchi hii kuchukua hatua za dhati kudhibiti hali kama hizi. Kila mtu ana maamuzi yake bila kujali kuwa nchi hii inaongozwa na taratibu zake na sheria. Ni lini kutakuwepo na viongozi wenye uchungu na nchi hii. Ni lini tutapata viongozi ambao watakuwa tayari kuifia nchi yetu kama walivyofanya baadhi ya machifu wetu? Kila mtu akiingia madarakani anafikiria atapora nini, atajiuzia nini, ataoa wanawake wangapi, ataenda disco nchi gani, ataiitaje NGO ya mkewe! list ni kubwa ila mimi naamini kama sio sasa basi soonest wako wajao ambao wataikomboa nchi! Watakaokata kamba za UFALME huu wa sasa wa kurithishana madaraka kwa watoto wao hata kama ni MAAMUMA kiasi gani.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 9. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushwahiba jamani!!! Apatikane ndava tu ndio tutafika.
   
 10. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  hahaaaaaaaaa hapo ndo utamu unakuja.
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na ikijulikana majority share holder wa hiyo petro station ni mwanafamilia wa muungwana.?.....
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wafadhili wakuu wa SISIEM unategemea nini kinafuata baada ya hapo?
   
 13. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Believed share holder mkubwa ni Mramba
   
Loading...