Kichwa kupata moto pekee yake ila mwili joto la kawaida

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Salaam wataalamu...

Nahitaji msaada ndugu zangu, Mwanangu wa kike aliwahi kulazwa Mnyamala kwa Pneumonia na anaemia akiwa na miezi 5 takriban.

Akatibiwa akapona ila hili TATIZO LA KICHWA KUWA CHA MOTO LIKIWA LIMEPUNGUA KIDOGO NA ALISAFIRI KWENYE BARIDI AKAPUNGUA KIASI SIO KUISHA KABISA.

Ila ndugu zangu Matatizo ya Mtoto wangu yako pale pale anaenda kutimiza mwaka kichwa kinakuwa na joto.. Na nikienda hospital watanieleza yale yale na kunijaza mwanangu ma PARACETAMOL NA ANTIBIOTICS tu na madawa ya damu.

Je kwenye experience kwenye taaluma ya afya. Je hii case mliipata na mkaishughulikiaje? Nina wasiwasi sio tu kichwa kinakuwa cha moto tu mwili ukiwa na joto la kawaida. Nina wasiwasi hata kichwa kinamuuma vilevile. Ila ni vile hawezi kusema tu. Ana mwaka sasa.

Ziada:-
Ana mwaka sasa hajaanza kutambaa. Ila hii kwa mtoto wa kwanza ilikuwa hivyo hivyo alichelewa stages zake. Ila hakuwa kama hivi kichwa kupata moto pekee yake.
 
Kuna specialist wa Watoto kariakoo ule mtaa unaotokea Msimbazi kwenda muhimbili kabla ya mataa ya fire kuna hospital mkono wa kulia nimesahau jina lake, nenda hapo kuna specialist wa kuaminika atajuwa shida ni nini.
 
Ahsante nashukuru kwa ushauri wako...

Nakaribisha ushauri wa wataalam wengine humu vilevile tafadhali...
 
Mwanangu ana 3yrs toka akiwa na miaka 2 niligundua ana tatizo kama hilo akilala hapo alipoweka kichwa panakuwa oameloa kabisa.katika kufatilia nikagundua tatizo linamuanza akilala usiku kichwa kinaweka moto huku sehemu zingine za mwili zipo kawaida.

Nimezunguka hospital kwa madaktari bingwa karibu wote hamna msaada.
 
Taja majina ya hao madaktari bingwa hapa tuwajuwe, halafu ujuwe si kila daktari bingwa ni bingwa wa magonjwa ya Watoto ilo ulifahanu vizuri, wapo wachache sana nchi nzima.
 
Wengi wamesomea tu profession lakini nao ni mtihani kwenye kuzigundua cases na kuzifanyia kazi...
 
Kuna specialist wa Watoto kariakoo ule mtaa unaotokea Msimbazi kwenda muhimbili kabla ya mataa ya fire kuna hospital mkono wa kulia nimesahau jina lake, nenda hapo kuna specialist wa kuaminika atajuwa shida ni nini.

Kwa dr Abbas
 
Back
Top Bottom