Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

Utakuwa muoga tu huna lolote! Huyu jamaa hajakosea lolote, la msingi huyo Kibwana aombe radhi tu! Huyo mtu ana dini yake, nini kimemtuma kuja kusema yale asiyoyajua! Huo moshi mweupe na mweusi ndio kaona uchawi?! Yaliyoko ndani ya dini yake hayamtoshi?

Kazi yetu Wakatoliki ni kuyasoma na kuyaelewa maandiko matakatifu na kisha kueneza injili ili watu wamjue Mungu vizuri. Hukumu na visasi ni kazi ya Mungu mwenyewe.

 
Tutetee imani na sio dhehebu.
Cheo alichokidhihaki kiliweka na Kristu mwenyewe na ni cheo juu ni daraja la mbingu na dunia, ni muongozo wa Kanisa Katoliki , nyaraka zote za Kanisa hutoka hapo na mwisho Kanisa huwateua kuwa watakatifu. Leo tuaminishwe kuwa ni ushirikina na tukae kimya, huo ni uoga mbaya kuliko uoga wenyewe. Alichoomba mtoa post ni kuwa AOMBE RADHI na viongozi wake basi, tatizo ni nini hapo?
 
Huyo kibwana kama nikweli kasema hivyo ni wakumdharau tu.

Watu wa aina kama yake huwa wanakuwaga na ma stress ya ajabu ajabu.
 
Jitazame ni mambo yapi yanakushughulisha kisha utagundua kuwa huna sababu ya kuwa kawa 'wao'. Tungelilelewa kwa chuki na kulipizana visasi, tusingekuwa taasisi kubwa. Sisemi kwamba alichoongea ni kizuri au kimenifurahisha, ila ni wazi hakinisumbui kwa kuwa kimesemwa na yeye.

Kama kauli hiyo ingetolewa na Askofu wa Kanisa Katoliki, ningelikuwa concerned. Be cool!

Jesus-The Violent.
"The Kingdom of heaven has suffered violent Attacks. And Violent Men try to seize it" (Mt 11:12) see also Mt 7:23, Mt 7:15, Mt 25:41, Mt 23:13-33...
The verses quoted above were said in different situations and backgrounds, yet they were all hard- hitting and vehement. We can sense the violence that stood out when He uttered these sentences.
"The people were amazed," "The disciples were shocked," "Astonished, "Feared,"
The violent words of Jesus were; radical ideas, firm warnings, bold challenges, frightful condemnations, just judgement, hard saying. Take care...
 
Sijakusikia hayo maneno lakini haina haja ya kubebea bango kauli ambayo ni ya jumuiya ya wakatoliki wote. Kama kanisa kupitia wasemaji wake wataona kuna haja ya kufuatilia kauli hiyo basi watafanya hivyo. Vinginevyo kwa mtu binafsi no swala la kupuuza tu na wala haliongezi wala kupunguza kitu.
Reaction dhidi ya Kibwana kwa namna hii inaweza leta impression kwamba pengine ameguza ukweli sensitive hata kama sio kweli.
 
kazi yetu Wakatoliki ni kuyasoma na kuyaelewa maandiko matakatifu na kisha kueneza injili ili watu wamjue Mungu vizuri. Hukumu na visasi ni kazi ya Mungu mwenyewe.

Nani amemuhukumu hapa mtu?? Au nani amekuwa na kisasi na mtu hapa?? Huyu bwana mdogo anayeitwa Kibwana acheze na dini yake na asiingilie mambo ya dini za wengine! Hayo mafundisho ya huko kwao ya kudanganyana yaishie kwenye vilinge vya misikiti yao na siyo public kama alivyofanya! Kuambiwa lazima aambiwe na siyo kumwacha alete uchokozi kwenye imani za watu wengine!
 
Nyie ndo wale ambao mnaamini hayo madhehebu ndo yatawapeleka peponi
 
Kama sio ushirikina basi mungeeleza huo moshi unatokeaje ili tuamini Dachi kaongopa
 
Sikubaliani na kashfa yoyote dhidi ya dini au imani ya mtu mwingine. Haipendezi, haifai na haikubaliki haswa kuzungumzwa na mtu anayejiita mwandishi au mchambuzi.

Lkn pia nitumie muda huu kuwakumbusha kuwa nguvu tunayotumia kutetea dini na madhehebu yetu, tungeiwekeza zaidi ktk kutetea wokovu. Yesu alileta wokovu na kwa kufanya hivyo akajikuta mara kwa mara anapingwa vikali na dini zilizokuwepo wakati huo!!!!

Na ni ajabu ktk kutetea dini mtu anawaza kulipiza kisasi, anaweza kutesa, kujeruhi na hata kuua. Lkn ktk kutetea wokovu muda wote anakuwa anaimba ' Baba Uwasamehe maana hawajui walitendalo'. Wewe fuatilia mentality wa watetezi wa dini zao mara nyingi ni panga, visu na silaha nyingine za kuua huwa nje nje, huku wakati huohuo wakihubiri upendo!!!!!!!!

Wokovu kwanza, dini baadae. Tumsifu Yesu Kristo!!
 
Kibwana Dachi sio muislam hilo jina lisikutishe.

Huyu huwa anasema mara kwa mara kuwa yeye ni muAngrikana haya ni kutokana na yeye mwenyewe kutamka mara kwa mara kwenye kipindi. Mkuu lakini umefika mbali kwa nini usibadili tu station mambo yakaisha kuliko kujiumiza moyo as if una kisa nae.

Maana hadi kukuharibia siku ina maana si jambo dogo.
 
Kijana, hayakusaidii lolote hayo mambo, hii dunia huwezi kumlazimisha kila mmoja awaze unavyowaza wewe, soo ukitaka kila kitu kiwe katika njia unayotaka wewe basi dunia isingekuwa hivi ilivyo
Acha utani ameudhihaki ukatoliki. Hili halitakubalika hata kidogo. Tuko naye popote atakapokwenda
 
Huyu mzee ninakaa nae jirani tatizo lake anajifanya mjuaji sana wa mambo ndio maana wakati mwingine anaropoka bila kuuliza
 
Ameniharibia siku huyu.
Watangulizi walisema ukitaka kujua busara ya mtu mpe nafasi aongee.
Huyu jamaa nilikuwa namheshimu sana , mwisho wangu imekuwa leo. Kwa busara ya kawaida tu huwezi kutangaza kwenye chombo kama redio kauli nzito namna hiyo hata kama unajua kuna mapungufu!

Hizi redio ndio zilileta mapigano nchi ya jirani kwa kutumiwa vibaya na watu wenye malengo tata!
Huwezi kujua huyu Kibwana anamtumikia nani, na huwezijua ana malengo yapi kutoa kauli hii.
Kwa nia njema ya amani, naiomba taasisi yake iingilie kati na kumpa onyo huyu mtu, vinginevyo wakimwachilia ataendelea na ukosefu wa nidhamu huo!

Tusitumie media kubwa kama redio kutamka maneno ya insinuation.
Sijajua alifunzwa chuo gani huyu mtu!
Kwa mwenye Busara , hata kama haamini dini ya wenzie, asiisemee kwa namna ya uharibifu!
Ni makosa makubwa sana amefanya huyu!
 
Sasa Wale Mliosema GENTAMYCINE NIMEKURUPUKA Na NIMEONGOPA Hii Radhi Ya KIBWANA DACHI Ameitoa Kimakosa au?

Najiamini Kunakotukuka Na Siku Nyingine Msikurupuke Na Kunishambulia Hovyo. Anyway Kwakuwa Mhusika Ameomba Radhi Na Mimi Nikiwa Kama Muanzisha Uzi Huu KWA MOYO MKUNJUFU TENA UKIFA NI MSAFI Na MWEUPE KAMA MOSHI WETU WA KIKATOLIKI NIMEMSAMEHE Mr. Kibwana Dachi Kutoka Katika SAKAFU YA MOYO NA Nina FURAHA KUBWA KUWA AMENIUMBULIA WATU WANAFIKI Na WENYE JICHO LA CHUKI Na HUSUDA KWANGU Na Akhsanteni UONGOZI MZIMA WA JAMII FORUMS KWA KULIFUATILIA NA HATIMAYE MHUSIKA AMEKIRI KOSA NA AMEJIRUDI.

Binafsi Yameisha Na Maisha Sasa Yasonge Mbele Na Nawaomba Wengine Pia MLIOGHAFILIKA Na ALICHOKISEMA KWA UJUMLA Tumsamehe, Tumuombee Na Tumpende Pia.

Na Kama Kuna MAHALA POPOTE KAKA YANGU KIBWANA DACHI NIMEKUKWAZA au PENGINE KUKUUDHI LABDA KWA LUGHA YANGU HUMU Na MIMI NAOMBA UNISAMEHE SANA Na LABDA TU NIKIRI KWAKO KUWA HUWA NAJIFUNZA VITU VINGI SANA UKIWA STUDIONI UNATUELIMISHA.........Nami Pia Najiamini KUNAKOTUKUKA, Ni Mtu Makini ILA HUWA SIFANYI SANA MAKOSA YA KIBINADAMU.

Akhsante!
 
Tumsifu Yesu Kristu!
Wakatoliki tunamsamehe huo Dachi kama Baba Askofu Pengo alivyomsamehe Gwajima!
Hila akiendle kuropoka atapata matatizo makubwa na atapotea ...
Tumsifu Yesu Kristu!

Milele Amina.
 
Back
Top Bottom