chakufia nini
JF-Expert Member
- Apr 14, 2015
- 692
- 456
Nachelea kukubaliana na Mkatoliki wewe, ambaye huoni athari ya maneno aliyoyatoa huyo mtangazaji, mfano endapo mwanao angekuwa ni mmoja wa waliosikiliza kipindi hicho na akaaminishwa kwa kusikia kuwa unaofanyika Rome ni uchawi, na hana nafasi ya kumuuliza huyo aliyetamka, huoni kuwa ataamini hilo?
Je, ni nani ambaye atakanusha kama sio kweli kuwa ule ni ushirikina? Maadhara ya kuaminishwa kuwa Kanisa Katoliki ni washirikina wakubwa huoni athari yake? Kesho mkiwa kwenye jumuiya mnasali, akija mtu kuwaita nyie ni wachawi chekelea tu maana imani yako inakukataza na unafurahia kutukanwa
Hayo yote yaliyosemwa hayajabadilisha imani ya Kanisa Katoliki wala imani ya Wakatoliki. Hebu angalia mfano wa kiongozi wetu Pengo. Mbona alifanyiwa udhalilishaji mkubwa sana na Gwajma? Uliona alichojibu? Hakumtaka hata Gwajma aombe radhi zaidi ya kutamka amemsamehe. Hivi unadhani angeanzisha ligi na Gwajma angekuwa anatetea imani? Lile la Gwajma halikuwa zaidi ya hili?