Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

HV hajaomba radhi mpaka sasa?...

AMESHATUOMBA JAPO NADHANI INGEFAA NA HATA KESHO PIA AKIWA KATIKA KIPINDI BASI KWA UKUBWA ULE ULE AOMBE RADHI ILI TUONE UUNGWANA WAKE. SAUTI YAKE NAYO ITATULIZA MIOYO YETU Na HASWA WANGU. NASUBIRI MSAHAMA WAKE WA SAUTI YAKE RASMI KESHO ASUBUHI JAPO NIMESHAMSAMEHE.
 
Ameniharibia siku huyu.
Watangulizi walisema ukitaka kujua busara ya mtu mpe nafasi aongee.
Huyu jamaa nilikuwa namheshimu sana , mwisho wangu imekuwa leo. Kwa busara ya kawaida tu huwezi kutangaza kwenye chombo kama redio kauli nzito namna hiyo hata kama unajua kuna mapungufu!

Hizi redio ndio zilileta mapigano nchi ya jirani kwa kutumiwa vibaya na watu wenye malengo tata!
Huwezi kujua huyu Kibwana anamtumikia nani, na huwezijua ana malengo yapi kutoa kauli hii.
Kwa nia njema ya amani, naiomba taasisi yake iingilie kati na kumpa onyo huyu mtu, vinginevyo wakimwachilia ataendelea na ukosefu wa nidhamu huo!

Tusitumie media kubwa kama redio kutamka maneno ya insinuation.
Sijajua alifunzwa chuo gani huyu mtu!
Kwa mwenye Busara , hata kama haamini dini ya wenzie, asiisemee kwa namna ya uharibifu!
Ni makosa makubwa sana amefanya huyu!

Mkuu Kwasababu Ameshatuomba Radhi / Msamaha WAKATOLIKI Wote Basi Nasi Pia Tumsamehe ILA Na Yeye Kwa UKUBWA ULE ULE Basi Natoa Rai Yangu Kwake Na Namwomba Na Yeye AOMBE RADHI / MSAMAHA Katika Kipindi Kile Kile Na Muda Ule Ule Kama Wa Leo Ili Radhi / Msamaha Wake Kwetu Uwe Na MASHIKO Na Namjua Kibwana Dachi Ni Muungwana ALIYETUKUKA Hivyo Kesho Atatuomba Radhi Na Mimi Kama Kawaida Yangu Nitatega Sikio Tangia Wanaanza Kipindi Saa 12 Asubuhi Hadi Wanamaliza Saa 3 Na Ikibidi Hata Huu MSAMAHA Wake Kwetu Auweke Katika Shop Rep Yake / Yao Morning Magic Ya Kesho Na NAWAOMBA TENA HUKU NIKIWASIHI Kuwa Hata Kesho WAKIWA KIPINDINI WASITHUBUTU KUTUMIA Muda Wao Mwingi KUNIJADILI Kwani Haitasaidia Na Badala Yake Wanaweza Ndiyo Wakajikuta WANAHARIBU Zaidi.
 
Kijana, hayakusaidii lolote hayo mambo, hii dunia huwezi kumlazimisha kila mmoja awaze unavyowaza wewe, soo ukitaka kila kitu kiwe katika njia unayotaka wewe basi dunia isingekuwa hivi ilivyo

Wewe km haujaiva ktk imani yako shauri yako,mambo ya imani usiingilie.
 
Mkuu GENTAMYCINE, tunashukuru ametuomba radhi huyu bwana asubuhi ya leo katika kipindi chao..asingefanya hivyo tungemshughulikia ipasavyo..
 
Huyu nae haujui ukatoriki wala yeye si wakwanza. Kama maaduivwangekua na nguvu dhidiv ya Ukatoriki leo kusingekua na RC. Atambue hakunaa dhehebu duniani lenye misingi Imara kama RC. Tanakusamehe kwakuwa hujui utendalo. Only Jesus died and raised. Wengine wote wamekufa na kuwa mavumbi ya dunia
 
Sijui hawa watangazaji wa vipindi vya asubuhi vya fm radios huwa wanawashwagwa na nini ktk makoo yao. Mana wengi wao huwa wanaongeleaga na kuchangia mada kama vile wapo ktk vijiwe vya kahawa na zhumna. Yaani ni utumbo mtupu na wanakosaga weledi,umakini na hata tasfida kwa baadhi ya maneno yao.
 
Hakika huyu amefanya la maana sana kuomba radhi!. Vinginevyo mimi binafsi nilikuwa tayari kuingia chimboni na kutafuta taarifa zake zote zinazomhusu. Taarifa Hizi zingesaidia sana kumjua kwa undani huyu ndugu, na kujua nguvu iliyopo nyuma yake inayomsukuma kukashifu dini ya wananchi wenzake kupitia vyombo vya habari.

Kwa niaba ya wengine naupokea msamaha wake kwa moyo wa ukamilifu, na yuko huru sasa. Sharti ni kuheshimu imani za wengine...basi!
 
Wana jamvi!
Mwana habari Mzee Kibwana Dachi mwandishi na mwana habari wa kituo cha Magic Fm anaye tangaza kwenye kipindi maarufu kama" kupaka rangi " ametoa ufafanuzi na kuomba radhi kwa matamshi aliyo yatoa jana kuhusu kanisa katoliki na amesema hakuwa na dhamira ya kuudhi au kumkwaza au kukashifu mtu yeyote au dini husika!

Amesema ana heshima sana dini husika maana imemlea na hata ingekuwa haijamlea asinge kuwa na nia ya kukwaza au kukashifu hivyo anaomba sana radhi walio guswa na kukwazwa na yaliyo semwa!

Uungwana ni vitendo naomba asemehewe hata mimi nilisikiliza kipindi kwakweli hakuwa na nia mbaya ..! Msameheni!
 
Huyo jamaa sijui yukoje... eti anadhani anaweza tu kusema pole na everything will be alright... Cc Mabosi @ magic FM!
 
Mkorofi sana huyu. Kama vitu havijui si akubali tu hajui na alipayuka. Hii kwangu inanionesha kuwa wala hajutii kitendo alichokifanya...ametaka tu kuwa "politically correct":

Idara hii ipo Vatican na nia yake ni kujua ukweli na si vinginevyo, lakini kutokana na hilo wengi wanahusisha uwepo wa tukio la kuwepo Moshi mweusi au mweupe wakati wa kumchagua PAPA ni tukio linalotokana na "utafiti huo", ukweli kinachosababisha hilo ni maombi ya dhati yanayofanywa na maaskofu na mapadri wakati wa mchakato wa kumpata Papa mpya haina uhusiano na utafiti huo narudia tena.

Angeweza hata ku-google tu kujua kinachosababisha moshi mweupe au mweusi badala ya kendelea kupotosha na "kuwasanifu" wakatoliki. Jinga kabisa!

Kwa usahihi kuhusu moshi (https://en.wikipedia.org/wiki/Papal_conclave):

Fumata nera and fumata bianca[edit]The color of the smoke indicates the results to the people assembled in St Peter's Square. Dark smoke (fumata nera) indicates that the ballot did not result in an election, while white smoke (fumata bianca) announces that a new pope was chosen.[SUP][85][/SUP] Originally, in the event a pope was not elected, damp straw was added to the fire to create dark smoke. In the event a new pope was elected, the ballots were burned alone, creating white smoke.
Prior to 1945 (when Pius XII changed the form of ballot to use anonymous oaths, first carried out in 1958), the sealing wax on the complex type ballots illustrated above had the effect of making the smoke from burning the ballots either black or white, depending on whether or not damp straw was added. This explains the confusion over the color of the smoke in the 1958 Papal conclave, caused by the lack of sealing wax on the ballots. The Siri Thesis was based on the confusion over the smoke color on the first day of that conclave.
Since 1963, chemicals have been added to the burning process, and beginning in 2005, bells ring after a successful election to augment the white smoke.[SUP][86][/SUP]
During the 2013 conclave, the Vatican disclosed the chemicals used to color the smoke:[SUP][87][/SUP][SUP][88][/SUP][SUP][89][/SUP]


Mkuu GENTAMYCINE , naomba uweke hiyo quote kuhusu moshi mweupe (na link) ili kuzuia upotoshaji zaidi.
cc: JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni kuwa hakuhusisha Ukatoliki na uchawi kama anavyodai mleta mada; alisema Katoliki wanayo idara maalumu ya kutafiti ushirikna. Tafasiri zetu ndio zimetufikisha kwenye madai kuwa Katoliki wanaamini ushirikina.

Vv
 
Back
Top Bottom