Kiboko cha EU lazima kituchape kuhusu Ngorongoro

Kiboko cha EU lazima kituchape kuhusu Ngorongoro

Shida yako unahamisha mawazo ya facebook na kuleta kwenye great thinkers. Haya sio mambo ya kirafiki ya Abunuasi na Bwana Heri. Na makubaliano ya kimataifa yanayolindwa na sheria na mikataba. Ndio maana tunalia kila siku nchi za kiafrika zifike mahali zijitegemee ili kuondokana na misaada yenye masharti dhalili ikiwemo kuingiliwa mambo ya ndani. Mfano wakati wa Magufuli alikiuka masharti ya fedha za elimu bure zinazotolewa na UN aliposema hawezi kusomesha wazazi na UN wakatishia kuzuia fedha na unakumbuka hasira ya Bulembo kwa Zzk?
Mimi sio mjinga kama unavyodhani wewe. Kama masharti ya mikopo sasa wanawazuia nini? nimekwambia weka huo mkataba wa mikopo na masharti yake. Mbona ushoga tumekataa. wamezuia mikopo?
 
Aibu sana. Kwanza hatupaswi hata kuja kukaguliwa, mpaka wanaona waje kukukagua kuna walakini na namna unavyojiendesha wewe mwenyewe.
 
Rais William Ruto wa Kenya aongea mazito ya kimataifa umuhimu wa tamaduni na asili katika uchumi


View: https://m.youtube.com/watch?v=a9wfFwJoQ3w

Rais William Ruto wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Kitamaduni la Maa katika lango la Sekenani, Maaasai Mara, Kaunti ya Narok, tarehe 22 Agosti 2023.

Rais Ruto alisema Serikali ina nia ya kutangaza utalii wa kitamaduni ili kupata mapato zaidi ya utalii. Alisema Serikali itatumia urithi wa kitamaduni wa Kenya ili kupanua vivutio vya utalii. Alisema kuwa utalii sio tu wa vituko na sauti tu bali pia watu
Source : State House Kenya
 
Maisha ya Mwafrica yanasikitisha sana, sitetei ujinga wa Viongozi wetu lakini pia sikubaliana na upumbavu wa Taifa kuingiliwa na kuamuliwa mambo yake na watu wengine.

Tujifunze kujitegemea na hata haki zetu tuzidai wenyewe na sio kuingiliwa na wengine
Acha kutoa povu Kwan wakijua mnavyotesa na kuua watu Kuna shida Gani..si misaada kutwa mnachukua kwao
 
Ngorongoro ni yetu, tuamue wenyewe mambo yetu yanayotuhusu. Kutegemea EU kutuamulia mambo yetu ni utumwa!!! Kama Kuna shida Ngorongoro ni sisi wenyewe wananchi kukubali kuitatua shida hiyo. Jamani, TUJITEGEMEE.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UJUMBE WA MAASAI WAMALIZA ZIARA YA UTETEZI ULAYA
Tarehe 2 Juni, 2023

Ujumbe wa Wamasai wakutana na Serikali za Ulaya na Wanasiasa kuhusu Mgogoro wa Kufukuzwa. Watembelea Bunge la Ulaya pia nchi za Germany, Austria, Italy, Vatican na Belgium

(ULAYA) Ujumbe wa jamii ya Wamasai ulihitimisha ziara ya wiki mbili barani Ulaya, ambapo walishirikiana na wawakilishi wa serikali na Umoja wa Ulaya (EU), mashirika ya kidini na mashirika ya kiraia kote Ujerumani, Austria, Italia na Ubelgiji.

Ujumbe huo kutoka Tanzania ulilenga kupata uungwaji mkono wa kimataifa dhidi ya ufurushwaji unaoendelea katika nchi yao katika maeneo ya Loliondo na Ngorongoro Mkoani Arusha, Tanzania. Ziara ya utetezi ilizalisha wimbi muhimu la mshikamano kutoka kwa wenzao wa Uropa.


Mgogoro wa kufukuzwa unalazimisha makumi ya maelfu ya wafugaji wa Kimasai kutoka katika ardhi ya mababu zao, kuvuruga maisha yao ya kitamaduni, na kuwa tishio kwa maisha yao.

Wajumbe hao kutoka Tanzania walileta masaibu yao katika ngazi ya kimataifa kwani uhuru wao wa kujieleza umebanwa sana nchini Tanzania.

Pia walisisitiza juu ya uhusiano usio wa moja kwa moja kati ya ufadhili wa Ulaya ambao unasaidia miradi ya uhifadhi wa mazingira nchini Tanzania, na kusababisha ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa Wamasai.

Serikali ya Tanzania inahalalisha uondoaji huu kama juhudi za kuhifadhi mazingira; hata hivyo ujumbe wa Wamasai ulisisitiza kuwepo kwa maslahi mengine, ikiwa ni pamoja na utalii na utalii maalum wa uwindaji wa nyara.

Iliitaka EU iweke masharti ya ufadhili wao kuhusu kuheshimiwa kwa haki za binadamu, ikisema: “Ikiwa huwezi kuhakikisha kwamba pesa zako EU haziungi mkono ukiukaji wa haki za binadamu, basi mzuie utoaji pesa!”

Katika mikutano yao nchini Ujerumani, wajumbe hao wa Wamasai kutoka Tanzania walitoa wito kwa Wizara ya Ushirikiano wa Maendeleo, Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Wanyama ya Frankfurt kusimamia haki za binadamu katika miradi yao nchini Tanzania.

Pia walitoa wito wa kusitishwa kufukuzwa kwa lazima toka Ngorongoro. Wakati Jumuiya ya Wanyama ya Frankfurt ikikanusha kuhusika kwao, maofisa wa serikali ya Ujerumani waliwahakikishia kuwa watawasilisha matatizo yao kwa Serikali ya Tanzania katika mazungumzo yajayo baina ya serikali. Aidha, walikubali kuzungumzia suala hili kupitia Ubalozi wao wa Germany uliopo Dar es Salaam kama kipaumbele cha dharura.

Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Bunge la Ujerumani iliahidi kuendelea kufuatilia hali hiyo kupitia ziara za wabunge nchini Tanzania na kufuatilia kwa karibu vitendo vya serikali ya Ujerumani.

Ziara ya wajumbe hao kutoka Ngorongoro nchini Austria ilizaa ahadi sawia, huku Wizara ya Mazingira na Wizara ya Mashauri ya Kigeni zikiahidi kufuatilia hali hiyo, huku Balozi wa Austria nchini Kenya pia akitangaza mipango ya kukutana na wajumbe wa Maasai.

Wajumbe hao pia walisafiri hadi Roma na kuiomba Vatican kuwasaidia kutoa kilio chao.
EU, ambayo kila mwaka hutenga Euro milioni 168 katika ushirikiano wa kimataifa na Tanzania, ilikuwa kituo cha mwisho katika ziara ya wajumbe.

Tume ya Umoja wa Ulaya, Huduma ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EEAS) na Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Ulaya wa Haki za Binadamu, Eamon Gilmore, waliuhakikishia ujumbe huo kuwa wanafahamu masuala hayo na wataendelea kuibua ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa mazungumzo yao na Serikali ya Tanzania. .

Wabunge kadhaa wa Bunge la Ulaya pia walijitolea kuchunguza njia za kuchochea mwitikio wa kibinadamu haraka.


Ujumbe wa Wamasai pia ulifanya mazungumzo ya wazi na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya kwenye meza ya duara katika Bunge la Ulaya.
Katika hafla hiyo, walikanusha madai yaliyowasilishwa na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania. Katika kujibu, Balozi wa Tanzania alikanusha shutuma hizo na kudai uwazi wa serikali, na akatoa mwaliko kwa Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Asili kutembelea Tanzania mwaka 2024 - jambo ambalo halijawezekana katika miaka iliyopita.

Zaidi ya hayo, Balozi wa Tanzania katika Jumuiya ya Ulaya aliwahakikishia wajumbe wa Kimasai kwamba usalama wao hautaathiriwa watakaporejea.


Ujasiri wa wajumbe wa wenyeji kutoka Ngorongoro kujadili kwa uwazi hali yao barani Ulaya, licha ya hatari ya kulipizwa kisasi, ulijitokeza miongoni mwa safu mbalimbali za viongozi wa kisiasa wa Ulaya, taasisi, mashirika ya kiraia.

Umma mpana wa kimataifa sasa unazidi kufahamu kuwa uhifadhi na utalii katika ardhi ya Wamasai unapaswa kuwa mikononi mwa Wamasai wenyewe. Wajumbe wa Wamasai wanaporejea Tanzania, wanabeba matumaini mapya ya mshikamano wa kimataifa na kuchukua hatua dhidi ya mzozo wa sasa wa kufukuzwa.

Ziara hii iliungwa mkono na kundi la NGOs na asasi za kiraia ambazo zinasimama kwa mshikamano na watu wa Kimasai. Wanafanya kazi ya kuongeza uelewa, kukuza mshikamano wa kimataifa na kutoa jukwaa kwa Wamasai, ambao wanazidi kufanyiwa uhalifu.

Pressemitteilung – Maasai-Delegation trifft sich mit europäischen Regierungen und Politiker:innen zur Vertreibungskrise​

02.06.2023
pingosforum-snip.png


(EUROPA) Eine Maasai-Delegation beendet eine zweiwöchige Europareise, auf der sie mit Regierungen, Vertreter:innen der Europäischen Union (EU und religiösen, sowie zivilgesellschaftlichen Gruppen in Deutschland, Österreich, Italien und Belgien zusammenkam. Ziel der Delegation war es, internationale Unterstützung gegen die anhaltenden Vertreibungen aus ihrer Heimat in den Gebieten Loliondo und Ngorongoro in der Region Arusha, Tansania, zu gewinnen.

Die Advocacy-Tour löste eine große Welle der Solidarität bei den europäischen Partner:innen aus.

Die Vertreibungskrise zwingt Zehntausende von Maasai-Pastoralist:innen, ihr angestammtes Land zu verlassen, unterbricht ihre traditionelle Lebensweise und bedroht sie in ihrer Existenz. Die Delegation brachte ihre Notlage auf die internationale Bühne, da ihr Recht auf freie Meinungsäußerung in Tansania stark eingeschränkt ist.
Die Delegation machte auch auf die indirekte Beziehung zwischen den europäischen Geldern, mit denen Naturschutzprojekte in Tansania unterstützt werden, und den daraus resultierenden Menschenrechtsverletzungen für das Volk der Massai aufmerksam.

Die tansanische Regierung rechtfertigt diese Vertreibungen mit Bemühungen um den Naturschutz, doch die Massai-Delegation betonte, dass es auch andere Interessen gibt, darunter Tourismus und Trophäenjagd. Sie forderte die EU auf, ihre Finanzierung an die Einhaltung der Menschenrechte zu knüpfen, und erklärte: „Wenn Sie nicht garantieren können, dass Ihr Geld keine Menschenrechtsverletzungen unterstützt, behalten Sie es!“
Bei ihren Treffen in Deutschland appellierte die Maasai-Delegation an das Ministerium für Entwicklungszusammenarbeit, das Auswärtige Amt und die Zoologische Gesellschaft Frankfurt, die Menschenrechte bei ihren Projekten in Tansania zu beachten. Außerdem forderten sie ein Ende der Zwangsräumungen. Während die Zoologische Gesellschaft Frankfurt ihre Beteiligung bestritt, versicherten die deutschen Regierungsvertreter:innen, dass sie der tansanischen Regierung ihre Bedenken in künftigen Regierungsgesprächen vortragen werden. Darüber hinaus erklärten sie sich bereit, dieses Thema über ihre Botschaft in Dar es Salaam vorrangig anzusprechen.

Der Menschenrechtsausschuss des Deutschen Bundestages sagte zu, die Situation weiterhin durch parlamentarische Besuche in Tansania und eine genaue Beobachtung der Maßnahmen der Regierung zu verfolgen.


Der Besuch der Delegation in Österreich führte zu ähnlichen Zusagen: Das Umweltministerium und das Außenministerium sagten zu, die Situation zu beobachten, während der österreichische Botschafter in Kenia ebenfalls ankündigte, sich mit der Massai-Delegation treffen zu wollen. Die Delegation reiste auch nach Rom und bat den Vatikan um Unterstützung bei der Artikulation ihres Protestes.

Die EU, die jährlich 168 Millionen Euro für internationale Partnerschaften mit Tansania bereitstellt, war die letzte Station auf der Delegationsreise. Die Europäische Kommission, der Europäische Auswärtige Dienst (EAD) und der EU-Sonderbeauftragte für Menschenrechte, Eamon Gilmore, versicherten der Delegation, dass sie sich der Problematik bewusst seien und die Menschenrechtsverletzungen in ihren Gesprächen mit der tansanischen Regierung weiterhin zur Sprache bringen würden. Mehrere Mitglieder des Europäischen Parlaments sagten außerdem zu, nach Möglichkeiten zu suchen, um rasch eine humanitäre Reaktion einzuleiten.

Bei einem Runden Tisch im Europäischen Parlament führte die Massai-Delegation auch einen offenen Dialog mit dem tansanischen Botschafter bei der EU. Während der Veranstaltung widerlegten sie die Behauptungen, die von den tansanischen Regierungsvertreter:innen aufgestellt wurden. Daraufhin wies der tansanische Botschafter die Anschuldigungen zurück, beteuerte die Transparenz der Regierung und lud den UN-Sonderberichterstatter für die Rechte indigener Völker ein, Tansania im Jahr 2024 zu besuchen – was in den letzten Jahren nicht möglich war.

Darüber hinaus versicherte der Botschafter den Maasai-Delegierten, dass ihre Sicherheit bei ihrer Rückkehr nicht gefährdet sei.

Der Mut der Delegierten, trotz des Risikos von Repressalien offen über ihre Situation in Europa zu sprechen, fand bei einem breiten Spektrum von führenden europäischen Politiker:innen, Institutionen, Organisationen und der Zivilgesellschaft Anklang. Eine breitere Öffentlichkeit wird sich nun zunehmend bewusst, dass der Schutz und der Tourismus auf dem Land der Massai in den Händen der Maasai selbst liegen sollte.

Die nun rückkehrenden Maasai-Delegierten bringen eine neue Hoffnung auf internationale Solidarität und Maßnahmen gegen die aktuelle Vertreibungskrise nach Tansania
 
Ngorongoro ni yetu, tuamue wenyewe mambo yetu yanayotuhusu. Kutegemea EU kutuamulia mambo yetu ni utumwa!!! Kama Kuna shida Ngorongoro ni sisi wenyewe wananchi kukubali kuitatua shida hiyo. Jamani, TUJITEGEMEE.
Mbona bandari mmeshindwa kuendesha mnampa mwarabu?
 
Ukisoma hii habari utagundua kwamba hakuna Masai anayehama Ngorongoro kwa hiyari isipokua uhalifu wa kidola unawalazimisha kuhama ili kutoa fursa kwa Mwekezaji.
Hao wawekezaji na walioidhinisha huo uwekezaji haramu ni wahalifu
 
Wewe unayo hiyo mikataba? ndio maana nimekwambia nikija kutaka kukupa msaada sharti langu nikague nyumba yako utakubali? Wa China hawatupi misaada? uliwasikia wanataka kukagua...
Shida yako unahamisha mawazo ya facebook na kuleta kwenye great thinkers. Haya sio mambo ya kirafiki ya Abunuasi na Bwana Heri. Na makubaliano ya kimataifa yanayolindwa na sheria na mikataba. Ndio maana tunalia kila siku nchi za kiafrika zifike mahali zijitegemee ili kuondokana na misaada yenye masharti dhalili ikiwemo kuingiliwa mambo ya ndani. Mfano wakati wa Magufuli alikiuka masharti ya fedha za elimu bure zinazotolewa na UN aliposema hawezi kusomesha wazazi na UN wakatishia kuzuia fedha na unakumbuka hasira ya Bulembo kwa Zzk?
Mimi sio mjinga kama unavyodhani wewe. Kama masharti ya mikopo sasa wanawazuia nini? nimekwambia weka huo mkataba wa mikopo na masharti yake. Mbona ushoga tumekataa. wamezuia mikopo?
Naomba nikueleze hivi mpaka sasa tunavyozungumza Tanzania imekubali kuweka wazi mikataba yake ya kimataifa katika eneo moja tu nalo ni Sheria ya maliasili ya mwaka 2017. Ambapo mpaka hivi majuzi kutokan ana sakat la bandari serikali ikaamua kuja na mabadiliko ya sheria hiyo kwa muswada uliowasilishw amwezi juni ili kurudisha usiri na mojawapo ya provision ni kuondoa nguvu ya bunge kujadili na kupitisha mikataba na makubaliano ya kimataifa. Jambo hili limezua mjadala hadi Bunge limekataa kupokea tena muswada huo wa mabadiliko ya sheria. kwa muktadha huo makubaliano na mikataba mingine yote imebakia kuwa ni siri ya baraza la mawaziri na tunachoona kila siku wakija viongozi wa nchi nyingine ni utiliaji saini makubaliano au mikataba ya mashrikiano, na wanataja tui maeneo bila kutaja terms and conditions. Sasa kuna makubaliano na mikataba pia tunayokubaliana under the umbrela of UN na Agencies zake na tuanita ratification. Kwa mfano maswala ya haki za binadamu tumesaini kwa sababu sisi ni wanachama wa umoja wa mataifa na lazima tukubaline na Azimio la haki za binadamu (UNIVERSAL DECLARATION OF HUMAN RIGHTS YA 1948) Kwa hiyo kama nchi mwanachama tunapokiuka tunakua liable kwa vikwazo iwe kiuchumi au kijamii na hata kisiasa, rejea mwanasiasa wetu Paulo Makonda alivyowekewa sanction ya kwenda US Kwa kile kilichoitwa kunyima haki ya watu kuishi. Nikuelimishe mpaka lini mikataba hatugawiwi huku mtaani kama condom inabakia wizarani na ikulu mjinga wewe.
 
EUROPA) Eine Maasai-Delegation beendet eine zweiwöchige Europareise,


Bunge la Ulaya (EU) -Ujumbe wa Wamasai ukizungumza

Europäisches Parlament (EU) – Massai-Delegation spricht

View: https://m.youtube.com/live/6ryrvQWKjF4?feature=share

Serikali ya Tanzania imeshindwa kujibu barua ya Bunge la Ulaya kwa ukamilifu kuhusu yanayoendelea Ngorongoro pamoja na Loliondo. Majibu ya barua ya serikali ya Tanzania yalikuwa mafupi sana ya kurasa mbili ambayo hayakuwa ya maelezo ya kutufahamisha kwa kina kinachoendekea Ngorogoro

Kutokana na hayo yaomba kufanya ziara Tanzania hapo serikali ya Tanzania itapotoa ushirikiano unaotakiwa kidiplomasia waweze kwenda Ngorongoro kuweza kuona hali halisi na pia kusikia maoni ya wenyeji kwa uhuru ili kuweza kupata picha kamili halisi ...
 
Mimi sio mjinga kama unavyodhani wewe. Kama masharti ya mikopo sasa wanawazuia nini? nimekwambia weka huo mkataba wa mikopo na masharti yake. Mbona ushoga tumekataa. wamezuia mikopo?
hakuna mahali tumekataa ushoga uache kuwa mjinga zaidi, hakuna tamko rasmi la serikali wala sheria iliyotungwa na Bunge ikiharamisha Ushoga Tanzania kama case ya UGANDA hivi karibuni na hatua walizochukua hao mabeberu. Kama sheria hiyo ipo ilete hapa tuisome wote na utueleze ilitungwa lini.
kilichopo mpaka sasa ni msimamo wa serikali ya TANZANIA kwamba alichokua anakipinga MAKONDA ni msimamo wake binafsi na sio msimamo wa serikali ya Tanzania. :Serikali ya Tanzania 'yamruka' Makonda - BBC News Swahili
ndio mana mikopo na misaada inaendelea kushuka kutoka huko.
 
Siyo meekezaji bali mwizi!
Wanahistoria tunasema alikuja kama mnyonyaji mkoloni tukamuondoa akatupa uhuru wa bendera sasa amerudi na jina jipya muwekezaji. hajabadilika na wala maslahi yake hayabadilika wala mahitaji yake kiuchumi hayabadilika
 
The Government should stop the Genocide of the Maasai people, period.
Huu upishaji wa Uwekezaji usituvue nguo zetu hadharani kama baadhi ya viongozi kuonekana wakifanya hivyo, kwenda kinyume na maadili,kwenda kinyume na utu, kuhadaa jamii n.k .nk Wakemewe.

Raisi ajaye Tanzania, katika uchaguzo mkuu wa 2025 ni lazima atangaze hadharani kuwa atawarudisha Wamaasai Ngorongoro na Loliondo. Vilevile Wamaasai Ndugu zangu, msikubalinkuwarudisha hawa CCM hata kwenye viti vya kata. Kataeni CCM

Stop the Genocide
Kataa DPW
Kataa Waarabu
Wavueni CCM madaraka , wakae pembeni wajitathmini na kutafakari kama wao bado wanafaa kuiongoza Nchi hii?.
 
Fatilia ujue kinachoendelea Ngorongoro siwezi kuandika hapa pakatosha na ukaelewa sawa eeh
kwanza kwa uandishi alioandika umemwelewa au umemjibu kumridhisha nimepandisha uzi wenye habari ya uchunguzi ya Mwananchi
 
Back
Top Bottom