Hako kabinti hakakubakwa na Kapuya kwa sababu ana umri zaidi ya miaka 18 na taarifa zillizopo zinadai kuwa amewahi kuzaa na ana mtoto.Madai ya huyu binti yatathibitishwa pekee na vitu vifuatavyo: Balozi wa nyumba kumi wake amtambue kama kweli ni raia wake.Mwalimu mkuu wa shule ya msingi aliyosoma amtambue kama kweli alikuwa mwanafunzi wake.Mwalimu mkuu wa shule ya secondary aliyosoma amtambue kama kweli alikuwa mwanafunzi wake.Hospitali aliyozaliwa taarifa zake zipo, pia wamtambue kama kweli alizaliwa hapo.Majirani zake pale nyumbani anapoishi vile vile wamtambue kama kweli ni mwenzao.Hivi ni vyanzo pekee ambavyo vitatoa taarifa sahihi kuhusu huyu binti.Na mwisho kama kweli amezaa kipimo cha DNA pekee ndicho kitachotoa jibu sahihi kuwa kweli mtoto ni wa Kapuya.Waandishi wa global puplishers wanaojiita mahiri hawana lolote ni wababaishaji wa hali ya juu.Wanamhoji binti pointi ambazo hazina mwelekeo kabisa na inaonyesha wazi kabisa kama wanaegemea upande fulani.Kama kweli ni mahiri waende kwenye maeneo niliyiyataja watuletee data sahihi za huyu binti.Kwa mujibu wa maelezo yake amewahi kulala na Kapuya mara mbili tu na kumjazaa mimba palepale.Je, kwani huko anakoishi hakulala na watu wengine? Kapuya asihofu amwache aende mahakamani ukweli utapatikana na atashinda tu.