mwanaizaya
Senior Member
- Apr 26, 2008
- 133
- 1
Kibarua kigumu kumbana Kubenea.. Dk Slaa aingia, Polisi sasa wahaha
Na Mwandishi Wetu
KAULI ya Mbunge Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Wilbroad Slaa kuwa alimpa nyaraka za benki mwandishi wa habari wa Mwanahalisi Saed Kubenea ambazo polisi wanazisaka, imelipa Jeshi la Polisi kibarua kigumu kumbana zaidi mwandishi huyo.
Kutokana na hali hiyo polisi sasa watatakiwa kumpekua pia Dk Slaa ambaye serikali imekuwa akimlalamikia mara kwa mara kwamba amekuwa akipata nyaraka nyingi za serikali isivyo halali na kuziweka hadharani.
Hata hivyo Jeshi la Polisi leo limesita kutamka linamchukulia hatua gani Mbunge huyo wa Jimbo la Karatu kwa kukiri kwake kuhusika na tuhuma hizo.
Jana Dk Slaa aliulizwa na waandishi wa habari (Sio wa gazeti hili) kuhusu tuhuma zinazomkabili Kubenea na endapo yeye (Dk Slaa) alikwishawahi kupekuliwa nyaraka ambazo serikali imekuwa akidai kwamba anazipata kwa njia haramu na kuziweka hadharani.
"Hizo nyaraka za benki ambazo polisi wanazitafuta ninazo mimi na ndiye niliyempa Kubenea na jambo hilo nilikwishawahi kulizungumza bungeni," alikaririwa akisema Dk Slaa.
Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai, Robert
Manumba alipoulizwa leo asubuhi na mwandishi wa gazeti hili kuhusu kauli hiyo ya Dk Slaa hakutaka kuingia kwa undani zaidi mbali na kusema tu kwamba uchunguzi unaendelea.
"Uchunguzi unaendelea bado hatujafahamu nani anahusika na tuhuma hizo," amesema huku akikata simu baada ya mwandishi wa gazeti hili kuulizwa swali hilo mara mbili.
Ofisi za mwandishi huyo jasiri wa habari mwishoni mwa wiki zilivamiwa na askari polisi waliojitambulisha kwamba wamepewa kibali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufanya ukaguzi wa nyaraka muhimu ambazo hawakuzitaja kabla ya kubeba kompyuta yake na kinyonyeo (flash disk).
Kesho yake Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Rober Manumba aliwaeleza waandishi wa habari kuwa upekuzi huo ulifanya na polisi kumchunguza mwandishi huyo wa habari dhidi ya tuhuma za kusambaza akaunti za baadhi ya wateja wa Benki ya NBC kwenye mtandao wa intaneti kinyume cha sheria.
Manumba alisema Kubenea na mfanyakazi mmoja wa NBC, Peter Msaki wamehusishwa na tuhuma za kuchukua akauti za wateja kwa siri na kisha kuzisambaza katika mtandao.
Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Mark Kalunguyeye alisema kuwa hakuwa na taarifa za upekuzi uliofanywa katika ofisi za mwandishi huyo.
Sakata la upekuzi kwenye gazeti hilo ambalo limekuwa moja ya magazeti yanaoibua kashfa mbalimbali za ufisadi bila woga limeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi wakisema kuwa serikali inajaribu kuwatisha waandishi wasiendelea kufichua uozo zaidi.
Kuhusu hatua ambazo anakusudia kuchukua, Kubenea amesema anamtafuta mtaalam wa kukagua kompyuta iliyokuwa imechukuliwa na makachero hao ili kubaini iwapo wameongeza nyaraka zozote ambazo zinaweza kumletea matatizo.
"Waliirudisha kompyuta yangu, na hapa nilipo namtafuta mtu wa IT (mtaalam wa kompyuta) kuikagua. Huwezi kujua wanaweza kuwa wameongeza kitu chochote au kuvuruga nyaraka zangu. Lakini sintoogopa vitisho," amesema.
Tukio la kupekuliwa kwa Kubenea limekuja miezi michache tu baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia ofisi za gazeti hilo na kumjeruhi kwa mapanga Mhariri Mshauri wa gazeti hilo Ndimara Tegambwage na kummwagia kitu kinachoaminika kuwa ni tindikali yeye Kubenea.