Kibarua kigumu kumbana Kubenea.. Dk Slaa aingia, Polisi sasa wahaha

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Kibarua kigumu kumbana Kubenea.. Dk Slaa aingia, Polisi sasa wahaha



Na Mwandishi Wetu

KAULI ya Mbunge Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Wilbroad Slaa kuwa alimpa nyaraka za benki mwandishi wa habari wa Mwanahalisi Saed Kubenea ambazo polisi wanazisaka, imelipa Jeshi la Polisi kibarua kigumu kumbana zaidi mwandishi huyo.

Kutokana na hali hiyo polisi sasa watatakiwa kumpekua pia Dk Slaa ambaye serikali imekuwa akimlalamikia mara kwa mara kwamba amekuwa akipata nyaraka nyingi za serikali isivyo halali na kuziweka hadharani.

Hata hivyo Jeshi la Polisi leo limesita kutamka linamchukulia hatua gani Mbunge huyo wa Jimbo la Karatu kwa kukiri kwake kuhusika na tuhuma hizo.

Jana Dk Slaa aliulizwa na waandishi wa habari (Sio wa gazeti hili) kuhusu tuhuma zinazomkabili Kubenea na endapo yeye (Dk Slaa) alikwishawahi kupekuliwa nyaraka ambazo serikali imekuwa akidai kwamba anazipata kwa njia haramu na kuziweka hadharani.

"Hizo nyaraka za benki ambazo polisi wanazitafuta ninazo mimi na ndiye niliyempa Kubenea na jambo hilo nilikwishawahi kulizungumza bungeni," alikaririwa akisema Dk Slaa.

Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai, Robert
Manumba alipoulizwa leo asubuhi na mwandishi wa gazeti hili kuhusu kauli hiyo ya Dk Slaa hakutaka kuingia kwa undani zaidi mbali na kusema tu kwamba uchunguzi unaendelea.

"Uchunguzi unaendelea bado hatujafahamu nani anahusika na tuhuma hizo," amesema huku akikata simu baada ya mwandishi wa gazeti hili kuulizwa swali hilo mara mbili.

Ofisi za mwandishi huyo jasiri wa habari mwishoni mwa wiki zilivamiwa na askari polisi waliojitambulisha kwamba wamepewa kibali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufanya ukaguzi wa nyaraka muhimu ambazo hawakuzitaja kabla ya kubeba kompyuta yake na kinyonyeo (flash disk).

Kesho yake Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Rober Manumba aliwaeleza waandishi wa habari kuwa upekuzi huo ulifanya na polisi kumchunguza mwandishi huyo wa habari dhidi ya tuhuma za kusambaza akaunti za baadhi ya wateja wa Benki ya NBC kwenye mtandao wa intaneti kinyume cha sheria.

Manumba alisema Kubenea na mfanyakazi mmoja wa NBC, Peter Msaki wamehusishwa na tuhuma za kuchukua akauti za wateja kwa siri na kisha kuzisambaza katika mtandao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Mark Kalunguyeye alisema kuwa hakuwa na taarifa za upekuzi uliofanywa katika ofisi za mwandishi huyo.

Sakata la upekuzi kwenye gazeti hilo ambalo limekuwa moja ya magazeti yanaoibua kashfa mbalimbali za ufisadi bila woga limeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi wakisema kuwa serikali inajaribu kuwatisha waandishi wasiendelea kufichua uozo zaidi.

Kuhusu hatua ambazo anakusudia kuchukua, Kubenea amesema anamtafuta mtaalam wa kukagua kompyuta iliyokuwa imechukuliwa na makachero hao ili kubaini iwapo wameongeza nyaraka zozote ambazo zinaweza kumletea matatizo.

"Waliirudisha kompyuta yangu, na hapa nilipo namtafuta mtu wa IT (mtaalam wa kompyuta) kuikagua. Huwezi kujua wanaweza kuwa wameongeza kitu chochote au kuvuruga nyaraka zangu. Lakini sintoogopa vitisho," amesema.

Tukio la kupekuliwa kwa Kubenea limekuja miezi michache tu baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia ofisi za gazeti hilo na kumjeruhi kwa mapanga Mhariri Mshauri wa gazeti hilo Ndimara Tegambwage na kummwagia kitu kinachoaminika kuwa ni tindikali yeye Kubenea.
 
Hiyo computer inabidi asiitumie kabisa, there is no telling wameifanya nini.Hata kuiformat haitafaa maana ianawezekana wameweka ka miniature hardware kinachorecord each keystroke na kutuma somewhere.
 
Mimi nafikiri aitumie tu hiyo computer ila iwe disconnected from the internet for the time being hadi hapo atakapopata mtu wa IT mzuri ili iwe formatted na kuanza upya. Ajitahidi kutotunza mambo yake ya siri katika computer alizonazo ofisini na nyumbani kwake. siku hizi hata uki-delete documents zako za siri bado tunaweza kuzi-create na kujua ulitunza nini kabla. beware !
 
Achana kabisa na hiyo computer. Nunua nyingine. Siku hizi computer si issue bei si kubwa. Pia Kubenea hakikisha search report over the computer uliiiona na umesaini wewe au mwanasheria wako. Naamini ulifanya hivyo ili wasikuchomekee issues zao. Otherwise, keep it up. Bravo.
 
Mwaonaje tumchangie anunue computer mpya nyingine na ile awarudishie POLICE waendelee kuitumia.
 
Mwaonaje tumchangie anunue computer mpya nyingine na ile awarudishie POLICE waendelee kuitumia.

Mi nimo.

Lakini ni ndoto. Wana JF wana vichwa vikali vya mawazo, sio matendo.

Ndio maana kina Makamba wanatuita watoto wa internet.

Hatufanyi chochote.
 
Nakubaliana computer isitumiwe kwanza.
Kwani pia ni kweli inawezekana wamemtega na kizibo.
 
Mi nimo.

Lakini ni ndoto. Wana JF wana vichwa vikali vya mawazo, sio matendo.

Ndio maana kina Makamba wanatuita watoto wa internet.

Hatufanyi chochote.

Na hapo ndipo unakuja kukugundua ya kwamba sisi wa bongo maneno mingi tu hatuna lolote,ukisha fika katika suala la pesa kila mtu anaingia mitini.Wakati kwa jinsi wanaJF tulivyo wengi tunaweza kumnunulia hata komputa tatu tukiamua.
 
Na hapo ndipo unakuja kukugundua ya kwamba sisi wa bongo maneno mingi tu hatuna lolote,ukisha fika katika suala la pesa kila mtu anaingia mitini.Wakati kwa jinsi wanaJF tulivyo wengi tunaweza kumnunulia hata komputa tatu tukiamua.

Let us not underestimate the power of words. Hata kama kwa matendo tumekuwa wazito lakini mawazo tunayochangia hapa ni chachu ya mabadiliko kwani watu wanaoweza kuchukua hatua kama akina dr Slaa, Mnyika etc wanapata direction ya kuchukua.
 
Mi naona totoe mchango tumnunulie nyingine hiyo tumpe manumba atumie. tunaomba atoe requirements za Computer gani inatakiwa ili tuangalie bei yake na tuanze kutoa michango PLS
 
Mi naona totoe mchango tumnunulie nyingine hiyo tumpe manumba atumie. tunaomba atoe requirements za Computer gani inatakiwa ili tuangalie bei yake na tuanze kutoa michango PLS

Naomba Address yako nikutumiye Computer mpya Laptop or Desktop, naomba specification zake.
 
Kwa ufupi,komputa hiyo iwekwe kabatini,naam anunue nyingine mpya na achape kazi.Hata hivyo naamini yeye pia anajua kuwa ni wanted.Ila mimi namtia moyo kuwa pambana mpaka kieleweke.

Tunaopenda kumchangia twende kimyakimya tumpe tafu ili anunue nyingine.Mzee usipokee computer kutoka kwa mtu,nunua mwenyewe tafadhali.
 
Mi naona totoe mchango tumnunulie nyingine hiyo tumpe manumba atumie. tunaomba atoe requirements za Computer gani inatakiwa ili tuangalie bei yake na tuanze kutoa michango PLS
...

Great..... Mi nina imani JF ina watu makini na hasa kwenye mambo sensitive yanayojali maslahi ya umma. I fully I agree. Mod kama kuna jinsi ya kuwasilisha contributions let's do it please!!!!
 
Tunaopenda kumchangia twende kimyakimya tumpe tafu ili anunue nyingine.Mzee usipokee computer kutoka kwa mtu,nunua mwenyewe tafadhali.

Ni kweli, hata maandiko matakatifu yamesema kwamba mkono wa kulia ukitoa msaada basi ule wa kushoto wala usijue.

Lakini hapa the point ni kutuma ujumbe kwa Wazee wenye nchi waliochukua computer yake, kwamba kuna watu tunamuunga mkono Kubenea. Na kwamba hawawezi kufanya uharamia na search warrant ya "Msaki and others" sisi tunaangalia tu.

Ndio hapo watakao ona kuna grass root efforts ziko macho kulinda haki za Wananchi kupata habari, na haki ya kutosachiwa sachiwa kuharamia.

Kwa hiyo tuchangie kama Jamiiforums.

That's the point.
 
Back
Top Bottom