Hebu peleka mawazo yako kidini kunakohusika, hapa sio mahali pake!Umeona mtu yeyote na ideas za udini katika hii thread?Shindwa!Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.
nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.
BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI
KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!
Huyo jamaa fikra mgando kanikera kweli!BIig up kwa kumwelewesha!Sijui anaelewa maana fikra mgando is big problem!Hayo ndo tunaita mawazo MGANDO. Mimi ni a proud Christian tena mkatoliki mbona ninamuunga mkono Zitto?, soma michango yangu hapo juu.
Ukiwa na dhana kuwa waislamu wanaonewa utaendelea kulalamika MILELE. ACHANA NA MAWAZO DHAIFU ndugu yangu. Kuonewa mtaonewaje wakati marais wawili waliopita ni wakristo na mmoja na aliyekuwapo ni muislamu?
Ni Rais gani aliyechukua taasisi ya serikali/umma akawapa WAISLAMU?
Katoliki wana uwezo gani kuwaonea? kwa kujenga mashule? au Lutheran walivyojenga KCMC na Bugando Hospitals au waanglikan kuwa na Universities?.
One thing for sure mnachokosea na unaendelea kukosea ni kuwa wakati wewe na wenzako mnalalamika WAKATOLIKI, WAANGLIKANA NA WALUTHERI WANAFIKIRIA NAMNA YA KUONGEZA vyuo vikuu, mahospitali na mashule!!!!!.
Thats the difference bro!
Nasikitika Kibanda kurudi kulekule na kukubali kukaa pembeni,sisikitiki kwa kuwa mekubaliana na mawazo yenu bali najua kuwa ni kwa vile anajua siku moja anayoyaongelea yanaweza kuwa kweli na watu wote wanaompinga wataona aibu......Zitto anafaa sna lakini achukue changamoto za Kibanda na kuzifanyia marekebisho ili awe kimsingi,makosa makubwa ya Zitto ni pamoja na muda mwingine kutoa mawazo yake wazi ata kama yanapingana na wanachadema wenzake,sawa ni uhuru lakini uhuru kwa sasa kama mwenyekiti mpya wa chedema mtarajiwa ni lazima uwe na mipaka...otherwise hongera sana Kibanda au baba S.Wanajamvi wote
Tukubaliane kupingana bila kupigana. Tumuache Zitto agombee uenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kwa wengine wengi ana uwezo na huu ni wakati wake.
Waswahili husema wakati ukuta na tumuombee ashinde na baada ya hapo kila mmoja atakuwa na la kusema baada ya kumpima. Speculative journalism ni kitu cha kawaida duniani na wala si unprofessional or unethical kama alivyoona mwanazuoni mmoja humu.
Makala yangu (Naliona Anguko la Zitto Kabwe) pamoja na mapungufu mengi ambayo hata mimi ninayaona kutokana na michango ya wanajamvi, haikulenga kumkatisha tamaa Zitto na wale waliomlazimisha kujaza fomu uwanja wa ndege la hasha. Ilikuwa ni ya tahadhari tu.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba pengine nilishindwa kuufikisha ujumbe niliokusudia. Nimewasiliana na Zitto mwenyewe leo, jana na juzi na tumebadilishana mawazo na kuonyeshana mapungufu ya hapa na pale.
Nimezungumza na Mbowe pia kuhusu maoni ya wanajamvi juu ya kile nilichokiandika na mlichoandika wenzangu. Naamini watatumia fursa hii kuhakikisha wanawanyima mahasimu wao fursa ya kuendelea kuwatuhumu kwa ukabila, ubadhirifu, ubinafsi, utoto na mambo mengi mengine wanayokabiliana nayo. Ni jambo jema kwamba japo kwa maneno wote wanasisitiza kwamba, watahakikisha Chadema inabakia moja hata baada ya Uchaguzi Mkuu.
Zitto amenihakikishia kwamba ameichukua makala ile na nyingine nyingi zilizompinga kama changamoto na kimsingi hawezi kujiangusha yeye mwenyewe, chama chake wala vijana ambao wameonyesha matumaini makubwa kwake. Sina sababu hata moja ya kumtilia shaka kwa msimamo wake huo.
Ni jambo la faraja sana kwamba, hata katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari amekuwa makini kujibu baadhi ya hoja zilizoandika katika makala ile ya anguko kama zile za uchanga wake katika siasa.
Amejenga hoja kuhalalisha uzoefu wake kiuongozi ndani ya chama na ndani ya Bunge. Pamoja na ukweli kwamba, bado naendelea kutofautiana na staili yake ya uchukuaji fomu, ikiwa ni pamoja na kushangazwa na hatua yake ya kukubali kuungwa mkono na baadhi ya watu ambao ama wana visasi, chuki binafsi binafsi dhidi ya Mbowe, Slaa, Komu, Mnyika, John Mrema na watendaji wengine wa makao makuu
Amenukuliwa akisema analo jukumu la kuponya majeraha ya makundi ndani ya Chadema yaliyoibuka kutokana na migogoro iliyowapokonya madaraka watu kama marehemu Chacha Wangwe na kuwakimbiza ndani ya chama hicho watu kama Dk. Walid Kabourou na wengine.
Katika hili naamini atakuwa amejipanga kuhakikisha matokeo ya uchaguzi utakaompa ama yeye au Mbowe ushindi, hayataibua makundi mapya ambayo yatampasa mwenyekiti ajaye kuanza kuyatibu.
Hoja ya Nchimbi ndani ya thread hii kwamba wao CCM hadi sasa wameshindwa kutibu majeraha ya Uchaguzi wa mwaka 2005 ni somo zuri kwa Zitto, Mbowe na viongozi na wanachama wote wa Chadema.
Wito wangu kwa wanajamvi ni kuweka mbele maslahi ya taifa wakati tunapojadili hoja za namna hii, ili kuepuka lugha za kudhalilishana na kupakana matope. Wale wanaoanza kupiga chini ya mikanda na wao wakajibiwa kwa utaratibu wao huo huo wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali kwamba wao ndiyo waanzilishi.
You all deserve my apology. I'm defeated, you have all won. The battle is on but the war have ended.
Goo Zitto...Goo Mbowe...Goo Chadema.. I always wish a strong multi party democracy.
sIJAJUA MSINGI WA KUNIKARIBISHA HAPA LEO WAKATI NIKO KWA ZAIDI YA MWAKA HAPA,ANGALIA JOIN DATE YANGU NI JUNE MWAKA JANA.SWALA LA KUSEMA HAPA KUNA UVUMI ITAKUWA NI SWALA LA MTAZAMO WANGU KUTOKANA NA WAKATI HUO NIKICHANGIA HIO MDA NA MIE SIO JIWE KWAMBA SIBADILIKI KAMWE....UWEZO WA MSINGI IMARA WA CHAMA NI KUWEZA KUHIMILI MPARAGANYIKO BAADA YA KUINGIA KATIKA MVUTANO KAMA HUO.Nchimbi karibu sana maana hatimaye umeamua kuingia .Siku za nyuma ulisema hapa kuna uvumi sana na hakuna ukweli mie nikasema is where we all dare openly karibu.Maneno yako ume yaandika vyema mno na yanavutia .Nadhani mwisho wa siku Zitto atasimama na Mbowe atasimama na kuamuliwa na wana Chadema na si zaidi ya hapo .Wazee kumpa Zitto nafasi itakuwa ni mambo ya huko CCM .Zitto hata akiwa mwenyekiti bado Chama kutakuwa cha wana Chadema wote sioni wasi wasi unatoka wapi juu ya hili .Wazee wanaenda kuwapika mtu na kaka yake ili wawe kampeni ambazi si chafu lakini naamini watawataka wasimame na sisi tushudie demokrasia.
Nimefatilia kwa karibu sana malumbano haya kwa kipindi kirefu,napenda kukiri kuwa Zitto ni mtu ambaye tunafahamina kwa karibu sana,aidha Kibanda najuana nae kwa karibu sana pia.Omary ni classmate wangu na Kitila ni kaka yangu....................kati ya hawa hakuna hata mmoja ni mjinga na wote ni wajuvi wa kutetea hoja zao.Mimi mawazo yangu ni kuwa Zitto Kabwe anafaa na hafai kuwa mwenyekiti wa Chadema:
1.Mimi kama mwana uvccm-anafaa kwa kuwa vijana wenye uwezo ndio wakati wao kujitokeza.
2.Mwanademokrasia-hatupaswi kuogopa haki za watu kugombea basi hakuna maaana ya kuwa na vyama vingi kama tunafinya demokrasia ya ndani ya chama
3.Mwana ccm-Zitto hafai kwa kuwa ana uwezo mkubwa a kupata influence za kimataifa ni itapelekea chadema kupata misaada mingi ya kimataifa na kutusumbua kwenye chaguzi zetu.
4.mzalendo-hasigombee kwa kuwa itakidhoofisha chadema kutokana na kushindwa kutibu majeraha baada ya uchaguzi,as mpaka leo ccm haijapona majeraha ya uchaguzi uliopita
5.Mtanzania-itafuta taswira kuwa chadema ni chama cha watu wa kaskazini
Zitto anajipoteza mwenyewe, hii inaitwa tamaa mbele mauti nyuma, angekuwa mtu mwenye subira, Dr angeingia ikulu then yeye tungempa wiazara ya nishati na madini aongoze, immediately after dr. Zitto tungempeleka ikulu moja kwa moja.
Maskini Zitto, sasa hakuna Mtanzania yeyote makini anayemuamini.
Hiiki kijamaa kimekuwa kinafiki hadi kinasahau kimeisha wahi kusema nini hiko nyuma!"...CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake.
"…(Wanasema) eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta ‘grassroots network' ya chama, (chama) hakikujengwa na mimi.
Endelea kuota kijana ukiamka ntakusimulia ndoto zako