- Ndugu Kibanda, kwanza karibu sana JF Kumkoma Nyani na Where We Dare, ninajaribu kutafakari kwa makini sana maneno yako na hii post, sasa wakati bado ninajaribu ku-catch the spirit na motivation behind your post, naomba kukuuliza hivi nini maana hayo maneno juu?
- Halafu what CCM has to do na Zitto kutaka kugombea uongozi wa juu wa Chadema, hapo I am lost nisaidie kidogo mkuu!
Ujumbe wangu katika hoja hii ni rahisi kabisa. Uamuzi wa Zitto kugombea uwe ni uamuzi binafsi au wa kusukumwa na watu walio ndani au nje ya Chadema unaungwa mkono sana na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM.
Unajua kwa hulka yake (kama nilivyo mimi pia) Zitto ni mtu wa kujichanganya sana. Amekuwa akikutana na kubadilishana mawazo na makada mbalimbali maarufu wa CCM ukianzia na vijana.
Tabia yake hii imekuwa ikimkutanisha na watu mbalimbali maarufu ndani ya chama hicho ambao mara nyingi wamekuwa wakimpa changamoto nyingi.
Ni jambo jema na baya kwamba vigogo hao wa CCM anaokutana nao mara nyingi wamekuwa wakimueleza kuwa yeye ni moja ya viongozi dhabiti ndani ya Chadema ambao kwa kiwango kikubwa wanayo dhamana nzito ya kukiongoza chama.
Mbali ya hilo vigogo hao wa CCM wamekuwa hawasiti kueleza pia wasifu wa Mbowe na wa Chadema kwa ujumla. vigogo hao ambao hata sisi wana habari tumekuwa tukikutana nao wamekuwa wakimuelezea Mbowe kuwa ni mkabila (akiwapendelea wachaga), mbinafsi (anayekerwa na umaarufu na uwezo wa Zitto) na mtu mwenye elimu ndogo (wakizungumzia elimu ya darasani.
Maneno ya namna hii yanaonekana kumuingia Zitto sana akilini (uamuzi wake wa kugombea) na kuna hatari kuwa anayaamini (kwani yana sehemu ya ukweli na uongo pia).
Nimefanya kazi na viongozi wote hao wawili wa Chadema; Mbowe na Zitto na katika kipindi cha miaka mitatu wamekuwa ni watu wangu wa karibu sana.
Kwa kiwango kikubwa makala niliyoandika inasema sehemu tu ya ukweli ambao wakati mwingine ni mgumu kuuweka katika maandishi.
Naweza kukuhakikishia kuwa Mbowe si mtu mjinga wala mpumbavu (Zitto analitambua hilo), ni mtu mwenye ufahamu wa masuala makubwa na mazito ya kitaifa na kimataifa.
Mbowe ni aina ya wanasiasa ambao japo hawakupata elimu kubwa ya darasani, ametumia muda mrefu kujisomea na kujielimisha kwa njia mbalimbali.
Ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja japo kuwa wakati mwingine huelemewa na jazba za kisiasa awapo jukwaani. Si mbinafsi, japo kuwa ni 'mtoto wa mjini' kutokana na mazingira aliyoishi na kukulia.
Tabia yake ya kujiamini kutokana na uwezo wake wa kifedha na kutokuwa tayari kujichanganya katika makundi tofauti ya kijamii hususan na wana siasa wa CCM imekuwa ikimfanya wakati mwingine aonekane dhaifu, japo ukweli ni tofauti.
Hata hivyo naweza kukuhakikishia kwamba, huyu jamaa, pamoja na mapungufu yake mengi ni mpiganaji na mpambanaji ambaye CCM ina muogopa na kila njia ya kujaribu kumfitini na kumchafua inaonekana kugonga mwamba.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba amekuwa mzito kuchukua hatua za kukabiliana na tuhuma na shutuma nyingi za uongo zinazoelekezwa kwake.
Hata katika masuala ambayo ukimsikiliza anayo majibu mazuri na mazito kukabiliana nayo kwa hoja, yeye huamua kukaa kimya na wakati mwingine kuhamaki akitamani kuchukua hatua za kibabe kukabiliana na wazushi dhidi yake na chama chake.
Hata hivyo anabakia kuwa mtu wa vitendo na upendo mkubwa kwa Chadema pengine kuliko kiongozi mwingine yeyote ndani ya chama hicho, ukiwaacha John Mnyika na John Mrema ambao uchapakazi wao si wa kutiliwa shaka.
Zitto Kabwe si mtu wa kutulia, ni mtu mwenye mambo mengi na mara zote amekuwa ni mwanasiasa anayeishi kwa mawasiliano ya simu ya mara kwa mara na vikao vingi kila siku. Japo kuwa ni msomaji mzuri wa vitabu na magazeti, bado ni kijana ambaye hadi sasa amekosa utulivu anaopaswa kuwa nao mwanasiasa aliyekomaa.
Ni wazi kwamba akili ya Zitto inafanya kazi haraka haraka kuliko vijana wengi ndani ya chama hicho. hata hivyo kutochangamana kwake na wana Chadema wenzake katika masuala mbalimbali ya kitaifa kumempotezea ukaribu na watu wengi katika ofisi za Makao Makuu ya Chadema.
Hayo ni sehemu ya mambo ambayo Zitto anapaswa kujifunza kabla hajakabidhiwa dhamana nzito. Sidhani kwamba wapinzani kwa wakati huu, wanao muda wa kumpata Mwenyekiti wa kujifunza ustaarabu wa siasa ndani ya vyama vingi. Huo ni mtazamo wangu.