Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
..Mbowe awaachie wengine wajaribu.

..nadhani akiondoka Mbowe basi hoja za kuiandama Chadema kwa Udini na Ukabila zitakwisha.

Sio mbowe anayeandamwa na hoja ya udini na ukabila ni Chadema ndio inayoandamwa. Atoke mbowe aje zitto bado Chadema itaandamwa, as long as it is a threat to CCM. Spin doctors wamejaa CCM, vingunge kwa vijana, hawawezi kuishiwa cha ku-spin eti kwa vile mbowe ameondoka.
 
Kibanda anatetea ajira yake ndio maana amekuwa mpiga debe wa bosi. Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo mimi simlaumu Kibanda lazima atetee ugali wake ili watoto waende choo.

Njaa mbaya sana!
 
hivi kumbe kibanda mwenyewe ni mwanajamvi?mzee kama ndiyo ww fikra zako hazijakomaa kwa yale uliyoyaandika,vinginevyo nashawishika kusema tena kwa uchungu kwamba we pia fisadi
Amejiunga jana kwa ajili ya mjadala huu wa Zitto vs Mbowe.
 
Kibanda anatetea ajira yake ndio maana amekuwa mpiga debe wa bosi. Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo mimi simlaumu Kibanda lazima atetee ugali wake ili watoto waende choo.

Njaa mbaya sana!

Kwa hiyo unatetea uozo huu? Unatetea mtu anayelipwa na Mbowe kuandika hii story iliyo one sided bila hata kutoa disclosure kwamba ni muajiriwa wake? Unatetea hii obvious conflict of interest?

Eti kisingizio "Bongo"?
 

Mhariri Mtendaji kwani Zitto kugombea kiti hicho ni kuiua Chadema? kukemea kwa sauti ya ukali ndio haya maneno uliyompa DR.KITILA MKUMBO?

mimi nadhani kwa kazi hii unayomfanyia Mbowe naona utaongezwa mshahara kwani maneno uliyompa Kitila Mkumbo yamenifanya nihisi kuwa Chadema ina wenyewe.
 

Kanda,

I guess Kibanda hakuwa too careful ku mask intentions zake.Kwa hiyo Zitto kushindania uenyekiti kutadhoofisha chama? Isn't this so CCM? Isn't this type of non democratic leadership the type of style that makes CCM so stale?

Watu tunategemea CHADEMA ionyeshe demokrasia ya kweli (look, democracy is even in the party's name) sasa haya mambo ya kuleta UCCM na Usultani/ Ukikwete (mtu anayepalilia kugombea peke yake) yanatoka wapi?
 
Kibanda,
Mkuu hapa ume smell.. kubali yaishe, kuendelea kubishana na mizunguko wala haitasaidia kitu, ndio kujifunza mkuu wangu kesho haitatokea tena.. Ukirudia makosa kama haya hapo tena itatuchosha sote!
 
- Mkuu Kibanda kama kweli unaajiriwa na Mwenyekiti wa Chadema kwenye biashara zake binafsi, kama ninavyoona wengi hapa wakisema then please drop this debate, maana huna moral authority kabisaa mkuu wangu na hii subject!

- Ni ushauri wa bure tu ndugu yangu, na tafadhali sana usipotee in the future maana tunakuhitaji sana hapa JF, nakuonea huruma sana maana you have good intentions za kutetea mlo wako, ila tu huna enough reasonable facts za kutetea unachokitaka, infact wala hakiko clear exactly ni nini hasa? Halafu picking up on Kitila, ni the worst strategy ndani ya hii forum.

- Halafu what you call the truth kwenye uandishi wako, huna facts za kuutetea hapa, just drop it ili uwastahi Zitto na Mbowe, na hasa Chadema.

Respect.


Field Marshall Es
 
Wagombea wa nafasi hii wangekuwa zaidi ya wawili tungekuwa tunaongea lugha nyingine nadhani.

Mjadala huu umenifungua macho sana... Lakini kuna kitu tunaandaa, kitafungua ukurasa mpya kwenye siasa za Tanzania!

- Saafi sana mkuu na tupo pamoja sana hapo, na ubarikiwe! by the way mkuu can you imagine wahariri wote wakubwa bongo wangeletwa hapa kuchambuliwa article zao, si tungelisaidia sana taifa letu jamani, I mean mind you gazeti lenye hiyo habari hapo juu limesomwa sana na wananchi, ambao siku zote wananyimwa the otherside yaani critique kama hii ya JF, ambayo ni the best ever kifungua macho,

- Unajua why JF ni the best kifungua macho? Ni kwa sababu sisi JF we have nothing to lose never, na hatulipwi na yoyote kutoa maoni yetu,

- Mkuu Kibanda, for once jaribu kuwasiliza watazamaji wa mchezo, badala ya wachezaji!

Respect.


FMEs!
 
Pamoja na kuwapa THANKS wachangiaji wengi, hasa Kitila na Kibanda, kwa kweli sijapendezwa kabisa na muelekeo wa mjadala huu ambao uko LIVE kwa maana ya kwamba wanasoma hata watu ambao baadhi ya mambo humu hayawahusu ama yanawasaidia kubomoa mambo ambayo wengi wetu tunayasimamia na hata wachangiaji hao wanayasimamia.

Kibanda ni kweli kwamba ukweli ndio msingi mkuu wa uandishi wa habari, lakini unafahamu fika kwamba si ukweli wote unaoandikwa kwa kuwa katika uandishi na katika maisha, utakumbana na mambo mengi mno, mengine huwezi na wala hutathubutu kuyaweka hadharani kama hapa na pengine hutamnong'oneza mtu yeyote hata mtu wa ndani ya familia yako hadi kifo. Tunayo/unayo mengi ambayo utakufa bila kuyasema ama kuyaandika.

Sasa katika hii mada, nimegundua kuna tatizo kubwa sana ambalo pengine kwa kujua ama kutojua linatupunguzia nguvu muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia yenye maslahi kwa taifa. Naungana na mwana JF mmoja anayetaka kuwepo kwa dikteta mwenye visheni ili kupunguza mambo kama haya.

Kibanda katika hili, hujasaidia upinzani, hujaisaidia Chadema, hujamsaidia Mbowe, hujamsaidia Zitto na wala hujatusaidia sisi tulio nyuma yako kiimani. Sababu ya maneno yangu ni wazi kwamba maneno yako yanatoa picha mbaya sana hata kwako binafsi, jambo ambalo mimi nikiwa rafiki ya wahusika wote wakuu katika mada hii NAUMIA SANA.

Sioni maslahi ya kuwakosa wote, Zitto, Mbowe, Kitila na Kibanda, lakini katika hili dalili si nzuri kabisa na maandiko yako Kibanda yalipaswa kuzingatia kuwaunganisha watu hawa watatu na wewe ukiwa wa nne na si kuzidi kujenga ufa. Hapa umeongeza ufa.

Kuna watu uliowataja kama Mnyika na John Mrema ambao wana mengi mazito ndani ya vifua vyao na hata Zitto na Mbowe wana mengi ndani ya vifua vyao, lakini hakuna kati yao aliyevianika humu, bali kwa uchache baadhi wamekuwa wakijadiliana na wasiri wao ukiwamo wewe. Wahusika wote hao hapo juu akiwamo Zitto wamekuwa wakikushirikisha katika mambo mazito na ya siri na hivyo maandiko yako ni lazima yawe na mipaka kaka.

Mwisho naomba tumwamini Zitto kwa dhamira yake. Naamini anachosema kwamba hana nia mbaya na chama chake na Kibanda unajua kwamba hata ikitokea kwamba yeyote (hata Zitto) akiwa na nia mbaya na Chadema au upinzani kwa sasa atapotea njia hata bila kusema ataanguka ama atakwisha, Anguko liko pale pale kwa yeyote anayeshindana na upepo. Tumeshuhudia jinsi CCM inavyopata shida kushindana na upepo na vivyo hivyo hakuna mwanasiasa makini kama Zitto atakayekubali kushindana na upepo.
 

- Duh! Mkuu Halisi, this is it, naenda kulala sasa, maana hii yako ni the end of the story line, mshaurini sana Ndugu Kibanda kwamba hapa JF sio mahali pa mchezo wa kampeni za siasa! Nafikiri coming form you labda ataelewa zaidi.

Respect.


FMEs!
 
Uchaguzi huu lazima uzingatie hali halisi ya nchi kwa sasa. Wananchi wamechoshwa sana na CCM, na wanategemea Chadema iwakomboe toka kwenye makucha ya CCM.

Wakati wa kuchagua viongozi wa Chadema, lazima kwenye background tunawaza ni nani kati yao ni Presidential Material. They are, in my considered opinion, Slaa and Mbowe, in that order.

Si lazima Slaa awe mwenyekiti wa Chadema, lakini ni muhimu Slaa awe ndiye mgombea urais kwa ticket ya Chadema.
 

Pamoja na barua-pepe nyingi humu za mwandishi Kibanda hasa kutetea waraka wake kwa nini Zitto asishindane na incumbent Mbowe kugombea uenyekiti wa CHADEMA,lkn ukweli unabaki palepale;SABABU ALIZOZITOA mwandishi Kibanda KWA NINI ZITTO ASIGOMBEE UENYEKITI WA CHADEMA ZINABAKI KUWA NI LEGELEGE SANA!

Kwangu bado haja-hit points HATA MOJA zinazonifanya niamini kuwa Zitto HAWEZI kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na wala chini ya uenyekiti wa Zitto eti CHADEMA haitakuwa bora!Nasisitiza tena SABABU ZA KIBANDA NI LEGELEGE MNO na HAZINA NGUVU YEYOTE KIKATIBA!

Kibanda tuache demokrasia ichukue mkondo wake hasa ukitilia maanani kuwa ndani ya katiba ya CHADEMA hamna sehemu inayomkataza mtu yeyote mwanachama asigombee wala eti ashauriane na incumbent akitaka kugombea!
 
Tatizo haliwezi kuwa Zitto kuchukua fomu kwani ana haki zote za kugombea uenyekiti na amefuata taratibu zote, Dr slaa amethibitisha hili. Mbowe amekakaririwa na magazeti akisema kwamba hana tatizo na hilo. Zitto nae amesema amechukua fomu ili aimarishe chama. Ni vema tukawaamini mpaka hapo watakapokwenda kinyume na maneno yao.

Tatizo nionavyo mimi ni wapambe. Wapambe wa wanasiasa siku hizi kampeni kwao ndio dili. They will go to any length kuhakikisha mtu wao anapita, yote haya kwa sababu ya kulinda maslahi yao ama kutegemea kupewa vyeo mgombea wao akipita. Wanapiga kampeni kama vile uchaguzi ukishapita basi walioshindwa watajitoa kwenye chama na kutokomea kusikojulikana. Hawa wakina RA na EL wako sana hata kwenye vyama vya upinzani. Zitto anatakiwa awe mwangalifu sana kushauriwa na marafiki ambao wanaiona chadema kama kituo cha polisi. Hawajali mustakabali wa chama. Hawa ndio wakina umar na msafiri mtalemwa "vijana wajinga" anayewaongelea huyu mhariri aliyekurupuka wa gazeti la mbowe.

Kibanda amejieleza vizuri sana hapa JF, mimi nimemwelewa. Anamfahamu zitto fika, hilo halina ubishi. Lakini kama kweli alikuwa anataka kukisaidia chadema haya maelezo aliyoyatoa humu angeyaweka kwenye makala yake angeeleweka na hata hiyo heading ya makala angeibadilisha. Alichokifanya ni kumshambulia zitto na kuchochea uhasama uliopo kati ya wapambe wa hawa viongozi wawili. Anaiendeleza hii vita kwa faida ya nani? Mwisho wa siku Kibanda nawe unakuwa kama hao "vijana wajinga", makala yako is very damaging to the party, ungekaa kimya kama bosi wako usubiri chadema waamue wenyewe. Upende usipende gazeti lako ambalo ni la mwenyekiti wa chadema lina influence sana kwa wanachama wa kawaida wa chadema. Kwa kutumia maneno yako mwenyewe "Lina shepu" mwelekeo wa chama....
 
Last edited:
Binafsi niliposikia habari za Zitto kugombea uenyekiti CHADEMA, nilishtuka.

Zitto ni mwanasiasa ambaye ninamkubali sana nchi hii and he can make a very good leader in the future lakini sio siri uamuzi wake wa kugombea uenyekiti CHADEMA si uamuzi sahihi.

Unajua Zitto ana laengo yake kisiasa, ya sasa na baadaye, hivyo uamuzi wake wa kugombea uenyekiti unaweza kumpotezea malengo yango yote kisiasa au kumjenga, lakini kwa kuzingatia umri wake zaidi utampotezea. Kwa umri wake wa 32 yrs now, atalazimika kusubiri takribani 10 yrs later. Hivyo, itamlazimu kwa kipindi hiki cha miaka 10 asiharibu katika uenyekiti wake (kama ataupata), kitu ambachi ni kigumu sana
 

Mkuu Barubaru,
umetoa mtazamo wako lakini sijajua kama wewe na wengi wanaohitaji mtu kupata uongozi wa juu wa siasa awe na umri mkubwa na uzoefu mmewahi kujiuliza vema kuwa je awe na sifa zipi na labda uzoefu huwa unapatikana wakati mtu akihudumu katika wadhifa gani, maana kuna watu wanakuwa viongozi makini bila hata historia ya kuwa mabalozi wa nyumba kumi kumi na yawezekana kwa Zitto kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa Chadema taifa ndio akawa na huo uzoefu mnaouhitaji.
Nadhani tusisukumwe na fikra finyu na hoja chakavu za watu ambao pengine yanaweza yakawa ni mawazo yao binafsi yasiyo na maana ni kuyumbisha fikra makini za watu ama misukumo mbalimbali kutoka kwa wanaowapa mkate wa kila siku au michezo tu ya kisiasa.
 
hata mimi naona kawahi kiasi chake walau 2014 ndio angegombea yes; 10 yrs ukiwa mwenyekiti lazima mizengwe itakuwa ilikuangushwa kisiasa; alitakiwa awe underground na msimamo wake uonekana; isije ikawa mtu ukipiga kamsimamo fulani watu wakapiga makofi hapo hapo unataka kugombea urais/uenyekiti; no; kama wamepanga is good sasa wanatangazwa lakini kama ana malengo ya muda mrefu; no thanks; amepiga hesabu somewhere kimakosa; anyway ndio demokrasia
 

Mkuu Halisi,

You have nailed the point.........! Respect sana
 
Kwa hiyo unatetea uozo huu? Unatetea mtu anayelipwa na Mbowe kuandika hii story iliyo one sided bila hata kutoa disclosure kwamba ni muajiriwa wake? Unatetea hii obvious conflict of interest?

Eti kisingizio "Bongo"?

Hujaelewa! sitetei uozo kwa namna yeyote ile bali kusema kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo haina maana kuwa ninan tetea uozo.

If you read between the lines you can see the obvious sarcastical nature of the post!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…