Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Kinana ni bingwa wa mikakati ya wizi wa kura au pale ambapo wapinzani wanapokubalika sana karatasi za kupigia kura hazipelekwi. Zikipelekwa na CCM ikashindwa basi anailazimisha tume ya uchaguzi, uchaguzi urudiwe.

Labda hicho ndo kimbumbuga anachokimaanisha Kibanda; maana hajadadavua hoja yake. Lakini kama ni fair play, Kinana hana lolote.
 

WABHEJASANA,
Pole sana kauli za matusi ndio msingi wa hoja kwa hawa Pro-Chadema JF.[/QUOTE]

Mkuu Ritz mimi hawaniwezi kabisa hawa jamaa tena kwa matusi yao haya nitakula nao sahani moja,sema tu mod bana sometime wanaonekana kuwabeba sana wewe ukijaribu kutoa matusi unakuwa Ban faster,lakini wao wanayatoa kweli ila sijaona wanakuwa baned,lakini ndio hivyo inabidi twende nao kimzobemzobe hivyo hivyo.
 
Lakini ukumbuke kwamba wakati huo mamlaka ya utawala hayakuwa mikononi mwake. Alikuwa anapokea tu instructions kutoka kwa walio juu yake wakati huo akina Makamba. what can you expect out of Makamba. Ninachojaribu kueleza hapa ni ule uzoefu wa kukabiliana na changamoto na misukosuko ya kisiasa akiwa kama kampeni manager. Ni wazi yeye akiwa ndiyo mshika usukani atakuwa na nafasi nzuri zaidi maana anajua ni wapi huwa kuna loophole katika uchaguzi na atatoa maagizo, tofauti na mwanzoni alipokuwa anaagizwa.
 

Hebu fumba macho dakika moja halafu fikiria ni Dada yako,Mke wako,au mama yako ndo kafanyiwa hivyo utajisikiaje???!!!!,au mkuki ni kwa Ngurue ila ka binadmu ni mchungu?leo hii hauwezi kuumiakwa abaabu hayajkufika,ila naomba fanya kama nilivyokueleza halafu bada ya kupata majibu paa hewani!!!!!!
 
Wenye Akili zao wanajua kwamba hata mpaka hapa tulipoleo, pepo za kusi kulekea kasi zimebadilisha hali ya hewa; tupende tusipende, hili halitokei kutoka kwa Kibanda tu, ni ukweli wenyewe, twaweza ficha vichwa vyetu kwenye mchanga kama mbuni tukidhani hatuonekani lakini tunaonekana.
 
Hii ni vita kali sana kati ya haki na wanyanyaswa yaani Watanzania .Leo Kinana anaweza kuwa bingwa wa kupanga wizi nk lakini akiwa anajiamini akafanya kosa kubwa kiasi kwamba Tanzania ikaingia siko na kumbuka si kila Mtanzania kila eneo anaipenda CCM na kwennye vikao vyao tunao watu hao tutayajua mapema .Kuhusu Kibanda mie namuona kama Le Mutuz just ignore his dead ideas na tujadili mambo ya maana hizi ndiyo mbinu za Kinana pia kuwanunua hawa akidhani watanzania wanajua maendeleo ya Nchi yao kupitia magazeti pekee .Kuna watu kule kwetu Kyamisana hawasoni magazeti wala kusikiliza radio nk na wanajua maisha ni magumu sana na wanataka maisha ya kesho na watoto yaeleweke .
 

Mkuu hawa wanajaribu kutumia jukwaa hili kuwaonesha watu kwamba CDM inakubalika kwa wananchi,utakuta mtu mmoja kwa upande wao ana ID 10 humu ndani na mwenzake 10,na wa tatu 10 wananzisha Thread na kuanza kukoment wao wenyewe,sasa unapotoa hoja ya ukweli tofauti na zao wanazotoa ni lazima wachanganyikiwe mwisho wa iku wanjikuta wakitoa matusi kwa sababu anakuwa amechanganyikiwa.
 
Maranya we kumbe KILAZA kabisa nilikuwa nadhani una timamu kumbe haim kabisa,yani kweli unashindwa kutambua kwamba kiongozi ambaye ameshindwa kulea na kuitunza familia yake hana uwezo wa kuingoza nchi?,hivi na hili ni jambo ambalo linakutaka kuwa na Masters moja au mbili kulifahamu?!,hebu nenda kwenye Biblia angalia hata maandiko matkifu yanvyosema juu ya mtu kama Dr.Slaa,hivi umeshinda kusimamia na kuiendesha na kuiongoza nyumba yenye watu watano,utaweza nchi yenye zaidi ya watu milioni 45?.

Hata lile ombi lako la Asubuhi kamba niendelee kukuheshimu naachana nalo moja kwa moja kwa sababu nimegundua wewe ni 'Kimburu',unachojua ni kula tu lakini kutafuta wala kuwinda hujui unsubiri wenzako wakutengenezee ndio wewe ufike na kubugia mwisho wa siku ndiyo hivyo tena unakula kisha unambiwa unatkiwa kulipa na mlipo yenyewe unachaguliwa namna y kulipa!

Sitaki kufikishana mbali sana na wewe lakini wito wangu kwako ni kwamba jifunze kukubali kukosolewa,hakuna mtu asiyempenda Slaa,lakini ili tumfanye akubalike na kuonekan ni kiongozi mzuri tumshauri na kumueleza madhambi yake ayajue.
 
Waandishi walitakiwa wasaidie mapambano ya kuondoa mzoga madarakani.Nchi imefika pabaya ndio maana ukiandika mambo yanayohusu CCM,watu lazima wabwatuke.Na ukumbuke ni nyinyi waandishi wa habari ndio mliomuuza JK.Na leo unataka kuleta propaganda za kumuuza Kinana. Hao wote ni wale wale, na mimi sioni tofauti ya kinana na Mukama, wala hakuna tofauti ya Mangula na Msekwa. Wote ni Recycling ya viongozi wale wale waliolifikisha taifa hapa lilipo. Kwani hujui kinana amepata kuwa waziri, kipi cha maana au legacy yake katika Uwaziri, Au pia hujui kwamba Mangula alikuwa katibu mkuu wa CCM wakati pesa za EPA zinaingia kwenye Chama, pia amepata kuwa mkuu wa mikoa ipi legacy yake Katika nafasi ya Ukuu wa mikoa aliotumikia?
Hatundanganyiki tena Kibanda. Mafisadi wanjua bei za wahariri wa habari lakini hawana bei ya CDM , NA DR Slaa.
 
Tunatatizo la vijana kuwa na mapenzi ya kupindukia juu ya jambo au mtu kiasi cha akili kuwa likizo wakati inapotakiwa kufanya kazi yake. Naungana na Kibanda katika aliyoandika kwenye makala hii na ile iliyopita. Kama mbinu hazibadiliki, Upinzani usitegemee mafanikio mengine katika msimu wa Uongozi wa Kinana na Mangula ndani ya ccm. Ni zaidi ya kuwa muhimu sana kwa mustakabali wa nchi kuwa chini ya upinzani baada ya Uchaguzi 2015. Lakini kama Upinzani haubadili mbinu na sura za kuongoza mapambano ili ku-nullify haya mapinduzi ya kweli yaliyofanyika ndani ya Jeshi la Adui basi haihitaji uaguzi kuuona ushindi wa Kishindo wa ccm 2015.

Mashabiki wakumbuke kuwa upinzani kama CDM bado wanasubiriwa na vizingiti vingi sana tena vya miiba katika njia yao ya kuelekea 2015. Viwili vya haraka ni uchaguzi mkuu wa ndani hapo mwakani na uteuzi wa wagombea (Uraisi, Ubunge na Udiwani). Wakati ccm kaishavuka uchaguzi wa ndani kwa mafanikio ya kihistoria! Ikumbukwe kuwa 2015 CDM itatikisika sana majimboni. Wabunge wanaomaliza muda wao watakuwa na wapinzania, watapingwa ndani ya chama, watavulugana na kule kwenye majimbo yasiyo ya wapinzani, watu wengi wajitokeza kugombea kupitia upinzani hasa CDM. Na kwa kuwa CDM hawana uzoefu wa kuhimili mikikimiki ya chaguzi za Kidemokrasia (Wagombea Wengi) basi hili nalo litawatikisa.

Anayeweza kusoma alama za nyakati kwa utulivu, umakini na bila kuongozwa na hisia mfu atagundua hawezi kupingana na Kibanda. Na atagundua kuwa ccm imeanza kufanya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuanzia 2012. Haiko kwenye ngazi ya maandalizi bali tayari inahesabu kura za Zanzibar kuhakikisha hakuna tena serikali ya msemo na huku bara inauzika moyo wa matumaini juu ya upinzani kuongoza nchi katika miaka 20 ijayo. Asiyeona haambiwi tazama!

Huyu bado tu hataenda habari corporation? Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume! Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri

Ni aibu kubwa kwa waandishi kama hawa katika Tanzania.
 
Kwa jicho la hekima ninaona kabisa Kibanda yuko mbioni kuondoka Tanzania Daima ila anatafuta sababu na mazingira ya kufanya hivyo.

Ila aache hii propaganda ya Kudai viongozi na wapenzi wa Chadema wanamwandama kwa makala yake!! Ni kiongozi gani wa Chadema amemtusi?

Ni wapi tena zaidi ya JF watu wamemkosoa hadharani?
 


Kaka Ben umemaliza kila kitu,uar so intelligent,wewe ni aina ya madini yenye thamani kubwa katika mgodi wa CDM,yanasubiri kuchimbwa.nakutabiria makubwa kwenye siasa za Tanzania,kuwa mvumilivu tu.nimekufatilia kwa muda mrefu..
 
Umetumia haki yako vizuri kutoa maoni yako, usigombe na wale wengine wakupingao na hawana nafasi katika gazeti lako isipokuwa kupitia jamii forum. Kinana Kimbunga unaemzungumzia umri wake ni sawa na Tanzania kujumlisha na Tanganyika sehemu kidogo, hivi mtu akakuuliza siasa za kinana ni zipi? ubora wake ni upi? umakini wake uko wapi? busara zake ziko wapi? Bwana kibanda utamjibu nini? kwa nini usije na hizo sifa halafu utupe kazi ya kuzipinga kuliko kutuletea nahau za yeye yu nani. Hivi mtu kuwa kampeini meneja katika mfumo dola wa uchaguzi dola unampa alama ngapi za weledi katika siasa? Huyu rafiki yako ambaye amekuajiri umpigie chapuo atakuondoa katika orodha ya waandishi wa kuheshimiwa, angalia Salva ametunikiwa faraja ya kupata pesa lakini sasa kitaaluma ameona gharama yake. Unahisi mgombea wa kinana atashinda na pengine unajiandaa kuwa salva baada ya awamu ya tano kuingia madarakani kama CCM itashinda. wenzako tunajiandaa kuendelea kubeba torchi ya uamsho kuelekea Tanzania yenye neema kwa kuwaepuka hata ndugu zetu wenye harufu kidogo tu ya ufisadi.
 
Mkuu unachokisema si kweli kabisa na kama una ushahidi fanya hivyo hapa.

Ni CCM pekee ndio ambao wameajili watu rasmi ya kukaa mitandaoni kwa ajili kusafisha au kuchafua hali ya hewa na ushahidi upo.

Bahati mbaya sana kila anayeipinga CCM humu nyinyi mnambatiza/mnamsilimisha kuwa ni CHADEMA kitu ambacho si kweli kabisa.
 

Arifu mbona unakuwa too low kiasi hiki. Yani nifumbe ,macho nimfikirie dada yangu? kwani Mungu alifanya makosa kumuumba mwanamke? Yani bila aibu unaendelea kuzungumzia mahusiano ya kingono ya dada yako? Mkuu mimi sikufundishwa hivyo kufuatilia nyendo za dada yangu.

Kama ikitokea dada yangu amebakwa hapo nitakuwa mstari wa mbele kupigania haki yake lakini mtu mzima na akili yake amekubali kuhamishia mapenzi kwa mwanaume anayemtaka na kumchagua mwenyewe mimi inanihusu nini? Nadhani hapo ndipo tunapotofautiana kati ya mwanaume na mtoto wa kiume.

Halafu nikwambie kitu kingine arifu, hayo mambo ya kulilia kujifungia chumbani na dume kama mimi ni aibu sana kwakuwa mimi situmii huo mtandao hata kwa mwanamke, sasa huoni aibu kutangaza hadharani kwamba unataka nikautumie?
 
Huyu Kibanda na kalamu yake..lol! Lakini kwa nini anayasema haya sasa? Natamani kujua "motive" ya Kibanda kuandika makala za namna hii wakati huu, maana kumekuwa na msururu wa matukio hapa Tanzania, matukio hayo yalipita bila kusoma andiko la Kibanda...halafu sio Kibanda huyu huyu aliyekataa kuchukua nafasi ya ujumbe wa kamati ya vazi la taifa?[h=3]KIBANDA AJITOA KWENYE MCHAKATO WA VAZI LA TAIFA Hoja za kukataa kwake zilikuwa ni zipi?[/h]
Hakika Kibanda na Mwanahabari nazo habari zimepata mpashaji. Kila la kheri Kibanda lakini halahala na matumizi ya hiyo kalamu!
 

Big up mkuu.
 

Nilichokuwa nataka ni kuthibitisha kama kweli niliyoelezwa kwamba wewe ni kichaa ni sahihi sasa nimethibitisha kwamba kweli wewe ni chizi kolea!!!,angalia thread zako zote za leo tangu nimekugusa ulipoanza kuchanganyikiwa halafu uone kati yangu na wewe nani ambaye anataka ajue kama mwenzake ni rijali?,umesema mimi sio rijali,mana yake ni kwamba ulishawahi nipa nikashindwa kitu ambacho natka niuthibitishie umma kwamba si kweli,ila kama unataka kuthibitisha kwamba niko fiti tena zaidi ya sana,niambie nikukute wapi ili ule dozi ya kufa mtu kama ile aliyokuwa anaizungumzia Bujibuji>
 

Tatizo iliaanza kwenye makala ya kwanza. Makala haikumjadili Kinana (As a political strategist) kwa undani. Taarifa zilikuwa juu juu tu. Kibanda could have and should have done a through analysis, with proper reasoning as to why Kinana is a force to reckon with in the current political landscape. The only argument he put forward was that he was the CCM campaign manager since Multi-party politics began. And he has never lost an election. Ina wezekana kwamba Kinana is a skilled political strategist, lakini Kibanda alishindwa katika ile makala yake kwanza, to provide a well reasoned argument. This , especially considering the current political environment and the last election, where we witnessed massive state intervention in the elections is a weak argument.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…