Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

LIE can't fight TRUTH.

Ukweli umekuwa tanuru la moto mpaka umemtoa nyoka PANGONI mwake.

Dr.Slaa anadai uzalendo umemshinda!. Uzalendo upi huo ambao umemshinda?.

Hakuna cha uzalendo hapa, bali ukweli ndiyo unamchoma.

Pole pole tutafika tu.

I have said before, you can spin the truth for time being but you can't change the truth to be a lie.
 
we nawe kumbe uelewa wako ni wa la saba,yaani unaleta tamthiliya za mwampamba hapa ivi unafikiri kweli? Ludo ni swaiba wa mwigulu na connect dot kwa ninni mwampamba anamsapoti ludo kua hawezi kusaliti? Tatzo ccm ni wahuni ila elimu ndogo

Hapo ulipo bold hujatutendea haki sie wa level hiyo inabidi utuombe radhi labda kama ungesema uelewa wake ni mdogo sana, hata sie darasa 7 sio hawa waliomaliza hivi karibuni tuna uwezo mkubwa wa kufikiri kwani ukiingia humu JF unapata elimu tosha kiasi kwamba najiona kama Form 6 though sina cheti
 
Kwani mtu akifanya kazi kwenye chama cha upinzani hawezi kuwa agent wa TISS??

Hebu kamuulize Mrema, Bagenda na wenzao...!!
Kwa hiyo CHADEMA ni tawi la TISS?
Si tulisikia mkilalamika juu ya Ighondu, kumbe mtu wenu?
 
Kibanda funguka vizuri kaka, tutoe gizani. Sema uliyemwona akifanya unyama, haya mambo ya kusema ati anafanana na Ludovick hayatupi uhakika.
 
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

Yumkini, HAMY-D unafanya kazi hii kwa malipo. Siamini unapata wapi muda wa kukaa na kubishana na kila mtu hapa jamvini. Yaani wewe umepewa desktop/laptop, ukanunuliwa bundle ya internet na kazi yako ni kuandika utumbo hapa JF. In a minute to come, you will be on my ignore list. Usihangaike hata kuijibu post hii kwani sitaiona.

Tiba
 
hata mjengwa alimkana ludo na kusema alikuwa
volunteer tu.

babu naye anamkana kijana wake baada ya kumtumia kama condoms.

kazi imekolea.
 
kama kuna mtu hapa anaamini ludovick afanye mpango wa kurekodi mkanda na malipo eti 50000 huyo ni mgonjwa.

malipo ya mkanda kama huo hayawezi kuwa 50000.

ludovick alikuwa anaishi kiujanja ujanja mjini na kuomba watu 50000. kuna wanasiasa wengi na waandishi habari walimpa hizo hamsini hamsini.

hii ya kibanda kuamini ludo mmoja wa waliomteka ni jambo baya kwa chadema.

hata ulimboka hawa hawa huenda walimteka na kumsingizia jamaa wa usalama wa taifa.
Sikia hapa Mwigulu anaeleza alivyokuwa anamtumia Ludovick.



Na ni wazi nia ni kuiangamiza Chadema!

Dr. Slaa aliposema kuna mapandikizi ya CCM alishambuliwa kuwa yeye ana kadi ya CCM. Matendo ya mapandikizi hao ndio haya matunda yake yanaonekana sasa.
 
Last edited by a moderator:
Dr.W.Slaa

Wakati mwingine tunajikuta tunalazimika kuyasema hata yale ambayo hatukupanga wala kufikiria kuyasema.,nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zangu na rafiki zangu ambao bado wako chadema wakiniuliza kwanini nimeamua kuyasema ninayoyasema, tena kwa lugha kama hii (inayobainisha), nami nimekuwa nikiwajibu kuwa "hivi haiwi faraja kwenu kuwa yupo mmoja aliyewahi kuwa mfano wenu anayetaka kuwaokoa na hatari yenye kuangamiza..?

Nadhani wengi katika wao wamenielewa lakini nitazidi kuwaeleweshaa wale ambao bado wanaubutu na kutu imejaa katika fikra na mitazamo yao.Nimeeleza juu ya kukanwa na usaliti uliofanywa kwa LuDOVICK na nikaishia hapo, nikidhani kuwa itakuwa imetosha kuwafungua mawazo na kuwasaidia vigezo na vipambanuzi vya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi, maamuzi huru ambayo yatatokana na fikra zinazojitawala za kila mmoja katika upekee wake, si fikra za mkumbo (mob psychology) wala si fikra mgando na zilizosinyaa (dormant and dead reasoning), lakini nitawaongeza na hili la leo kuyaamsha mawazo hayo yaliyoganda na kuwafanya muishi kwa Uhai wa fikra Huru.

Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema.

Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:

-i) DEUS MALLYA:
Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA. Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijanakutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum. Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutetanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.

Hata baada ya kesi ya DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai)Lakini haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachfuka kwa kuonekana MALLYA pale.Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema kuendelea asili yao hiyo.

ANGALIZO:
Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;

IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao
.

Mkuu, asante kwa kuweka ushuhuda wako kuhusu USALITI unaofanywa na viongozi waandamizi wa CHADEMA pale makao makuu.

Ni mtu alie kwenye gereza la fikra ndiye atasita kuamini USALITI huu wa hawa viongozi.

Raia yangu kwa vijana mnaotumika na hawa watu wa makao makuu ya CHADEMA, jitambueni na mjifunze kutoka kwa walio watangulia.

Dr Slaa badala aeleze kinaga ubaga ya kuwa, kwa ukaribu wake na Ludovick, na tukio ambalo Ludovick anakisiwa kulifanya na bwana Kibanda, kuwa halina baraka zake yeye kama mtu wa karibu na Ludovick.

Hii ya Dr Slaa kuni-challenge kuhusu whether Ludovick ni mwajiriwa ama volunteer sidhani kama ni la msingi sana ukilinganisha na kiini cha mada yetu hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kwani mtu akifanya kazi kwenye chama cha upinzani hawezi kuwa agent wa TISS??

Hebu kamuulize Mrema, Bagenda na wenzao...!!

Hivi TISS huwa ina agents kwenye vyama vya siasa? Hebu tupe data zaidi mkuu inaonekana unajua mambo mazito na ya siri.
 
Dr Slaa, kwa kauli yako kuwa Ludovick ni volunteer wa chadema unatuthibitishia kuwa ni mfanyakazi wa chama chenu. Kwa hali hiyo kama alijitolea kufanya kazi za chama na wakati huo huo amehusishwa na rukio la Kibanda, ni wazi kuwa chadema hamwezi kukwepa uhusika wenu katika hilo.

Ingekuwa busara tu kwako na chama chako kukubali katika hilo na kumwomba radhi Kibanda. Mara zote mnasisitiza kuwa collective responsibility ndiyo demokrasia ya kweli. Na mara zote mmekuwa mkishinikiza viongozi wa ngazi zajuu wa serikali kujiuzulu kwa makosa waliyofanya watu wa chini yao.

Kama ludovick alikuwa anafanya kazi za chadema mpaka anakamatwa, ni jukumu lako wewe binafsi ukiwa ndiye unayeratibu kazi za volunteers wote wa chadema kujitathmini juu ya uhalali wako wa kuendelea katika wadhifa huo. Vinginevyo tutakubaliana kuwa alichokifanya Ludovick dhidi ya Kibanda ni kutekeleza maagizo yako na ya chama chako.

Over

Lizaboni,

You've said it all.
 
Last edited by a moderator:
Clearly something, somewhere along the line is very wrong.

CHADEMA inatakiwa kujitathimini kujua kama the line is fault or the switch.

It can't keep going with flash point along the way.

CHADEMA lazima kwanza ijitakase mbele ya jamii.
 
Hela hizo hizo pia alimuingizia Nassari, au hujui? Sasa na Nassari nae ni msaliti?

Tulia mtoto wa kiume umeulizwa maswali ya msingi jibu hoja! Sasa mpesa imeonesha alimtumia ludo ya nasari hakuna ushaidi sasa kazi kwako
 
Huyu kijana nilimuona kwenye TV anapelekwa mahakamani pamoja na boss wake Lwakatare, huku wakionyesha alama za Chadema, kumbe ndiyo aliyemteka Kibanda.
 
Sasa story ipo hivi:
Baada ya Nchemba kumtuma Ludovick akamrecord Lwakatare, na kupeleka ile video polisi, halafu akaona polisi hawachukui hatua, ndipo alimtuma Ludovick akamshambulie Kibanda ili ionekana mipango ya Lwakatare ndiyo imetimia.

Ndiyo maana mara tu baada ya Kibanda kushambuliwa, video ya Lwakatare iliwekwa kwenye mitandao.
Kwa hiyo ile video ya lwakatare ni sahihi eh.
 
Dr Slaa, kwa kauli yako kuwa Ludovick ni volunteer wa chadema unatuthibitishia kuwa ni mfanyakazi wa chama chenu. Kwa hali hiyo kama alijitolea kufanya kazi za chama na wakati huo huo amehusishwa na rukio la Kibanda, ni wazi kuwa chadema hamwezi kukwepa uhusika wenu katika hilo.

Ingekuwa busara tu kwako na chama chako kukubali katika hilo na kumwomba radhi Kibanda. Mara zote mnasisitiza kuwa collective responsibility ndiyo demokrasia ya kweli. Na mara zote mmekuwa mkishinikiza viongozi wa ngazi zajuu wa serikali kujiuzulu kwa makosa waliyofanya watu wa chini yao.

Kama ludovick alikuwa anafanya kazi za chadema mpaka anakamatwa, ni jukumu lako wewe binafsi ukiwa ndiye unayeratibu kazi za volunteers wote wa chadema kujitathmini juu ya uhalali wako wa kuendelea katika wadhifa huo. Vinginevyo tutakubaliana kuwa alichokifanya Ludovick dhidi ya Kibanda ni kutekeleza maagizo yako na ya chama chako.

Over


Mkuu hauko serious.
Dr Slaa anawezaje kuhojiwa kwa volunteers wa chama walioko kila kona ya nchi hii. Unajua maana ya volunteer? Maana yake ni mtu anayejitolea kufanya kazi za chama bila malipo. Watu wa namna hii wako ktk kila ngazi- usiwapotoshe watu humu bila sababu. Wako wanaojitolea au kuvolunteer ktk ngazi za kijiji/mtaa, kata, wilaya mkoa au Taifa. Na watu hawa huwezi kuwatawala ktk utendaji wao wa kila siku kwa sababu hujawaajiri.

Kwa hiyo, volunteer anaweza kwenda ktk eneo analojitolea mara mbili kwa wiki kwa wiki au mara 1 kwa mwezi ktk ngazi yo yote. Vile vile anaweza kufanya kazi saa moja kwa siku akaondoka na huwezi kumhoji.
Sasa, kutaka kuhoji Chadema kwa sababu ya Volunteer ambaye hujatumbia alitolea mara ngapi kwa mwezi au mwaka makao makuu ni upotoshaji wa makusudi ambao hauwezi kuijenga ccm.

Tatu, collectivie responsibility ni kwa watu walioajiriwa ambao wanaongozwa na utaratibu tofauti na waliochaguliwa ktk ngazi mbali mbali kwa sababu wanafanya hayo wakiwa na dhamana kubwa zaidi ya chama. Volunteer ni kama mwanachama wa kawaida anavyojitolea kujenga chama mahali po pote. Tofauti ni tu ni kwamba Ludo alikwenda makao makuu mara kadhaa japo hatujaambiwa mara ngapi kwa mwaka.

Mwisho hatujaambiwa kama alianza kujitolea makao makuu akiwa tayari ana mahusiano ya karibu na akina mwigulu Nchmba au la.
 
Pole Kibanda mi mbona nilishahisi hilo kitambo.Hawa jamaa ni wa kuwakalia mkao wa tahadhari.
 
Mkuu wewe kama mgeni JF, unaandika taarifa zinazojulikana halafu unageuza kashfa ya dola kuwa ya Chadema.
Ni polisi wa chadema au ccm waliomtoa nje ya mahabusu na kumhoji na kumrudisha ndani kinyume cha utaratibu?
Ni mbunge wa chadema au ccm aliyemtumia 50,000 kwa njia ya M pesa?
Ni mbunge wa chadema au ccm aliyekuwa anawasiliana na Ludovick mara nyingi kuliko mke wake kabla ya tukio hilo?
Ni polisi wa ccm au chadema waliomkamata Ludovick siku hiyo hiyo Kibanda alipotekwa huku simu yake ikiendelea kuwa hewani kinyume cha sheria?
Ninayo maswali mengi zaidi ya hayo, kwa uzi huu huisaidii ccm, unaizamisha katka matope hayo. Mzee wako hatakanyaga ikulu whether you like or not.
hivi bado yupo ndani au kshapata dhamana?
...kama hajapata dhamana ni kwa nini wakati masharti ya dhamani hayakuwa magumu sana!
 
Mkuu hauko serious.
Dr Slaa anawezaje kuhojiwa kwa volunteers wa chama walioko kila kona ya nchi hii. Unajua maana ya volunteer? Maana yake ni mtu anayejitolea kufanya kazi za chama bila malipo. Watu wa namna hii wako ktk kila ngazi- usiwapotoshe watu humu bila sababu. Wako wanaojitolea au kuvolunteer ktk ngazi za kijiji/mtaa, kata, wilaya mkoa au Taifa. Na watu hawa huwezi kuwatawala ktk utendaji wao wa kila siku kwa sababu hujawaajiri.

Kwa hiyo, volunteer anaweza kwenda ktk eneo analojitolea mara mbili kwa wiki kwa wiki au mara 1 kwa mwezi ktk ngazi yo yote. Sasa, kutaka kumhoji Dr Slaa kwa sababu ya Volunteer ambaye hujatumbia alitolea mara ngapi kwa mwezi au mwaka makao makuu ni upotoshaji wa makusudi ambao hauwezi kuijenga ccm.
Mkuu Mikael Aweda, punguza mahaba ya kisiasa babu anamfahamu Ludo alichokana ni kumuajiri.Inawezekana hata alikuwa private kachelo wake lakini hakuwa kwenye payrolls za Chadema.
 
maelezo ya bwana Kibanda nadhani wana-JF mnaweza ku-connect dots.
Ungekuwa wa maana zaidi ungetuambia huyu Kibanda unamjua vizuri! Wewe una quote so called "maelezo ya Kibanda"...... Anza ku - connects hizo dots kwa kumchambua yeye - ni mtu mwenye misimamo ipi? Ameajiriwa wapi, na kama wafadhili wake wakuu wana political leanings, huyu Kibanda utatarajia aseme lipi ili ili aendelee kuwa katika good books zao. Simple logic!
 
Back
Top Bottom