Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.
Mwigulu Nchemba hajawahi kukanisha na aje hapa abishe alivyomtuma Ludovick.... Endelea kuchimba not long utaupata ukweli
 
Last edited by a moderator:
Hii ya Kibanda inaweza kuwa ni nini maana yake?

Baada kuvamiwa kwake, suala la ugaidi likahusishwa na chadema. Kibanda huyu kanyamaza hadi mabomu wanapigwa chadema ndipo anadhani ni muda mzuri wa kuihushisha chademakwa namna moja au nyingine na kipigo kwake.

Nahisi kama vile Igh'andu na Msangi wapo kazini kuupotosha umma kama vile walivyowatenda wengine. Kitu kimoja ni dhahiri, wote waliofikwa na madhara na wakapona kwa miujiza ya Mungu, ama wamekuwa wakiweweseka au hawatamani tena kuwa na misimamo yao ya awali ama kwa hofu, majinamizi au kwa mwendelezo wa kisiri wa vitisho toka kwa wababe wa mateso na mauajiwa chama cha mafisadi ambao hata watawala wamekiri kuwa kuugusa mtandao wao kunatishia ustawi wa nchi.
 
sasa hapo cdm au ccm na mwigulu kama akili aitoshelizi tumia makamansii ya kwenye pua yako
 
Hii habar sio mpya wana cdm wenyewe walihitimisha kuwa ludovick ni ganda lililojipenyeza cdm na limeshastukiwa cha kushangaza Mwigulu hataki kumtoa mwenzie jela

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

Kumbe hata ukweli wenyewe huna ndo unatafuta halaf unajifanya kutuletea facts hapa mbele ya GTs.
 
Mkuu, kwa ukaribu wa Ludovick na Dr Slaa sidhani kama angeweza kumsaliti Dr Slaa kwa kushinikizwa na Mwigulu, hemu angalia Mwampamba anavyotoa ushuhuda wake kuhusu Ludo;
Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Hutaki tu kutumia akili "kama ilivyo kawaida yenu" ile inayodaiwa video ya Rwakatare mtu alikuwa anaongea nae ni Ludovick na ndie hasa alie mrekodi......

Swali kwa mtu mwenye akili:
Mtu aliyekuwa mwaminifu kwa CDM alipelekaje Video ile tena kwa Mwigulu? Aweje na mawasiliano na mwigulu hadi kutumiwa pesa? Kwanini CDM hawajahangaika nae kama kweli walimtuma? Si aseme sasa alikuwa na nani kwenye kumtesa Kibanda? Kwanini hadi sasa hajakiri polisi kuwa alishiriki kumtesa Kibanda pamoja na CHADEMA kumtosa?
 
Hayo unayoyasema kwa mjibu wa taarifa za cdm kuhusiana na utekwaji wa kibanda ni kweli Ludovic atakuwa alihuska na mwiguru nchemba kwani katka siku za utekaji alifanya mawasiliano mala kadhaa kulko anavyowasilana na mke wake na pesa alizokuwa anamtumia ludovic kwa njia ya m pesa zilikuwa za kufanya nini?
 
My take;

Ndugu Ludovick ambae kwa sasa bado yupo mahabusu, alikuwa ni mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, chini ya kurugenzi ya ULINZI na USALAMA kabla ya kukutwa na mkasa wake ambao ndio umemuweka rumande mpaka hivi sasa. Kuwepo kwa kijana huyu kwenye hii kurugenzi na maelezo ya bwana Kibanda nadhani wana-JF mnaweza ku-connect dots.

CHADEMA ukweli ni kwamba mwaka 2013 umekuwa mwaka 'tasa' kwenu, kwani mikakati mingi ya kichama imekuwa ikibuma na mbaya zaidi ni pale mpaka siri za ndani ya chama kuzagaa mitaani, haya yote ya kubuma na kuvuja kwa siri ovyo ovyo hivi, kuna sababishwa na 'uchanga' wenu katika kusimamia shughuli za kichama, mna safari ndefu sana.

Source: DIRA YA MTANZANIA.
shida yako ilikuwa hilo hitimisho lako,hapo kwenye blue hapo... labda tukuulize mkuu, mbona siri za CCM na barua zao za siri tunazipata na kuzisoma?je wajua ni kwa nini?kwasababu kule ndani kuna watu CCM shati tu lakini moyoni wao ni chadema, kwa hivo kwa huyo kijana yawezekana kapelekwa chadema kwa Lengo hili haswaaa, ili ionekane ni chadema wanahusika...haya connect the dots...same guy inasemekana alikuwa na mawasiliano na Mwigulu, na mpaka Kutumiana Pesa kwa Mpesa je Mwigulu ni wa chama gani?Connect dots basi..... au hapo (kwenye hilo) hupend kuconnect dots?
 
hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? Sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

hata mwagulu mwenyewe alikiri kumtumia ludo hizo hela. Upo hapo?
 
hata mwagulu mwenyewe alikiri kumtumia ludo hizo hela. Upo hapo?

Hata ile video tulijua ni ya mipango ya kumteka Kibanda sio msaki. Tulishangaa jinsi ilivyokuwa tofauti na kugeuzwa ilihali Ludo alikiri kuwa amepata taarifa ya kuumizwa kibanda saa tsa za usiku na RB yake ya kigogo mpaka leo haijapatikana. Ni kweli Ludo aliyekwa CDM alihusika, tunaomba HAMY D na serkali yenu mmbane ludo tujue nani wahusika maana ni ngumu mtu mmoja kutimiza hayo yote.
 
Unakurupuka wewe! kuna uzi ulikuja hapa juu ya huyo Ludovick siku ya kutekwa kwa kibanda, sasa hayo ndio muendelezo tu wa waliyoyapanga, ila kila kitu mungu atakiweka waziiiii very soon.
 
...
Ndugu Ludovick ambae kwa sasa bado yupo mahabusu, alikuwa ni mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, ...
Yeah, hata Tambwe Hiza naye alikuwa Katibu Mwenezi wa CUF
 
Wana-JF!!

Mnamkumbuka mhariri ABSALOM KIBANDA? AMBAE ALITEKWA NA KUTESWA?, amesema yafuatayo kuhusu wahusika ambao walimfanyia vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vimempa ulemavu wa kudumu wa jicho lake. Nanukuu;

"Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia. Mmoja wa watu walio nishambulia ana fanana kwa sura na umbile la Ludovick Rwezaura yule kada wa CHADEMA aliyewekwa ndani na Lwakatare ambae nimemuona kupitia magazeti na mitandao ya kijamii.


umenukuu vizuri Mkuu NACHOSEMA HAPA NI wazi kabisa Mwigulu nchemba anahusika kwasababu.

Ludoviki tayari alikuwa ameshamrekodi LWAKATARE na kumpelekea video mwigulu nchemba sasa vipi afanye tena tukio la ugaidi kabla ya kumtaalifu Nchemba.
Jibu haiwezekani-

kwahiyo si tu nchemba alijua kabla kuwa kibanda Atatekwa bali ndiye alipanga tukio lote.

Swala linalomuhusu Ludo wakutuhumiwa ni Mwigulu nchemba
 
Wewe inaonekana taarifa zinakupitia pembeni. Mbona hili jambo lipo wazi kabisa siku nyingi. Tena watu walileta na evidence za Ludovick mwenyewe akijitetea kwamba siku Kibanda amepigwa yeye Ludovick alikuwa ametekwa?

Sasa story ipo hivi:
Baada ya Nchemba kumtuma Ludovick akamrecord Lwakatare, na kupeleka ile video polisi, halafu akaona polisi hawachukui hatua, ndipo alimtuma Ludovick akamshambulie Kibanda ili ionekana mipango ya Lwakatare ndiyo imetimia.

Ndiyo maana mara tu baada ya Kibanda kushambuliwa, video ya Lwakatare iliwekwa kwenye mitandao.

Kwani kisa cha CHADEMA kumtosa Ludovick ni nini? Ni baada ya kugundua kwamba Ludovick ni mmafia. Hilo lipo wazi mkuu, kama hukuwa na taarifa basi uipate saa hivi.

Mwigulu Nchemba ndiye aliyemtuma Ludovick akamdhulu Kibanda ili apate cha kusema kuhusu video ya Lwakatare ambayo waliitengeneza na Ludovick.

Asante mkuu,ningesha kula ban sasa hivi maana nilijaa upepo,nisingeweza kumfundisha vizuri hivi!BADALA AJIULIZE KWA NINI CHADEMA WAMEMTELEKEZA huyo ----- mwenzie?
 
Last edited by a moderator:
Ndo madhara ya kung'olewa MAJICHO. anaona watu wawiliwawili. Alivomvua nguo MKULU kwenye gazeti alifikiri hatalipiziwa? Mkulu mtu wa fitna, na ashukuru Mungu hata anapumuwa.
 
Intelligence ya kichina hyo,kafanye utafit wa matembele kwanza ukifanikiwa jaribu kwa Ludo na Vicky wako,usi2sumbue tena humu Jf!!!
 
Mkuu Lukolo, kwa ukaribu wa Ludovick na Dr Slaa sidhani kama angeweza kumsaliti Dr Slaa kwa kushinikizwa na Mwigulu, hemu angalia Mwampamba anavyotoa ushuhuda wake kuhusu Ludo;
Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Hoja yako imepoteza uhalali. Mbona hii kitu ilisha pitwa na wakati! Kwani kilicho mfanya Ludovick kuachwa solemba na CHADEMA unajifanya hukijui?

Haya, ushatimiza wajibu wako ulio tumwa na MABWANA zako, chapchap Lumumba kasaini vocha.
 
Kwani mtu akifanya kazi kwenye chama cha upinzani hawezi kuwa agent wa TISS??

Hebu kamuulize Mrema, Bagenda na wenzao...!!

Hawezi kujua mambo hayo huyu mtoto, hiyo iko juu sana ya levo yake. Msamehe bure tu.
 
Sio Mwigulu Nchemba tuu hata Nape na ccj walihusika kwenye shambulio la kibanda hii ni kutaka kuhujumu harakati za Mh.Lowasa kwani Kibanda alimpenda sana na alionekana kkuwa kambi ya Mh.Lowassa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom