Uchaguzi 2020 Kibamba: CHADEMA wadai Mwanachama wa CCM amechukua fomu ya kugombea Ubunge kwa jina lao

Kisheria ipoje? inawezekanaje mwanachama wa chama kingine kuchukua fomu kwa jina la chama kingine, Wakati Mkurugenzi wa uchaguzi anazo taarifa za wagombea wote na vyama vyao? hapa Imechukuliwa fomu kwa jina la Chama Kikuu Chadema je kuna hasara gani Chadema kitazipata?
hujui ni sawa na kusema musiba akigombea uraisi badala ya magufuli ccm watapata hasara gani
 
Ishu nyeti km hii mtu anatoa fomu kienyeji hivi kweli! Loose stool! NEC toeni muongozo kwa hao wasimamizi wenu kuepusha huu uzezeta! Ikiwezekana mgombea alieteuliwa na chama aambatane na viongozi waandamizi wa chama ndani ya jimbo husika! Mnafanya mambo ya hovyo watu wakireact mnasema vyama vya upinzani vinasababisha vurugu..hivi kweli mtu anapewa fomu bila kutoa taarifa zozote kwenye ofisi ya mkurugenzi?? Huyo mama aondolewe mara moja atatuharibia uchaguzi!
 
Hapo yupo mbele ya camera bado anajibu majibu yanayodhihirisha nia ovu. He wayafanyayo gizani?
 
Kuna mambo mawili naamini CDM watayafanya
1. Kutoa taarifa polisi, pamoja na hili kupeleka malalamiko yao tume ya uchaguzi kwa kilichotokea

2. Waonyeshe jinsi msimamizi wa uchaguzi anavyo lifanya jambo hili kuwa hawezi kuchukua hatua hadi pale atakaporudishiwa fomu iliyochukuliwa. Nimemsikiliza kiongozi wa CDM akieleza kuwa fomu ilichukuliwa kabla CDM hawajachagua mgombea wao. Katika yote hili ndio rahisi kujiridhisha kama ni kweli na kama ni hivyo basi ile formu ni batili moja kwa moja. Pia kuna list ya CDM je ni nani alichaguliwa?
Sasa mama kushinikiza CDM wamleteee ile fomu anategemea wao watampata wapi huyo "mhalifu"? Cha ajabu kabisa inasemekana hawana namba za simu za wagombea wala anuani za makazi yao. Hivi ni vitu ambavyo havina mjadala vinatakiwa viwepo vinginevyo NEC hawako serious. Mama anashikilia barua aliyoletewa ni halali-anajuaje kuwa ni halali wakati wahusika wana mwambia si halali. Uhalali si signature tu bali na contents za barua. Anasema sio swala la busara ni swala la sheria. Kama sheria ina mapungufu unafanya je.

Matokeo kama haya yanathibitisha bado tuna elements za ushenzi. Badala ya kudhibiti washenzi, tunajaribu kuwakingia kifua kwa manufaa ya kisiasa.

Mambo yafuatayo yametokea.

1. Mhusika amechukua fomu ya kugombea siku ambayo CDM ilikuwa bado haijatangaza mgombea wa jimbo la Kibamba.

2. Aliyechukua fomu jina lake halipo kabisa ktk orodha ya wanachama wa CDM waliotia nia kugombea jimbo la Kibamba.

3. Mhusika hakuacha copy ya kitambulisho chake, pia hakuacha anuani yake wala nambari za simu kwa msimamizi wa Uchaguzi.

4.CDM wana utaratibu wa kuwasindikiza wagombea wao kuchukua fomu. Mhusika aliyechukua fomu aliambatana na mtu mmoja tu.

5.Barua haiwezi kuwa halali kwasababu imeandikwa wakati vikao vya chama havijafanya uteuzi wa mgombea wa ubunge jimbo la Kibamba.
 
Nitaendelea kuomba tafasiri ya kauli "Sasa basi" japo hakuna wa kunijibu. Why is it not applied in such circumstance!!
 
Ninawashauri Chadema wasipoteze muda kubishana na hao wahuni. Wafanye coordination na Act Wazalendo kuona iwapo kuna mgombea competent basi huyu wa Chadema amuunge mkono, Kama Act- Wazalendo hawana mgombea basi huyo wa Chadema ahamie huko achukue form na kugombea kupitia Act-Wazalendo. Wanatakiwa kuwa pragmatic, hakuna haja ya kubishana na kupoteza muda kwa kuwa hawa wahuni wa CCM wanataka kuchukua jimbo bila kupingwa. Fikirini kijeshi and smartly.
 
Mbona simple tu, yeye atoe fomu nyingine halafu utaratibu wakati wa kurudisha hiyo fomu awepo kiongozi wa ngazi za juu za CDM( Mwenyekiti au katibu) Hapo atajulikana halali ni yupi.

Hayo anayosema CHADEMA waende polisi wamtafute huyo mgombea fake fomu irudishwe kwake ndiyo atoe fomu nyingine, huko ni kupoteza muda, na kuweka mazingira ya CDM kukosa mgombea.

Huyu mkurugenzi kwa jinsi alivyokuwa anajieleza inaelekea anajua kabisa kuwa huyo mgombea alikuwa fake na hawezi kurudisha hiyo fomu.
 
Watu kama huyo mama ndio tatizo ugumu huko wapi hapo wa kutoa form nyingine. Huyo mwingine akirudisha si ndio awaite polisi.

Mambo kama hayo CDM sasa ndio wanatakiwa wakaripoti NEC kwa mtu yeyote atakaesikiliza ni ubabaifu; it doesn’t make sense wape watu form.
 
Back
Top Bottom