Ze Heby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 5,251
- 5,316
Samahani mkuu hiyo lugha ni katika kueleweshana na sio kejeliNi hivi Mimi ni principal human resources officer grade 1 niliajiriwa serikalini Kama human resources officer grade II mwaka 2006 ninafahamu yote kuhusu utumishi wa umma nje ndani.
Ninafahamu kwamba Ili mtu asomeke kwamba alikuwa mtumishi wa umma ni kupitia mfumo unaoitwa LAWSON ambao ni mfumo unaotumika kulipia mishahara kupitia hazina,
Ninafahamu pia kuwa LAWSON inatumika Sana mawizarani, sekretarieti za mikoa , halmashauri na baadhi ya taasisi za umma.
Ninafahamu pia kwamba baadhi ya taasisi za umma hazitumii mfumo wa LAWSON kulipia mishahara hivyo ni ngumu kumfahamu.
Hata hiyo LAWSON yenyewe inamapungufu nakupatia scenario ya mapungufu ya LAWSON Kuna mtu namfahamu alikuwa ameajiriwa Serikalini yupo halmashauri Kama afisa ustawi huyu jamaa aliruhusiwa kwenda kusoma masters mshahara wake akawa analipwa Kama kawaida.
Baada ya kumaliza course work kipindi Cha research akaomba kazi flani aliiona imetangazwa na sekretarieti ya ajira akaotwa kwenye interview na akafaulu sekretarieti ya ajira wakampangia kasi hiyo ilikuwa ni wizara ya mambo ya ndani ambapo walimpokea na wakaanza kumlipa na mshahara,
Yaani nakwambia hutu mtu alikuwa anakula mishahara miwili kwa kipindi Cha karibia miezi 6 alippmaliza research akaenda kule halmaahauri akaacha kazi akachukua kabisa LAPF yake akaendelea na kazi wizara ya mambo ya ndani.
Usipende kutoa kaahfa kwa watu usiowajua kwa kifupi hata wewe Kama unataka kazi Serikalini na unasifa niambie ninakonection kubwa sekretarieti ya ajira Kama Kuna kazi wametangaza na una sifa nikikurecomend kwake lazima akupangie hiyo kazi
Nashukuru Mungu mimi tayari nimeshapata kazi kwenye shirika la umma(kupitia utumishi)
Ahsante.