Kibali cha kurejea Utumishi huchukua muda gani?

Nsanzamahoro

New Member
Jan 29, 2022
4
2
Wakuu saalam! Mimi nina swali tu nataka kuuliza. kuhusu utaratibu wa kirejea utumishi wa umma kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi na baadae kuacha kazi ama kufukuzwa kazi.

Mimi nipo katika hilo kundi la kwanza niliacha kazi kwa sababu ambayo sotaitaja hapa, lakini baadae nilipata kazi tena katoka taasisi fulani ya serikali na hivyo nikafuata utaratibu wa kuombewa kibali na mwajori wangu kurejea utumishi na kuendelea kutumia check namba ile ya awali.

Sasa hapa ninataka kujua kwa waluowahi kupitia katika utaratibu huu. Je huchukua muda gani mpaka kupata majibu kuwa umekybaliwa ama kukataliwa?

Ikumbukwe pia nimepita kwenye mahojiano kwa watu waluonitafuta na kunihoji kupata taarifa zangu, kina wakati ana kwa ana na wakati mwingine kwa Simu, ikiwa ni zaidi ya mara tatu.

Ombi uilo kwa sasa lina muda wa miaka 3 na bado mpaka sasa sijajibiwa na nimefuatilia pale utumishi mara kadhaa ninaambiwa tu kwa ufupi kuwa bado wanashughulikia.

Sasa mwenye ufahamu wa hili tafadhali anifahamishe.
 
Mm mwaka wa pili sijajibiwa mpaka nimeamua kufanya ishu nyingine tu na kazi yenyewe sijawahi hata kula mshahara wake maafisa utumishi walinidumbukiza na kunipa check namba wakati ajira zilisitishwa na Rais na wakasema tusubiri tutaitwa wakati wa kuitwa sikupewa taarifa sahihi kumbe tayari wameshaniweka kwenye payroll
 
Mkuu miongoni mwa vigezo vikuu vya kuajiriwa kwa miaka hii ya karibuni ni AWE HAJAWAHI KUACHA AU KUFUKUZWA KAZI SERIKALINI AKIWA AMEAJIRIWA AJIRA YA KUDUMU. Hii ndo sababu hujibiwi.
 
Hivi nasikia ukikaa miaka zaidi ya mitano inajifuta yenyewe, halafu mbona kuna baadhi ya watu wanaacha wanarudi tu bila kukamatwa mfano kuna jamaa alikuwa askari akaacha baada ya mwaka akaajiriwa kama dereva wa mkurugenzi na mshahara ukatoka bila wasiwasi.
 
Wakuu saalam! Mimi nina swali tu nataka kuuliza. kuhusu utaratibu wa kirejea utumishi wa umma kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi na baadae kuacha kazi ama kufukuzwa kazi.

Mimi nipo katika hilo kundi la kwanza niliacha kazi kwa sababu ambayo sotaitaja hapa, lakini baadae nilipata kazi tena katoka taasisi fulani ya serikali na hivyo nikafuata utaratibu wa kuombewa kibali na mwajori wangu kurejea utumishi na kuendelea kutumia check namba ile ya awali.

Sasa hapa ninataka kujua kwa waluowahi kupitia katika utaratibu huu. Je huchukua muda gani mpaka kupata majibu kuwa umekybaliwa ama kukataliwa?

Ikumbukwe pia nimepita kwenye mahojiano kwa watu waluonitafuta na kunihoji kupata taarifa zangu, kina wakati ana kwa ana na wakati mwingine kwa Simu, ikiwa ni zaidi ya mara tatu.

Ombi uilo kwa sasa lina muda wa miaka 3 na bado mpaka sasa sijajibiwa na nimefuatilia pale utumishi mara kadhaa ninaambiwa tu kwa ufupi kuwa bado wanashughulikia.

Sasa mwenye ufahamu wa hili tafadhali anifahamishe.
Ni ngumu sana kurejea kwenye Utumishi wa Umma baada ya kuacha mwenyewe kwa hiyari yako. Zidisha maombi ndugu ili wenye mamlaka wakuonee huruma.
 
Hii hutokea kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi wa umma na akaacha kazi au alifukuzwa kazi. Utaratibu ni mwajiri anakuombea kibali cha kuendelea kutumia check namba na kurrjea utumishi. Mchakato huu ni mrefu kidogo unaweza kuchukua mpka miaka miwili hadi mitatu. inatakiwa uvumilivu sana tu, kama una mishe zingine komaa nazo, mradi una hakika kuwa mchakato unaendelea kama wamewahi kukutafuta na kukuhoji ipo siku utrejeshwa.
 
Nafikiria ni ushenzi wetu tu. Sioni sababu yeyote ya msingi kwa nini swala kama hili lisiishe chini ya miezi sita.
Gatekeepers ndio wanaelewa ukiritimba hapa.
 
Tunakumbushana tu. Usiache kazi PERMANENT & PENSIONABLE kisa umepata kikaz cha mkataba.

Kama biashara ni yako na imefikia faida nzuri na una aseti ndipo unaweza kuomba likizo ya bila malipo na hapo uwe umetumikia mika 15.
 
Hivi nasikia ukikaa miaka zaidi ya mitano inajifuta yenyewe, halafu mbona kuna baadhi ya watu wanaacha wanarudi tu bila kukamatwa mfano kuna jamaa alikuwa askari akaacha baada ya mwaka akaajiriwa kama dereva wa mkurugenzi na mshahara ukatoka bila wasiwasi.
Yawezekana hakuwahi kuacha kazi, ni kahama tu
 
Njia rahisi ni kubadili jina,mfano jina lako ni Jakaya Mrisho Kikwete(Jina hili ndio lipo kwenye Ajira ya kwanza na lipo kwenye Cheki Number na Data za Utumishi),ukifukuzwa kazi au ukiacha kazi kwenye Utumishi wa Umma,ukija kuomba tena omba kwa jina la Mrisho Kikwete Jakaya,chezesha tu majina ili jina lako kule Utumishi isionekane kama Lina exist,kuna jamaa yangu alifanya hivyo
 
Namba ya cheti cha form four unaifanyaje?
 
Hivi nasikia ukikaa miaka zaidi ya mitano inajifuta yenyewe, halafu mbona kuna baadhi ya watu wanaacha wanarudi tu bila kukamatwa mfano kuna jamaa alikuwa askari akaacha baada ya mwaka akaajiriwa kama dereva wa mkurugenzi na mshahara ukatoka bila wasiwasi.
Portal ya vyombo vya ulinzi na usalama ni tofauti na Lawson, ndio maana jamaa anadunda
 
Back
Top Bottom