Kibali cha kuomba tena kazi utumishi

Sioni Kufanikiwa Kwa Hili! Serikalini Kutoka Ni Rahisi Sana Lakini Kuingia Ndiyo Shuhuli.
 
Wakuu habari?
Naomba kuulizia nawezaje kupata kibali cha kuweza kuomba tena kazi serikalini kwakuwa niliacha kazi kutokana na matatizo je naweza kupata wapi kibali?
Kila halmashauri niombayo kazi wananiambia niombe kibali kwa katibu mkuu kiongozi ingalipo sijui ofisi yake ipo wapi? Na anuani yake Sina .
Msaada please kwa yoyote ajuaye.
Nawasilisha.
Habari za kazi ndugu,
Vp umefanikiwa kupata kibali hicho ndugu? Maana leo nimekutana na mtu anaulizia swali kama hilo
 
Wewe omba kazi utakayoiona ambayo unasifa nayo, Aidhaa kwenye CV yako usiseme ulishawahi kuajiriwa serikalini, tena kama vipi omba kwenye haya mashirika ya umma ambayo yanajilipa mishahara yenyewe kimsingi hautagundulika kirahisi labda upangiwe Kwa muajiri wako wa zamani uliyeacha ajira yako, au mtu mbaya wako akisikia umepata kazi akuchongee kwamba uliacha kazi serikalini.
Hii ilikuea zamani system now ni moja utagundulika tu ww omba kibali
 
Kuna kitu unatakiwa kukufaham Arif.
Ukiajiriwa serikali kuu (wizara, idara, tume) au Local government (halmashauri za jiji, manispaa, wilaya, miji) wewe utakua unalipwa na HAZINA na lazima upewe namba yako maalum ya kwenye payroll ndo inaitwa CheckNo. Hyo namba ukiacha kazi inablockiwa kwenye payroll hivo ukitaka kurudi tena kwenye taasisi yyte kati ya hizo hautaweza kuingizwa kwenye payroll mpaka kibali cha katibu mkuu kiongozi.

Ukiajiriwa kwenye Mashirika ya Umma (NSSF, PPF, TANESCO) au baadhi ya taasisi za serikali (BOT, TRA) mshahara wako utakua unalipwa hapohapo na mwajiri wako, SIO HAZINA. kwahyo hautakuwa na CheckNo kwakuwa hautaingizwa kwenye payroll ya HAZINA.

Sasa basi, kama uliacha kazi Serikali Kuu/LGA na CheckNo ya kublockiwa itakua ni issue sana ww kuajiriwa tena kwakuwa ukiajiriwa lazima taarifa zako zitagoma kuingia kwenye payroll na zitaonyesha ulikuwemo badae ukablockiwa. Hivo ni lazima uombewe kibali na utatakiwa kufanyiwa upekuzi wa kina ili ukiwa na vigezo vya kurudi utakuwa unblocked.

Kama ulikua serikali kuu/LGA na ukaacha kazi, ukaajiriwa upya kwenye kundi la pili yaani Mashirika ya Umma au taasisi zinazojitegemea hautapata tatizo lolote kwakuwa wao hawaongizi taarifa zako kule ulikoblockiwa (HAZINA) wanajilipa wenyewe tu. Na ndicho kilichotokea kwa huyo Muaustralia. Na kwasababu hiyo hakua hata na ulazima wa kuficha kwamba aliwah kufanya kazi akaacha coz hakuna mwingiliano wowote. Ispokua serikali ikibadili sera na kulazimisha BOT walipwe na HAZINA huyo jamaa atakua kwwnye trouble.
Ninavyo helewa mimi now mfumo ni moja ata kwenye mashirika ya umma coz watu wanahama sana na kuchanganywa changanywa
 
Nataka niombe nafadi nkasome then nkafanye zangu kazi ughaibuni huko miaka 3 ikiisha narudi zangu

Sasa kama kazi ya ulinzi au store keeper mtu anakula 2ml-3ml mbele huko na middle east,full accomodatio,transport and medical insurance
Salary ata iwekubwa vipi serikalini utoboi ni ww akili yko ya kujiongeza ktk biashar au fursa zingine hali coz serikalin awa bani sana kwenye ruhusa
 
Jamaa yuko sahihi.
Yaani ni hivi,aombe kazi kwenye mamlaka Kama Tanroads,Tanesco,Tbs bila kupitia utumishi.
Na kwenye CV yake asiandike kwamba aliwah kufanya utumishi.
Sidhani Kama watamfuatilia huko kote

Siku hizi ajira zote zinapita utumishi au kusimamiwa na utumishi halafu hakuna taasisi isiyotumia check number kwasababu mishahara yote inatoka hazina
 
Wewe omba kazi utakayoiona ambayo unasifa nayo, Aidhaa kwenye CV yako usiseme ulishawahi kuajiriwa serikalini, tena kama vipi omba kwenye haya mashirika ya umma ambayo yanajilipa mishahara yenyewe kimsingi hautagundulika kirahisi labda upangiwe Kwa muajiri wako wa zamani uliyeacha ajira yako, au mtu mbaya wako akisikia umepata kazi akuchongee kwamba uliacha kazi serikalini.
Hujui chochote kuhusu system ya ajira serikalini.(Serikali kuu,serikali za mitaa na mashirika/taasisi za umma)
 
Jamaa yuko sahihi.
Yaani ni hivi,aombe kazi kwenye mamlaka Kama Tanroads,Tanesco,Tbs bila kupitia utumishi.
Na kwenye CV yake asiandike kwamba aliwah kufanya utumishi.
Sidhani Kama watamfuatilia huko kote
Atapataje na zote zinapita utumishi mkuu
 
Atapataje na zote zinapita utumishi mkuu
Sio kazi zote zinatangazwa na utumishi.
Kuna kazi zingine taasisi huwa zinatangaza zenyewe na kuwafanyia interview wenyewe ila kwenye utoaji wa mishahara hapo ndio sina uhakika wanatoaje.
 
Sio kazi zote zinatangazwa na utumishi.
Kuna kazi zingine taasisi huwa zinatangaza zenyewe na kuwafanyia interview wenyewe ila kwenye utoaji wa mishahara hapo ndio sina uhakika wanatoaje.
Hizo ni za mkataba au za muda mfupi
 
Back
Top Bottom