Kibaka alivyosulubishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibaka alivyosulubishwa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Sep 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Haya mambo bwana, usishangae sasa hata kuiba hajaiba. Kuna siku tulikuwa tunasafiri kwenye daladala toka ubungo kwenda posta. Humo ndani alipanda kibaka, akachomoa simu ya mtu, mwenye simu alipogundua akatangaza kwamba ameibiwa. Kibaka alipoona inataka kuwa soo akaamua kuidumbukiza ile simu kwenye begi ya mdada mmoja humo kwenye daladala.

  Aliyeibiwa simu akaanzisha msako kwa kila abiria, yule mdada wa watu bila hili wala lile akalitoa begi lake kwa kujiamini kabisa lisachiwe. On her suprise simu ilikuwa mle, alikula kibao hadi anajikojolea kama si abiria wengine kuamua kumtetea. Nadhani yule dada angeishia pale. Yule kibaka baada ya kuona abiria wameanza kuweka doubt alitoka mbio za ajabu. Hata kumkimbiza ilikuwa vigumu.

  Kila siku huwa nakumbuka ile incidence halafu najiuliza, kwamba suppose ile simu ingetumbukizwa kwenye mfuko wa suruali wa kijana mmoja mchafuchafu aliyechoka na maisha? Au suppose abiria wasingejenga moyo wa kumwamini yule dada wakaamua kumkomalia kwa mawe na manondo?

  Kwakweli kuwe na mipaka katika maamuzi ya kumpiga mtu kwa kumhisi kuwa ni kibaka.
  Kuna incidence nyingine ilitokea mabibo hosteli waliowahi kuishi huko wanaweza kuwa wanaifahamu. Mkaka wa watu akauawa kwa kudhaniwa ni mwizi kumbe ni ugomvi kati yake na girlfriend wake. Tuwaelimishe wananchi juu ya hatua hizi za kujichukulia sheria mikononi.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lukolo,
  Ni kweli kuna haja ya wananchi kujifunza ustaarabu wa kuwakabidhi watuhumiwa mikononi mwa polisi, na polisi nao wajenge uaminifu siyo mtu anapelekwa kituoni halafu siku inayofuata mnamkuta mitaani na kesi imefutwa polisi...wananchi wanakosa imani ndiyo mambo haya yanatokea. Hatari yake anaweza kuuwawa mtu hana hatia kabisa.
   
 4. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nchi imeoza kuanzia kwa president mpaka kwa walinda usalama hapo vituoni ukimpeleka kituoni siku mbili unamkuta mtaani na atakuumiza wewe.Kama mkasa ulionikuta nilivyotembelea sehemu fulani kipindi niko vacancy.Kwa mimi nasapoti kama ameshikwa na ushahidi iwe tit for tat na yeye anapewa kichapo cha paka mwizi.Na ikiwezekana ni kumtoa roho ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hapo pekundu ndio kwenye shida katika issue za mob justice. Ndio maana watuhumiwa wanatakiwa kupelekwa mahakamani - katika hali nyingi kama ilivyosemwa na wadau watu huuawa na baadaye ushahidi huonyesha kwamba hawakuwa majambazi.

  Nakumbuka kwa huzuni tukio moja la Mabibo miaka kadhaa iliyopita. Bwana moja akiitwa Gonelimali aliingiliwa na majambazi usiku, akapiga kelele kuomba msaada. Watu waliitikia lakini wakamwua mwenyewe. Alikuwa ametoka nje kufuatilia majambazi akawa katika migomba iliyo around nyumba yake. Maskini akadhaniwa ndiye jambazi. Kelele za kujitambulisha hazikusaidia. "Mob justice!"
   
 6. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sasa ndugu yangu kama mimi ambaye nilikwenda nyumbani siku moja nikaamua kusimamia biashara yangu mwenyewe ya daladala na kuishia kukabwa na vibaka pale Victoria nitaachaje kusuport mob psychology wakati mwizi wangu ninamuona anatokomea na pesa yangu?
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,670
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  Chanzo cha mob justice ni utendaji mbovu wa jeshi la polisi uliojaa rushwa na mizengwe ya kijinga. Wananchi wakitaka haki itendeke kwa kufuata mkondo wake, Polisi wanavuta uchache kisha vibaka hao wanarudi mtaani KWA KASI ZAIDI, CHUKI ZAIDI NA VISASI ZAIDI hivyo raia wema wanachukua hatua hizi ambazo sio nzuri hata kidogo, ila wafanyeje kama Polisi ndio hivyo?
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa kutumia nguvu ya kutosha kumweka chini ya ulinzi na kumfikisha Polisi/Mahakamani. Hata hiyo nguvu ya kutosha ikiwa kumvunja miguu - sawa.

  Ni wazi nami natambua sana udhaifu wa vyombo vyetu vya dola vya kutokushughulikia sawasawa uhalifu. Lakini jee suluhisho ni mob justice ambayo mara nyingine huua wasio na hatia? La. Suluhisho ni kuiandama/kuibadilisha serikali hadi ulinzi tunaoulipia kodi uwepo na wananchi tuwe na usalama.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ndugu umenikumbusha : Nina visa viwili navyo fanana na hiki: tulikuwa natabia ya kuacha pipa nje kutokana na ukame wa maji hasa kipindi cha mvua ili kama mvua ikinyesha niwe nauhakika wakupata maji, likaja kuibiwa pipa nilikasilika sana, baada ya siku mbili, jirani yetu alikuja kuniamsha mida ya saa 12 asubuhi, akanieleza kuna mtu kalala kwenye kibanda chetu ambacho kilikuwa kama mita 30 kutoka kwenye nyumba yetu, lakini huyo jamaa alielala humo anapanga na kisu pembeni haraka haraka nikaamka nikavaa nikachukua wire ambao huwa wanatumia kufungia baskeli tukaenda kwenye kile kibanda tukamkuta jamaa amelala mpaka nakoloma, tukafungua kipanda tukazichukua panga na kisu, ndiyo tukaanza kumpiga huku tukiita mwizi watu walijaa kila aliyekuja alitusaidia kumtwanga daah jamaa tulimpiga ile mbaya, akaja balozi akatutaka tumpeleke polisi kabla hatuja mpeleka polisi akatokea jamaa ambae anakaa mtaa ulele akatuambia huyu jamaa walikunywa nae pombe mpaka saa 10 usiku kwenye baa moja ambayo iko maeneo hayo hayo naalikuwa amelewa sana, ndipo watu wakaanza kumhoji yeye ni nani ametokea wapi, jamaa alisema yeye ni fundi ujenzi kuna site anajenga jana yake akuwa kwenye baa iliyotajwa maka usiku…alikuja kwenye kile kibanda baada ya kulewa na kuishiwa na ilikuwa usiku sana ndipo alipo amua kuingia kwenye hicho kibanda na panga na kisu sio vyake, ndipo watu wakaamua kumfaata mwenye kibanda(mpangaji wakibanda) akavitambu panga na kisu kuwa ni vyake, nilicholopoka kwenda nyumbani maana nilijua sasa kibano kinatugeukia baadae jamaa aliombwa na balozi atusamehe naakapewa Tshs 20000 akatibiwe…baada ya miezi mitano kupita nilikumbana na kisa cha pili: Nilienda kwa rafiki yangu baada ya miezi mitatu bila kwenda kwake....kisa kilianza baada ya kufika mahali hapo nilikuta akina mama wanasukana sikuto salaam nikaingia ndani nikimwita shemeji yangu maana nilikuwa na utani nae kilicho nishangaza nilikuta kila nilicho kiona kilikuwa kigeni kwangu, nyumba yenyewe ilikuwa ni chumba na sebule nilipo angalia chumbani liona mpaka viatu mashuka tofauti nikashituka nikatoka nje kumbe wale akina mama wananisubilia nje na mbaya zaidi majuzi yake waliibiwa, ile natoka wakaita mwizi mwizii mwizi mwizi nikajua nimekwisha watu wakaja bahati nzuri watu wa kwanza kuja walikuja watu ambao wananifahamu na nusu saa iliyopita nilikuwa nasheza nao mpira...wakanipa nafasi ya kujieleza ndiyo watu walipo gundua mimi siyo mwizi na kosa nililofanya ni kuta wasalimia wale akina mama kwani wangeweza kuniuliza naenda wapi... kabla hata sijaingia ndani...

  Tangu hapo huwa sikurupuki kupiga mwizi..
   
Loading...