Mkuu vipi leo.. ama hizi ndio hatari za ku copy na kupaste?.. Ni wapi wewe umezungumzia IMF au Saudia na Afghanstan mbona hatuelewani?..Mkuu Mkandara.
Uache kukurupuka...soma kwa makini hiyo taarifa niliyoibandika.
Unaona umeleta suala la OIC, jumuiya ya kiislamu...makala inazungumzia OIC hii;the Indian Ocean Commission (IOC), a regional cooperation body whose current members are Comoros, Mauritius, Seychelles, Madagascar and Reunion......
Nimeisoma habari vizuri sana na nimepingana nayo na kukueleza sababu zake halafu paraghraph iliyofuata nimesema nachoweza kubaliana na wewe ni Zanzibar kujiunga na OIC (Organisation of Islamic coopreration) japokuwa pia nimeeleza hofu yangu.
Na hii sii mara yangu ya kwanza mimi kuzungumzia kuafiki swala hili kwa sababu Zanzibar ilitawaliwa na Oman (Sultan) na nimeshatoa mifano ya Quebec kuwa wanachama wa umoja wa nchi za Kifaransa wakati the rest of canada ni mwanachama wa Commonwealth..Halfu pia lengo kubwa la OIC ni kufundisha watu kuvua samaki na sio kupewa kipande cha samaki..
Hiyo OIC (Indian Ocean Commission) inahusiana na mazingira na nimekwambia vizuri kwa nini nyie msipeleke vijana wenu wakajifunze taaluma ya mabadiliko ya hali ya hewa (climate changes) badala ya kutegemea wageni ambao kwanza inakula kwenu, sasa unataka nieleze nini zaidi. Na bila shaka umewahi kunisoma, mimi huunganisha habari nyingi kwa wakati mmoja kuwataarifu ubaya wa jambo na yanayowezekana..Hakuna mahala umeniuliza kuhusu IMF, Saudia wala OIC na nimeyaweka baada ya kuchambua yako kuonyesha wapi napakubali. Siku zote hujibu swali halafu nakupa alternative solution, huu ndio uandishi wangu siku zote.
Kuhusu wafadhili na mikopo tunaihitaji sana tu ikiwa tutalenga ujenzi wa miundombinu na kuwafundisha vijana wetu elimu dunia kulingana na mazingira yetu. Leo hii kweli kinachofanyika ni usanii mtupu maana JK majuzi ati ndio anatangaza kuanzisha chuo cha madini nchini.
Jambo zuri lakini tulikuwa wapi siku zote hadi tumegawa karibu 3/4 ya miradi yote mikubwa ya madini wakati Nyerere alituachia usia ambalo kila Mtanzania anaujua wakati akiwaambiwa mabeberu (Imperialist) kwamba anaacha madini huko chini hadi sisi wenyewe tutakapo kuwa na ujuzi wa kuyachimba.
Kwa nini hatukuendelea kuwafunza vijana wetu? Kwa hiyo usanii upo kila sehemu na ndio maana sikubaliani na mawazo ya wageni kuwekeza ktk madini, Uranium na sijui gesi matokeo yake tunanyimwa hata share ya maana kutokana na kwamba hatuna cha ku offer..